Sera ya maelezo ya kimatibabu yanayopotosha

YouTube hairuhusu maudhui yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana kwa kueneza maelezo ya kimatibabu yanayopotosha, ambayo yanakinzana na mwongozo wa mamlaka ya afya katika eneo (LHAs) au Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhusu bidhaa na hali mahususi za kiafya. Sera hii inajumuisha aina zifuatazo:

  • Maelezo ya kupotosha kuhusu uzuiaji 
  • Maelezo ya kupotosha kuhusu matibabu 
  • Maelezo ya kupotosha ya kupinga kuwepo kwa ugonjwa

Kumbuka: Sera za YouTube za maelezo ya kimatibabu yanayopotosha zinaweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya mwongozo kutoka mamlaka za afya au WHO. Huenda kukawa na tofauti ya muda kati ya mwongozo mpya wa mamlaka ya afya katika eneo au wa Shirika la Afya Duniani (LHA/WHO) na masasisho ya sera zetu. Kwa hivyo, huenda sera zetu zisishughulikie mwongozo wote wa LHA/WHO kuhusu bidhaa na hali mahususi za kiafya.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Usichapishe maudhui kwenye YouTube iwapo yanajumuisha moja kati ya yafuatayo:

Maelezo ya kupotosha kuhusu uzuiaji: Haturuhusu maudhui yanayotangaza maelezo ambayo yanakinzana na mwongozo wa mamlaka ya afya kuhusu kuzuia au kusambaza hali mahususi za afya au kuhusu usalama, ufanisi au viambato vya chanjo zinazotolewa sasa na zilizoidhinishwa.

Maelezo ya kupotosha kuhusu matibabu: Haturuhusu maudhui yanayotangaza maelezo yanayokinzana na mwongozo wa mamlaka ya afya kuhusu matibabu ya hali mahususi za afya ikiwa ni pamoja na kutangaza matumizi ya bidhaa au vitendo ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka ya afya katika eneo au Shirika la Afya Duniani, kwamba ni salama au vyenye ufanisi au vimethibitishwa kusababisha madhara makubwa.

Maelezo ya kupotosha ya kupinga: Haturuhusu maudhui ambayo yanapinga kuwepo kwa hali mahususi za kiafya.

Sera hizi zinatumika kwenye video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au kipengele kingine chochote cha YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii si kamili. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zinatumika kwa viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa kutamka, pamoja na njia zingine.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube. Hii si orodha kamili.

Maelezo ya kupotosha kuhusu uzuiaji

Bidhaa na vitendo vyenye madhara kama mbinu za uzuiaji
  • Utangazaji wa bidhaa na matibabu yafuatayo yanayoweza kusababisha hatari kubwa ya majeraha mabaya ya mwili au kifo:
    • Mchanganyiko wa Miracle Mineral Solution (MMS)
    • Black Salve
    • Terafini
    • B17/amygdalin/pichi au mbegu za aprikoti
    • Peroksaidi ya haidrojeni ya kiwango cha juu
    • Tiba ya kuondoa madini ya chuma mwilini ili kutibu ugonjwa wa akili wa watoto
    • Seramu ya dawa ya rangi ya fedha
    • Petroli, dizeli na mafuta ya taa
  • Maudhui yanayopendekeza matumizi ya Ivermectin au Hydroxychloroquine katika uzuiaji wa COVID-19.
Maelezo ya kupotosha kuhusu mbinu iliyohakikishwa ya kuzuia hali za kiafya
  • Madai ya kuwepo kwa mbinu iliyohakikishwa ya kuzuia COVID-19. 
  • Madai kuwa matibabu au chanjo yoyote ni mbinu iliyohakikishwa ya kuzuia COVID-19.
Maelezo ya kupotosha kuhusu chanjo
  • Madai ambayo yanakinzana na mamlaka ya afya na mwongozo wa Shirika la Afya Duniani kuhusu usalama, ufanisi na viambato vya chanjo zinazotolewa kwa sasa ambazo zimeidhinishwa na kuthibitishwa 
    • Usalama wa chanjo: Maudhui yanayodai kuwa chanjo husababisha madhara ya kudumu, kama vile saratani au maradhi ya kupooza, mbali na athari ambazo zinatambuliwa na mamlaka za afya.
      • Mifano:
        • Madai kuwa chanjo za MMR husababisha ugonjwa wa akili wa watoto.
        • Madai kuwa chanjo yoyote inasababisha kuambukizwa COVID-19.
        • Madai kuwa chanjo ni njama ya kupunguza idadi ya watu.
        • Madai kuwa chanjo ya mafua husababisha madhara ya kudumu kama vile utasa au husababisha kuambukizwa COVID-19.
        • Madai kuwa chanjo ya HPV husababisha madhara ya kudumu kama vile maradhi ya kupooza.
        • Madai kuwa chanjo iliyoidhinishwa ya COVID-19 itasababisha kifo, utasa, kutoa mimba, ugonjwa wa akili wa watoto au magonjwa mengine yanayoambukiza.
        • Madai kuwa kupata kingamaradhi inayotokana na chanjo au maambukizi ya awali kupitia maambukizi ya kawaida ni salama kuliko kuwachanja watu.
        • Maudhui yanayotangaza matumizi ya chanjo za COVID-19 ambazo hazijaidhinishwa au zilizotengenezewa nyumbani.
    • Ufanisi wa chanjo: Maudhui yanayodai kuwa chanjo hazipunguzi uambukizaji au usambaaji wa ugonjwa.
      • Mifano:
        • Madai kwamba chanjo hazipunguzi hatari ya kuambukizwa magonjwa.
        • Madai kwamba chanjo hazipunguzi makali ya ugonjwa, ikiwa ni pamoja na kulazwa hospitalini au kifo.
        • Madai kuwa chanjo yoyote ni mbinu ya kuzuia COVID-19 iliyohakikishwa.
    • Viambato kwenye chanjo: Maudhui yanayowakilisha kwa uongo viungo vilivyomo kwenye chanjo.
      • Mifano:
        • Madai kuwa chanjo zina bidhaa ambazo haziko kwenye orodha ya viambato vya chanjo hiyo, kama vile dutu za kibaolojia kutoka kwa vijusi (k.m. tishu za vijusi, viini vya vijusi) au bidhaa za wanyama.
        • Madai kwamba chanjo zina bidhaa au vifaa vinavyonuiwa kufuatilia au kutambua wale wanazozipokea.
        • Madai kuwa chanjo hubadilisha miundo ya kijenetiki vya mtu.
        • Madai kuwa chanjo zitafanya watu wanaozipokea wavutie sana.

Nyenzo za ziada

Maelezo zaidi kuhusu chanjo, ikiwa ni pamoja na usalama na ufanisi wake, yanaweza kupatikana hapa chini.

Maelezo ya chanjo ya mamlaka ya afya:

Maelezo ya ziada ya chanjo:

Maelezo ya uambukizaji

  • Maudhui yanayotangaza maelezo kuhusu uambukizaji yanayokinzana na maelezo ya mamlaka ya afya katika eneo au Shirika la Afya Duniani.
    • Maudhui yanayodai kuwa COVID-19 haiambukizwi na virusi.
    • Madai kuwa COVID-19 inasababishwa na miale ya mitandao ya 5G.
    • Maudhui yanayodai kuwa COVID-19 haiwezi kuambukizwa.
    • Maudhui yanayodai kuwa COVID-19 haiwezi kusambaa katika hali fulani za hewa au jiografia.
    • Maudhui yanayodai kuwa kikundi au mtu yeyote ana kingamwili dhidi ya virusi hivyo au hawezi kuvisambaza.

Maelezo ya kupotosha kuhusu matibabu 

Bidhaa na vitendo vyenye madhara kama mbinu za matibabu.

  • Utangazaji wa bidhaa na matibabu yafuatayo yenye hatari ya kusababisha madhara ya mwili au kifo.
    • Mchanganyiko wa Miracle Mineral Solution (MMS)
    • Black salve
    • Terafini
    • B17/amygdalin/pichi au mbegu za aprikoti
    • Peroksaidi ya haidrojeni ya kiwango cha juu
    • Tiba ya kuondoa madini ya chuma mwilini ili kutibu ugonjwa wa akili wa watoto
    • Seramu ya dawa ya rangi ya fedha
    • Petroli, dizeli na mafuta ya taa
  • Maudhui yanayopendekeza matumizi ya mbinu mahususi za kutibu saratani wakati mbinu hizo hazijaidhinishwa na mamlaka ya afya katika eneo au Shirika la Afya Duniani kama mbinu salama au zinazofaa au mbinu hizo zimethibitishwa kuwa na madhara au hazifai katika kutibu saratani.
    • Mifano:
      • Maudhui yanayohimiza matumizi ya mbinu zifuatazo za kutibu saratani, nje ya majaribio ya kimatibabu:
        • Kloridi ya cesium (chumvi ya cesium)
        • Matibabu ya Hoxsey
        • Kuingiza kahawa iliyo na halijoto ya kawaida ndani ya rektamu
        • Matibabu ya Gerson
      • Maudhui yanayodai kuwa mbinu zifuatazo ni salama au zinafaa kwa matibabu ya saratani, nje ya majaribio ya kimatibabu:
        • Tiba kupitia mchanganyiko wa asidi inayopatikana kwenye mkojo na damu
        • Quesetini (Sindano ya mishipa)
        • Methadona
        • Tiba ya kuondoa madini ya chuma mwilini kwa kutumia dawa ambazo hazijaagizwa na daktari.
  • Maudhui yanayopendekeza matumizi ya Ivermectin au Hydroxychloroquine kwa matibabu ya COVID-19.
Maelezo ya kupotosha kuwa matibabu fulani yamehakikishwa
  • Maudhui yanayodai kuwa kuna tiba iliyohakikishwa ya saratani mbali na matibabu yaliyoidhinishwa.
  • Maudhui yanayodai kuwa kuna tiba ya hakika ya COVID-19.
Mbinu mbadala zenye madhara na kukatisha tamaa ya kutafuta matibabu ya kitaalamu
  • Maudhui yanayodai kuwa tiba zilizoidhinishwa za saratani hazina ufanisi.
    • Mifano:
      • Maudhui yanayodai kuwa tiba zilizoidhinishwa za saratani, kama vile kemotherapi au miale, haifanyi kazi kamwe.
      • Maudhui ambayo yanayokatisha watu tamaa ya kutafuta matibabu yaliyoidhinishwa ya saratani.
  • Madai kuwa matibabu mbadala ni salama au yanafaa zaidi kuliko matibabu yaliyoidhinishwa ya saratani.
    • Maudhui ambayo yanadai kuwa matumizi ya juisi yanaleta matokeo bora kuliko kemotherapi kama njia ya kutibu saratani.
  • Maudhui yanayopendekeza matibabu mbadala ya saratani badala ya matibabu ya saratani yaliyoidhinishwa.
    • Maudhui yanayotangaza matumizi ya lishe na mazoezi badala ya kutafuta matibabu yaliyoidhinishwa ya saratani.
  • Kuwahimiza watu wasishauriane na mtaalamu wa matibabu au kutafuta ushauri wa matibabu wakiugua kutokana na COVID-19.
  • Maudhui yanayohimiza matibabu ya kujifanyia nyumbani, maombi au matambiko badala ya matibabu ya hospitalini ya COVID-19 kama vile kushauriana na daktari au kwenda hospitalini.
  • Maudhui ambayo yanakinzana na mwongozo wa mamlaka ya afya katika eneo au Shirika la Afya Duniani kuhusu usalama wa uavyaji mimba kwa njia ya kemikali na upasuaji:
    • Madai kwamba uavyaji mimba husababisha saratani ya matiti.
    • Madai kwamba uavyaji mimba kwa kawaida husababisha au humweka mtu katika hatari kubwa ya utasa au kuharibika kwa mimba siku zijazo.
  • Uhimizaji wa njia mbadala za kuavya mimba badala ya njia za kemikali au upasuaji zinazochukuliwa kuwa salama na mamlaka za afya.
  • Uhimizaji wa maziwa mbadala ya watoto kwa watoto wachanga badala ya maziwa ya mama au maziwa ya watoto ya dukani.

Maelezo ya kupotosha ya kupinga kuwepo kwa ugonjwa  

  • Maudhui yanayopinga kuwepo kwa COVID-19 au kwamba watu hawajafariki kutokana na COVID-19.
    • Mifano:
      • Kupinga kuwepo kwa COVID-19
      • Madai kuwa watu hawajafariki au kuugua kutokana na COVID-19
      • Madai kuwa hamna maambukizi au vifo katika nchi ambako maambukizi au vifo vimethibitishwa na mamlaka ya afya katika eneo au WHO

Maudhui ya elimu, hali halisi, sayansi au sanaa

Tunaweza kuruhusu maudhui yanayokiuka sera za maelezo ya kupotosha zilizobainishwa kwenye ukurasa huu ikiwa maudhui hayo yanajumuisha muktadha wa ziada kwenye video, faili ya sauti, mada au maelezo. Hii si idhini ya kuendeleza maelezo ya kupotosha. Muktadha wa ziada unaweza kujumuisha maoni yanayokanusha kutoka mamlaka ya afya katika eneo au wataalamu wa matibabu. Tunaweza pia kuruhusu maudhui ikiwa kusudi lake ni kushutumu, kupinga au kukejeli maelezo ya kupotosha yanayokiuka sera zetu. Tunaweza pia kuruhusu maudhui yanayojadili matokeo ya utafiti mahususi wa matibabu, yanayoonyesha mijadala ya hadharani, kama vile kupinga au kusikilizwa kwa kesi hadharani, ilimradi maudhui hayo hayana nia ya kutangaza maelezo ya kupotosha yanayokiuka sera zetu.

YouTube pia inaamini kuwa watu wanapaswa kuweza kushiriki hali walizopitia, ikijumuisha matumizi ya kibinafsi ya chanjo, kwa mfano. Hii inamaanisha kuwa huenda tukaruhusu maudhui ambayo watayarishi wanaelezea hali ambazo walipitia wao au familia zao. Vile vile, tunatambua kuwa kuna tofauti kati ya kushiriki hali ambayo mtu binafsi anapitia na kutangaza maelezo ya kupotosha. Ili kukabiliana na hili, bado tutaondoa maudhui au vituo ikiwa vinajumuisha ukiukaji mwingine wa sera au kuonyesha mtindo wa kutangaza maelezo ya kimatibabu yanayopotosha.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yatakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kwamba kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukaondoa kiungo hicho.

Iwapo hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, huenda utatumiwa tahadhari bila kupewa adhabu kwenye kituo chako. Vinginevyo, tunaweza kukipa kituo chako onyo. Ukipata maonyo 3 ndani ya siku 90, kituo chako kitafungwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo hapa.

Tunaweza kusimamisha kituo chako au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha kituo au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au kituo kikikiuka sera mara kwa mara. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kusimamishwa kwa kituo au akaunti hapa

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13021206622132485716
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false