Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Kipengele cha Muziki wa Watayarishi

Kipengele cha Muziki wa Watayarishi sasa kinapatikana kwa watayarishi wa Marekani walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Upanuzi kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube nje ya Marekani unashughulikiwa.
Yafuatayo ni baadhi ya maswali yanayoulizwa sana na watayarishi kuhusu kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi. Maswali Yanayoulizwa Sana yamewekwa kwenye aina 3:
 
 

Maswali ya Jumla Yanayoulizwa Sana

Muziki wa Watayarishi ni nini?
Muziki wa Watayarishi ni orodha kubwa inayokua ya muziki unaovuma unaoweza kutumika kuchuma mapato kwenye video bila kuhofia madai ya hakimiliki. Kipengele cha Muziki wa Watayarishi kinawapa watayarishi mbinu nyingi za kutumia muziki, kulingana na masharti ya matumizi yaliyowekwa na wenye hakimiliki za muziki. Kwa mfano:
  • Baadhi ya nyimbo zinaweza kupewa leseni, yaani watayarishi wanalipa ada ya mapema (au kwa baadhi ya nyimbo, hakuna ada) ili watumie muziki kwenye video zao na kuhifadhi mapato ya video. Pata maelezo zaidi.
  • Baadhi ya nyimbo zinaweza kushiriki mapato, yaani watayarishi hawalipi ada yoyote ya mapema na hugawana mapato ya video zao na wenye hakimiliki za muziki. Pata maelezo zaidi.
Ninawezaje kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi?

Kipengele cha Muziki wa Watayarishi kinapatikana kwenye Studio ya YouTube na hukuruhusu kuvinjari, kukagua na kupakua nyimbo za kutumia kwenye video zako za YouTube. ​​Kwa kila wimbo, unaweza kuona chaguo zifuatazo za matumizi:

  1. Kununua leseni: Lipa ada ya mapema ili utumie muziki na upate ugavi sawa wa mapato unaotakiwa kwenye maudhui yako bila muziki.
  2. Ugavi wa mapato: Shiriki mapato ya video na wenye hakimiliki za wimbo.
Chaguo za utumiaji hutofautiana kulingana na wimbo. Kumbuka kuwa unaweza kuona baadhi ya nyimbo ambazo hazipatikani kwa ajili ya kupewa leseni au ugavi wa mapato. Ukichagua kutumia mojawapo ya nyimbo hizo, huenda video yako ikapata dai la Content ID au ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
Kwa nini hakuna chaguo la kukagua upakuaji kwa baadhi ya nyimbo?

Kwa sasa tunaruhusu tu upakuaji wa nyimbo zilizopewa leseni kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi.

Kwa nyimbo zinazostahiki ugavi wa mapato, utahitaji kutafuta upakuaji wa wimbo nje ya kipengele cha Muziki wa Watayarishi.

Je, ninaweza kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi kwenye mitiririko yangu mubashara?
Kwa sasa, kipengele cha Muziki wa Watayarishi hakitoi leseni kwa maudhui mubashara.
Kwa nini bado sina idhini ya kufikia kipengele cha Muziki wa Watayarishi?
Tunasambaza kipengele hicho hatua kwa hatua kwa watayarishi wa Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) nchini Marekani na tunapanga kuzindua kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube nje ya Marekani hapo baadaye.
Sipo katika Mpango wa Washirika wa YouTube, je, ninaweza kupata idhini ya kufikia kipengele cha Muziki wa Watayarishi?
Tunazindua kipengele cha Muziki wa Watayarishi hatua kwa hatua kwa watumiaji zaidi kadiri muda unavyosonga na tunajitahidi kuwapa watayarishi wote vipengele vipya vinavyohusiana na muziki. Kwa sasa, watayarishi waliojiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube ndiyo tu wanaoweza kununua leseni.
Kipengele cha Maktaba ya Sauti kimehamishiwa wapi?
Ikiwa unaweza kufikia kipengele cha Muziki wa Watayarishi, tumeweka nyimbo zote za Maktaba ya Sauti ya YouTube ili uweze kupata mahitaji yako yote ya nyimbo katika sehemu moja. Kwa sasa, kichupo cha awali cha Madoido ya Sauti kinaweza kupatikana chini ya sehemu ya Aina. Nyimbo zilizohifadhiwa hapo awali katika Maktaba ya Sauti ya YouTube zinaweza kufikiwa kwa kubofya Rudi kwenye Maktaba ya Sauti chini ya ukurasa wa kwanza wa kipengele cha Muziki wa Watayarishi.
Siwezi kupata wimbo kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi. Je, hali hiyo ina maana gani?
Iwapo huwezi kupata wimbo unaotafuta kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi na ungependa kuutumia kwenye video yako, huenda ikamaanisha kwamba wimbo huo haupatikani kwa ajili ya ugavi wa mapato au utoaji leseni. Kwa hivyo, utakuwa katika hatari ya kupata Dai la Content ID au ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwenye video yako ukichagua kutumia wimbo ambao huna hakimiliki ya kuutumia.
Nimepata Dai la Content ID la wimbo tofauti na niliotumia. Ninaweza kufanya nini?
Iwapo unaamini ulipokea Dai la Content ID kimakosa, unaweza kupinga dai hilo.

Kwa nini video yangu imezuiwa nchini Urusi au Belarusi?

Baadhi ya wenye hakimiliki za muziki wanaweza kuamua kuzuia nyimbo zao kwenye maeneo fulani yakiwemo Urusi na Belarusi.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Leseni

Leseni ni nini?
Leseni inampa mtu ruhusa rasmi ya kutumia maudhui ambayo watu wengine wanamiliki haki zake. Kwa kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi, tumeboresha mchakato wa kuwasiliana na wenye hakimiliki hawa moja kwa moja kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu utoaji leseni kwenye Kituo chetu cha Usaidizi.
Ni wakati gani ninapaswa kulipia leseni?
Unaweza kulipia leseni moja kwa moja kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi au unapopakia video inayotumia wimbo wa kipengele cha Muziki wa Watayarishi. Pata maelezo zaidi kuhusu utoaji leseni wa nyimbo.
Nikinunua leseni, je, inamaanisha kuwa ninaumiliki muziki huo sasa?
Hapana, iwapo umenunua leseni, haimaanishi kuwa unaumiliki muziki. Inamaanisha unanunua ruhusa ya kutumia muziki. Hasa, unanunua leseni ya usawazishaji wa matumizi katika tukio moja (au “sawazisha”) inayokuruhusu kusawazisha video kwa kutumia muziki uliopewa leseni kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni.
Je, bei za leseni hupangwa vipi? Je, bei zinaweza kubadilika?

Washirika wa muziki wenye hakimiliki za nyimbo, huweka bei na masharti ya leseni. Kumbuka kuwa, baadhi ya nyimbo zimewekewa bei kwa watayarishi wote, ilhali nyingine zinaweza kuwa na bei maalum kulingana na ukubwa wa kituo chako.

Ukinunua leseni, haitaathiriwa na mabadiliko ya bei kwa kipindi cha matumizi cha leseni.

Je, hali hiyo itaathiri ununuzi niliofanya awali, ikiwa bei ya leseni itabadilika?
Mabadiliko yoyote ya bei ya leseni hayataathiri ununuzi na matumizi yako ya awali ya leseni.
Je, nini kitatokea ikiwa sitanunua leseni, lakini ninatumia wimbo kwenye video yangu?
Baadhi ya nyimbo zinazoweza kupewa leseni kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi zinapatikana kwa ajili ya ugavi wa mapato. Hii inamaanisha kuwa mapato ya video yatagawanywa kati yako na wenye hakimiliki ya wimbo.
Nyimbo zingine ambazo hazipatikani kwa ajili ya utoaji leseni au ugavi wa mapato zinaweza kusababisha Dai la Content ID au ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwenye video yako linalokuzuia kuchuma mapato kabisa.
Unaweza kuangalia maelezo ya matumizi kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi ili uone ni masharti yapi yanatumika kwenye wimbo husika.
Ikiwa nimenunua leseni, je, ninaweza kutumia wimbo uliopewa leseni kwenye video nyingi?
Kwa sasa tunaruhusu tu leseni zinazotumika mara moja. Hii inamaanisha kuwa ukinunua leseni ya wimbo, unaweza kutumia wimbo huo kwenye video moja tu. Ikiwa ungependa kutumia wimbo mmoja kwenye video nyingi, utahitajika kununua leseni kwa kila video.
Je, ninaweza kutumia nyimbo nyingi zilizopewa leseni kwenye video moja?
Ndiyo! Hakuna ukomo wa idadi ya leseni zinazoweza kuwekwa kwenye video. Kumbuka kwamba ni lazima upate haki zote zinazohitajika za maudhui yote kwenye video ili uweze kuchuma mapato.
Je, ninaweza kutumia nyimbo zilizopewa leseni kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi katika mifumo mingine kando ya YouTube?
Hapana, ukipata leseni ya wimbo kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi, unaweza kutumia wimbo husika kwenye video zilizopakiwa kwenye YouTube pekee. Pata maelezo zaidi kuhusu maelezo ya matumizi ya kipengele cha Muziki wa Watayarishi.
Je, nini kinatokea kwenye video leseni inapoisha muda wake?
Unaweza kusasisha leseni yako. Usiposasisha leseni, sheria na masharti ya matumizi ya muziki yatarejea kuwa masharti chaguomsingi ya ugavi wa mapato (ikiwa wimbo unatimiza masharti ya ugavi wa mapato).
Vinginevyo, video inaweza kuwa na vizuizi vya uchumaji mapato au uonekanaji kwa kuwa itakuwa hatarini kupata Dai la Content ID au ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki mara tu wimbo ulio katika video ukibainika kutokuwa na leseni au ugavi wa mapato.
Je, ninawezaje kuomba kurejeshewa pesa ya leseni niliyonunua?

Unaweza kuomba kurejeshewa pesa ya leseni ya kipengele cha Muziki wa Watayarishi moja kwa moja kwenye ukurasa wa Maktaba ya Muziki wa Watayarishi katika Studio ya YouTube. Ili uombe kurejeshewa pesa:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Muziki wa Watayarishi .
  3. Chagua kuchupo cha Maktaba Yako.
  4. Tafuta wimbo wenye leseni ambao ungependa kurejeshewa pesa.
    • (Si lazima) Ili kuangalia tu nyimbo zako zilizopewa leseni, bofya Zilizopewa leseni kwenye sehemu ya juu ya ukurasa.
  5. Kwenye safu mlalo ya wimbo, bofya "Vitendo zaidi" kisha Omba kurejeshewa pesa.
  6. Kamilisha fomu ya kuomba kurejeshewa pesa.

Baada ya kuwasilisha fomu yako ya ombi la kurejeshewa pesa, timu yetu ya usaidizi itakurejeshea pesa iwapo ombi hilo linatimiza masharti chini ya sera ya kipengele cha Muziki wa Watayarishi cha kurejesha pesa. Ili kukagua sera ya kurejesha pesa, nenda kwenye sehemu ya "Kughairi na Kurejesha Pesa" ya Sheria na Masharti ya kipengele cha Muziki wa Watayarishi.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Ugavi wa Mapato

Je, ni wakati gani ninastahiki kushiriki mapato?
  • Unapoona aikoni ya kushirki mapato kando ya wimbo
    • Unaweza kutumia nyimbo nyingi kwenye video ya urefu wowote.
  • Iwapo wimbo unastahiki kupewa leseni, lakini usingependa kununua leseni
    • Ni lazima Matumizi yako ya wimbo yawe chini ya sekunde 30 katika video yenye urefu wa zaidi ya dakika 3.
Mgawo wa mapato ni nini?

Kwa kutumia Muziki kwa Watayarishi, ikiwa video ndefu inatumia nyimbo zinazostahiki katika ugavi wa mapato, kiwango cha kawaida cha asilimia 55 ya ugavi wa mapato hurekebishwa ili kufidia gharama za kuidhinisha haki za muziki kama ilivyoonyeshwa kwenye mifano hapa chini. Hali hii hutegemea:

  • Idadi ya nyimbo zilizotumika: Idadi ya nyimbo zinazostahiki katika ugavi wa mapato ambazo mtayarishi hutumia kwenye video zake (angalia mifano hapa chini).
  • Gharama za haki za ziada za muziki: Makato ya kufidia gharama za haki za ziada za muziki, kama vile haki za utendaji. Makato haya yanaweza kuwa hadi asilimia 5 na yataonyesha gharama iliyochanganywa ya haki hizi za ziada za muziki katika nyimbo zilizo kwenye Muziki wa Watayarishi ambazo zinastahiki katika ugavi wa mapato.
Mifano ya ukokotoaji wa ugavi wa mapato

Mfano: Matumizi ya wimbo 1 unaoweza kutumika katika ugavi wa mapato

Mfano: Mtayarishi anatumia wimbo 1 unaoweza kutumika katika ugavi wa mapato kwenye video yake ndefu na anapata nusu ya kiwango cha kawaida cha asilimia 55 ya ugavi wa mapato (asilimia 27.5). Ikiwa kama mfano, makato ya gharama za haki za ziada za muziki yanaweza kuwa asilimia 2.5.

Kwenye video hii, mtayarishi angeweza kupata asilimia 25 ya mapato ya jumla (asilimia 27.5 - asilimia 2.5).

 
Mfano: Matumizi ya wimbo 1 unaoweza kutumika katika ugavi wa mapato
Mfano Ugavi wa mapato: asilimia 55 ÷ 2 Asilimia 27.5
Mfano Gharama za haki za ziada za muziki Asilimia - 2.5
Mfano Jumla ya mapato Asilimia 25

Mfano: Matumizi ya nyimbo 2 zinazoweza kutumika katika ugavi wa mapato na wimbo 1 uliopewa leseni

Mfano: Mtayarishi anatumia nyimbo 2 zinazoweza kutumika katika ugavi wa mapato na wimbo 1 uliopewa leseni kwenye video yake ndefu na anapata theluthi ya kiwango cha kawaida cha asilimia 55 ya ugavi wa mapato (asilimia 18.33). Ikiwa kama mfano, makato ya gharama za haki za ziada za muziki inaweza kuwa asilimia 2.

Kwa video hii, mtayarishi angeweza kupata asilimia 16.33 ya mapato ya jumla (asilimia 18.33 - asilimia 2).

 
Mfano: Matumizi ya nyimbo 2 zinazoweza kutumika katika ugavi wa mapato na wimbo 1 uliopewa leseni
Mfano Ugavi wa mapato: asilimia 55 ÷ 3 Asilimia 18.33
Mfano Gharama za haki za ziada za muziki - asilimia 2
Mfano Mapato ya jumla Asilimia 16.33
Kwa nini video yangu haina ugavi wa mapato?
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea video yako kushindwa kutimiza vigezo vya ugavi wa mapato:
  • Content ID imeshindwa kutambua wimbo unaotimiza masharti ya ugavi wa mapato kwenye video yako. Ikiwa wimbo utatambuliwa na Content ID baadaye kuwa unatimiza masharti ya ugavi wa mapato, video yako itawezeshwa kwa ugavi wa mapato wakati huo.
  • Wenye hakimiliki wanaweza kuwa wamezima ugavi wa mapato kwenye wimbo baada ya muda uliopakia video yako.
  • Leseni inapatikana kwa ununuzi, lakini matumizi yako ya wimbo si chini ya sekunde 30 katika video yenye urefu wa zaidi ya dakika 3.
  • Video yako ina Dai la Content ID kwa maudhui ya wengine ambayo hayastahiki ugavi wa mapato. Pata maelezo kuhusu chaguo zako za kushughulikia Dai la Content ID.
Je, video ambazo tayari nimezipakia zinatimiza masharti ya ugavi wa mapato?
Hapana, utoaji leseni au ugavi wa mapato utatumika tu kwa video zilizochapishwa baada ya kupata idhini ya kufikia kipengele cha Muziki wa Watayarishi. Haitatumika awali.
Je, ugavi wa mapato wa kipengele cha Muziki wa Watayarishi ni tofauti na ugavi wa mapato wa Video Fupi?
Ndiyo, unatofautiana. Ugavi wa mapato wa Video Fupi huwaruhusu watayarishi kupata asilimia ya ugavi wa mapato ya Video zao Fupi walizopakia. Ugavi wa mapato wa kipengele cha Muziki wa Watayarishi huwaruhusu watayarishi kushiriki mapato na wenye hakimiliki za muziki wanapotumia muziki unaostahiki katika video zao ndefu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3126863615701016412
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false