Sera za maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi

Tarehe 2 Juni 2023, tulisasisha jinsi sera hii inavyotumika kwa matokeo ya uchaguzi wa Marekani uliopita. Pata maelezo zaidi kwenye blogu yetu.

YouTube hairuhusu aina fulani za maudhui yanayopotosha au ya udanganyifu yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana. Hii ni pamoja na aina fulani za maelezo ya kupotosha ambayo yanaweza kusababisha madhara katika mazingira halisi, kama vile aina fulani za maudhui ambayo yamebadilishwa kwa kutumia teknolojia na maudhui yanayoathiri michakato ya demokrasia.

Sera ya Maelezo ya Kupotosha Kuhusu Chaguzi: Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube

Ikiwa utapata maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya yetu yanapatikana hapa. Ikiwa umepata maoni au video nyingi kutoka kwenye chaneli moja ambayo ungependa kuripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Maana ya sera hizi kwako

Ikiwa unachapisha maudhui

Sera hizi haziruhusu aina fulani za maudhui yanayohusiana na uchaguzi huru na haki na wa kidemokrasia. Usichapishe maudhui yanayohusiana na uchaguzi kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapo chini.

  • Mbinu ya kuzuia au kukatisha tamaa wapiga kura: Maudhui yanayolenga kupotosha wapiga kura kuhusu wakati, mahali, njia au masharti ya kustahiki kupiga kura au madai ya uongo ambayo yanaweza kukatisha tamaa zaidi watu kupiga kura.
  • Ustahiki wa mgombeaji: Maudhui yanayoendeleza madai ya uongo yanayohusiana na masharti ya kiufundi ya kustahiki kwa wagombeaji wa sasa wa siasa na wafanyakazi wa serikali wa sasa waliochaguliwa. Masharti ya kujiunga yanayozingatiwa yanalingana na sheria inayotumika ya kitaifa na yanajumuisha umri, uraia, au hali muhimu.
  • Uchochezi ili kukatiza michakato ya demokrasia: Maudhui yanayohimiza wengine kukatiza michakato ya demokrasia. Hii inajumuisha kuzuia au kuingilia utaratibu wa kupiga kura.
  • Uadilifu wa uchaguzi: Maudhui yanayoendeleza madai ya uongo kuwa makosa, hitilafu au ulaghai ulitokea kwenye maeneo mengi wakati wa chaguzi fulani zilizopita za kubainisha wakuu wa nchi. Au, maudhui yanayodai kuwa matokeo yaliyothibitishwa ya chaguzi hizo yalikuwa ya uongo. Sera hii kwa sasa inatumika kwenye:
    • Uchaguzi wa serikali ya Ujerumani 2021
    • Uchaguzi wa Urais wa Brazili wa 2014, 2018 na 2022

Kumbuka kuwa hii si orodha kamili.

Mifano

Aina zifuatazo za maudhui haziruhusiwi kwenye YouTube. Hii si orodha kamili.

Mbinu ya kuzuia au kukatisha tamaa wapiga kura
  • Kuwaambia watazamaji kuwa wanaweza kupiga kura kupitia njia zisizo sahihi kama vile kutuma kura yao kwa SMS kwenye nambari fulani.
  • Kutoa masharti bandia ya kustahiki kwa mpiga kura kama vile kusema kuwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ndio tu wanapaswa kushiriki kwenye uchaguzi fulani.
  • Kuwaambia watazamaji tarehe ya uchaguzi isiyo sahihi.
  • Kudai kuwa uanachama wa mpiga kura kwenye chama cha kisiasa unapatikana kwenye bahasha ya kupiga kura kwa barua.
  • Madai ya uongo kuwa wapiga kura wasio raia waliamua matokeo ya chaguzi zilizopita.
  • Madai ya uongo kuwa mashine za kupiga kura za Brazili zilidukuliwa hapo awali ili kubadilisha kura ya mtu.
Ustahiki wa mgombeaji
  • Madai kuwa mgombeaji au mfanyakazi wa serikali aliyechaguliwa hastahiki kuchaguliwa kutokana na maelezo ya uongo kuhusu umri unaohitajika ili kuchaguliwa katika nchi/eneo hilo.
  • Madai kuwa mgombeaji au mfanyakazi wa serikali hastahiki kuchaguliwa kutokana na maelezo ya uongo kuhusu masharti ya hali ya uraia ya kuchaguliwa katika nchi/eneo hilo.
  • Madai kuwa mgombeaji au mfanyakazi wa serikali aliyechaguliwa hastahiki kuchaguliwa kutokana na madai ya uongo kuwa aliaga dunia, ana umri mdogo au hatimizi masharti ya ustahiki.
Uchochezi ili kukatiza michakato ya demokrasia
  • Kuwaambia watazamaji wapange foleni ndefu za kupiga kura kwa lengo la kufanya iwe vigumu kwa wengine kupiga kura.
  • Kuwaambia watazamaji wadukue tovuti za serikali ili kuchelewesha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
  • Kuwaambia watazamaji wachochee vita halisi na maafisa wa uchaguzi, wapiga kura, wagombea au watu wengine katika maeneo ya kupigia kura ili kuzuia upigaji kura.
Uadilifu wa uchaguzi
  • Maudhui yanayoendeleza madai ya uongo kuwa ulaghai, hitilafu au makosa mengi yalibadilisha matokeo ya chaguzi za ubunge nchini Ujerumani (Bundestag), kupinga uhalali wa serikali mpya au kuchaguliwa na kuteuliwa kwa Waziri Mkuu wa Ujerumani anayefuata.
  • Madai ya uongo kuwa makosa, hitilafu au ulaghai uliotokea katika maeneo mengi ulibadilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa Brazili wa 2018.  

Maudhui ya kielimu, kihalisia, kisayansi au kisanii

Wakati mwingine, maudhui ambayo huenda yanakiuka sera hii yanaruhusiwa kusalia kwenye YouTube ikiwa yana muktadha wa Kielimu, Kihalisia, Kisayansi au Kisanii (EDSA) kwenye video, sauti, mada au maelezo. Hiki si kibali cha kutangaza maelezo ya kupotosha. Muktadha wa ziada unaweza kujumuisha maoni ya kukanusha madai ya uongo au ikiwa maudhui yanashutumu, kupinga au kudhihaki maelezo ya kupotosha yanayokiuka sera zetu. Pata maelezo kuhusu jinsi YouTube inavyotathmini maudhui yenye muktadha wa kielimu, kihalisia, kisayansi au kisanii (EDSA).

Sera zinazohusiana

Maudhui yanayohusiana na uchaguzi pia yanatathminiwa kutegemea sehemu nyingine za Mwongozo wa Jumuiya. Hii huenda ikajumuisha, kwa mfano:

  • Kwa mujibu wa Sera zetu dhidi ya unyanyasaji na uchokozi wa mtandaoni, haturuhusu maudhui yanayotishia watu binafsi kama vile wafanyakazi wa uchaguzi, wagombea au wapiga kura.
  • Kwa mujibu wa Sera zetu dhidi ya maelezo ya kupotosha, haturuhusu maudhui ambayo yamebadilishwa au yamechezewa kwa kutumia teknolojia kwa namna ambayo yanapotosha watumiaji - kwa kawaida kando na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha - na yanaweza kusababisha madhara mabaya sana. Kwa mfano, video iliyohaririwa kwa njia bandia ili kumfanya mgombea wa ofisi ya umma atoe madai ya uongo kuwa anajiondoa kwenye kinyang'anyiro.
  • Kwa mujibu wa Sera zetu dhidi ya maelezo ya kupotosha, haturuhusu maudhui yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana kwa kudai kwa njia ya uongo kuwa video kutoka tukio la zamani imetoka kwenye tukio la sasa. Kwa mfano, video inayoonyesha mkuu wa nchi akiunga mkono mzozo wa vurugu ambao kamwe hakuunga mkono.
  • Kwa mujibu wa Sera zetu dhidi ya maudhui yenye vurugu au ya kuogofya, haturuhusu maudhui yanayowahimiza wengine kutenda vitendo vya vurugu, ikiwa ni pamoja na vitendo vinavyowalenga wafanyakazi wa uchaguzi, wagombea au wapiga kura.
  • Kwa mujibu wa Sera yetu dhidi ya matamshi ya chuki, haturuhusu maudhui yanayohimiza vurugu au chuki dhidi ya watu au vikundi kwa misingi ya sifa fulani. Hii inajumuisha, kwa mfano, maudhui ambayo yanaonyesha mtu aliyehudhuria mkutano wa kisiasa akidhalilisha kikundi fulani kwa misingi ya sifa inayolindwa, kama vile mbari, dini au mwelekeo wa kingono.
  • Kwa mujibu wa Sera yetu dhidi ya uigaji, haturuhusu maudhui yanayolenga kuiga mtu au chaneli, kama vile mgombea wa kisiasa au chama chake cha kisiasa.
  • Maudhui ambayo yana viungo vya nje vinavyoelekeza kwenye nyenzo ambazo zinaweza kukiuka sera zetu na kusababisha hatari kubwa, kama vile maudhui ya kupotosha au ya udanganyifu yanayohusiana na uchaguzi, matamshi ya chuki yanayolenga vikundi vya watu wanaolindwa au unyanyasaji unaolenga wafanyakazi wa uchaguzi, wagombea au wapiga kura. Hii inaweza kujumuisha URL za kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyinginezo katika video kwa kutamka, pamoja na njia nyinginezo za kushiriki viungo.

Kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unafikiri kuwa yanaweza kukiuka sera hizi. Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji pia unatumika. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL zinazobofyeka, unazoweza kutumia kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine kwenye video kwa matamshi, pamoja na njia zingine.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8648570699980269544
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false