Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Kuangalia hali ya madai yako

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Unapodai maudhui, unaashiria kwamba unamiliki haki za kipekee za kusambaza maudhui hayo mtandaoni katika nchi/maelezo ambapo sera zinazokuhusu zinatumika.

Katika kipengele cha Kidhibiti Maudhui cha Studio, madai huwekwa kwenye vikundi kulingana na video mahususi, zinazojulikana kama video unazodai, kwa hivyo unaweza kudhibiti madai yote kwenye video kwa wakati mmoja.

Ili uangalie hali ya madai yako:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Video unazodai .
  3. Ili uchuje orodha, bofya upau wa kuchuja kisha Hali ya dai.
  4. Teua kisanduku kilicho karibu na hali moja au zaidi ya madai: Yanayoendelea, Yanayoweza kutokea, Yanayopingwa, Yanayokatiwa rufaa, Yaliyosimamishwa, Yanayosubiri kushughulikiwa, Yanayopaswa kuondolewa, Yaliyocheleweshwa Kuondolewa na Ombi la kuondoa video linalokaguliwa.
  5. Bofya TUMIA
Kumbuka:
  • Vichujio vya ziada vitaonekana katika kila mojawapo ya dai utakalolichagua. Pata maelezo zaidi kuhusu vichujio hivi katika sehemu ya Maelezo zaidi kuhusu hali za madai hapo chini.
  • Zaidi ya hali moja ya dai inaweza kutumika katika video unayodai.
  • Madai yanayohitaji uchukue hatua yanaweza kujumuisha madai Yanayoweza kutokea, Yaliyopingwa na Yaliyokatiwa rufaa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kukagua na kuchukua hatua kuhusu masuala ya madai.

Maana ya hali za madai

Dai linaloendelea

Madai yanayoendelea ni madai yanayohusishwa na akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui ambayo yanaendelea kwa sasa.

Katika kichujio cha Dai linaloendelea, unaweza kuchagua kichujio cha ziada cha Ombi la kupinga dai lililorejeshwa. Utapata orodha ya madai yako yanayoendelea yaliyopingwa na mtumiaji, kisha wewe ukarejesha madai.

Dai linaloweza kutokea

Madai yanayoweza kutokea ni yale ambayo bado hayaendelei kwa sababu yanasubiri ufanye ukaguzi. 

Ikiwa unataka kuchuja kwenye madai yako yanayoweza kutokea, unaweza kuchagua kutoka vichujio hivi vya ziada:

  • Yanayopendekezwa kukaguliwa: Madai yanayohitaji uyafanyie ukaguzi mwenyewe kulingana na mipangilio yako ya Kidhibiti Maudhui cha Studio au sera ya zinazolingana. Pata maelezo zaidi kuhusu kupendekeza madai ili yafanyiwe ukaguzi na mtu mwenyewe.
  • Video zinazolingana ni fupi: Madai yanayopendekezwa kufanyiwa ukaguzi kwa sababu video zinazolingana ni fupi.
  • Video zilizopakiwa na mtumiaji mwingine wa Kidhibiti Maudhui: Madai yanayohitaji ukaguzi kwa sababu mtumiaji mwingine wa Kidhibiti Maudhui alipakia maudhui yanayolingana.
  • Yenye kiwango cha chini cha kuaminika: Madai yanayohitaji ukaguzi kwa sababu mfumo wa Content ID ulitambua maudhui hayo kuwa yenye kiwango cha chini cha kuaminika baada ya kulinganisha.
  • Yanayokiuka Sera ya uchumaji wa mapato kwenye YouTube: Madai yanayohitaji ukaguzi kutokana na uwezekano kwamba dai husika linakiuka sera ya uchumaji wa mapato kwenye YouTube.
  • Yaliyozuiwa awali: Madai ya uzuiaji yaliyotolewa kutokana na kiwango cha chini cha kuaminika kwa video baada ya video kupakiwa kwenye YouTube. Hii inaweza kusababishwa na hali ya kuchelewa kuwasilisha marejeleo au kuboreshwa kwa mfumo wa Content ID.
Dai lililopingwa

Madai yaliyopingwa ni madai ambayo aliyepakia video unayodai ameyapinga. YouTube haitatekeleza dai lililopingwa hadi ulikague.

Unaweza kuchuja madai yako yaliyopingwa kulingana na sababu alizotoa aliyepakia video yeye mzozo, ambazo alichagua wakati wa kuwasilisha maombi yake ya kupinga dai:

  • Nyenzo yenye hakimiliki imetambuliwa visivyo: Maombi ya kupinga dai yaliyotolewa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui yanayodaiwa kwenye video yake yalitambuliwa kimakosa.
  • Matumizi ya haki: Maombi ya kupinga dai yaliyotolewa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa amebadilisha maudhui yanayodaiwa kwenye video yake kwa kiasi kikubwa au anadai kuwa video yake imelindwa na kanuni za matumizi ya haki, matumizi yasiyo ya biashara au hali sawa na hizo zisizofuata kanuni za hakimiliki.
  • Kuidhinishwa: Maombi ya kupinga dai yaliyotolewa kwa sababu aliyepakia anadai kuwa ana idhini au leseni ya kutumia maudhui yanayodaiwa kwenye video yake.
  • Maudhui halisi: Maombi ya kupinga dai yaliyotolewa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui hayo ni yake halisi na ana haki zote za kuyamiliki.
  • Wazi Kutumiwa na Umma Maombi ya kupinga dai yaliyotolewa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui yanayodaiwa kwenye video yake yako wazi kutumiwa na umma na kamwe hayajalindwa na hakimiliki.
Dai linalokatiwa rufaa

Madai yanayokatiwa rufaa ni madai ambayo aliyepakia video unayodai anakata rufaa baada ya wewe kurejesha dai alilolipinga.

Unaweza kuchuja madai yako yanayokatiwa rufaa kulingana na sababu alizotoa aliyepakia video inayokatiwa rufaa, ambazo alichagua wakati wa kukata rufaa yake:

  • Nyenzo zenye hakimiliki zimetambuliwa visivyo: Rufaa zilizokatwa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui yanayodaiwa kwenye video yake yalitambuliwa kimakosa.
  • Matumizi ya haki: Rufaa zilizokatwa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa amebadilisha maudhui yanayodaiwa kwenye video yake kwa kiasi kikubwa au anadai kuwa video yake imelindwa na kanuni za matumizi ya haki, matumizi yasiyo ya biashara au hali sawa na hizo zisizofuata kanuni za hakimiliki.
  • Kuidhinishwa: Rufaa zilizokatwa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa ana idhini au leseni ya kutumia maudhui yanayodaiwa kwenye video yake.
  • Maudhui halisi: Rufaa zinazokatwa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui hayo ni maudhui yake halisi na ana haki zote za kuyamiliki.
  • Wazi Kutumiwa na Umma Rufaa zilizokatwa kwa sababu aliyepakia video anadai kuwa maudhui yanayodaiwa kwenye video yake yako wazi kutumiwa na umma na kamwe hayajalindwa na hakimiliki.
Dai lililokoma

Madai yaliyokoma ni madai ambayo hayaendelei tena.

Ikiwa unataka kuchuja kwenye madai yaliyokoma, unaweza kuchagua kutoka vichujio hivi vya ziada:

  • Muda wa ukaguzi ulikwisha: Madai yaliyokuwa na uwezo wa kutokea ambayo hayakukaguliwa ndani ya siku 30. Unaweza kudai tena madai yaliyokoma ambayo yana uwezo wa kutokea ili uyaendeleze tena.
  • Video zilizoondolewa na aliyezipakia: Madai yaliyokoma kwa sababu mtumiaji alifuta video. Ni video zilizofutwa hivi karibuni pekee ndizo zinazoonyeshwa, si video zote zilizofutwa zamani.
  • Yenye ilani ya kukanusha kutoka kwa mtumiaji: Madai yaliyoondolewa baada ya mtumiaji kuwasilisha arifa ya kukanusha. Pata maelezo zaidi kuhusu arifa za kukanusha.
  • Ombi la kuhamisha kipengee: Madai yaliyoondolewa kutokana na uhamishaji wa umiliki wa kipengee. Pata maelezo zaidi kuhusu uhamishaji wa umiliki wa vipengee.
  • Chaneli ipo kwenye orodha ya chaneli zinazoruhusiwa: Madai yaliyoondolewa baada ya chaneli iliyopakia video unayodai kuwekwa kwenye orodha yako ya chaneli zinazoruhusiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu chaneli zisizojumuishwa kwenye madai ya Content ID.
  • Utatuzi wa mzozo: Madai uliyoondoa mwenyewe baada ya mtumiaji kuyapinga au yaliyoondolewa kiotomatiki baada ya muda wa dai lililopingwa kuisha.
  • Video imerekebishwa: Madai yanayoondolewa baada ya mtumiaji kubadilisha maudhui yaliyo na hakimiliki. Pata maelezo zaidi kuhusu kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video.
  • Yaliyofungwa na mshirika: Madai ambayo hayakuwa sehemu ya mchakato wa kupiga dai na yaliondolewa na mtumiaji wa Kidhibiti chako cha Maudhui. Madai yanaweza kuondolewa wakati wowote. Pata maelezo zaidi kuhusu kuondoa madai.
  • Marejeleo yaliondolewa au hayakujumuishwa: Madai yaliyoondolewa kutokana na hatua ya mshirika mwenyewe kutojumuisha marejeleo, marejeleo kuzimwa au sehemu ya marejeleo kuwekwa alama kuwa inatiliwa shaka.
  • Ambayo nafasi yao ilichukuliwa dai lingine: Madai yaliyoondolewa wakati maudhui yanayolingana zaidi yalipatikana na dai jipya likaanzishwa ambalo lilichukua nafasi ya dai la kwanza.
  • Umiliki uliondolewa kwenye kipengee: Madai yaliyoondolewa baada ya umiliki kuondolewa kwenye kipengee. Pata maelezo zaidi kuhusu kusasisha umiliki wa kipengee.
  • Yaliyofungwa (hakuna AdSense au AdSense katika YouTube): Madai yaliyoondolewa baada ya AdSense au akaunti ya AdSense katika YouTube, kama yanavyotumika, yalifungwa.
  • Yaliyofungwa (hakuna uchumaji wa mapato): Madai yaliyoondolewa baada ya mchakato wa uchumaji wa mapato kuzimwa.
  • Yaliyofungwa (video inayolingana ni ya mmiliki): Madai yaliyoondolewa kwa sababu mmiliki wa chaneli ni mmiliki wa video inayolingana iliyodaiwa.
Dai linalosubiri hatua ichukuliwe

Madai yanayosubiri hatua ichukuliwe ni madai ambayo yanategemea mhusika mwingine anayekagua dai lililopingwa au linaloweza kutokea. Huwezi kuchukua hatua kuhusu madai haya hadi mhusika huyo mwingine akague madai yake. Madai yanayosubiri hatua ichukuliwe yanaweza kutokana na:

  • Vipengee vilivyopachikwa
    • Wachapishaji wa Muziki wanaweza kupachika kipengee cha utungo wao kwenye Rekodi ya Sauti na huenda kukawa na dai linaloweza kutokea kutokana na Rekodi hii ya Sauti.
    • Wachapishaji wanaweza kuangalia dai hili lenye kidokezo cha “Linasubiri hatua ichukuliwe (wamiliki wengine)” lakini hawawezi kuchukua hatua yoyote.
  • Wamiliki wengi wa kipengee na sera za kupeleka kufanyiwa ukaguzi
    • Ikiwa dai linasubiri likaguliwe na wamiliki wengine, hatua ya mshirika yeyote kulikubali itafanya dai hilo liwe linaloendelea kwa wahusika wote.
    • Ikiwa mshirika mmoja ataondoa dai linalosubiri hatua ichukuliwe, basi washirika wengine wote watahitaji kuthibitisha hilo ili liweze kuondolewa.
  • Marejeleo yasiyo sahihi yanayosubiri ukaguzi
    • Marejeleo yasiyo sahihi yanaweza kukaguliwa kwenye ukurasa wa Matatizo :
      • Kwenye upau wa kuchuja , bofya Hali kishaLinalosubiri.
      • Chagua chuja  kisha Aina ya Tatizo kisha Marejeleo Yasiyo Sahihi.
Dai la kuondoa
Madai ya kuondoa ni madai kwenye video ambazo zimeondolewa kwa sababu ya ombi la kuondoa video. Pata maelezo zaidi kuhusu maombi ya kuondoa video.
Kuchelewesha kuondoa
Kuchelewa kuondoa kunarejelea madai kwenye video ambazo zimeratibiwa kuondolewa kutokana na ombi la kuondoa video. Wenye hakimiliki wanaweza kutuma ombi la kuchelewesha kuondoa video linalompatia aliyepakia video muda wa siku 7 ambazo zikiisha, video hiyo itaondolewa. Pata maelezo zaidi kuhusu maombi ya kuchelewesha kuondoa video.
Ombi la kuondoa video linakaguliwa
Ombi la kuondoa video linalokaguliwa inarejelea madai kwenye video ambazo ni sehemu ya ombi la kuondoa video ambalo timu ya YouTube inakagua kwa sasa. Pata maelezo zaidi kuhusu maombi ya kuondoa video.

 

Keep in mind:

When a channel linked to your Content Manager uploads a video that gets a copyright claim:

  • Any 1st party claims (“uploader claims”) stay active unless manually closed by the uploader or closed due to video deletion.
  • Match policies associated with the claim aren't applied until the third-party Content ID claim is resolved (except for any geo-fencing block policies the uploader set before the third-party claim).

When you claim a video uploaded by another channel:

  • Any 1st party claims (“uploader claims”) stay active unless manually closed by the uploader or closed due to video deletion. However, only certain videos will be monetized on the uploader’s side, such as videos eligible for the cover revenue sharing.

Note: To view the monetization status of a video, check the Videos page.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11271853714603497870
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false