Matatizo ya uchapishaji

Unaweza kupata majibu ya maswali mengi kuhusu matatizo ya kuchapisha programu katika Kituo cha Usaidizi wa Dashibodi ya Google Play. Timu yetu ya usaidizi inaweza kutatua yaliyosalia.

Maswali kuhusu usanidi wa programu

Ili upate usaidizi kuhusu usanidi wa programu za Android, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate hati za kiufundi, zana za Studio ya Android, mwongozo wa wasanidi programu na mafunzo kuhusu jinsi ya kusanidi programu yako ya kwanza.

Ikiwa unasanidi mchezo, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia huduma za michezo ya Google Play na upate hati yote kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Matatizo ya kuambatisha cheti kwenye programu au funguo za kupakia

Programu zilizoandikishwa kwenye mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu

Ikiwa umeandikisha programu yako katika mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu na unahitaji kutunga ufunguo mpya wa kupakia, mmiliki wa akaunti yako anaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi ili kushughulikiwa.

Zifuatazo ni sababu za kawaida zinazokufanya uhitaji kuunda ufunguo mpya wa kupakia:

  • Ufunguo wako binafsi ulipotea au kuvamiwa.
  • Hakuna ufunguo wa kupakia ulioundwa kwa ajili ya programu iliyopo.

Programu ambazo hazijaandikishwa kwenye mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu

Ukipoteza ufunguo wako wa duka, utahitaji kuchapisha programu mpya ukitumia ufunguo na jina jipya la kifurushi. Tunakushauri usasishe programu yako halisi ili uwaruhusu watumiaji wako wajue kuhusu programu yako mpya na ubatilishe uchapishaji wake ili uzuie isipakuwe wakati ujao.

Kumbuka: Tumeshindwa kufuta au kuruhusu programu nyingi zitumie jina sawa la kifurushi.

Pata maelezo zaidi kuhusu vyeti na funguo

Kwa maelezo zaidi kuhusu vyeti, funguo za duka na kuambatisha cheti kwenye programu yako, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Hitilafu wakati wa kupakia faili

Ikiwa unatatizika kupakia faili, huenda ukawa na matatizo kwenye kivinjari chako.

Ili upate hali bora ya utumiaji kwenye Dashibodi ya Google Play, tunapendekeza utumie Chrome. Ili tukusaidie kutatua matatizo, hakikisha kuwa unatumia toleo jipya zaidi la kivinjari chako.

Kama tayari unatumia toleo jipya zaidi la kivinjari chako, zifuatazo ni baadhi ya njia za kusuluhisha matatizo ya kawaida:

  • Futa vidakuzi na akiba ya kivinjari chako.
  • Ikiwa hutumii Chrome, jaribu kuitumia au utumie kivinjari tofauti.
  • Ikiwa umesakinisha viendelezi au programu jalizi za kivinjari, zinaweza kusababisha ukinzani katika Dashibodi ya Google Play. Jaribu kuzima viendelezi au programu jalizi kisha uziwashe moja baada ya nyingine ili utambue ukinzani wowote unaoweza kutokea.
  • Ikiwa umesakinisha programu ya kingavirusi au kinga mtandao, huenda ikasababisha matatizo ya kupakia faili za APK au picha. Ikiwa unatatizika kupakia faili, jaribu kwanza kuzima programu kwa muda kisha upakie faili tena.

Kagua programu yako ili ubaini matatizo

Ikiwa unaendelea kutatizika wakati wa kupakia programu yako, unaweza kutumia Android Lint ili ukague programu yako na ubaini matatizo yanayoweza kuwepo. Ukitumia Android Lint, unaweza kuangalia programu yako ili ubaini matatizo mbalimbali ukitumia kiolesura cha mstari wa amri, Eclipse au IntelliJ.

Fanya jaribio la vipengele vinavyohitajika na programu yako

Iwapo unataka kuona jinsi Google Play itakavyochuja programu yako kulingana na vipengele na ruhusa zilizobainishwa, tumia zana ya aapt ambayo imejumuishwa katika SDK ya Android.

Kwa kutumia amri ya dump badging, aapt itachanganua faili ya maelezo ya programu yako na kutumia masharti yanayotumiwa na Google Play kubaini vipengele ambavyo programu yako inahitaji.

Je, bado unatatizika?

Kama bado huwezi kupakia faili au kuchapisha programu, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi. Jumuisha maelezo yoyote kuhusu tatizo lako, ikiwa ni pamoja na picha za skrini, kipengele cha beji za aapt na faili yako ya APK.

Siwezi kupata programu inayochapishwa kwenye Google Play

Ikiwa umechapisha programu au sasisho hivi karibuni, inaweza kuchukua saa kadhaa kabla ya mabadiliko uliyofanya kuonekana kwenye Google Play. Pia, hakikisha kuwa programu yako imechapishwa katika toleo la umma au kwenye jaribio la watumiaji wengi.

Ili kutatua matatizo mahususi, tembelea sehemu ya Matatizo ya kugundulika na kuonekana kwa programu.

Kufuta programu iliyochapishwa

Kama sehemu ya Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu, watumiaji wanaweza kusakinisha mara nyingi kila programu ambayo wamepakua kwenye Google Play. Hivyo basi, programu zinazosakinishwa haziwezi kufutwa kabisa. Hata hivyo, ili kuzuia watumiaji wapya wasipakue programu yako, unaweza kubatilisha uchapishaji wa programu wakati wowote.

Kama programu yako haijasakinishwa kwenye kifaa chochote, wasiliana na timu yetu ya usaidizi ili uiombe ifute data ya programu yako kabisa.

Matatizo ya kupakia vipengee vya picha

Ili kutatua matatizo ya upakiaji wa vipengee vya picha, hakikisha kuwa unapakia faili ambazo zinatimiza masharti kwa kila aina ya kipengee kuhusu ukubwa, vipimo na aina ya faili. Kama faili zako zimetimiza masharti yote lakini bado unatatizika, jaribu kutumia kivinjari tofauti.

Wakati mwingine, ikiwa umesakinisha programu ya kingavirusi au kinga mtandao, huenda ikasababisha matatizo wakati wa kupakia picha. Ikiwa unatatizika kupakia faili, jaribu kwanza kuzima programu kwa muda kisha upakie faili tena.

Kuchapisha sasisho kwa kusambaza kwa hatua

Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuchapisha sasisho la programu ambalo linafikia asilimia fulani ya watumiaji wako inayoweza kuongezeka baada ya muda fulani, soma makala ya Kituo chetu cha Usaidizi kuhusu kusambaza kwa hatua.

Kuweka jaribio la programu mpya au iliyopo

Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya majaribio ya programu ukitumia makundi mahususi au jaribio la watumiaji wengi wakiwemo watumiaji wa Google Play, soma makala ya Kituo chetu cha Usaidizi kuhusu kuweka majaribio ya watumiaji wengi, watumiaji wachache na majaribio ya ndani.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12890945006881824306
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false