Sera za maelezo ya kupotosha

YouTube hairuhusu aina fulani za maudhui yanayopotosha au ya udanganyifu yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana. Hii ni pamoja na aina fulani za maelezo ya kupotosha ambayo yanaweza kusababisha madhara katika ulimwengu halisi, aina fulani za maudhui ambayo yamebadilishwa kwa kutumia teknolojia na maudhui yanayoathiri michakato ya kidemokrasia.

Ikiwa utapata maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya yetu yanapatikana hapa. Ikiwa umepata maoni au video nyingi ambazo ungependa kuripoti, unaweza kuripoti chaneli.

Maana ya sera hizi kwako

Ikiwa unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube iwapo yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

  • Kuwazuia watu kushiriki kwenye sensa: Maudhui yanayolenga kuwapotosha wanaoshiriki katika sensa kuhusu wakati, mahali, njia au masharti ya kujiunga kwenye sensa au madai ya uongo yanayoweza kufanya watu wasishiriki kwenye sensa.
  • Maudhui yaliyobadilishwa kwa hila: Maudhui ambayo yamebadilishwa au yamechezewa kwa kutumia teknolojia kwa namna ambayo yanapotosha watumiaji (kwa kawaida mbali na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) na yanaweza kusababisha madhara mabaya sana.
  • Maudhui yasiyo halisi: Maudhui yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana kwa kudai kwa njia ya uongo kwamba video ya zamani kutoka kwenye tukio la zamani imetoka kwenye tukio la sasa.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

Kuwazuia watu kushiriki kwenye sensa
  • Kutoa maelekezo yasiyo sahihi kuhusu jinsi ya kushiriki kwenye sensa.
  • Kukatisha watu tamaa ya kushiriki kwenye sensa kwa kutoa madai ya uongo kuwa hali ya uhamiaji ya mshiriki itaripotiwa kwa polisi.
Maudhui yaliyobadilishwa kwa hila
  • Kutafsiri manukuu ya video kwa njia isiyo sahihi ambayo inachochea mihemko ya siasa za kimaeneo na kusababisha madhara mabaya sana.
  • Video ambazo zimebadilishwa kwa njia bandia ( kwa kawaida mbali na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) ili kufanya ionekane kuwa mfanyakazi wa serikali ameaga dunia.
  • Maudhui ya video ambayo yamebadilishwa kwa njia bandia (kwa kawaida mbali na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) ili kubuni matukio ambayo yanasababisha madhara mabaya sana.
Maudhui yasiyo halisi
  • Maudhui yanayowasilishwa kwa njia isiyo sahihi kama yanayorekodi matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu katika eneo maalum ambayo kihalisia ni maudhui kutoka kwenye tukio au mahali pengine.  
  • Maudhui yanayoonyesha wanajeshi wakiwashambulia waandamanaji na madai yasiyo ya kweli kuwa maudhui hayo ni ya tukio la sasa, wakati kihalisia video hiyo ni ya miaka kadhaa iliyopita.

Kumbuka kuwa hii ni baadhi tu ya mifano na usichapishe maudhui ikiwa unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hizi. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zitatumika kwa viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL zinazobofywa, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa matamshi, pamoja na njia zingine.

Maudhui ya elimu, hali halisi, sayansi au sanaa

Tunaweza kuruhusu maudhui yanayokiuka sera za maelezo ya kupotosha zilizobainishwa kwenye ukurasa huu ikiwa maudhui hayo yanajumuisha muktadha wa ziada kwenye video, faili ya sauti, kichwa au maelezo. Hiki si kibali cha kutangaza maelezo ya kupotosha. Tunaweza kuruhusu maudhui ikiwa kusudi la maudhui hayo ni kushutumu, kupinga au kukejeli maelezo ya kupotosha yanayokiuka sera zetu.

Pia, tunaruhusu maoni ya kibinafsi kuhusu mada zilizo hapo juu ilimradi hayakiuki sera zozote ambazo zimebainishwa hapo juu.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yatakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yatakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kwamba kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukaondoa kiungo hicho.

Iwapo hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, huenda utatumiwa tahadhari bila kupewa adhabu kwenye kituo chako. Vinginevyo, tunaweza kukipa kituo chako onyo. Ukipata maonyo 3 ndani ya siku 90, kituo chako kitafungwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo hapa.

Tunaweza kusimamisha kituo chako au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kufunga kituo au akaunti yako baada ya kesi moja ya matumizi mabaya zaidi au wakati kituo kinakiuka sera mara kwa mara. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kusimamisha kituo au akaunti hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8037940009214428158
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false