Sera za maudhui yenye vurugu au ya kuogofya

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu maudhui ya vurugu au yanayoangazia umwagaji wa damu, ambayo lengo lake ni kutisha au kuudhi watazamaji, pia hairuhusu maudhui yanayohimiza wengine kufanya vitendo vya vurugu.

Iwapo unaamini mtu yeyote yupo hatarini, unapaswa kuwasiliana na taasisi ya utekelezaji wa sheria iliyo karibu ili uripoti hali hiyo mara moja.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Ikiwa unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

Maudhui ya kuogofya au yenye vurugu:

  • Kuchochea watu wengine kufanya matendo ya unyanyasaji dhidi ya mtu au kundi fulani la watu.
  • Mapigano yanayohusisha watoto.
  • Hii inajumuisha video, sauti au picha zinazohusisha ajali za barabarani, majanga ya asili, matokeo ya vita, matokeo ya mashambulizi ya kigaidi, mapigano ya mitaani, mashambulizi ya kimwili, unyanyasaji, mateso, maiti, maandamano au ghasia, wizi, taratibu za matibabu au matukio mengine kama hayo ambayo nia yake ni kuogofya au kuudhi watazamaji.
  • Video au picha inayoonyesha ugiligili wa mwili, kama vile damu au matapishi ambayo nia yake ni kuogofya au kuudhi watazamaji.
  • Video ya maiti yenye majeraha makubwa, kama vile yenye viungo vilivyokatika.

Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wanyama:

  • Maudhui ambayo binadamu hulazimisha wanyama kupigana.
  • Maudhui ambayo binadamu humshambulia mnyama na kumsababishia mateso kinyume na taratibu za kawaida. Mifano ya taratibu za kawaida ni pamoja na uwindaji au utayarishaji wa chakula.
  • Maudhui ambayo binadamu humweka mnyama katika mazingira duni kinyume na desturi za kawaida. Mifano ya taratibu za kawaida ni pamoja na uwindaji au utayarishaji wa chakula.
  • Maudhui yanayochochea au kukuza vitendo vya utelekezaji, unyanyasaji au kudhuru wanyama.
  • Maudhui yanayoonyesha uokoaji wa mnyama uliopangwa na unaomweka mnyama katika hali hatarishi.
  • Maudhui ya kuogofya yanayojumuisha wanyama ambayo nia yake ni kuogofya au kuudhi watazamaji.

Maudhui yaliyoigizwa au yaliyobuniwa:

  • Video za maudhui yaliyoigizwa au yaliyobuniwa zilizopigwa marufuku na mwongozo huu ambapo mtazamaji hapewi muktadha wa kutosha ili kuelewa kuwa video hiyo ni ya kuigiza au imebuniwa.

Kumbuka haturuhusu aina zifuatazo za maudhui hata ikiwa ni ya muktadha wa elimu, makala ya hali halisi, sayansi au kisanii.

  • Mashambulizi ya kimwili ya unyanyasaji wa kingono (video, picha mnato au sauti).
  • Video iliyorekodiwa na mhalifu wakati wa tukio kubwa la vurugu au tukio hatari ambapo silaha, vurugu au watu waliojeruhiwa wanaonekana au wanasikika.

Tafadhali kumbuka kuwa hii si orodha kamili.

Kumbuka kuwa sera hii pia inatumika kwa video, maelezo ya video, vijipicha, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au kipengele kingine chochote cha YouTube. Tafadhali kumbuka sera hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa kutamka pamoja na njia zingine.

Maudhui yanayolenga kutoa elimu

Tunaweza kuruhusu aina za maudhui yenye vurugu au ya kuogofya yaliyobainishwa hapo juu katika baadhi ya matukio katika maudhui ya elimu, makala ya hali halisi, sayansi au kisanii. Hiki si kibali cha kupakia maudhui ambayo nia yake ni kuogofya au kuudhi au kuchochea watazamaji wengine kutenda vitendo vya vurugu na haturuhusu maudhui fulani kama vile video zinazoonyesha mashambulizi ya kimwili ya unyanyasaji wa kingono. Kwa maudhui ya elimu yaliyo na maudhui ya kuogofya au vurugu yaliyobainishwa hapo juu, muktadha huu unapaswa kubainishwa katika picha au sauti ya video yenyewe. Kuelezea muktadha katika kichwa au maelezo hakujitoshelezi.

Kwa maudhui ya elimu, makala ya hali halisi, sayansi au kisanii ambayo yana maudhui ya kuogofya au ya watu wazima, tunaweza kuzingatia ukadiriaji wa wataalamu wa sekta nyingine ili kuamua ikiwa maudhui hayo yabakizwe kwenye YouTube. Maudhui yanayofuata sera zetu lakini hayafai kutazamwa na hadhira zote yamewekewa mipaka ya umri. Maudhui yenye mipaka ya umri hayaonyeshwi kwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 au aliyeondoka kwenye akaunti.

Maudhui yenye mipaka ya umri

Tunaweza kuweka mipaka ya umri badala ya kuondoa maudhui ya kuogofya au vurugu iwapo maudhui hayo yana muktadha wa kutosha kuyaelewa. Kwa mfano, maudhui yanayoonyesha majeraha ya waathiriwa katika ajali ya barabarani yanaweza kuondolewa, lakini tunaweza kuweka mipaka ya umri katika maudhui hayo hayo iwapo yataonekana katika habari inayofafanua kuhusu hali au muktadha huo. Kwa matumizi ya elimu ya maudhui ya kuogofya au vurugu, muktadha huu ni lazima uonyeshwe katika picha au sauti ya video yenyewe. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa muktadha hapa.

Pia, tunazingatia maslahi ya umma katika uamuzi wa kuondoa au kuweka mipaka ya umri kwenye maudhui. Kwa mfano, tunaweza kuweka mipaka ya umri kwa maudhui ya kuogofya au vurugu yanayoonyesha maeneo ya vita.

Pia, tunaweza kuweka mipaka ya umri kwa maudhui ya vurugu yaliyobuniwa ikiwa yana matukio ya kuogofya, kama vile watu kukatwa vipande vipande, kukatwa vichwa au maiti zenye majeraha makubwa. Kwa ujumla, tunaruhusu maudhui ya vurugu yaliyoigizwa tunapofahamishwa na maudhui au metadata kuwa maudhui hayo ni ya kubuni au ikiwa yanatokana na maudhui husika kama vile maudhui yaliyohuishwa au michezo ya video.

Tunaweza kuzingatia sababu zifuatazo tunapoamua kuweka mipaka ya umri au kuondoa maudhui. Kumbuka kuwa hii si orodha kamili:

  • Iwapo video inaonyesha picha ya vurugu au umwagaji wa damu. Kwa mfano, video inayoangazia sehemu inayoogofya zaidi ya filamu au mchezo wa video.
  • Iwapo nia ya kichwa, maelezo, lebo au data nyingine ni ya kuwaogofya au kuudhi watazamaji.
  • Iwapo picha au sauti ya vurugu imetiwa ukungu, imefichwa au haionekani vizuri.
  • Kiwango cha muda ambao picha inayoonyesha vurugu au sauti imeonekana kwenye maudhui.
  • Iwapo kuna muktadha unaowafahamisha watazamaji kwamba picha ni ya kuigiza au ya kubuni. Kwa mfano, kupitia maelezo katika video, kichwa au maelezo mengineyo.
  • Iwapo vurugu ni sehemu ya desturi ya kidini au kitamaduni na aliyepakia anawapatia watazamaji muktadha.
  • Iwapo maudhui yanaonyesha mauaji ya mnyama kupitia desturi za kitamaduni au za kawaida za uwindaji, kidini au utayarishaji wa chakula.

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Kuwahimiza watu wengine kwenda mahali fulani kufanya vurugu, kufanya vurugu wakati fulani au kulenga kufanyia watu au vikundi fulani vurugu.
  • Mapigano halisi kati ya watoto kwenye uwanja wa michezo. Tunaweza kuruhusu maudhui ikiwa watoto wanacheza michezo ya kupigana na ikiwa hilo linaonekana wazi kwa watazamaji.
  • Mapigano au ghasia nje ya muktadha wa kitaalamu au matukio ya michezo yanayosimamiwa kitaalamu.

Mifano zaidi

Maudhui ya kuogofya au yenye vurugu
Aina zifuatazo za maudhui haziruhusiwi kwenye YouTube. Hii si orodha kamili.
  • Video za taratibu za kimatibabu ambazo maudhui yanaonyesha vidonda na hayatoi elimu au maelezo kwa watazamaji.
  • Video za uhalifu kama vile uhalifu wa kutumia silaha ambazo maudhui yake hayatoi elimu au maelezo kwa watazamaji.
  • Video za simu za mkononi, kamera kwenye dashibodi au kamera za uchunguzi zilizofichwa zinazoonyesha waliojeruhiwa au kufariki katika ajali ya barabarani zikiwa na kichwa kama vile "Ajali ya ajabu" au "Onyo: Damu nyingi yamwagika."
  • Video zinazoonyesha watu wakikatwa vichwa.
  • Mashambulizi ya upande mmoja yenye kichwa kama vile "Tazama mtu huyu akipigwa!"
Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wanyama
Unyanyasaji kwa wanyama ni maudhui yanayoonyesha vitendo vya kihasidi vya kuwadhuru wanyama kimwili au kiakili na kuwasababishia wanyama mateso. Tunaweza kuruhusu maudhui yanayoonyesha taratibu zinazokubalika kama vile uwindaji, kutega wanyama, kudhibiti wadudu, kutayarisha chakula, matibabu au uchinjaji wa wanyama unaoathiri mnyama au kundi la wanyama.

Ifuatayo ni mifano zaidi ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube:

  • Mapigano ya mbwa, mapigano ya jogoo au mapigano mengine ya kulazimisha ambapo wanadamu hulazimisha wanyama kushambuliana. Tunaruhusu maudhui yanayoonyesha wanyama wakipigana porini, kama vile kwenye filamu inayoelezea hali halisi.
  • Maudhui yanayoonyesha mnyama akiteseka, akiwa ametelekezwa au unyanyasaji ambayo nia yake ni kumtisha mtazamaji au kuchochea mateso na si ya muktadha wa elimu, makala ya hali halisi, kisanyansi au kisanii.
  • Maudhui yanayoonyesha mafahali waliopigana wakiwa na majeraha, kama vile fahali kuwa amechomwa na upanga mwilini.
  • Uwindaji kwa kutumia taratibu zisizo za kawaida, kama vile matumizi ya mabomu au sumu.
  • Uokoaji wa wanyama uliopangwa ambapo wanyama huumizwa makusudi au huwekwa katika mazingira hatarishi kwa ajili ya maonyesho ya kusisimua.

Orodha iliyobainishwa hapo juu si orodha kamili.

Kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu, usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14498572286669642336
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false