Kufuta ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Ikiwa uliwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kimakosa, unaweza kulifuta. Kufuta ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki:

  • Kutaondoa onyo la hakimiliki kwenye chaneli ya aliyepakia, isipokuwa iwapo maudhui mengine yanachangia kusababisha onyo hilo.
  • Kutarejesha maudhui ya aliyepakia kwenye YouTube, isipokuwa pale ambapo aliyepakia alifuta maudhui.

Ikiwa wewe ni mpakiaji ambaye maudhui yako yaliondolewa, unaweza kuomba dai lifutwe.

Ikiwa umewasilisha ombi la kuondoa video

Kuna njia 2 za kufuta ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki:

  • Futa ombi katika Studio ya YouTube
  • Futa kwa barua pepe
Futa ombi katika Studio ya YouTube

Ikiwa ombi la kuondoa limeshashughulikiwa na kusababisha kuondolewa kwa maudhui, unaweza kulifuta kwenye Studio ya YouTube.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube kwenye kompyuta.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Hakimiliki .
  3. Kwenye kichupo cha Maombi ya Kuondoa , pata video uliyoitumia ombi la kuondoa.
  4. Bofya "Panua" ili uonyeshe maelezo zaidi kuhusu video.
  5. Ikiwa video imeshaondolewa, bofya FUTA KUONDOLEWA. Ikiwa video inasubiri kuondolewa kutokana na ombi lililoratibiwa la kuondoa, bofya FUTA OMBI.
  6. Katika dirisha ibukizi, bofya FUTA.
Dokezo kwa washirika wa YouTube: Ikiwa una akaunti ya CVP au idhini ya kufikia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube, unaweza kufuta au kukatisha maombi ya kuondoa ukitumia mifumo hii. Hakikisha kuwa umeingia katika Akaunti ile ile ya Google iliyotumiwa kuwasilisha ombi halisi la kuondoa. Kumbuka kuwa video zinazolingana hazitadaiwa baada ya dai kufutwa.
Futa kwa barua pepe

Unaweza kufuta ombi la kuondoa kwa njia ya barua pepe ili mradi tu barua pepe inakidhi masharti haya:

  1. Ni lazima barua pepe itumwe kutoka kwa mlalamikaji halisi aliyedai mwanzo au mwakilishi aliyeidhinishwa (kama vile wakili) kwa niaba ya mlalamikaji.
  2. Ni sharti barua pepe itumwe kupitia anwani ile ile ya barua pepe au kikoa cha shirika kilichotumika kutuma ombi halisi la kuondoa.
  3. Ni lazima barua pepe ijumuishe taarifa zifuatazo:
    • Viungo vyenye muundo sahihi vinavyoelekeza kwenye maudhui ya ombi lako la kuondoa: Kwa video, muundo sahihi wa URL ni www.youtube.com/watch?v=xxxxxxxxxxx. Kwa maudhui yasiyo ya video, tumia muundo wa URL wa aina sahihi ya maudhui iliyoorodheshwa hapa.
    • Taarifa ya kufuta dai: Kwa mfano, "Ninaondoa dai langu la ukiukaji wa hakimiliki." Kumbuka kuwa tunaweza tu kukubali kufuta dai la ombi la kuondoa. Hatuwezi kukubali kufuta tu dai la onyo la hakimiliki kama vile "Ninafuta onyo langu la hakimiliki."
    • Sahihi ya kieleketroniki: Katika sehemu ya chini ya barua pepe, mlalamishi au mwakilishi aliyeidhinishwa, ni sharti aweke jina lake rasmi kamili kama sahihi yake. Jina rasmi kamili haliwezi kuwa jina la kampuni.
  4. Ni lazima barua pepe itumwe kwa copyright@youtube.com.
Kumbuka: Picha za wasifu za chaneli ya YouTube hupangishwa kwenye Google. Ili ufute ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa picha ya wasifu, jibu barua pepe ya kuthibitisha uliyopokea kutoka Google kuhusu ombi lako halisi la kuondoa. Hakikisha kuwa barua pepe yako inatimiza masharti 1 hadi 3 yaliyoorodheshwa hapo juu.
 
Kumbuka: Tunaweza tu kukubali ombi la kufuta madai lililowasilishwa kwenye Studio ya YouTube au kupitia barua pepe ambayo inatimiza masharti yote yaliyoelezwa hapo juu.

Ikiwa maudhui yako yaliondolewa

Ikiwa wewe ni mpakiaji ambaye maudhui yako yaliondolewa kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, unaweza kuwasiliana na mlalamishi moja kwa moja na uombe kufuta dai. Baadhi ya watayarishi huorodhesha njia ambazo unaweza kuwasiliana nao katika chaneli zao.

Kumbuka kuwa, kwa sheria, YouTube haiwezi kutafuta upatanisho katika mizozo ya umiliki wa hakimiliki.

 

Kitakachotokea baada ya kufuta dai

Baada ya kufuta ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, utapata arifa ya barua pepe ili kukufahamisha kuwa ombi lako la kuondoa limefutwa. Mpakiaji pia atapewa arifa kuhusu hali ya onyo la hakimiliki linalohusiana na maudhui yake yaliyoondolewa.

Maelezo zaidi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3464331730237872760
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false