​Sera inayohusu kujiua, kujijeruhi na matatizo ya ulaji

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.
Kumbuka: Tarehe 18 Aprili, 2023, tulisasisha sera yetu kuhusu matatizo ya Ulaji ili kuilinda vyema jumuiya dhidi ya maudhui nyeti yanayoweza kuwa ya hatari kwa baadhi ya hadhira. Tunaweza kuondoa maudhui ya kuigwa, kuwekea maudhui mipaka ya umri au kuonyesha kidirisha cha nyenzo za dharura kwenye video zinazohusu mada za matatizo ya ulaji au kujijeruhi. Sera ifuatayo imesasishwa ikiwa na mabadiliko haya. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mbinu yetu katika chapisho hili kwenye blogu.

Katika YouTube, tunachukulia kwa umakini afya na siha ya watayarishi na watazamaji wetu wote. Ufahamu na hamasa kuhusu afya ya akili ni muhimu na tunawahimiza watayarishi washiriki simulizi zao, kama vile kuchapisha maudhui yanayojadili hali zao za mfadhaiko, kujijeruhi, matatizo ya ulaji, au matatizo mengine ya afya ya akili.

Hata hivyo, haturuhusu kwenye YouTube maudhui yanayohimiza matukio ya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji, ambayo yananuia kugutusha au kukera au yanayoweza kusababisha hatari kubwa kwa watazamaji.

Hatua ya kuchukua ukipata maudhui haya

Iwapo unaamini kuwa mtu fulani yuko hatarini:

  • Wasiliana na huduma za dharura za karibu ili upate usaidizi
  • Ripoti video ili utufahamishe

Ukiona kuwa unaathiriwa vibaya na maudhui yoyote yanayohusiana na afya ya akili, kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji, fahamu kuwa unaweza kupata usaidizi na hauko peke yako. Katika sehemu inayofuata unaweza kupata orodha ya nyenzo na maelezo ya mawasiliano ya mashirika yanayoweza kutoa ushauri.

Ili upate maelekezo ya jumla ya jinsi ya kuzungumza na mtu ambaye una wasiwasi kumhusu, piga simu za usaidizi za eneo lako.

Hatua ya kuchukua iwapo unahitaji usaidizi

Iwapo una mfadhaiko, mawazo ya kujiua, kujijeruhi au tatizo la ulaji, fahamu kuwa unaweza kupata usaidizi na hauko peke yako. Watu wengi wanaweza kupitia matatizo haya wanapokumbwa na hisia za kusikitisha. Kuzungumza na mtoa huduma wa afya ya akili kunaweza kusaidia kubaini iwapo una ugonjwa wa akili unaohitaji kushughulikiwa. Kunaweza pia kukusaidia kutambua mikakati bora ya kukabiliana na hali na kupata ujuzi wa kudhibiti hisia mbaya.

Nyenzo za usaidizi wa kuzuia kujiua na kujijeruhi

Ifuatayo ni orodha ya mashirika yanayojitolea kuwasaidia wanaoathiriwa katika nchi na maeneo tofauti. Hawa ni washirika wanaotambuliwa wa huduma za dharura. Ushirika unatofautiana kulingana na nchi au eneo.

Tovuti za findahelpline.com na www.wikipedia.org/wiki/List_of_suicide_crisis_lines zinaweza kukusaidia upate mashirika katika maeneo ambayo hayajaorodheshwa hapa.

Australia

Lifeline Australia

Simu ya Usaidizi kwa Watoto

13 11 14

1800 55 1800

Ajentina Centro de Asistencia al Suicida - Buenos Aires

135 (desde Capital y Gran Buenos Aires) 

(011) 5275-1135 (desde todo el país)

Brazili Centro de Valorização da Vida 188
Ubelgiji

Centre de Prévention du Suicide /

Zelfmoordlijn 1813

0800 32 123

1813

Bulgaria Български Червен Кръст 02 492 30 30
Jamhuri ya Zechia Psychiatrická léčebna Bohnice - Centrum krizové intervence
+420 284 016 666
Denmaki Livslinien 70201201
Ufaransa S.O.S Amitié 09 72 39 40 50
Ufini Suomen Mielenterveysseura / Kansallinen kriisipuhelin 09-2525-0111
Ujerumani Telefonseelsorge 0800-1110111
Ugiriki ΚΛΙΜΑΚΑ 1018
801 801 99 99
Hong Kong 香港撒瑪利亞防止自殺會 2389 2222
Hangaria S.O.S. Telefonos Lelki Elsősegély Szolgálat 06 1 116-123 
India आसरा
AASRA
91-9820466726
Ayalandi Samaritans 116 123
Israeli ער"ן - עזרה ראשונה נפשית 1201
Italia Samaritans Onlus 800 86 00 22
Japani こころの健康相談統一ダイヤル 0570-064-556
Nyuzilandi Lifeline New Zealand 0800 543 354
Uholanzi Stichting 113Online 0900-0113
Singapoo Samaritans of Singapore 1800-221-4444
Uhispania

Telèfon de l'Esperança de Barcelona

Teléfono de la Esperanza

93 414 48 48

717 003 717

Korea Kusini 보건복지부 자살예방상담전화 1393
Taiwani 生命線協談專線 1995
Tailandi กรมสุขภาพจิต กระทรวงสาธารณสุข 1323
Uingereza Samaritans 116 123
Marekani

Suicide & Crisis Lifeline

988 /Gumzo

Ili usome vidokezo na utazame video zinazoweza kukusaidia ujihisi salama zaidi kwenye YouTube, tembelea Kituo cha Usalama cha Watayarishi.

Nyenzo za usaidizi wa kuzuia matatizo ya ulaji

Ifuatayo ni orodha ya mashirika yanayowasaidia watu walio na matatizo ya ulaji. Mashirika haya  yanashirikiana na watoa huduma za afya ya akili. Ushirika unatofautiana kulingana na nchi au eneo.

Marekani NEDA +1 800 931-2237
Uingereza BEAT Eating Disorders +44 0808 801 0677 Uingereza
    +44 0808 801 0432 Skotlandi
    +44 0808 801 0433 Wales
    +44 0808 801 0434 N. Ayalandi
India Vandrevala Foundation +91 9999 666 555

Mwongozo wa Jumuiya wa kuchapisha maudhui yanayohusiana na kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji

Watumiaji wa YouTube hawapaswi kuogopa kuzungumza wazi kwa njia zinazosaidia na zisizodhuru kuhusu mada za afya ya akili, matukio ya kujiua, kujijeruhi na matatizo ya ulaji.

Hata hivyo, kuna nyakati ambapo maudhui yanayobuniwa ni nyeti na yanaweza kuhatarisha baadhi ya watumiaji. Unapobuni maudhui yaliyo na mada zinazohusiana na matukio ya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji, zingatia athari mbaya ambazo maudhui yako yanaweza kusababisha kwa watumiaji wengine, hasa watoto na watumiaji ambao wanaweza kuathiriwa na maudhui haya.

Tafadhali fuata Mwongozo wa Jumuiya ulio hapa chini wakati unabuni maudhui yanayohusiana na matukio ya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji, ili uwalinde na uwasidie watazamaji wako na watumiaji wengine. Kutofuata Mwongozo huu wa Jumuiya kunaweza kusababisha kupokea onyo, kuondolewa kwa maudhui yako au vikwazo vingine ili kuwalinda watumiaji. Pata maelezo zaidi.

Sera hii ya Mwongozo wa Jumuiya inatumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vya YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zitatumika kwa viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa kutamka pamoja na njia zingine.

Usichapishe maudhui yafuatayo:

  • Maudhui yanayotangaza au kuhimiza matukio ya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji
  • Maagizo kuhusu jinsi ya kufa kwa kujiua, kushiriki katika vitendo vya kujijeruhi au matatizo ya ulaji (ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuyaficha)
  • Maudhui ambayo yanalenga watoto yanayohusiana na vitendo vya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji
  • Picha za kuogofya za matukio ya kujijeruhi
  • Video za maiti za waathiriwa waliojiua isipokuwa ziwe zimetiwa ukungu au kufunikwa ili zisionekane kabisa
  • Video zinazoonyesha matukio ya kusababisha kujiua au majaribio ya kujiua na video za kuokoa anayejiua bila muktadha wa kutosha
  • Maudhui yanayoonyesha kushiriki au maagizo ya mashindano ya kujiua na kujijeruhi (k.m. mashindano ya Blue Whale au Momo)
  • Barua au maandishi ya kujiua bila muktadha wa kutosha
  • Maudhui yanayoangazia uchokozi unaohusishwa na uzani katika muktadha wa matatizo ya ulaji

Katika hali fulani tunaweza kudhibiti, badala ya kuondoa maudhui yenye matukio ya matatizo ya ulaji, kujiua au kujijeruhi iwapo yanatimiza kigezo kimoja au vigezo zaidi kati ya vifuatavyo (kwa mfano, kwa kuweka mipaka ya umri, tahadhari au Kidirisha cha Nyenzo za Dharura kwenye video). Tafadhali kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika:

  • Maudhui ambayo ni ya elimu, hali halisi, kisayansi au kisanii
  • Maudhui ambayo ni ya maslahi ya umma
  • Maudhui ya kuogofya ambayo yametiwa ukungu wa kutosha
  • Maigizo au maudhui ya kuigiza, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu uhuishaji, michezo ya video, video za muziki na klipu kutoka kwenye filamu na vipindi
  • Mijadala ya kina kuhusu maeneo, mazingira hatari na mbinu za kujiua au kujijeruhi
  • Maelezo ya kuogofya kuhusu matukio ya kujijeruhi au kujiua
  • Maudhui ya jinsi ya kupata nafuu baada ya matatizo ya ulaji, yanayoweza kuwashawishi watazamaji walio hatarini

Desturi bora kwa watayarishi wanaochapisha maudhui kuhusu matukio ya kujiua, kujijeruhi au matatizo ya ulaji

Tunapendekeza utumie desturi hizi bora katika maudhui yanayohusiana na matukio ya kujiua au kujijeruhi ili uwalinde watazamaji wako kutokana na madhara na mfadhaiko:

  • Usionyeshe mtu aliyefariki kwa kujiua na uheshimu faragha yake pamoja na faragha ya familia yake. Pata maelezo zaidi.
  • Tumia maneno ambayo ni mazuri na ya kutia moyo, yanayolenga kuponya, kuzuia na hadithi za matumaini.
  • Jumuisha maelezo na nyenzo za kuzuia matukio ya kujiua na kujijeruhi na mikakati ya kukabiliana na hali hizo. Jaribu kuyajumuisha katika video na maelezo ya video.
  • Usitumie lugha ya kuchochea mihemko au video za madoido ya kidrama.
  • Toa muktadha, lakini usijadili jinsi mwathiriwa alivyofariki kwa kujiua. Usitaje mbinu au maeneo.
  • Tia ukungu maudhui yaliyo na picha za watu waliojiuwa. Unaweza kutia ukungu kwenye video yako kupitia Kihariri katika Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Tunapendekeza utumie desturi hizi bora katika maudhui yanayohusiana na matatizo ya ulaji ili uwalinde watazamaji wako dhidi ya madhara na mfadhaiko:

  • Zingatia zaidi athari ya tatizo badala ya maelezo kuhusu tabia ya tatizo la ulaji.
  • Fahamisha hadhira yako kwamba matatizo ya ulaji kwa kawaida yanaweza kusababisha madhara makubwa.
  • Jumuisha maelezo na nyenzo za kuzuia matatizo ya ulaji na mikakati ya kukabiliana na hali hiyo. Jaribu kuyajumuisha katika video na maelezo ya video.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Mwisho, tunaweza pia kudhibiti uwezo wako wa kufikia mtiririko mubashara iwapo utabainisha kuwa utatiririsha mubashara maudhui ambayo yatakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya mitiririko mubashara.

Tahadhari na nyenzo za usaidizi

YouTube inaweza kuonyesha vipengele au nyenzo kwa watumiaji wakati maudhui yana mada za kujiua au kujijeruhi. Kwa mfano:

  • Tahadhari kwenye video yako kabla ianze kucheza, kuashiria kuwa ina maudhui yanayohusiana na matukio ya kujiua na kujijeruhi
  • Kidirisha kilicho chini ya video kilicho na nyenzo muhimu kama vile namba za simu za mashirika ya kuzuia matukio ya kujiua

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11169528009440102722
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false