Kufuatilia Vituo vya YouTube

Unaweza kufuatilia vituo unavyopenda ili uone maudhui zaidi kwenye vituo hivyo. Unaweza kupata kitufe cha Fuatilia chini ya video yoyote au kwenye ukurasa wa kituo. Ukianza kufuatilia kituo, video zozote mpya ambazo kitachapisha zitaonekana katika mipasho ya Vituo Unavyofuatilia.

Huenda pia ukaanza kupata arifa wakati kituo unachofuatilia kinachapisha maudhui mapya. Kwa chaguomsingi, tutakutumia mihtasari kutoka kwenye kituo pekee hicho. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti arifa zako.

Kuanza kutumia | Jinsi ya kufuatilia chaneli ya YouTube na sababu za kufuatilia

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kufuatilia chaneli ya YouTube

  1. Fungua programu ya YouTube au uende kwenye m.youtube.com.
  2. Ingia kwenye YouTube.
  3. Ikiwa upo kwenye kichupo cha Ukurasa wa Mwanzo :
    • Chini ya video kutoka kituo unachotaka kufuatilia, gusa aikoni ya kituo.
    • Gusa Fuatilia .
  4. Iwapo unatazama video kutoka kituo ambacho ungependa kufuatilia:
    • Chini ya video, gusa Fuatilia .

Baada ya kufuatilia kituo, utaona orodha ya vituo vinavyopendekezwa kwenye skrini yako. Vinatokana na vituo vinavyohusiana ambavyo hufuatilii. Unaweza pia kuangalia maudhui ya kituo kabla ya kukifuatilia.

Utakapopata arifa

Unapofuatilia kituo, tutakutumia arifa kiotomatiki kuhusu mihutasari kutoka kituo hicho. Unaweza kuchagua kupata arifa kila wakati kituo kinapochapisha maudhui kwa kubadilisha mipangilio yako ya arifa

Kumbuka kuwa ukiacha kufuatilia kituo na kisha uanze kukifuatilia tena, mipangilio yako ya arifa itabadilishwa.

Hutapata arifa iwapo mipangilio ya kituo imewekwa kuwa inalenga watoto. Vile vile, kengele ya arifa itawekewa mipangilio ya hamna arifa . Hutaweza kubadilisha mipangilio hii. 

Kujiondoa kwenye chaneli ya YouTube

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video kutoka kituo ambacho ungependa kuacha kufuatilia.
  3. Chini ya kicheza video, bofya Fuatilia kisha Acha kufuatilia.
  4. Katika sehemu ya chini ya skrini, utapata arifa inayothibitisha kuwa umeacha kufuatilia.

Kudhibiti vituo unavyofuatilia kwenye YouTube

Kupata vituo vya kufuatilia

YouTube hukuonyesha video na vituo ambavyo tunafikiria utapenda kwenye kichupo cha ukurasa wa Mwanzo  na ukishatazama video. Tunapendekeza video hizi kulingana na ulichotazama na kinachovuma.  

Ikiwa hupendi tunachopendekeza, unaweza kutufahamisha kuwa huvutiwi.

  • Kuvinjari kulingana na aina: Ikiwa ungependa kuona vituo kuhusu mada mahususi, nenda kwenye Gundua ili uone vituo maarufu katika aina tofauti.
  • Tafuta: Jaribu kutafuta mambo yanayokuvutia kwenye YouTube. Kisha unaweza kutumia kichujio kwenye matokeo ya utafutaji ili kuonyesha vituo vinavyohusiana na utafutaji wako. 

Kuona vituo vya YouTube unavyofuatilia

Unapofuatilia kituo, utaona video mpya katika kichupo cha Vituo Unavyofuatilia . Kichupo cha Ukurasa wa Mwanzo  huonyesha pia video kutoka vituo unavyofuatilia, pamoja na mapendekezo ya vituo au video ambavyo huenda vikakuvutia.

Ili upate Vituo unavyofuatilia, fuata maagizo haya:

  1. Fungua programu ya YouTube.
  2. Ingia kwenye YouTube.
  3. Gusa kichupo cha Vituo Unavyofuatilia

Unaweza kwenda kwenye orodha ya vituo vyako kwa kugusa Vyote na kuchuja matokeo yako ukitumia kishale cha menyu kunjuzi katika sehemu ya juu.

Kituo unachofuatilia kinapokuwa na maudhui mapya, utaona nukta karibu na jina la kituo. Ikiwa kituo unachofuatilia kinatiririsha mubashara maudhui, utaona neno “Mubashara” karibu na jina la kituo.  

Kutatua hitilafu katika vituo unavyofuatilia kwenye YouTube

Vikomo vya vituo unavyofuatilia kwenye YouTube

Ukiona ujumbe kuhusu hitilafu unaosema "Unafuatilia vituo vingi mno," basi umefikia kikomo chako cha vituo unavyofuatilia. Unaweza kufuatilia hadi vituo 75 kwa siku.

Kwa ujumla, unaweza kufuatilia hadi vituo 2,000. Lakini, kikomo chako cha chaneli unazofuatilia huongezeka kadri chaneli yako cha YouTube inavyoimarika — hutokana na idadi ya wanaofuatilia chaneli yako na muda ambao akaunti yako imekuwepo. Vikomo vyako halisi vinabadilika kadri muda unavyopita.

Tunapendekeza uweke kikomo cha 5,000 cha vituo unavyofuatilia kwenye akaunti yako ili kuhakikisha mipasho ya vituo unavyofuatilia na orodha ya vituo inakupa hali bora ya utumiaji.

Viendelezi vya wengine vinavyokufanya ufuatilie vituo bila ruhusa yako

Ukipata arifa ya video na vituo ambavyo hukufuatilia, au maudhui ambayo uliacha kufuatilia, huenda hali hii ikatokana na kiendelezi cha kivinjari kinachokufanya ufuatilie vituo bila ruhusa yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti viendelezi vya kivinjari.

Tofauti kati ya Mipasho ya Vituo Unavyofuatilia na Arifa

Mipasho ya Chaneli Unazofuatilia, inayopatikana kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta, huonyesha video zozote zilizopakiwa hivi karibuni kutoka kwenye chaneli unazofuatilia.

Arifa zinaweza kukueleza kunapokuwa na video mpya, kutuma masasisho kutoka kwa usajili wako na pia zinaweza kukuarifu kuhusu maudhui ambayo unaweza kuyapenda. Tutakutumia barua pepe, arifa zilizowekewa mapendeleo kwenye vifaa vya mkononi au arifa kwenye kikasha katika kompyuta au kifaa chako cha mkononi. Unapofuatilia chaneli, utapata kiotomatiki arifa zilizowekewa mapendeleo zinazoangazia shughuli.

Arifa kwenye kikasha hupangwa kulingana na wakati, arifa mpya zaidi zikiwa katika sehemu ya juu. Baadhi ya arifa zinaweza kuangaziwa juu ya arifa mpya zaidi katika sehemu ya "Muhimu", ambayo inaangazia arifa tunazodhani zinaweza kuwa muhimu zaidi kwako. Mifano ya arifa muhimu inaweza kujumuisha jibu kwa maoni yako au watu wanapotuma video zako.

Ili upate arifa zote kutoka kwenye chaneli unayofuatilia, gusa kengele ya Arifa  . Kisha kengele hiyo itabadilika na kuwa kengele inayolia  ili kuashiria kuwa umechagua arifa zote.

Hutapata arifa iwapo mipangilio ya chaneli imewekwa kuwa inalenga watoto. Kengele ya arifa itawekewa mipangilio ya hamna arifa . Huwezi kubadilisha mipangilio hii.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5095363883981615290
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false