Kuandaa na kudhibiti usajili

Mnamo mwezi Mei 2022, tulifanya mabadiliko katika namna ambayo bidhaa zinazolipiwa zinabainishwa na kudhibitiwa kwenye Dashibodi ya Google Play. Iwapo una usajili uliopo na unahitaji kufahamu jinsi mabadiliko haya yatakavyoathiri usajili wako, soma Mabadiliko ya usajili ya hivi majuzi kwenye Dashibodi ya Google Play.

Ukurasa huu unafafanua namna ya kuanzisha na kusimamia usajili kwenye Dashibodi ya Google Play. Kabla ya kuendelea, tunapendekeza usome makala haya ili ufahamu zaidi kuhusu dhana za usajili, vipengee na jinsi usajili unavyofanya kazi.

Unapotumia Dashibodi ya Google Play, utahitaji kutenganisha uwekaji mipangilio na udhibiti wa usajili, mipango ya msingi na ofa kwa kufuata mpangilio huo.

Upatikanaji

Ikiwa upo katika eneo linaloruhusu huduma ya usajili wa wauzaji, unaweza kutumia mfumo wa utozaji kupitia Google Play.

Ikiwa unaishi katika eneo linalotumia huduma hiyo na ungependa kuanza kutumia vipengele vya mfumo wa utozaji wa Google Play kwenye programu zako, weka mipangilio ya taarifa za malipo na ukague hati ya API ya mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kuweka na kudhibiti usajili

Bofya sehemu hapa chini ili uipanue au uikunje.

Anzisha usajili mpya

Kabla ya kuanzisha usajili, hakikisha kuwa unapanga vitambulisho vya bidhaa zako kwa umakini. Vitambulisho vya Bidhaa vinapaswa kuwa vya kipekee kwa programu yako na haviwezi kubadilishwa au kutumiwa tena baada ya kuwekwa.

  • Ni lazima Vitambulisho vya Bidhaa vianze na nambari au herufi ndogo, vinaweza pia kuwa na mistari chini (_), nukta (.) na vinaweza kuwa na herufi zisizozidi 40.
  • Kumbuka: Huwezi kutumia kitambulisho cha bidhaa cha android.test pamoja na vitambulisho vyote vya bidhaa ambavyo vinaanza na android.test.

Kuelewa majukumu yako

Kabla ya kuanzisha usajili, pitia Sera yetu ya Usajili. Ni muhimu uelewe kikamilifu sera hii na kuitii. Ni lazima ubainishe ofa yako kwa uwazi kwa watumiaji. Hii ni pamoja na kuwa dhahiri kuhusu sheria na masharti ya ofa, ikiwa ni pamoja na bei ya usajili, kipindi cha kutozwa na iwapo usajili unahitajika ili kutumia programu. Watumiaji hawapaswi kutekeleza hatua yoyote ya ziada ili kukagua maelezo.

Pia, ni lazima programu zilizo na huduma za usajili au maudhui ziwe na kiolesura au UX ya uwazi ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanaweza kutafuta na kuchagua kwa urahisi chaguo lililoteuliwa. Kwa mfano, ikiwa unauza usajili ndani ya programu zako, unapaswa kuhakikisha kuwa programu zako zinafumbua kwa uwazi namna mtumiaji anavyoweza kudhibiti au kughairi usajili wake. Unapaswa pia ujumuishe kwenye programu zako idhini ya kufikia njia iliyo rahisi kutumia ya mtandaoni ili kughahiri usajili.

Ili uanzishe usajili:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Bofya Weka usajili.
  3. Weka maelezo ya usajili wako.
    • Kitambulisho cha Bidhaa: Ni lazima Kitambulisho cha Bidhaa kianze na namba au herufi ndogo, kinaweza pia kuwa na mistari chini (_), nukta (.), na kinaweza pia kuwa na herufi zisizozidi 40.
    • Jina: Jina fupi la usajili wako lisilozidi herufi 55. Watumiaji wataliona kwenye barua pepe na kituo cha usajili.
      • Wewe, kama msanidi programu, sharti uwe mwazi kuhusu huduma zozote za usajili au maudhui unayotoa ndani ya programu yako.
      • Jina la usajili wako lazima liwiane na ofa yako kwa usahihi. Kwa mfano, usiupe usajili wako jina la "Jaribio Lisilolipishwa."
  4. Bofya Anzisha.
  5. Bofya Badilisha maelezo ya usajili ili uangalie na ubadilishe ukurasa wa "maelezo ya Usajili". Una chaguo la kuweka maelezo zaidi hapa.
  6. Karibu na "Manufaa", Bofya + Weka manufaa na uweke maelezo ya kipengele cha usajili wako. Unaweza kuweka hadi manufaa 4 (yenye herufi zisizozidi 40 kila moja).
    • Manufaa yanapaswa kuangazia vipengele ili kuwapa watumiaji ufahamu bora kuhusu huduma zinazotolewa na usajili wako, kama vile "Orodha kamili ya filamu na vipindi vya televisheni."
    • Kwa kuwa si watumiaji wote watakaotimiza masharti ya kupata bei ya ofa au jaribio lisilolipishwa, manufaa hayapaswi kutaja bei au jaribio lisilolipishwa, kwa mfano, huruhusiwi kutaja “Jaribu kwa siku 7 bila malipo”.
  7. Karibu na "Maelezo", weka maelezo yasiyo ya lazima ya usajili wako. Maelezo haya ni kwa ajili ya matumizi yako ya ndani tu, hayaonyeshwi kwa watumiaji kwenye Google Play.
  8. Unaweza kutakiwa kutoa maelezo kuhusu bidhaa unayosambaza kwa madhumuni ya sheria ya watumiaji au kodi. Ikiwa unatakiwa kutoa maelezo, nenda kwenye sehemu ya "Kodi na utiifu" kisha ubofye Dhibiti mipangilio. Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya kodi na utii.
  9. Bofya Hifadhi mabadiliko.

Ili usajili upatikane kwa watumiaji wa Google Play, anzisha na uwezeshe angalau mpango mmoja wa msingi. Kumbuka kwamba, mara tu unapoanzisha mpango wa msingi hutaweza tena kufuta usajili. Badala yake, utahitaji kuweka usajili huo kwenye kumbukumbu mara tu unapoacha kuuza usajili.

Badilisha usajili uliopo
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na usajili unaotaka kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uone maelezo ya usajili.
  3. Bofya Badilisha maelezo ya usajili na ufanye mabadiliko yako.
  4. Bofya Hifadhi mabadiliko.

Kuweka na kudhibiti mipango ya msingi

Bofya sehemu inayofuata hapa chini ili uipanue au uikunje.

Kuweka na kufungua mpango wa msingi

Kabla ya kuanzisha mpango wa msingi, hakikisha unapanga vitambulisho vya mpango wako wa msingi kwa umakini. Vitambulisho vya mpango wa msingi vinapaswa kuwa vya kipekee katika usajili wa programu yako na haviwezi kubadilishwa au kutumiwa tena baada ya ofa kuanza kutumika.

Ni lazima vitambulisho vya mpango wa msingi vianze kwa herufi ndogo au namba. Unaweza kutumia namba (0-9), herufi ndogo (a-z) na vistari.

Ili uanzishe mpango wa msingi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unapohitaji kuweka mpango wa msingi, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Bofya Weka mpango wa msingi.
  4. Weka kitambulisho cha mpango wa msingi. Kitambulisho cha mpango wa msingi kinapaswa kuwa cha kipekee katika usajili na hakiwezi kubadilishwa au kutumiwa tena baada ya ofa kuanza kutumika.
  5. Chagua aina:
    • Usasishaji otomatiki: Inasasisha kiotomatiki isipokatishwa na mtumiaji.
    • Kulipia mapema: Watumiaji watahitaji kufanya malipo wenyewe ili kuongeza muda wa mpango wao.
    • Awamu (zinapatikana katika nchi au maeneo mahususi): Watumiaji hulipa kiasi mahususi cha kila mwezi kwa kipindi cha malipo ili wapate muda wa kustahiki kutumia usajili kwa kipindi cha malipo. Kwa wakati huu, mpango huu wa msingi unapatikana tu ili usambazwe katika nchi zifuatazo: Brazili, Ufaransa, Italia na Uhispania.
  6. (Mpango wa msingi unaojisasisha kiotomatiki tu) Ikiwa unaweka mpango wa msingi unaojisasisha kiotomatiki, fafanua yafuatayo:
    • Kipindi cha bili: Chagua muda wa kustahiki kutumia usajili. Vipindi vya bili vilivyopo ni:
      • Kila wiki
      • Kila baada ya wiki 4
      • Kila mwezi
      • Kila baada ya miezi 2
      • Kila baada ya miezi 3
      • Kila baada ya miezi 4
      • Kila baada ya miezi 6
      • Kila baada ya miezi 8
      • Kila mwaka
    • Muda wa kutumia bila kutozwa: Chagua kikomo cha juu cha muda ambao watumiaji watadumisha stahiki za usajili wakati tatizo la malipo ya usasishaji yaliyokataliwa linaendelea kushughulikiwa.
    • Kusimamisha akaunti kwa muda: Chagua kikomo cha juu cha muda kabla tatizo la malipo ya usasishaji ambalo halijatatuliwa halijasababisha kuisha kwa muda wa usajili. Kipindi hiki cha kusimamisha akaunti kwa muda kinaanza baada ya muda wowote wa kutumia bila kutozwa kuisha. Wakati wa kipindi cha kusimamishwa kwa akaunti kwa muda, watumiaji hawapaswi kuwa na uwezo wa kufikia manufaa ya usajili.
    • Mabadiliko katika ofa na mpango wa malipo: Chagua jinsi ya kutumia siku zozote za malipo zilizosalia wakati watumiaji wanabadilisha ofa.
    • Jisajili tena: Ikiwa imewashwa, watumiaji wanaweza kununua upya usajili wa kusasishwa kiotomatiki ambao muda wake umeisha kwenye Duka la Google Play.
  7. (Mpango wa msingi unaolipiwa mapema tu) Ikiwa unaweka mpango wa msingi unaolipiwa mapema, fafanua yafuatayo:
    • Muda: Chagua muda wa kustahiki kutumia usajili. Chaguo za muda zilizopo ni:
      • Siku 1
      • Siku 3
      • Wiki 1
      • Wiki 4
      • Mwezi 1
      • Miezi 2
      • Miezi 3
      • Miezi 4
      • Miezi 6
      • Miezi 8
      • Mwaka 1
    • Ruhusu nyongeza: Ikiwa imewashwa, watumiaji wanaweza kuongeza muda wa usajili unaolipiwa mapema unaotumika kwenye Duka la Google Play.
  8. (Mpango wa msingi wa awamu tu) Iwapo unaweka mpango wa msingi wa awamu, fafanua yafuatayo:
    • Kipindi cha malipo: Weka kipindi cha malipo katika miezi (lazima kiwe kati ya miezi 3 na 24).
    • Aina ya usasishaji: Chagua Hujisasisha kiotomatiki kila mwezi au Hujisasisha kiotomatiki kwa kipindi kimoja.
    • Muda wa kutumia bila kutozwa: Chagua kikomo cha juu cha muda ambao watumiaji watadumisha stahiki za usajili wakati tatizo la malipo ya usasishaji yaliyokataliwa linaendelea kushughulikiwa.
    • Kusimamisha akaunti kwa muda: Chagua kikomo cha juu cha muda kabla tatizo la malipo ya usasishaji ambalo halijatatuliwa halijasababisha kuisha kwa muda wa usajili. Kipindi hiki cha kusimamisha akaunti kwa muda kinaanza baada ya muda wowote wa kutumia bila kutozwa kuisha. Wakati wa kipindi cha kusimamisha akaunti kwa muda, watumiaji hawapaswi kuwa na uwezo wa kufikia stahiki za usajili.
    • Mabadiliko katika ofa na mpango wa malipo: Chagua jinsi ya kutumia siku zozote za malipo zilizosalia wakati watumiaji wanabadilisha mpango. Ikiwa unafanya hivyo kwa mpango wa msingi wa awamu, tembelea tovuti ya wasanidi programu wa Android ili upate maelezo zaidi.
    • Jisajili tena: Ikiwa imewashwa, watumiaji wanaweza kununua upya usajili wa kusasishwa kiotomatiki ambao muda wake umeisha kwenye Duka la Google Play.
  9. (Si lazima) Weka lebo ili ubainishe mpango wa msingi au ofa kwenye API. Lebo zinaweza kutumika kubainisha ofa za kuonyesha kwa mtumiaji anapokidhi vigezo vya kupata ofa zaidi ya moja. Unaweza kuweka hadi lebo 20.
  10. Katika upande wa juu kulia mwa sehemu ya "Bei na upatikanaji", bofya Dhibiti upatikanaji katika nchi au eneo. Ili uchague maeneo ambapo mpango wako wa msingi utapatikana:
    • Watumiaji wataweza tu kununua usajili wako kwenye maeneo ambayo mpango wako wa msingi unapatikana. Nchi ambako watumiaji wanatumia Google Play inatumika kubainisha mipango ya msingi inayopatikana kwa ajili yao.
    • Ikiwa utaweka usajili wa mpango wako wa msingi upatikane kwenye "Nchi au maeneo mapya," Google itakaporuhusu matumizi ya sarafu mpya ya ununuzi katika nchi ambako tayari unasambaza programu yako, tutafanya mpango wako wa msingi upatikane kiotomatiki pia. Pata maelezo zaidi kuhusu kuuza programu katika sarafu mbalimbali.
    • Ukichagua aina ya mpango wa msingi unaopatikana kwa watumiaji katika nchi au maeneo fulani pekee, kama vile mpango wa msingi wa malipo ya awamu, basi nchi au maeneo hayo pekee ndiyo yanaweza kuchaguliwa.
  11. Baada ya kuteua chaguo zako, bofya Tekeleza.

Ili uweke bei ya mpango wa msingi kwenye nchi au maeneo mbalimbali kwa wakati mmoja:

  1. Bofya Sasisha bei na uchague nchi au maeneo unayotaka kuweka bei kwa wingi.
  2. Bofya Weka bei.
  3. Weka bei isiyo na kodi pamoja na sarafu unayotaka kutumia.
    • Bei hii itabadilishwa katika sarafu inayofaa kwa kila nchi au eneo, kodi itaongezwa kwa maeneo ya kimamlaka ya kodi kisha bei zitawekwa ili kutii sheria za forodha za eneo husika.
  4. Bofya Sasisha.
  5. Bofya Hifadhi.

Ili uweke bei ya mpango wa msingi kwenye nchi au eneo moja:

  1. Bofya aikoni ya penseli kwenye safu wima ya "Bei" ya jedwali ili uweke bei katika eneo hilo.
    • Kodi zitaongezwa kiotomatiki baada ya kuweka bei.
    • Kwenye maeneo ambayo Google Play haitumii sarafu ya nchi uliyopo, unaweza kubainisha upatikanaji wa mpango wako wa msingi katika sarafu ya USD au EUR.
  2. Bofya Hifadhi.

Ili uanzishe mpango wa msingi:

  1. Bofya Hifadhi.
  2. Bofya Anzisha ili ufanye mpango wa msingi upatikane kwa watumiaji.
Badilisha mpango wa msingi uliopo

Kama ungependa kubadilisha bei za mpango wako wa msingi, soma kuhusu kubadilisha bei za mpango wa msingi na ofa kwanza.

Ili ubadilishe mpango wa msingi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na usajili unaotaka kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa," bofya kishale cha kulia karibu na mpango wa msingi unaotaka kubadilisha.
  4. Unapokamilisha kufanya mabadiliko, bofya Hifadhi mabadiliko.

Kumbuka: Unapoondoa eneo kwenye mpango wa msingi, mpango huo wa msingi hautapatikana tena kwa watumiaji walio katika eneo hilo kwa ununuzi mpya. Hata hivyo, watumiaji ambao tayari wamejisajili kwenye mpango wa msingi unaojisasisha kiotomatiki wataendelea kusasisha kiotomatiki hata kama eneo walilopo litaondolewa kwenye mpango wa msingi.

Kusitisha au kuanzisha tena mpango wa msingi

Unaweza kusitisha mpango wa msingi ili uzuie ununuzi mpya. Hatua hii haiathiri usajili wowote uliopo. Ili usitishe mpango wa msingi:

Muhimu: Unapositisha mpango wa msingi utasitisha pia ofa zake zote.

Ili usitishe mpango wa msingi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unaotaka kubadilisha, bofya kishale cha kulia karibu na mpango wa msingi unaotaka kusitisha.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa," bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya mpango wa msingi.
  4. Katika upande wa kulia juu ya ukurasa, bofya Sitisha.

Ili kufungua tena mpango wa msingi na uruhusu ununuzi mpya:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na usajili unaotaka kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa," bofya kishale cha kulia karibu na mpango wa msingi unaotaka kufungua tena.
  4. Katika sehemu ya chini ya ukurasa, bofya Fungua tena.

Weka na udhibiti ofa

Bofya sehemu inayofuata hapa chini ili uipanue au uikunje.

Weka na ufungue ofa

Kabla ya kuanzisha ofa, hakikisha unapanga vitambulisho vya ofa kwa umakini. Vitambulisho vya ofa vinapaswa kuwa vya kipekee ndani ya mpango wa msingi na haviwezi kubadilishwa au kutumiwa tena baada ya ofa kuanza kutumika.

Ni lazima vitambulisho vya ofa vianze kwa herufi ndogo au namba. Unaweza kutumia namba (0-9), herufi ndogo (a-z) na vistari.

Kabla hujaanza kuweka ofa, zingatia yafuatayo:

  • Ni lazima ubainishe ofa yako kwa uwazi katika matangazo yoyote ya ndani ya programu au skrini za utangulizi.
  • Ni lazima ubainishe dhahiri sheria na masharti ya ofa zako, wakati ambapo ofa itaisha, ikiwa ni pamoja na kiasi ambacho watumiaji watatozwa, kipindi cha kutozwa, jinsi wanavyoweza kughairi na iwapo usajili unahitaji watumie programu. Watumiaji hawapaswi kutekeleza hatua yoyote ya ziada ili kusoma maelezo.
  • Ofa si za lazima; huhitaji kuweka ofa ili kupata mpango wako wa msingi.
  • Ni lazima uwe na mpango wa msingi uliohifadhiwa (rasimu au unaotumika) ili uweke ofa. Kwa kawaida ofa huunganishwa na mpango mmoja wa msingi.
  • Kwa chaguomsingi, ofa zinapatikana kwenye maeneo unapopatikana mpango wa msingi husika. Ndani ya ofa, unaweza kudhibiti upatikanaji uwe katika kikundi kidogo cha maeneo ya mpango wa msingi iwapo utapenda kufanya hivyo.

Ili uweke ofa:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na usajili unaotaka kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uone maelezo ya usajili.
  3. Kwenye sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa", bofya Ongeza ofa.
  4. Chagua mpango wa msingi unaotaka kuuongezea ofa kutoka kwenye orodha kunjuzi kisha ubofye Ongeza ofa.
    • Kumbuka kuwa ofa zinaweza tu kuongezwa kwenye mipango ya msingi inayojisasisha kiotomatiki
  5. Weka kitambulisho cha ofa. Kitambulisho cha ofa kinapaswa kuwa cha kipekee ndani ya mpango wa msingi na hakiwezi kubadilishwa au kutumiwa tena baada ya ofa kuanza kutumika.
  6. Ofa yako inarithi kiotomatiki upatikanaji wa mpango husika wa msingi. Ili ubadilishe hali hii, bofya Dhibiti upatikanaji katika nchi au eneo. Unaweza tu kuchagua maeneo yanayolengwa na mpango wako wa msingi.
  7. Chagua masharti ya kujiunga ya ofa ili kubainisha wateja wanaolengwa na ofa; Kupata wateja wapya, Boresho au Iliyobainishwa na msanidi programu. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya ofa.
  8. Kwa ofa ya upataji wa wateja wapya, teua mojawapo ya chaguo hizi:
    • Watumiaji ambao hawajawahi kuwa na usajili huu: Ofa hii itapatikana kwa watumiaji ambao hawajawahi kuwa na usajili huu.
    • Watumiaji ambao hawajawahi kuwa na usajili wowote: Ofa hii itapatikana kwa watumiaji ambao hawajawahi kuwa na usajili wowote kwenye programu yako.
  9. Kwa ofa iliyoboreshwa, jaza sehemu zifuatazo:
    • Usajili wa sasa: Ofa inapatikana tu kwa watumiaji wenye usajili huu.
    • Kipindi cha bili kilichopo: Ofa itapatikana tu kwa watumiaji wenye kipindi hiki cha bili. Hii inafaa, kwa mfano, kuweka toleo jipya la ofa la kila mwaka kwa watumiaji ambao tayari wana ofa yoyote au mpango wa msingi wa mwezi.
    • Ukomo wa matumizi: Ni mara ngapi mtumiaji anaweza kununua ofa hii (mara moja au bila ukomo)
  10. Kwa ofa inayobainishwa na msanidi programu, ni wewe unayebainisha masharti ya kujiunga kwenye programu yako. Mifano ni pamoja na majaribio ya mara ya pili yasiyolipishwa au ofa zilizorejeshwa kwa ajili ya watumiaji waliozikosa.
  11. (Si lazima) Weka lebo ili ubainishe mpango wa msingi au ofa kwenye API. Lebo zinaweza kutumika kubainisha ofa za kuonyesha kwa mtumiaji anapokidhi vigezo vya kupata ofa zaidi ya moja. Unaweza kuweka hadi lebo 20.

Ili uongeze awamu kwenye ofa:

  1. Chini ya "Awamu", bofya Weka awamu ili uweke jaribio lisilolipishwa na au awamu za bei ya utangulizi. Ni lazima ofa iwe na angalau awamu moja ya uwekaji bei.
  2. Chagua aina ya awamu ya uwekaji bei:
    • Aina: Chagua aina ya awamu kutoka kwenye yafuatayo:
      • Malipo ya mara moja: Watumiaji hulipia kabla ya matumizi kwa kipindi mahususi
      • Malipo yanayojirudia: Watumiaji hulipia kila kipindi kwa idadi mahususi ya vipindi
      • Jaribio lisilolipishwa: Watumiaji hupokea idadi mahususi ya siku, wiki, miezi au miaka bila malipo.
        • Majaribio yasiyolipishwa sharti yapatikane kuanzia kati ya siku 3 hadi miaka 3.
    • Kipindi cha muda: Kwa jaribio lisilolipishwa na aina za malipo ya mara moja, weka idadi ya siku, wiki au miezi.
    • Vipindi vya bili: Ikiwa aina ni malipo yanayojirudia, chagua idadi ya vipindi vya bili.
    • Ubatilishaji wa bei: Kwa malipo ya mara moja au yanayorudiwa, chagua aina ya ubatilishaji wa bei kwenye aina zifuatazo:
      • Kiasi kisichobadilika: Kiasi kisichobadilika, kama vile $5
      • Asilimia ya punguzo: Asilimia ya punguzo kutoka kwenye bei msingi kwa mfano, asilimia 50
      • Punguzo mahususi: Punguzo lisilobadilika kutoka kwenye bei ya msingi kwa mfano, punguzo la $1

Kuweka bei au punguzo katika nchi au maeneo mengi kwa wakati mmoja:

  1. Bofya Sasisha bei zote za punguzo au Sasisha bei zote na uchague nchi au maeneo unayotaka kuweka bei kwa wingi.
  2. Bofya Weka bei/Weka punguzo.
  3. Weka bei isiyo na kodi pamoja na sarafu unayotaka kutumia.
    • Bei hii itabadilishwa katika sarafu inayofaa kwa kila nchi au eneo, kodi itaongezwa kwa maeneo yanayojumuisha kodi na (kwa ajili ya ofa zenye kiasi mahususi pekee) bei zitawekwa ili kutii sheria za forodha za eneo husika.
  4. Bofya Sasisha.
  5. Bofya Weka.

Ili uweke bei au punguzo kwenye nchi au eneo moja:

  1. Bofya aikoni ya penseli kwenye safu wima ya "Bei" ya jedwali ili uweke bei katika eneo hilo.
    • Kodi zitakatwa kiotomatiki baada ya kuweka bei.
    • Kwenye maeneo ambayo Google Play haitumii sarafu ya nchi uliyopo, unaweza kubainisha upatikanaji wa mpango wako wa msingi katika sarafu ya USD au EUR.
  2. Bofya Weka.

Ili uanzishe ofa:

  1. Baada ya kuweka awamu zako, bofya Hifadhi.
  2. Bofya Anzisha ili ofa ipatikane kwa watumiaji waliotimiza masharti.
Badilisha ofa iliyopo

Iwapo unahitaji kubadilisha bei za ofa yako, soma kuhusu kubadilisha mpango wa msingi na bei za ofa kwanza.

Ili ubadilishe ofa:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unayohitaji kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa", bofya kishale cha kulia karibu na sehemu ya ofa unayotaka kubadilisha.
  4. Unapokamilisha kufanya mabadiliko, bofya Hifadhi mabadiliko.
  5. Bofya Hifadhi mabadiliko.
Sitisha au ufungue tena ofa

Unaweza kusitisha ofa ili kuzuia ununuzi mpya. Hata hivyo, wafuatiliaji wowote waliopo wataendelea kunufaika na ofa.

Ili kusitisha ofa:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unayohitaji kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa" bofya kishale cha kulia karibu na ofa unayohitaji kusitisha.
  4. Kwenye upande wa kulia juu ya ukurasa, bofya Sitisha.

Ili kufungua tena ofa na kuruhusu tena ununuzi mpya:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unayohitaji kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa" bofya kishale cha kulia karibu na ofa unayohitaji kufungua tena.
  4. Katika sehemu ya chini ya ukurasa, bofya Fungua tena.

Jinsi ya kuhitimisha makundi ya bei iliyopitwa na wakati

Kwa mipango ya msingi inayosasishwa kiotomatiki, unaweza kuamua kuhitimisha kundi la bei iliyopitwa na wakati na kuwahamishia watumiaji waliopo katika kundi hilo kwenye bei ya sasa ya mpango wa msingi. Kabla ya kufanya hivyo, ni muhimu kukagua na kuelewa vizuri Kubadilisha bei za mipango ya msingi na ofa.

Kuhitimisha kundi la bei iliyopitwa na wakati

Ili uhitimishe kundi la bei iliyopitwa na wakati:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na usajili husika, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa," bofya aikoni ya nukta tatu karibu na mpango wa msingi wenye kundi la bei iliyopitwa na wakati ambalo ungependa kuhitimisha, kisha uchague Angalia viwango vya bei iliyopitwa na wakati.
  4. Chagua tarehe ya kuanza ya kundi ambalo ungependa kuhitimisha.
  • Muhimu: Kuhitimisha kundi kutahitimisha pia makundi yoyote ya awali ya mpango huo huo wa msingi na nchi au maeneo husika. Kwa kuwa kila kundi linaweza kuwa na bei tofauti, huenda ikawa aina tofauti ya badiliko la bei (ongezeko la kujiondoa, ongezeko la kujijumuisha au punguzo).
  1. Chagua nchi au maeneo ambayo ungependa kuhitimisha kundi.
  • Muhimu: Iwapo makundi yoyote yaliyo na ongezeko la bei hayatimizi vigezo vya eneo, urudiaji au kiasi vinavyofafanuliwa hapo juu, utaona aikoni za tahadhari kuwa ongezeko litakuwa la kujijumuisha. Unaweza kuona sababu kwa kuwekelea kiashiria juu ya aikoni hizi. Unaweza kuendelea na maongezeko haya ya kujijumuisha au uache makundi haya yaendelee kutumia bei ya sasa kwa kuacha kuchagua nchi au eneo husika au kwa kuchagua tarehe tofauti ya kuanza.
  1. Bofya Kagua uhamishaji ili uendelee.
  2. Kagua idadi ya nchi au maeneo na maelezo kuhusu mabadiliko ya bei. Ikiwa kundi moja au zaidi linatimiza masharti ya ongezeko la bei unalofaa kujiondoa na ungependa maongezeko yawe ya kujiondoa panapowezekana, ni lazima ukague masharti na uthibitishe kuwa yanafuatwa kwa kuteua chaguo husika. Kumbuka kwamba hata ikiwa umeteua chaguo la kujiondoa, makundi ambayo hayatimizi masharti ya maongezeko ya bei ya kujiondoa yatapokea kiotomatiki maongezeko ya kujijumuisha.
  • Iwapo masharti haya hayatimizwi au hungependa maongezeko ya kujiondoa, chagua Tumia maongezeko ya bei unayofaa kujijumuisha kila wakati. Ikiwa hungependa maongezeko ya kujiondoa katika maeneo mahususi, fanya uhamishaji tofauti unaojumuisha maeneo hayo pekee.
  1. Bofya Anzisha uhamishaji.

Kuwasha au kuzima kipengele cha kusitisha usajili

Kwa kuwasha kipengele cha kusitisha katika mipangilio yako ya usajili, watumiaji wanaweza kusitisha usajili wao badala ya kughairi. Kumbuka yafuatayo:

  • Kipengele cha kusitisha usajili hakipatikani kwa jaribio lisilolipishwa au usajili wa mwaka.
  • Huwezi kuwasha kipengele cha kusitisha usajili kwa usajili wenye vipindi vinavyojirudia vinavyozidi miezi mitatu.
  • Vikomo vya kusitisha usajili vya wiki moja na miezi mitatu vinaweza kubadilika wakati wowote.

Pata maelezo zaidi kuhusu kusitisha usajili na masharti ya kutekeleza tukio la kusitisha usajili kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Ili uwashe au uzime kipengele cha kusitisha usajili:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mipangilio ya uchumaji wa mapato (Chuma mapato > Mipangilio ya uchumaji wa mapato).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio ya usajili", chagua Weka au Zima karibu na "Sitisha."
  3. Bofya Hifadhi Mabadiliko.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5025120039810721178
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false