Sera ya barua taka, tabia za udanganyifu na ulaghai

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.
Kidokezo: Hivi majuzi, tulisasisha Mwongozo wetu wa Jumuiya ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu sera zetu zinazohusiana na Maelezo ya kupotosha kwenye YouTube. Ili ukague sera hizi, soma makala yetu kuhusu Maelezo ya kupotosha na Maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi.

YouTube hairuhusu taka, ulaghai au tabia za udanganyifu zinazotumia vibaya Jumuiya ya YouTube. Pia, haturuhusu maudhui ambayo lengo lake kuu ni kuwahadaa wengine waondoke kwenye YouTube na kwenda kwenye tovuti nyingine.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Jinsi sera hizi zinavyohusiana na matumizi yako

Iwapo unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

  • Video Taka: Maudhui yanayochapishwa kupita kiasi, yanayorudiwarudiwa au yasiyokuwa na lengo mahususi na yanatekeleza lengo moja au zaidi kati ya yafuatayo:
    • Kuahidi watazamaji kuwa wataona kitu fulani lakini badala yake yanawaelekeza nje ya YouTube.
    • Kupata mibofyo au watazamaji kutoka YouTube kwa kuahidi kuwa watapata pesa haraka.
    • Kuelekeza hadhira kwenye tovuti zinazosambaza programu hatari, zinazojaribu kuiba taarifa binafsi au tovuti zingine hasidi.
  • Metadata au Vijipicha Vinavyopotosha: Kutumia jina, vijipicha au maelezo kuwahadaa watumiaji ili waamini kuwa maudhui ni kitu tofauti na jinsi yalivyo.
  • Ulaghai: Maudhui yanayotoa zawadi za kifedha, mipango ya “kutajirika haraka”, au mipango ya kuzalisha pesa kupitia mfumo wa piramidi (kutuma pesa bila bidhaa halisi katika mfumo wa piramidi).
  • Kichocheo Taka: Maudhui yanayouza vipimo vya ushirikishaji kama vile mara iliyotazamwa, alama za imenipendeza, maoni au kipimo kingine chochote kwenye YouTube. Aina hii ya taka inaweza pia kujumuisha maudhui ambayo madhumuni yake kuu ni kuongeza idadi ya wanaofuatilia, idadi ya wanaotazama au vipimo vingine. Kwa mfano, kujitolea kufuatilia chaneli ya mtayarishi mwingine ili tu naye afuatilie chaneli yako, inayojulikana pia kama maudhui ya "Kufuatiliana".
  • Maoni Taka: Maoni ambayo madhumuni yake kuu ni kukusanya taarifa binafsi kutoka kwa watazamaji, kuwaelekeza watu kwenye tovuti zilizo nje ya YouTube kwa njia potovu au kutekeleza tabia zozote kati ya zilizopigwa marufuku hapo juu.
  • Maoni yanayorudiwarudiwa: Kuchapisha maoni mengi mno yanayofanana, yasiyolenga hadhira yoyote au yanayorudiwarudiwa.
  • Maudhui ya wahusika wengine: Mitiririko mubashara inayojumuisha maudhui ya wahusika wengine ambayo hayajaidhinishwa na kurekebishwa baada ya kupokea maonyo kadhaa kuhusu uwezekano wa matumizi mabaya. Wamiliki wa chaneli wanapaswa kufuatilia kwa karibu mitiririko yao mubashara na kurekebisha matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza kwa wakati unaofaa.

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kwamba orodha hii haijakamilika. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zinatumika kwa viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa kutamka, pamoja na njia zingine.

Kumbuka: Unaruhusiwa kuwahimiza watazamaji wafuatilie chaneli, wabonyeze kitufe cha imenipendeza, washiriki au watoe maoni.

Video Taka

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.

  • Maudhui yanayowaahidi watazamaji kuwa yanahusu mada fulani lakini badala yake yanawaelekeza kutazama nje ya YouTube.
  • Kuchapisha maudhui yale yale kwa kurudiarudia kwenye chaneli moja au zaidi.
  • Kupakia kwa wingi sana maudhui uliyokusanya kutoka kwa watayarishi wengine.
  • Kuwahadaa watazamaji wasakinishe programu hatari, au kuwaelekeza kwenye tovuti zinazoweza kuathiri faragha yao.
  • Maudhui yaliyozalishwa kiotomatiki ambayo yanachapishwa na kompyuta bila kuzingatia ubora au hali ya utazamaji.
  • Kuahidi pesa, bidhaa, programu au manufaa ya michezo ya video bila malipo watazamaji wakisakinisha au wakipakua programu au wakitekeleza vitendo vingine.
  • Kuchapisha kwa wingi sana maudhui ya washirika katika akaunti maalum.
  • Kupakia kwa kurudiarudia maudhui usiyomiliki na ambayo si EDSA.

Vijipicha au metadata inayopotosha

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.
  • Kijipicha kinachoonyesha mtu mashuhuri asiyehusiana na maudhui kwa njia yoyote.
  • Kutumia jina, vijipicha au maelezo kuwahadaa watumiaji kuwa maudhui ni kitu tofauti na jinsi yalivyo. Kwa mfano, wakati kuna uwezekano mkubwa wa hatari kutokea.

Ulaghai

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.
  • Kutoa ahadi zilizotiwa chumvi, kama vile madai kuwa watazamaji watatajirika haraka au kuwa matibabu ya kimuujiza yanaweza kutibu magonjwa sugu kama vile saratani.
  • Kutangaza zawadi za pesa taslimu au mipango ya kuzalisha pesa kupitia mifumo ya piramidi.
  • Akaunti zinazoendeleza utoaji zawadi za pesa taslimu.
  • Video zinazoahidi "Utapata $50,000 kesho kupitia mpango huu!"

Kichocheo Taka

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.
  • Video ambapo madhumuni ni kuwahimiza watazamaji kufuatilia.
  • Video za "Kufuatiliana".
  • Video zinazouza alama za "imenipendeza".
  • Video inayodai kuwa mfuatiliaji wa 100,000 atapewa chaneli bila maudhui mengine yoyote.

Maoni Taka

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.
  • Maoni kuhusu tafiti au ofa zinazotangaza mipango ya kuzalisha pesa kupitia mifumo ya piramidi.
  • Kuchapisha viungo vinavyoelekeza vya "Lipa kwa Kila Mbofyo" katika maoni.
  • Maoni yanayodanganya kuwa yanatoa maudhui ya video kamili. Maudhui ya aina hii yanaweza kujumuisha:
    • Filamu
    • Vipindi vya Televisheni
    • Tamasha
  • Kuchapisha viungo vinavyoelekeza kwenye programu hatarishi au tovuti ya wizi wa data binafsi katika maoni: "Weh! Nimepata kibunda cha pesa kutoka hapa! - [tovuti ya wizi wa data ya xyz].com"
  • Maoni yenye viungo vinavyoelekeza kwenye maduka bandia.
  • "Hebu, angalia chaneli/video yangu hapa!” wakati chaneli/video haihusiani na video ambako ilichapishwa.
  • Kuchapisha maoni yale yale kwa kurudiarudia yakiwa na kiungo kinachoelekeza kwenye chaneli yako.

Maudhui ya wengine

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.
  • Kutumia simu yako kutiririsha kipindi cha televisheni.
  • Kutumia programu ya mhusika mwingine kutiririsha mubashara nyimbo kutoka kwenye albamu.

Kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tunaweza kusimamisha uchumaji wako wa mapato au kufunga chaneli au akaunti yako. Pata maelezo zaidi kuhusu sera za uchumaji wa mapato na usimamishaji wa chaneli au akaunti

Kwa baadhi ya ukiukaji, huenda tukaondoa maudhui na kuipa chaneli yako tahadhari au onyo. Tukifanya hivi, tutakutumia barua pepe ili kukufahamisha.

Unaweza kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa maudhui yako yatakiuka sera ile moja ndani ya kipindi cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na kituo chako kitapewa onyo. Ukiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa onyo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
12322851565884527203
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi