Kudhibiti maelezo ya msingi ya Kituo chako cha YouTube

Unaweza kudhibiti maelezo ya msingi kuhusu chaneli yako ya YouTube kama vile jina, maelezo, tafsiri na viungo vya chaneli.

Jina

Unaweza kubadilisha jina la chaneli yako ya YouTube, hakikisha tu kuwa jina hilo linafuata Mwongozo wetu wa Jumuiya. Baada ya kubadilisha jina lako, inaweza kuchukua siku chache kabla ya jina jipya kubadilika na kuonekana kwenye YouTube. Ukibadilisha jina na picha kwenye chaneli yako ya YouTube, mabadiliko yataonekana tu kwenye YouTube. Unaweza kubadilisha jina na picha ya Akaunti yako ya Google hapa (bila kufanya mabadiliko yoyote kwenye jina la chaneli yako ya YouTube).

Kumbuka: Unaweza kubadilisha jina la chaneli yako mara mbili ndani ya siku 14. Kubadilisha jina lako kutaondoa beji yako ya uthibitishaji. Pata maelezo zaidi.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuweka mapendeleo kisha Maelezo ya msingi.
 3. Weka jina jipya la kituo chako.
 4. Bofya CHAPISHA.

Choosing Your YouTube Channel Name

 

 

Utambulisho

Utambulisho ni kitambulisho cha kipekee kinachokurahisishia kuanzisha na kudumisha utambulisho wako wa kipekee kwenye YouTube.

Kumbuka: Unaweza kubadilisha kitambulishi chako mara mbili ndani ya siku 14.

 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Kuweka mapendeleo kisha Maelezo ya msingi.
 3. Chini ya sehemu ya Kitambulishi, unaweza kuangalia au kubadilisha kitambulishi chako.
 4. Ukibadilisha kitambulishi chako, bofya CHAPISHA ili ukithibitishe.

Maelezo

Unaweza kubadilisha maelezo yako kwenye YouTube, hakikisha tu kuwa yanafuata Mwongozo wetu wa Jumuiya. Maelezo yako yanaweza kufikiwa katika kichwa cha chaneli.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuweka mapendeleo kisha Maelezo ya msingi.
 3. Weka maelezo mapya ya kituo chako.
 4. Bofya CHAPISHA.
Pata vidokezo kuhusu maelezo ya video kwa watayarishi.

Kuweka au kubadilisha viwakilishi vyako

Unaweza kuweka viwakilishi vyako kwenye chaneli yako ili viweze kuonyeshwa kwenye ukurasa wa chaneli yako. Unaweza kuchagua iwapo ungependa kuonyesha viwakilishi vyako kwa kila mtu au kuvionyesha tu kwa wanaofuatilia chaneli yako.
Viwakilishi ni sehemu muhimu ya vile mtu anavyojitambulisha na kujibainisha. Baadhi ya maeneo ya mamlaka yana sheria zinazohusu utambulisho wa kijinsia. Zingatia sheria za eneo ulipo unapotumia kipengele hiki cha umma cha kujijumuisha kwenye YouTube.
Ikiwa viwakilishi havipatikani kwenye ukurasa wa chaneli yako, tunajitahidi kupanua ufikiaji wa kipengele hiki kwenye nchi au maeneo na lugha zaidi.
Kumbuka: Kipengele cha viwakilishi  hakipatikani katika akaunti za Workspace au zinazodhibitiwa.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Katika menyu ya kushoto, chagua Kuweka mapendeleo  kisha Maelezo ya Msingi kisha WEKA VIWAKILISHI .
 3. Anza kuweka viwakilishi vyako na uchague vile vinavyokufaa. Unaweza kuweka hadi viwakilishi vinne.
  1. Unaweza kubadilisha vile ulivyochagua kwa kubofya  karibu na mojawapo ya viwakilishi vyako ili kukiondoa.
 4. Chagua anayeweza kuona viwakilishi vyako:
  1. Vionekane kwa kila mtu AU
  2. Vionekane tu kwa wanaofuatilia kituo changu
 5. Bofya CHAPISHA.

Tafsiri ya jina na maelezo ya kituo

Unaweza kuweka tafsiri za jina na maelezo ya kituo chako ili usaidie video zako kufikia hadhira ya kimataifa.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuweka mapendeleo kisha Maelezo ya msingi kisha WEKA LUGHA.
 3. Chagua Lugha halisi kisha uchague Lugha ya tafsiri.
 4. Weka tafsiri za jina na maelezo ya kituo chako.
 5. Bofya NIMEKAMILISHA.

URL ya kituo

URL ya kituo chako ndiyo URL ya kawaida ambayo vituo vya YouTube hutumia. Inatumia kitambulisho cha kipekee cha chaneli yako, ambacho ni namba na herufi zilizo mwishoni mwa URL.
Viungo vya wasifu wa kituo
Unaweza kuangazia hadi viungo 14 kwenye Kichupo cha ukurasa wa mwanzo cha chaneli yako, hakikisha tu kuwa viungo hivyo vinafuata sera ya viungo vya nje. Kiungo chako cha kwanza kitaonyeshwa moja kwa moja katika sehemu ya wasifu karibu na kitufe cha kufuatilia na viungo vyako vilivyobaki vitaonyeshwa hadhira yako inapobofya ili kuangalia viungo zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu kuruhusu hadhira yako ifikie viungo.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuweka Mapendeleo kisha Maelezo ya msingi.
 3. Katika sehemu ya Viungo, bofya Weka kiungo na uweke jina na URL ya tovuti yako.
 4. Bofya CHAPISHA.
Maelezo ya mawasiliano
Unaweza kuweka maelezo ya mawasiliano kwenye kituo chako ili uwafahamishe wengine jinsi ya kuwasiliana nawe kwa ajili ya maswali yanayohusu biashara.
 1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuweka Mapendeleo kisha Maelezo ya msingi.
 3. Chini ya maelezo ya mawasiliano, weka anwani yako ya barua pepe.
 4. Bofya CHAPISHA.

Kutazama jinsi ya kudhibiti maelezo ya msingi ya kituo chako

Tazama video ifuatayo kwenye chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube kuhusu jinsi ya kubadilisha jina, maelezo, tafsiri na viungo vya chaneli yako.

 

Customize Your Channel Branding & Layout: Add a Profile Picture, Banner, Trailer, Sections, & more!

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu