Linda akaunti yako ya msanidi programu

Ili kulinda akaunti ya Dashibodi ya Google Play, Google inatoa zana nyingi na mbinu bora ambazo zinaweza kusaidia kuweka akaunti yako salama.

Kama sehemu ya Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu, ni wajibu wako kudumisha usalama na faragha ya maelezo ya wateja wako.

Hizi ni baadhi ya njia za kulinda akaunti yako ya msanidi programu:

Unda nenosiri salama

Unapounda nenosiri, tumia nenosiri la kipekee (tofauti na unalotumia kwenye tovuti nyingine) ambalo lina mchanganyiko wa herufi, nambari na alama. Pia, badilisha nenosiri lako mara kwa mara ili kusaidia kuzuia ufikiaji bila idhini.

Kwa vidokezo kuhusu kuunda nenosiri thabiti, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi cha Akaunti za Google.

Usishiriki nenosiri lako

Ikiwa unatumia Gmail au Kituo cha malipo ya Google ukitumia akaunti moja ya Google unayotumia katika Dashibodi ya Google Play, kushiriki nenosiri pia kutampa mtu ufikiaji wa akaunti zako nyingine.

Kushiriki nenosiri lako kunaweza kuwapa watu wengine uwezo wa kufikia maelezo yako ya kifedha, yaliyohifadhiwa katika akaunti yako ya Google na barua pepe zako katika Gmail, ambazo zinaweza kuwa na maelezo nyeti kuhusu wateja au biashara yako.

Ikiwa watu wengine wanahitaji uwezo wa kufikia Dashibodi ya Google Play, wamiliki wa akaunti wanaweza kuongeza watumiaji kwenye akaunti ya msanidi programu.

Dhibiti uwezo wa kufikia akaunti

Badala ya kushiriki akaunti, wamiliki wa akaunti wanaweza kuongeza watumiaji wengine kwenye akaunti ya msanidi programu. Baada ya kuongezwa kwenye akaunti yako, watumiaji wanaweza kuingia katika Dashibodi ya Google kwa kutumia anwani zao za barua pepe.

Ni wazo zuri kwa wamiliki wa akaunti kukagua mara kwa mara watumiaji walio na idhini ya kufikia akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play. Pia, weka sera ya timu yako ya kuwaondoa mara moja watumiaji wasiohitaji tena kufikia akaunti yako ya msanidi programu.

Tumia akaunti tofauti kwenye akaunti yako ya Msanidi Programu

Kama akaunti yako ya Msanidi Programu imeunganishwa kwenye Akaunti yako ya binafsi ya Google, unaweza kufungua akaunti mpya ili uitumie kwenye akaunti yako ya Msanidi Programu. Kwa njia hii, akaunti moja ikiathirika, akaunti nyingine bado inaweza kuwa salama.

Kama umejiunga tayari, timu yetu ya usaidizi itahamishia programu zako kwenye akaunti mpya. Ili uhamishie programu zako kwenye akaunti tofauti, sajili akaunti mpya ya msanidi programu, kisha andaa na uombe kuhamishiwa na timu yetu ya usaidizi.

Kumbuka: Ukifunga akaunti yako ya zamani, tutakurejeshea ada yako wa usajili wa awali ya $25.

Sasisha anwani zako za barua pepe

Mbali na Akaunti ya Google uliyotumia kujiandikisha kupata akaunti yako ya msanidi programu, tunapendekeza utumie anwani tofauti ya barua pepe ili wateja waweze kuwasiliana nawe kuhusu programu yako. Unapotumia akaunti mbili tofauti, akaunti moja ikiathirika, akaunti nyingine bado inaweza kuwa salama.

Kwenye ukurasa wa programu yako Ukurasa wa Programu katika Google Play, chini ya "Maelezo ya Mawasiliano," unaweza kusasisha anwani ya barua pepe inayopatikana kwa watumiaji kwenye Google Play.

Ikihitajika, Google itatumia anwani ya barua pepe iliyotumika katika usajili wa akaunti yako ya Msanidi Programu ili kuwasiliana nawe. Ili uhakikishe kuwa hukosi ujumbe wowote muhimu, angalia barua pepe yako katika akaunti yako ya msanidi programu mara kwa mara.

Epuka barua pepe za kuiba data binafsi

Wizi wa data binafsi ni kitendo cha kujaribu kuiba taarifa binafsi au kuingia kwenye akaunti za mtandaoni kwa kutumia barua pepe, ujumbe, matangazo au tovuti danganyifu zinazofanana na zile ambazo tayari unazitumia. Kwa mfano, barua pepe ya kuiba data binafsi huenda ikaonekana kama vile imetoka kwenye benki yako na kuomba taarifa ya faragha kuhusu akaunti yako ya benki.

Ujumbe au maudhui ya wizi wa data binafsi yanaweza: 

  • Kukuomba taarifa zako binafsi au za kifedha.
  • Kukuomba ubofye viungo au upakue programu.
  • Kuiga shirika linaloheshimika, kama vile benki yako, mtandao wa kijamii unaotumia au mahali unapofanyia kazi. 
  • Kuiga mtu unayemfahamu, kama vile mwanafamilia, rafiki au mfanyikazi mwenza.
  • Kuonekana kama vile ujumbe kutoka kwa shirika au mtu unayemwamini.

Tafadhali zingatia kuwa utapokea barua pepe za usaidizi wa akaunti na sasisho la sera kutoka kwenye barua pepe inayoishia na @google.com.

Ikiwa umetoa taarifa zako za akaunti ya Google katika tovuti yoyote inayohusishwa na arifa yenye shaka, tunakushauri ubadilishe nenosiri lako mara moja. Unaweza kufuatilia maagizo yaliyotolewa kwenye Kituo cha Usaidizi cha Akaunti za Google ili ubadilishe nenosiri lako la Akaunti ya Google.

Tunashauri utembelee Kituo cha Usaidizi cha Gmail ili upate maelezo zaidi kuhusu kukwepa na kuripoti barua pepe za kuiba data binafsi.

Akaunti zilizovamiwa

Ikiwa unafikiri kuwa akaunti yako imevamiwa, wasiliana na timu yetu ya usaidizi uwape maelezo yoyote uliyonayo. Timu yetu ya usaidizi itakagua akaunti yako kwa dalili za shughuli zisizoidhinishwa.

Ili usaidie kuchunguza na kurejesha uwezo wa kufikia akaunti yako, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi cha Gmail kwa usaidizi kwa akaunti zilizovamiwa.

Kumbuka: Kama akaunti yako imevamiwa, unapaswa kuilinda ili usaidie kuzuia matatizo ya baadaye katika akaunti. Unaweza kusaidia kudumisha usalama wa watumiaji na akaunti yako ya msanidi programu kwa kuwasha uthibitishaji wa hatua mbili.

Matatizo ya jina la mtumiaji na nenosiri

Ikiwa unakumbana na tatizo la kuingia katika akaunti yako, unaweza kutembelea ukurasa wa Mbinu za Kurejesha Uwezo wa Kufikia Akaunti ya Google ili upate usaidizi.

Nenda kwenye Mbinu za Kurejesha Uwezo wa Kufikia Akaunti

Usalama wa ziada wa akaunti

Uthibitishaji wa Hatua Mbili

Njia salama ya kusaidia kulinda akaunti yako ya msanidi programu ni kuwasha Uthibitishaji wa Hatua Mbili katika akaunti zote zinazoweza kufikia Dashibodi ya Google Play.

Kwa kutumia Uthibitishaji wa Hatua Mbili, unatumia kifaa cha mkononi au nambari ya simu ili kurejesha nambari ya kuthibitisha ambayo inahitajika unapoingia kwenye akaunti ukitumia kifaa kipya. Unaweza kuidhinisha vifaa vingi na uweke mipangilio ya chaguo mbadala.

Pia, kama unatumia akaunti ya Google Apps, msimamizi wako anaweza kusanidi Uthibitishaji wa Hatua Mbili kwa kikoa chako. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi cha Google Apps.

Kagua shughuli za akaunti

Unaweza kufuatilia shughuli katika akaunti yako kwa kutumia njia nyingi:

Jisajili kwenye Huduma ya Google Play ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu au hifadhi nakala ya funguo zako za duka

Hakikisha umejiandikisha katika Huduma ya Google Play ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu au  hifadhi nakala ya funguo zako za duka mahali salama. Bila msimbo wako wa duka, hutaweza kusasisha programu zako kwa sababu unahitaji kutia sahihi matoleo yote ya programu yako ukitumia msimbo huo huo.

Kidokezo: Kama unataka kuhifadhi nakala ya ufunguo wako wa duka (Hifadhi ya Google, Gmail, nk) ukitumia Akaunti ya Google, tumia Akaunti ya Google iliyo tofauti na ile unayotumia kwenye akaunti yako ya msanidi programu. Kwa kuhifadhi nakala rudufu ya ufunguo wako wa duka ukitumia akaunti tofauti, unaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupoteza ufunguo wako wa duka, ikiwa akaunti yako ya Msanidi Programu itashambuliwa.

Vidokezo zaidi vya usalama

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7933555180095971266
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false