Mabadiliko kwenye masharti ya malipo ya Google Play kwa wasanidi programu wanaohudumia watumiaji nchini Korea Kusini

Kuanzia tarehe 2 Agosti 2023, ni sharti wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji nchini Korea Kusini watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Ili uanze, angalia maelezo yafuatayo na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API ya mfumo mbadala wa utozaji.

Kutokana na sheria, tunawapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji kando ya mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji wao wa vifaa vya mkononi na kompyuta kibao nchini Korea Kusini Ikiwa mtumiaji atalipa kupitia mfumo mbadala wa utozaji, ada ya huduma ya Google Play itapunguzwa kwa asilimia 4. Kwa maelezo zaidi, angalia Sera ya malipo.

Ikiwa hutaki kutoa mfumo mbadala wa utozaji, huhitaji kuchukua hatua yoyote.

Ujumuishaji wa mfumo mbadala wa utozaji

Ili kudumisha hali thabiti na salama ya utumiaji, wasanidi programu watahitaji kutimiza masharti kadhaa.

Ikiwa ungependa kuwapa watumiaji nchini Korea Kusini chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na ule wa Google Play, ni lazima ukamilishe hatua zifuatazo:

  1. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango kupitia timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo).
  2. Fuata masharti ya uaminifu na usalama kwa kuthibitisha kutii masharti ya PCI DSS na kuwapa watumiaji njia ya kuripoti miamala ya kilaghai.
  3. Kamilisha mchakato wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji kama inavyoelezwa kwenye mwongozo huu wa ujumuishaji wa API.
  4. Sasisha mipangilio yako ya mfumo mbadala wa utozaji wa Dashibodi ya Google Play ili kujijumuisha au kujiondoa kwenye kila mojawapo ya programu zako, kudhibiti nembo za njia ya kulipa na URL za udhibiti wa usajili.
  5. Ripoti kwa Google Play miamala yote iliyoidhinishwa inayofanywa na watumiaji nchini Korea Kusini, ndani ya saa 24 ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji.
  6. Lipa ada ya huduma ya Google Play iliyorekebishwa, kwa miamala iliyotolewa ankara iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji, nje ya mfumo wa utozaji wa Google Play.

Ikiwa umemaliza kujaza fomu ya taarifa, umekamilisha mchakato wa kujiandikisha na unahamia kwenye API za mfumo mbadala wa utozaji, utahitajika kukamilisha hatua ya 3 na ya 4 kwenye sehemu inayotangulia. Ukishaanza kuripoti miamala ukitumia API, huhitaji tena kuituma wewe mwenyewe.

Ikiwa una maswali yoyote ya ziada, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi.

 

Fungua fomu ya tangazo

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini bado unahitaji mfumo wa utozaji wa Google Play pamoja na mfumo wa msanidi programu?

Google Play inaamini kuwa watumiaji wanapaswa kuwa na chaguo la kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play wanapofanya ununuzi wa bidhaa dijitali kwenye programu zilizosakinishwa kutoka kwenye Google Play. Tumeunda mfumo wa utozaji wa Google Play kwa viwango vya juu vya usalama na faragha ili watumiaji wawe na uhakika wanapofanya ununuzi wa ndani ya programu. Pia, mifumo mbadala ya utozaji huenda isitoe viwango vile vile vya ulinzi au chaguo na vipengele vya malipo vya mfumo wa utozaji wa Google Play, kama vile vidhibiti vya wazazi, njia za kulipa za familia, udhibiti wa usajili, kadi za zawadi za Google Play na Pointi za Google Play.

Kwa nini bado mnatoza ada ya huduma?
Ada ya huduma ya Google Play haijawahi kamwe kuwa ada ya uchakataji wa malipo tu. Huonyesha thamani inayotolewa na mfumo wa Android na Google Play na huendeleza uwekezaji wetu tunaoendelea kufanya katika mfumo wa Android na Google Play, ambao hutuwezesha kubuni vipengele vya watumiaji vya kutegemewa. Ingawa ada za huduma za kusambaza programu kupitia mfumo wa Android na Google Play zitaendelea kutozwa kulingana na mauzo dijitali kwenye mfumo, tunatambua kuwa wasanidi programu watatozwa gharama za kuendeleza mfumo wao wa utozaji. Kwa hivyo, mtumiaji anapochagua mfumo mbadala wa utozaji, tutapunguza ada ya huduma ya msanidi programu kwa asilimia 4.
Ni kwa bidhaa aina zipi ambazo ninaweza kuwapa chaguo la mfumo mbadala wa utozaji watumiaji wa nchini Korea Kusini?

Mifumo mbadala ya utozaji inaweza kutumiwa kwa ununuzi wa ndani ya programu na usajili unaouzwa kwa watumiaji wa vishikwambi na simu za mkononi. Ili upate maelezo zaidi, angalia Sera ya malipo iliyosasishwa.

Je, ni kiasi gani cha ada ya huduma kinatozwa kwa miamala dijitali, ukitumia mfumo mbadala wa utozaji?

Kwa watumiaji wanaochagua mfumo mbadala wa utozaji, ada ya huduma itakayotozwa itakuwa ni ada yako ya sasa ya huduma ikipunguzwa kwa asilimia 4. Kwa watumiaji wanaochagua mfumo wa utozaji wa Google Play, ada ya huduma haitabadilika. Ada ya huduma itakayotozwa kwa wasanidi programu wanaoendelea kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play pekee haibadiliki, ambapo asilimia 99 ya wasanidi programu wanatimiza masharti ya kutozwa ada ya huduma ya asilimia 15 au chini yake.

Ada ya huduma hutathminiwa na kutumwaje kwa miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Ada ya huduma hutathminiwa kulingana na miamala iliyolipwa kutoka kwa watumiaji wa kompyuta kibao na simu za mkononi nchini Korea Kusini. Utapokea bili yenye tarehe ya kukamilisha na maagizo ya malipo.

Je, ni kwa jinsi gani na ni lini ninaweza kutuma miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Kuanzia tarehe 6 Aprili 2023, miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji inaweza kuripotiwa kupitia API za mfumo mbadala wa utozaji na ni sharti iripotiwe ndani ya saa 24 ya malipo kuidhinishwa. API hizi zinafanya iwe rahisi kwa wasanidi programu kuripoti na pia kuruhusu miamala kupitia mfumo mbadala wa utozaji ionekane kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Ikiwa bado hujajumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, bado unaweza kuendelea kuripoti miamala wewe mwenyewe hadi tarehe 2 Agosti 2023. Katika hali hii, unahitajika kuripoti wewe mwenyewe, kiasi cha miamala iliyolipwa kufikia siku ya 5 ya kazi ya mwezi mara moja kwa mwezi. Kwa mfano, ripoti ya miamala iliyofanywa mwezi Desemba 2021, itapaswa kuripotiwa kufikia tarehe 7 Januari 2022.

API za mfumo mbadala wa utozaji zina faida gani? Ninaweza kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji kabla ya kutumia API kuripoti miamala?

Ili kurahisisha hali ya utumiaji ya msanidi programu, API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa ili kujumuishwa na kutumiwa pamoja. API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yafuatayo:

  • Skrini za mfumo mbadala wa utozaji zinazotekelezwa na Google Play, kumaanisha kuwa huhitaji kuunda na kudumisha maelezo na au skrini za chaguo wewe mwenyewe.
  • Mchakato wa kuripoti miamala uliorahisishwa. Hii haondoa chaguo la kugusa kwa mikono na hukabili hitilafu za ujumuishaji au ulinganishaji.
  • Miamala ya mfumo mbadala wa utozaji iliyoripotiwa kupitia API itaonyeshwa kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Zaidi ya hayo, pia tumefanya maboresho yafuatayo ili iwe rahisi kwako kuanza kutumia mfumo mbadala wa utozaji:

  • Tumerahisisha hali ya utumiaji ya chaguo la mtumiaji.
  • Udhibiti wa hali ya kujihudumia katika mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kupitia Dashibodi ya Google Play, kama vile kuwasha au kuzima kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwa kila programu inayotimiza masharti kwa kila soko, kudhibiti nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  • Ripoti zinazoweza kuhamishwa za miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji iliyoripotiwa kupitia API iliyo na maelezo ya ziada kama vile kiwango cha ubadilishaji kilichotumika, kitambulisho cha kifurushi cha programu husika na kiwango cha ada ya huduma.
Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji?

Ni rahisi kupanua ujumuishaji wako uliopo na mfumo wa utozaji wa Google Play ili kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji. API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa kwa kutumia miundo ile ile ya usanifu na kanuni, sawa na Maktaba yetu ya Malipo kupitia Google Play na API za Msanidi Programu ya Google Play. Hii inamaanisha inaoana na miundo yako iliyopo na timu zako zitakuwa na ufahamu nayo.

Katika mwongozo wetu wa ujumuishaji, tunatoa mwongozo wa kina na nyenzo kuhusu jinsi ya kuanza na kushughulikia masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mara moja na unaorudiwa. Kuna vijisehemu vya msimbo vya mfano vya kufanya iwe rahisi kutekeleza. Tunakaribisha maoni ya wasanidi programu kuhusu API hizi na nyenzo zozote za ziada zinazoweza kusaidia. Ikiwa una maswali yoyote au maoni kuhusu API za mfumo mbadala wa utozaji, wasiliana nasi.

Tayari ninashiriki kwenye mpango, ninahitaji kufanya nini ili nianze kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji?

Utahitaji kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji na usasishe mipangilio yako ya mfumo mbadala wa utozaji katika Dashibodi ya Google Play. Ukishaanza kuripoti miamala ukitumia API, huhitaji tena kuituma wewe mwenyewe.

Je, ninaweza kutoza bei tofauti kwenye mfumo mbadala wa utozaji ikilinganishwa na bei ninayotoza kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play?

Ndiyo, wasanidi programu wanaweza kuweka bei tofauti kwenye kila mfumo wa utozaji wakipenda.

Wasanidi programu wanaweza kutangaza mfumo mbadala wa utozaji kwenye programu zao?

Ndiyo, wasanidi programu wanaotumia mfumo mbadala wa utozaji wanaweza kutangaza mfumo huo mbadala wa utozaji ndani ya programu zao, lakini lazima pia wafuate mwongozo wetu wa UX ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanaelewa chaguo lililotolewa na wanakuwa na hali thabiti ya utumiaji.

Je, Google Play inaruhusu viungo vya nje katika ununuzi wa maudhui dijitali nchini Korea Kusini?

Ndiyo, Google Play inaruhusu wasanidi programu kuweka viungo vya nje ndani ya programu zao, kuwasilisha malipo yanayofanya kupitia kwa wavuti kama njia mbadala ya kulipa kwa watumiaji wa vifaa vya mkononi na kompyuta kibao nchini Korea Kusini. Kama zilivyo njia nyingine mbadala za kulipa, hizi zitazingatia masharti ya kujumuisha mfumo mbadala wa utozaji ambao tumeorodhesha kwenye ukurasa huu.

Ni muhimu kuzingatia kuwa malipo ya viungo vya nje ni malipo ya kwenye wavuti yanayotekelezwa kupitia kiolesura cha wavuti. Tunahitaji chaguo la kiungo cha nje lionyeshwe ndani ya programu ya msanidi programu inayotumia mwonekano wa wavuti uliopachikwa ili kuleta hali ya utumiaji ambayo ni usalama, inayoeleweka zaidi na thabiti.

Pia tunahitaji wasanidi programu wafuate masharti yetu ya uaminifu na usalama na hali ya utumiaji yaliyoelezewa zaidi kwenye mwongozo wetu wa UX. Na kama tulivyotangaza tayari, wasanidi programu hupokea punguzo la asilimia 4 la ada ya huduma kwa miamala inayofanywa na watumiaji waishio nchini Korea Kusini wanapolipa kupitia njia hii mbadala ya kulipa kupitia kiungo cha nje.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kuwasiliana na watumiaji wako walio nchini Korea Kusini kuhusu njia mbadala za kulipa, angalia sera ya Malipo ya Google Play.

Je, inawezekana kuomba kuongezewa muda wa kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji?

Hatukubali tena maombi ya kuongezewa muda kwa kuwa tarehe ya mwisho ya kuhama imepita. Kuanzia tarehe 2 Agosti 2023, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji nchini Korea Kusini, wanapaswa kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8049099886519639313
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false