Sera dhidi ya matamshi ya chuki


 
Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.
Note: On June 5, 2019, we announced some changes to our hate speech policies. You can learn more about those changes here. The below policy has been updated with those changes.

YouTube hairuhusu matamshi ya chuki. Haturuhusu maudhui yanayohimiza vurugu au chuki dhidi ya vikundi au watu kulingana na sifa yoyote kati ya zifuatazo, zinazoonyesha hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa kwa mujibu wa sera za YouTube:

  • Umri
  • Tabaka
  • Ulemavu
  • Ukabila
  • Mwonekano na Utambulisho wa Kijinsia
  • Uraia
  • Mbari
  • Hali ya Uhamiaji
  • Dini
  • Jinsia
  • Mwelekeo wa Kingono
  • Waathiriwa wa tukio kuu la vurugu na wanafamilia wao
  • Hali ya kuwa Mwanajeshi Aliyestaafu

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Iwapo unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa lengo la maudhui hayo ni kufanya jambo moja au zaidi kati ya yafuatayo:

  • Kuhimiza vurugu dhidi ya vikundi au watu kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa. Haturuhusu vitisho kwenye YouTube na tunachukulia vitendo vya vurugu visivyo dhahiri kuwa vitisho halisi. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu sera zetu za vitisho na unyanyasaji.
  • Kuchochea chuki dhidi ya watu au vikundi kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa.

Aina nyinginezo za maudhui yanayokiuka sera hii

  • Kudhalilisha vikundi au watu kwa kuwadunisha, kuwalinganisha na wanyama, wadudu, wadudu waharibifu, ugonjwa au sifa nyinginezo zisizo za kibinadamu kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Kusifu au kutukuza vitendo vya vurugu dhidi ya vikundi au watu kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Matumizi ya matusi dhidi ya mbari, dini au matusi na kasumba nyinginezo zinazochochea au kuhimiza chuki kulingana na hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa. Hii inaweza kuwa katika hali ya matamshi, maandishi au picha zinazotangaza kasumba hizi au kuzichukulia kama za kweli.
  • Kudai kuwa vikundi au watu ni duni kimwili au kiakili, kuwa wana mapungufu au ni wagonjwa kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa. Hii ni pamoja na kauli kuwa kikundi kimoja ni duni kuliko kingine, kudai kuwa ni wajinga, wana uwezo mdogo au wana kasoro. Hii pia inajumuisha kutoa mwito wa kufanya vikundi au watu kuwa watumwa kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Kutangaza ubabe wenye chuki kwa kudai kikundi fulani kina hadhi ya juu kuliko kile cha watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa ili kutetea vurugu, ubaguzi au utengaji. Hii inajumuisha maudhui yaliyo na propaganda ya ubabe wenye chuki, kama vile uandikishaji wa wanachama wapya au kuomba misaada ya kifedha ili kuendeleza itikadi yao na video za muziki zinazotangaza ubabe wenye chuki katika mashairi, metadata au picha.
  • Madai ya ujanja kuwa vikundi au watu ni waovu, mafisadi au hasidi kulingana na hali yao ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Kupinga au kupuuza tukio kubwa la vurugu ambalo limerekodiwa kwenye vyanzo vya kuaminika au hali ya waathiriwa wa tukio hilo.
  • Mashambulizi dhidi ya vikundi au watu kutokana na kuvutiwa kwao na watu wengine kihisia, kimahaba na au kingono.

Maudhui ya elimu, hali halisi, sayansi na ya kisanii

Tunaweza kuruhusu maudhui yanayojumuisha matamshi ya chuki ikiwa maudhui hayo yamejumuisha muktadha wa ziada wa kielimu, kihalisia, kisayansi au kisanii. Muktadha wa ziada unaweza kujumuisha kukemea, kupinga, kujumuisha maoni kinzani au kukejeli matamshi ya chuki. Hiki si kibali cha kuhimiza matamshi ya chuki. Mifano ni kama:

  • Makala yanayoangazia hali halisi kuhusu kikundi cha chuki: Tunaweza kuruhusu maudhui ya kielimu ambayo hayaungi mkono kikundi hicho au hayahimizi itikadi hizo. Haturuhusu makala yanayoangazia hali halisi yanayohimiza vurugu au chuki.
  • Makala ya utafiti wa kisayansi kuhusu wanadamu: Makala kuhusu jinsi nadharia zilivyobadilika kadri muda ulivyopita, hata ikiwa inajumuisha nadharia kuhusu hali duni au ubabe wa vikundi mahususi, yanaweza kuruhusiwa kwa sababu yana lengo la kutoa elimu. Hatutaruhusu makala yanayodai kwamba kuna ushahidi wa kisanyansi unaodharau watu au unaoonyesha kuwa mtu au kikundi fulani ni duni.
  • Video ya kihistoria ya tukio, kama vile Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ambayo haihimizi vurugu au chuki. 

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko ya moja kwa moja na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL zinazobofyeka, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyinginezo kwa kutamka kupitia video pamoja na njia nyinginezo. 

Kwa maudhui yanayojumuisha matamshi ya chuki katika muktadha wa kielimu, uhalisia, sayansi au kisanii, ni lazima muktadha huu uonekane kwenye picha au sauti ya video husika. Kuelezea muktadha katika kichwa au maelezo hakutoshelezi.

Uchumaji wa mapato na adhabu nyinginezo 

Katika baadhi ya matukio ambayo ni nadra kutokea, tunaweza kuondoa maudhui au kutoa adhabu nyinginezo wakati mtayarishi:

  • Anahimiza tabia mbaya kwa hadhira mara kwa mara.
  • Analenga, kutukana na kufedhehesha kikundi fulani mara kwa mara kwenye maudhui mengi anayopakia kulingana na hali kuwa kipo katika kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Anafichua kikundi cha watu walio katika kikundi cha watu wanaolindwa ili kuwaweka katika hatari ya kupata madhara ya kimwili kulingana na muktadha wa kijamii au kisiasa wa eneo husika.
  • Anatayarisha maudhui yanayoathiri mfumo wa YouTube kwa kuendelea kuchochea uhasama dhidi ya kikundi cha watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa kwa nia ya kujinufaisha kifedha.

Mifano

Ifuatayo ni mifano ya matamshi ya chuki yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • "Nimefurahi kuwa [tukio hili la vurugu] limetokea. Wamepata kile walichostahili [akimaanisha watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa].”
  • “[Watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni mbwa” au “[watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni kama wanyama.”

Mifano zaidi

  • “Jitokeze na umpige ngumi [mtu mwenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa].”
  • “Kila mtu aliye katika [vikundi viliyo na watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni wahalifu au majambazi.”
  • “[Mtu mwenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni mtu mbaya kabisa.”
  • “[Watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni ugonjwa fulani.”
  • “[Watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni wajinga kutuliko kwa sababu wana akili ndogo.”
  • “[Kikundi kilicho na watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] kinatishia uwepo wetu, kwa hivyo tunapaswa kukiondoa kwa namna yoyote ile.”
  • “[Kikundi kilicho na watu wenye hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] kina ajenda ya kutawala dunia na kutuangamiza.”
  • “[Hali ya kuwa katika Kikundi cha watu wanaolindwa] ni aina tu ya ugonjwa wa akili inayohitaji kutibiwa.”
  • “[Mtu aliye katika hali ya kikundi cha watu wanaolindwa] hapaswi kusomeshwa shuleni kwa sababu hastahili kuelimishwa hata kidogo.”
  • "Wote wanaoitwa waathiriwa wa tukio hili la vurugu ni waigizaji tu. Hakuna mtu aliyeumia na hii ni ripoti ya uongo mtupu.”
  • "Ni kweli watu walifariki katika tukio, lakini si wengi kiasi hicho."
  • Kumpigia mtu kelele kwa kusema “[watu walio na hali ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa] ni wadudu waharibifu!” bila kujali ikiwa mtu huyo yupo katika kikundi cha watu wanaolindwa au la. 
  • Video game content which has been developed or modified (“modded”) to promote violence or hatred against a group with any of the attributes noted above.

Tafadhali kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Ikiwa tunaona kuwa maudhui yako yanakaribia kuwa matamshi ya chuki, tunaweza kudhibiti vipengele vya maudhui hayo katika YouTube. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vinavyodhibitiwa hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2888637415614401201
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false