Sera dhidi ya Maudhui ya Ngono na Uchi

Note: On September 7, 2022, we updated our Nudity and sexual content policy to more consistently enforce our Community Guidelines. You can learn more about these changes on our forum. This policy has been updated with these changes.
Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu maudhui machafu yanayochapishwa kwa lengo la kuchochea ngono. Kuchapisha ponografia kunaweza kusababisha maudhui kuondolewa au chaneli kusimamishwa. Video zilizo na maudhui yanayohusu mapendeleo ya ngono zitaondolewa au kuwekewa mipaka ya umri. Katika hali nyingi, YouTube hairuhusu maudhui yanayohusu mapendeleo ya ngono yenye vurugu, yanayodhalilisha au ya kuogofya.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

YouTube hairuhusu maudhui dhahiri ya ngono yanayoangazia watoto na maudhui yanayowanyanyasa watoto kingono. Tunaripoti maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono kwenye Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa, ambacho hufanya kazi na mashirika ya utekelezaji wa sheria kote duniani.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Iwapo unachapisha maudhui

Maudhui machafu yanayokiuka sera hii yanaweza kusababisha kufungwa kwa chaneli. Sera hii inajumuisha maudhui katika ulimwengu halisi, yanayoigizwa, yanayoonyeshwa na yaliyohuishwa, ikijumuisha maonyesho ya ngono, michezo ya video na muziki.

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanaonyesha:

  • Sehemu za siri, matiti au makalio ambayo yamefunikwa kwa nguo au yasiyofunikwa kwa nguo kwa lengo la kuchochea ngono.
  • Ponografia, maonyesho ya vitendo vya ngono au mapendeleo ya ngono yasiyo ya kawaida kwa madhumuni ya kuchochea ngono.

Aina nyinginezo za maudhui yanayokiuka sera hii

  • Kupiga punyeto
  • Kupapasa sehemu nyeti, matiti au makalio
  • Kutumia vifaa vya ngono ili kuchochea ngono kwa watazamaji
  • Uchi au uchi kidogo kwa lengo la kuchochea ngono
  • Vitendo vya ngono bila ridhaa au kutangaza au kuhimiza vitendo vya ngono bila ridhaa, kama vile unyanyasaji wa kingono, kushiriki ngono na maharimu, kujamiiana na wanyama au hisia za kingono kwa wanyama
  • Mawasiliano ya kimapenzi bila ridhaa kama vile picha zinazoshirikiwa bila idhini au uchunguliaji wa watu walio uchi au wanaojamiiana
  • Matukio ya kuvuja kwa picha za uchi au mtu kubaki uchi bila kukusudia kutokana na ajali ambapo mavazi yake yanafunuliwa
  • Kuvuta karibu au kuangazia kwa muda mrefu au kuonyesha sana matiti, makalio au sehemu nyeti kwa madhumuni ya kuchochea ngono
  • Maudhui yenye mapendeleo ya kingono yenye vurugu, ya kuogofya au yanayodhalilisha yenye madhumuni ya kuchochea ngono
  • Kujumlisha maudhui yanayolenga kuchochea ngono
  • Maudhui yoyote ya ngono yanayohusisha watoto, angalia ukurasa wetu wa Usalama wa Watoto kwenye YouTube ili upate maelezo zaidi

Kumbuka: Orodha iliyo hapa juu si kamili.

Maudhui yenye mipaka ya umri

Huenda tukaweka mipaka ya umri ikiwa maudhui yanajumuisha uchi au maudhui mengine ya ngono lakini hayaonyeshi chochote kilichoelezwa hapo juu. Tunaweza kuzingatia vigezo vifuatavyo tunapoamua iwapo tutaweka mipaka ya umri au kuondoa maudhui.

  • Iwapo lengo la video ni kuonyesha matiti, makalio au sehemu nyeti zilizofunikwa kwa nguo au zisizofunikwa kwa nguo
  • Iwapo mhusika anaonyeshwa katika hali inayonuiwa kuamsha hisia za kingono kwa mtazamaji
  • Iwapo lugha inayotumika katika video hiyo ni ya kuogofya au ni lugha chafu
  • Iwapo vitendo vya mhusika katika video vinahimiza kuamsha hamu ya ngono, kama vile kwa kupapasa matiti au sehemu nyeti au kuonyesha mavazi ya ndani
  • Iwapo kwa ujumla, huenda mavazi yasikubalike katika miktadha ya umma, kama vile nguo za ndani za kike
  • Iwapo picha au sauti ya kingono imetiwa ukungu, imefichwa au haionekani vizuri
  • Iwapo picha au sauti ya kingono inaonyeshwa kwa muda mfupi au inaonyeshwa kwa muda mrefu kwenye maudhui
  • Iwapo maudhui yanawaalika wengine ili washiriki katika mashindano yanayohusisha vitendo vya ngono

Kumbuka: Orodha iliyo hapa juu si kamili.

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara, sauti na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Maudhui ya elimu

Tunaweza kuruhusu maudhui ya ngono wakati lengo kuu ni kutoa elimu, makala yanayoangazia hali halisi, sayansi au kazi ya kisanii na hayana nia ya kuchochea ngono. Kwa mfano, makala yanayoangazia hali halisi ya saratani ya matiti kwa kuonyesha matiti wazi yanafaa, lakini kuchapisha klipu zisizo na muktadha kutoka kwenye makala hayo kwa nia ya kuchochea ngono hairuhusiwi. Maonyesho ya uchi nje ya muktadha katika jamii asili, wakati wa taratibu za kimatibabu, wakati wa kujifungua mtoto, wakati wa utendaji wa kazi ya sanaa au wakati wa kunyonyesha mtoto huenda yasitimize masharti yetu ya hali zisizofuata kanuni kuhusiana na makala ya hali halisi. 

Hali hii inatumika pia katika maonyesho ya matukio ya ngono katika maudhui ya kisanaa kama vile filamu, simulizi za sauti, muziki au michezo ya video. Kwa mfano, tunaweza kuruhusu filamu inayoonyesha tukio la ngono iwapo imejumuisha maelezo kama vile jina la filamu, mwekelezi, waigizaji kwenye maudhui ya video na katika maelezo ya video. Kumbuka kuwa hatua ya kuweka muktadha katika maudhui, mada na maelezo itatusaidia pamoja na watazamaji wako kubaini lengo kuu la video.

Kwa maudhui ya elimu, makala ya hali halisi, sayansi au kisanii ambayo yana maudhui ya kuogofya au ya watu wazima, tunaweza kuzingatia ukadiriaji rasmi wa wataalamu wengine ili kuamua ikiwa maudhui hayo yaendelee kuwepo kwenye YouTube. Maudhui yanayofuata sera zetu lakini hayafai kutazamwa na hadhira zote yanawekewa mipaka ya umri. Maudhui yenye mipaka ya umri hayaonyeshwi kwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 au aliyeondoka kwenye akaunti.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Klipu zilizotolewa kwenye filamu, maonyesho au maudhui mengine yasiyo ya ponografia ili kuonyesha tu sehemu iliyo na maudhui ya ngono (ya ulimwengu halisi au ya kisanii)
  • Kupapasa sehemu nyeti, kubusu, kupiga punyeto hadharani, “kufunua mavazi”, kuchungulia watu walio uchi au wanaojamiiana, maonyesho ya unyatiaji au maudhui yoyote mengine yanayoonyesha mtu kwa njia ya kingono bila kibali chake
  • Maudhui yanayoonyesha vitendo, tabia za kingono au vifaa vya ngono vinavyonuiwa kuchochea ngono

Kumbuka: Hii iliyo hapa juu ni mifano tu. Iwapo unafikiri kuwa huenda maudhui yakakiuka sera hii, usiyachapishe.

Mifano zaidi

  • Orodha za kucheza zinazoweka pamoja maudhui yenye mada za uchi au ngono kwa madhumuni ya kuchochea ngono
  • Kucheza dansi za kuamsha hamu ya ngono ambapo sehemu nyeti, makalio au matiti ya anayecheza dansi huangaziwa zaidi au dansi inayojumuisha upapasaji wa sehemu nyeti
  • Maudhui yanayofanya vitendo vya ubakaji vionekane vya kingono kwa namna yoyote ile, au yanayoweka pamoja klipu za matukio ya kuigiza vitendo vya ubakaji
  • Maonyesho ya sauti au maandishi ya vitendo vya kingono kwa madhumuni ya kuchochea ngono
  • Maudhui yanayoonyesha ugiligili wa mwili, kama vile mkojo, kwa madhumuni ya kuchochea ngono
  • Maudhui yanayotumia vifaa au matukio ambayo ni ya kawaida, kama vile udungaji sindano au ulaji, kwa madhumuni ya kuchochea ngono
  • Maudhui ya mchezo wa video ambayo yamebuniwa au yameboreshwa ("yamerekebishwa") kwa lengo la kuchochea ngono au yanayoangazia mada za mawasiliano ya kimapenzi bila ridhaa 

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Iwapo maudhui yako yana ponografia, huenda tukasimamisha chaneli yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5436486527527786830
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false