Masharti ya kodi ya Marekani kwenye mapato ya YouTube

Muhimu: Tunapoelekea mwisho wa mwaka, watayarishi wanaochuma mapato wanapaswa kuangalia taarifa zao za kodi kwenye AdSense katika YouTube. Hakikisha kuwa umewasilisha fomu ya kodi na ikiwa unastahiki, dai manufaa ya mkataba wa kodi kufikia tarehe 10 Desemba, 2023. Panapofaa, Google itakokotoa upya kodi za mwaka 2023 na kurejesha salio.

Usiposhiriki taarifa za kodi, huenda Google ikahitajika kuzuia kodi kutokana na mapato unayochuma ulimwenguni kote kwa kutumia kiwango cha juu zaidi cha kodi ya zuio. Ukishiriki taarifa zako za kodi, kiwango cha kodi utakacholipa kinaweza kuwa hadi asilimia 30 ya mapato yako nchini Marekani.

Kuangalia taarifa zako za kodi na kudai manufaa ya mkataba wa kodi:

  • Hakikisha kuwa tumepata taarifa zako za kodi. Hakikisha kuwa hali ya fomu yako ya kodi ni kijani kumaanisha kuwa “Imeidhinishwa” kwenye AdSense katika YouTube.
  • Wasiliana na mshauri wako wa kodi ili uthibitishe kuwa unastahiki kudai manufaa ya mkataba wa kodi. Manufaa ya mkataba wa kodi yanaweza kupunguza kiwango cha kodi ya zuio katika aina fulani za mapato:
    • Mirabaha Mingine ya Hakimiliki (kama vile Mpango wa Washirika wa YouTube na Google Play)
    • Huduma (kama vile Google AdSense)

Pata maelezo zaidi kuhusu kuzuia kodi kwenye YouTube au usome Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kutuma taarifa zako za kodi ya Marekani kwenda Google.

Google inatakiwa kukusanya taarifa za kodi kutoka kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Iwapo makato yoyote ya kodi yanatumika, Google itazuia kodi kwenye mapato ya YouTube yanayotokana na watazamaji nchini Marekani walioshiriki katika utazamaji wa tangazo, YouTube Premium, Super Chat, Super Stickers na Uanachama katika Chaneli.

Sababu ya Google kuzuia kodi za Marekani

Mtayarishi aliye kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube anapochuma mapato ya mirabaha kutoka kwa watazamaji nchini Marekani, Google inawajibu wa kukusanya taarifa za kodi, kuzuia kodi na kuripoti kwa Internal Revenue Service (mamlaka ya kodi nchini Marekani, ambayo pia inafahamika kama Mamlaka ya Mapato Marekani) kwa mujibu wa Sura ya 3 ya Kanuni ya Mapato ya Ndani ya Marekani.

Kumbuka: YouTube na Google haziwezi kukupa ushauri kuhusu masuala ya kodi. Wasiliana na mtaalamu wa kodi ili uelewe vyema hali yako ya kodi.

Kuwasilisha taarifa za kodi kwenda Google 

Watayarishi wote wanaochuma mapato kwenye YouTube, bila kujali mahali walipo duniani, wanahitajika kutoa taarifa za kodi. Tafadhali wasilisha taarifa za kodi haraka uwezavyo. Usipowasilisha taarifa za kodi, Google inaweza kuhitajika kukata hadi asilimia 24 ya jumla ya mapato uliyochuma ulimwenguni kote.

Unaweza kufuata maagizo yaliyo hapa chini ili uwasilishe taarifa zako za kodi ya Marekani kwa Google. Kumbuka kuwa unaweza kuombwa uwasilishe upya taarifa za kodi kila baada ya miaka mitatu na unaweza tu kutumia herufi za Kilatini unapowasilisha fomu za kodi (kutokana na masharti ya Mamlaka ya Mapato Marekani); pata maelezo zaidi hapa

  1. Sign in to your AdSense account.
  2. Click Payments kisha Payments info.
  3. Click Manage settings.
  4. Scroll to "Payments profile" and click edit Edit next to "United States tax info".
  5. Click Manage tax info.
  6. On this page you'll find a guide that will help you to select the appropriate form for your tax situation.
    Tip: After you submit your tax information, follow the instructions above to check the “United States tax info” section of your Payments profile to find the tax withholding rates that may apply to your payments.

    You’ll also be able to make any edits in case your individual or business circumstances change. If you've changed your address, make sure your updated permanent address is the same in both sections: "Permanent residence address" and "Legal address". This will ensure that your year-end tax forms (e.g., 1099-MISC, 1099-K, 1042-S) are delivered to the correct location. If you’re in the US, you must resubmit your W-9 form with your updated legal address

Ili kukusaidia ujiandae kutuma taarifa zako za kodi kwenye AdSense katika YouTube, nenda kwenye Kutuma taarifa za kodi ya Marekani kwa Google. Ili upate mwongozo mahususi wa Mitandao ya Chaneli Mbalimbali (MCN), nenda kwenye Masharti ya kodi ya Mitandao ya Chaneli Mbalimbali na chaneli za washirika

Masharti ya kodi ya Marekani yanakotumika

Kila mtayarishi aliye kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube anahitajika kuwasilisha taarifa za kodi ya Marekani kwa Google, bila kujali mahali alipo. Kwa mujibu wa sheria ya kodi nchini Marekani, Google inatakiwa kukata kodi kwenye mapato yako ya YouTube yanayotokana na watazamaji walio nchini Marekani, ikiwa wapo. Masharti ya kuzuia kodi yanaweza kutofautiana kulingana na nchi unakoishi, iwapo unatimiza masharti ya kudai manufaa ya mkataba wa kodi na iwapo unajitambulisha kama Mtu binafsi au Biashara.

  • Watayarishi walio nje ya Marekani:  Ukiwasilisha taarifa za kodi ya Marekani, viwango vya kodi ya zuio ni asilimia 0-30 kwenye mapato unayochuma kutokana na watazamaji walio Marekani na vinategemea kama nchi unakoishi ina uhusiano wa mkataba wa kodi na Marekani. 
  • Watayarishi walioko Marekani: Google haitazuia kodi kwenye mapato ikiwa umewasilisha taarifa sahihi za kodi. Watayarishi wengi walioko Marekani wameshawasilisha taarifa zao za kodi ya Marekani.

Muhimu: Iwapo hutatoa taarifa zozote za kodi ya Marekani, huenda Google ikahitajika kuzuia kodi kwa kutumia kiwango cha juu zaidi cha kodi ya zuio. Kiwango chako cha kodi kitategemea aina ya akaunti yako ya AdSense katika YouTube na nchi unakoishi:

  • Aina ya akaunti ya Biashara: kiwango chaguomsingi cha kodi ya zuio kitakuwa asilimia 30 ya mapato yaliyochumwa Marekani ikiwa anayelipwa yuko nje ya Marekani. Biashara zilizo Marekani zitatozwa asilimia 24 ya kodi ya zuio kwenye jumla ya mapato yaliyochumwa kote duniani.
  • Aina ya akaunti ya mtu binafsi: kiasi maalum cha mapato kitakatwa kwa ajili ya kodi na asilimia 24 ya jumla ya mapato yaliyochumwa kote duniani itazuiwa.

Viwango hivi vya kodi ya zuio vitarekebishwa katika kipindi cha malipo kinachofuata baada ya kutoa taarifa sahihi za kodi ya Marekani kwenye AdSense katika YouTube. Unaweza kufuata maagizo haya ili ubaini aina ya akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube unayotumia.

Muhimu: Google haitawahi kukutumia ujumbe ambao hujauomba, unaokuomba nenosiri au taarifa zako nyingine binafsi. Kabla ya kubofya kiungo, hakikisha kila wakati kuwa barua pepe imetumwa kutoka kwenye anwani ya barua pepe ya @youtube.com au @google.com .

Maswali Yanayoulizwa Sana

Ni nini maana ya kuzuia kodi?

Kwa kifupi, kuzuia kodi hutokea pale ambapo kodi imekatwa kwenye malipo yako na kulipwa kwa serikali ili kutimiza dhima ya anayelipwa ya kulipa kodi ya Marekani.

Kwa mujibu wa sheria ya kodi nchini Marekani, Google ni wakala wa kodi ya zuio anayehitajika kutii sheria ya kodi ya Marekani na panapohitajika, kuzuia kodi kwenye mapato husika ya YouTube.

Hali hii itaathiri vipi mapato yangu kwenye YouTube?

Ukitoa taarifa sahihi za kodi, kuzuia na kuripoti kodi kutaathiri tu sehemu ya mapato uliyochuma kutokana na watazamaji walio Marekani.

Kiwango halisi cha kuzuia kodi kitabainishwa na taarifa za kodi unazoipatia Google. Baada ya kutuma fomu yako, unaweza kuangalia kiwango chako cha kuzuia kodi katika sehemu ya Dhibiti taarifa za kodi kwenye Mipangilio ya Malipo ya akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Viwango vya kodi ya zuio havionekani katika Takwimu za YouTube.

Mfano dhahania

Ufuatao ni mfano dhahania: mtayarishi wa YouTube nchini India aliye kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube alipata USD $1,000 kutoka YouTube mwezi uliopita. Kati ya kiasi hicho cha USD $1,000, chaneli yake ilipata USD $100 kutokana na watazamaji walio Marekani.

Zifuatazo ni baadhi ya hali za kuzuia kodi zinazoweza kutokea:

  • Mtayarishi hajawasilisha taarifa za kodi: makato ya mwisho ya kodi ni USD $240 kwa sababu kiwango cha kodi ya zuio ni hadi asilimia 24 ya jumla ya mapato yaliyochumwa kote duniani ikiwa mtayarishi hajawasilisha taarifa za kodi. Hii inamaanisha kuwa hadi mtayarishi atakapowasilisha taarifa kamili za kodi, tutahitaji kukata hadi asilimia 24 ya jumla ya mapato aliyochuma kote duniani, si mapato aliyochuma Marekani tu.
  • Mtayarishi amewasilisha taarifa za kodi na amedai manufaa ya mkataba: makato ya mwisho ya kodi ni USD $15. Hii ni kwa sababu India na Marekani wana uhusiano wa mkataba wa kodi unaopunguza kiwango cha kodi hadi asilimia 15 ya mapato yaliyotokana na watazamaji walio nchini Marekani.
  • Mtayarishi amewasilisha taarifa za kodi, lakini hajatimiza masharti ya kupata manufaa ya mkataba wa kodi: makato ya mwisho ya kodi yatakuwa USD $30. Hii ni kwa sababu kiwango cha kodi bila mkataba wa kodi ni asilimia 30 ya mapato yaliyotokana na watazamaji walio nchini Marekani.

Kukokotoa kodi yako ya zuio iliyokadiriwa

Angalia jinsi mapato yako ya YouTube yanavyoweza kuathiriwa ukitumia mfano ufuatao wa ukokotoaji:

  1. Fikia Ripoti ya Mapato kwenye Takwimu za YouTube kisha uweke kichujio cha tarehe kiwe kipindi cha malipo kinachofaa (k.m. tarehe 1 hadi 31 Okt). Inaweza kusaidia zaidi ukiweka Takwimu zako za YouTube katika sarafu inayotumiwa kukulipa (k.m. USD).
  2. Weka kichujio cha jiografia ili uone mapato yanayokadiriwa kutoka kwa watazamaji walio nchini Marekani. Pata maelezo zaidi kuhusu Hadhira yako kwenye Takwimu za YouTube.
  3. Nenda kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube ili uone kiwango chako cha kuzuia kodi. Kiwango chako cha kodi ya zuio huonekana baada ya kutuma taarifa zako za kodi ya Marekani.
  4. Zidisha matokeo ya hatua ya 2 na 3 hapo juu.

Kumbuka kuwa kufuata hatua zilizo hapo juu hukupa tu kadirio la kuzuia kodi. Google ikianza kuzuia kodi, utaona kiasi halisi kilichozuiwa katika Ripoti yako ya kawaida ya Miamala ya Malipo kwenye AdSense katika YouTube (ikiwa kodi yoyote imezuiwa).

Itakuwaje iwapo kwenye chaneli yangu sichumi mapato kutokana na watazamaji walio Marekani?

Watayarishi wote walio kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube wanapaswa kuwasilisha taarifa za kodi kwa Google, bila kujali kama wanachuma mapato kutokana na watazamaji walio nchini Marekani au la. Kuwasilisha taarifa zako za kodi ya Marekani kutasaidia kubaini kiwango sahihi cha kodi ya zuio, endapo utachuma mapato kutokana na watazamaji walioko nchini Marekani baadaye.

Mnatumia vigezo gani kubaini iwapo mimi ni mtayarishi aliye Marekani au la?

Mahali ulipo hubainishwa na nchi uliyoweka kwenye taarifa zako za kodi kama nchi unakoishi.

Ina maana kuwa nitatozwa kodi katika nchi ninakoishi na Marekani pia?

Google inahitajika tu kuzuia kodi ya Marekani kwenye mapato ya YouTube uliyochuma kutokana na watazamaji walio nchini Marekani. Sheria za kodi ya mapato za nchi uliko bado zinaweza kutumika kwenye mapato yako ya YouTube.

Nchi nyingi zina mikataba ya kodi inayopunguza au kuzuia kutozwa kodi mara mbili. Zaidi ya hayo, baadhi ya nchi zinaweza kuruhusu uondoaji wa kiasi fulani cha kodi ya nchi za kigeni ili kusaidia kupunguza mzigo wa kodi ya kimataifa. Kwa kudai mkataba wa kodi kwenye zana ya kodi kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube, unaweza kupunguza mzigo wako wa kodi. Tafadhali wasiliana na mshauri wako wa kodi. Pata maelezo zaidi hapa

Je, Google hutoa aina zipi za hati za kuripoti kodi?

Utaona viwango vya mwisho vya kuzuia kodi kwenye Ripoti ya Malipo kulingana na kipindi chako cha malipo. Kwa kawaida, viwango vya kodi iliyozuiwa huonekana katika mwezi wa malipo unaofuata kwa mfano, viwango vya kodi iliyozuiwa mwezi Aprili huorodheshwa katika ripoti ya malipo ya mwezi Mei. Ikiwa kuna uahirishaji wa malipo au matatizo mengine kwenye akaunti yako, viwango halisi vya kuzuia kodi kwa miezi kadhaa vinaweza kuorodheshwa kwa pamoja kwenye ripoti ya malipo ya tarehe ya baadaye.

Watayarishi wote waliowasilisha taarifa za kodi ambao wanapokea malipo yaliyotimiza masharti, watapokea fomu ya kodi (k.m. 1042-S,) mnamo au kabla ya tarehe 14 Aprili kila mwaka kwa ajili ya kodi iliyozuiwa mwaka uliotangulia (kwa kawaida, Fomu za 1099-MISC zinazotolewa kwa watayarishi nchini Marekani hutumwa kufikia mwanzoni mwa Machi). Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi ili uombe nakala, usahihishaji au ubatilishe fomu ya kodi ya Marekani ya mwisho wa mwaka.

Tax document delivery preferences 

Your document delivery options and document statuses for year-end tax forms you receive are under Settings kisha  Manage tax info in the tax tool in your AdSense for YouTube account. You can choose online delivery of digital tax documents or select paper mail.

  • If you select online delivery, you'll receive documents online only.
  • If you select paper mail, we'll send documents to the mailing address provided on your tax form and your documents will still be available online.

If your mailing address has changed, update your tax info in your payments profiles. Google will use the info you submitted on the U.S. tax form in your payments profile.

Je, ninaweza kurejeshewa pesa za kodi iliyozuiwa hapo awali?

Katika hali fulani, Google inaweza kurejesha pesa ulizolipia kodi ya zuio ya Marekani ikiwa utawasilisha taarifa za kodi zilizosasishwa kabla ya tarehe 10, Desemba. Kwa mfano, ukiwasilisha kwa wakati unaofaa fomu ya kodi ya W-8 yenye dai la kiwango cha kodi kilichopunguzwa pamoja hati nyingine zinazohitajika, Google itakokotoa upya viwango vya kodi ya zuio na kurejesha salio.

Kumbuka kwamba huenda ukatakiwa kutupatia hati ya kiapo inayothibitisha kuwa hali yako haijabadilika na ubainishe kuwa mabadiliko uliyofanya kwenye fomu yako yanatumika katika tarehe husika iliyopita, ikiwa inafaa. Unaweza kufanya hivi kwenye sehemu ya “Hati ya kiapo ya kubadilisha hali” katika Hatua ya 6 ya zana ya kodi kwenye AdSense yako katika YouTube.

Pesa hizi zitakazorejeshwa zitaonekana katika kipindi cha malipo kinachofuata baada ya kusasisha fomu yako.

Hali hizi ni chache na ni lazima tupokee taarifa sahihi za kodi kufikia mwisho wa mwaka wa kalenda ambao kodi ilizuiwa. Usipotupatia taarifa sahihi za kodi kufikia mwisho wa mwaka wa kalenda, utahitaji kuwasilisha ombi la kurejeshewa pesa moja kwa moja kwa Mamlaka ya Mapato Marekani (IRS). Tunapendekeza uombe ushauri wa wataalamu wa kodi kuhusu suala hili.

Pesa zozote zinazorejeshwa zitaonekana kwenye Ripoti ya Malipo ya mwishoni mwa kipindi cha malipo baada ya kusasisha taarifa zako za kodi kwenye AdSense katika YouTube.

Washirika katika mitandao ya chaneli mbalimbali (MCN)

Huenda vituo vya washirika katika Mitandao ya Vituo Mbalimbali (MCN) vikatimiza masharti ya kurejeshewa pesa kuanzia mwaka 2023. Ni lazima washirika watupatie hati halali inayothibitisha kuwa malipo ya awali yalitegemea bei ya chini zaidi. Kodi zilizozuiwa katika mwaka huo huo wa kalenda ndizo tu zitastahiki kurejeshwa. Mabadiliko haya hayatumiki kwa mwaka 2022 au miaka yoyote iliyotangulia. Baada ya kutimiza masharti, pesa zitarejeshwa kwa mmiliki wa maudhui halisi ambaye kodi ilizuiwa kutoka kwake.

Je, hali hii inatumika kwenye mapato yangu ya AdSense tofauti na YouTube?

Kwa mujibu wa Sura ya 3, ukiwasilisha taarifa sahihi za kodi, kodi za zuio ya Marekani zitatumika tu kwenye mapato yako ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3594688110061452638
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false