Kutazama na kushiriki kwenye mitiririko mubashara yenye mkao wa wima katika programu ya YouTube

Unapovinjari mitiririko mubashara au Video Fupi kwenye programu ya YouTube, unaweza kupata mitiririko mubashara iliyo katika muundo wa wima, ikimaanisha kuwa imerekodiwa kwa urefu zaidi kuliko upana. Iwapo utapata mtiririko mubashara wa aina hii, unaweza kuugusa ili uingie kwenye mipasho mubashara yenye mkao wa wima. Kwenye mipasho unaweza:

  • Kutazama mtiririko mubashara kwenye skrini nzima.
  • Kushiriki kwenye mtiririko mubashara, ikiwa ni pamoja na kupiga gumzo au kununua uanachama katika kituo. 
  • Kuendelea kutelezesha kidole ili upate mitiririko zaidi mubashara yenye mkao wa wima. 

Unaweza pia kuingia kwenye mipasho mubashara yenye mkao wa wima kwa kugusa Sitisha kwenye Video fupi, kisha uguse kitufe cha Mubashara.

Maonyesho ya kwanza na mitiririko mubashara iliyoratibiwa haitaonyeshwa kwenye mipasho mubashara yenye mkao wa wima.

Kumbuka: Mipasho mubashara yenye mkao wa wima inapatikana tu kwenye programu ya YouTube na kwa sasa haipatikani kwenye vishikwambi.

Kupiga gumzo kwenye mitiririko mubashara yenye mkao wa wima

Iwapo kipengele cha gumzo la moja kwa moja kimewashwa, unaweza kutumia kisanduku cha maandishi kilicho sehemu ya chini ya mtiririko mubashara kupiga gumzo na kutuma miitikio.

Ikiwa ungependa kuzima kipengele cha gumzo, gusa menyu  katika sehemu ya juu kulia ya video, kisha uzime Gumzo la Moja kwa Moja.

Kununua uanachama katika kituo

Ili ununue uanachama katika kituo:

  1. Gusa alama ya dola ndani ya gumzo la moja kwa moja.
  2. Gusa Uanachama.
  3. Gusa Jiunge.
Kumbuka: Kwa sasa, kipengele cha kununua uanachama katika kituo kwenye mipasho mubashara yenye mkao wima hakipatikani kwenye iPhone, kinapatikana kwenye simu za Android pekee.

Kununua Super Sticker au Super Chat

Ili ununue Super Sticker au Super Chat:

  1. Gusa alama ya dola  ndani ya gumzo la moja kwa moja.
  2. Chagua moja kati ya yafuatayo:
    1. Super Sticker and then pata kifurushi cha vibandiko unachopenda and then chagua kibandiko mahususi ili ununue.
    2. Super Chat and then ili uchague kiasi, buruta kitelezi au uandike thamani unayopenda and then weka ujumbe wa hiari.
  3. Gusa Nunua na Utume.

Kugundua chaguo zaidi

Gusa menyu  katika sehemu ya juu kulia ya video ili uone chaguo zaidi za kujishirikisha kwenye mtiririko mubashara, ikiwa ni pamoja na:

  • Kuweka alama ya imenipendeza au haijanipendeza
  • Kushiriki 
  • Kuwasha vichujio vya gumzo
  • Kutopendekeza kituo hiki
  • Kuripoti kituo hiki
  • Usaidizi na maoni

Unaweza pia kugusa Ununuzi  ili uvinjari na ununue bidhaa zinazongaziwa

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17185145024711735758
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false