Pata idhini ya kufikia vipengele vya wastani na vipengele vya kina

Kumbuka: Makala haya hayajumuishi beji za uthibitishaji wa chaneli. Kwa maelezo zaidi kuhusu beji za uthibitishaji, tembelea makala ya Kituo cha Usaidizi

YouTube hukupatia zana na vipengele vingi ili kukusaidia unufaike zaidi na kituo chako. Watayarishi wengi wanaweza kufikia vipengele hivi, lakini baadhi ya vipengele huhitaji uthibitishaji wa ziada ili kuvifungua. Vigezo hivi vya ziada vya ufikiaji hufanya isiwe rahisi kwa walaghai, watumaji taka na watendaji wengine wabaya kusababisha hatari. Wamiliki wakuu pekee wa vituo ndio wanaweza kuthibitisha utambulisho wao ili waweze kufikia vipengele vya kina.

Kufikia vipengele vya wastani

Kamilisha uthibitishaji kwa nambari ya simu ili upate idhini ya kufikia

Ukikamilisha uthibitishaji kwa nambari ya simu, utapata idhini ya kufikia vipengele vya wastani. Hapa, unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kufikia vipengele vya kina.

  1. Katika kompyuta, ingia kwenye Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Kituo.
  4. Bofya Masharti ya kipengele kisha Vipengele vya wastani kisha THIBITISHA NAMBARI YA SIMU.

Utaombwa kuweka namba ya simu. Tutatuma namba ya kuthibitisha kupitia SMS au kupiga simu ya sauti kwenye namba hiyo ya simu.

Kufikia vipengele vya kina

Vipengele vya kina ni seti ya vipengele vya YouTube vinavyojumuisha, kwa mfano, uwezo wa kubandika maoni na vikomo vya juu vya upakiaji wa kila siku.

Unaweza kufikia vipengele vya kina kwa kukamilisha kwanza uthibitishaji kwa nambari ya simu. Kisha, unaweza kuchagua kukuza historia ya kutosha ya kituo chako au ukamilishe uthibitishaji kwa kutumia kitambulisho au video iliyo hapo chini.

Mbinu ya uthibitishaji kwa kitambulisho na video haipatikani kwa watayarishi wote. Wakati wowote, hali yako ya sasa ya kustahiki kufikia vipengele katika Studio ya YouTube itakuonyesha hatua unazopaswa kuchukua ili ufikie vipengele vya kina.

Kutumia uthibitishaji kwa nambari ya simu na kitambulisho au video ili upate idhini ya kufikia

Kukamilisha uthibitishaji kwa nambari ya simu

  1. Katika kompyuta, ingia kwenye Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Kituo.
  4. Bofya Masharti ya kipengele kisha Vipengele vya wastani kisha THIBITISHA NAMBARI YA SIMU.
  5. Utaombwa kuweka namba ya simu. Tutatuma namba ya kuthibitisha kupitia SMS au kupiga simu ya sauti kwenye namba hiyo ya simu.

Baada ya kukamilisha hatua ya uthibitishaji kwa nambari ya simu, hatua inayofuata ni kukamilisha uthibitishaji kwa kutumia video au kitambulisho.

Kumbuka: Kwa kawaida, njia ya uthibitishaji kwa kutumia video au kitambulisho chako hufutwa ndani ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya miaka 2 iwapo hujatumia vipengele vya kina.

Kukamilisha Uthibitishaji kwa kitambulisho

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Kituo
  4. Bofya Masharti ya vipengele  kisha  Vipengele vya kina  kisha FIKIA VIPENGELE.
  5. Chagua Tumia kitambulisho chako, kisha ubofye Pata barua pepe . Google itakutumia barua pepe. Unaweza pia kuchanganua msimbo wa QR badala yake. 
  6. Kwenye simu yako, fungua barua pepe kisha uguse Anza uthibitishaji. .
  7. Soma ufafanuzi wa jinsi Google itakavyotumia na kuhifadhi kitambulisho chako. Ili uendelee na uthibitishaji, bofya Ninakubali
  8. Fuatilia vidokezo ili upige picha ya kitambulisho chako. Kumbuka: Hakikisha kuwa tarehe ya kuzaliwa iliyo kwenye kitambulisho chako inalingana na tarehe uliyoweka kwenye Akaunti yako ya Google
  9. Bofya Wasilisha. Ukishawasilisha, tutakagua kitambulisho chako. Kwa kawaida mchakato huu huchukua saa 24.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi data ya uthibitishaji wa kitambulisho chako inavyotumika.

Au

Kamilisha uthibitishaji kwa video

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio .
  3. Bofya Kituo.
  4. Bofya Masharti ya vipengele kisha Vipengele vya kina kisha FIKIA VIPENGELE.
  5. Chagua Tumia njia ya uthibitishaji kwa video, kisha ubofye Inayofuata kisha Pata barua pepe.
    • Google itakutumia barua pepe. Unaweza pia kuchanganua msimbo wa QR badala yake.
  6. Kwenye simu yako, fungua barua pepe kisha uguse Anza uthibitishaji.
  7. Fuatilia vidokezo ili utekeleze kitendo, kama vile kufuatilia nukta au kugeuza kichwa chako.
  8. Ukishamaliza kupakia video yako ya uthibitishaji, tutaikagua.
    • Kwa kawaida ukaguzi huchukua saa 24. Utapokea barua pepe utakapoidhinishwa.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi data yako ya uthibitishaji kwa video inavyotumika.

Kutumia historia ya chaneli ili kupata idhini ya kufikia

Ili upate idhini ya kufikia kipengele cha kina ukitumia historia ya chaneli yako, utahitaji pia kukamilisha uthibitishaji kwa namba ya simu.

Kukamilisha uthibitishaji kwa nambari ya simu

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Kituo.
  4. Bofya Masharti ya kipengele kisha Vipengele vya wastani kisha THIBITISHA NAMBARI YA SIMU.
  5. Utaombwa kuweka namba ya simu. Tutatuma namba ya kuthibitisha kupitia SMS au kupiga simu ya sauti kwenye namba hiyo ya simu.

Data yako ya historia ya chaneli inatumika kubaini iwapo maudhui na shughuli zako zimefuata mwongozo wa jumuiya ya YouTube kila wakati.

Historia ya chaneli yako ni rekodi ya:

  • Shughuli zako kwenye kituo (kama vile upakiaji wa video, mitiririko mubashara na ushiriki wa hadhira.)
  • Data yako binafsi inayohusiana na Akaunti yako ya Google.
    • Wakati ambao akaunti iliundwa na jinsi ilivyoundwa.
    • Inatumika mara ngapi.
    • Njia uliyotumia kuunganisha kwenye huduma za Google.

Chaneli nyingi ambazo tayari zinatumika zina historia ya kutosha ya chaneli ili kufungua vipengele vya kina bila kitendo chochote cha ziada kuhitajika. Lakini, tunafahamu kuwa wakati mwingine tunafanya makosa, ndio maana tunatoa chaguo nyinginezo za uthibitishaji kwa ufikiaji wa haraka.

Kuunda na kudumisha historia ya chaneli yako

Vipengele vya kina ni seti ya vipengele vya YouTube vinavyojumuisha, kwa mfano, uwezo wa kubandika maoni na vikomo vya juu vya upakiaji wa kila siku. Watayarishi wanaweza kupata idhini ya kufikia vipengele vya kina kwa kufuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube kila wakati na kuunda historia ya kutosha ya chaneli. Hali ya kutotii sera zetu itachelewesha ustahiki na. Kwa vituo ambavyo tayari vina idhini ya kufikia vipengele vya kina, hali hiyo inaweza kusababisha kupoteza ustahiki.

Angalia mifano hapo chini ya vitendo vinavyoweza kusababisha ucheleweshaji au kiwango kilichodhibitiwa zaidi cha ufikiaji wa vipengele vya kituo. Kumbuka kuwa hii si orodha kamili:

Kupata tena idhini ya kufikia vipengele

Ikiwa idhini yako ya kufikia vipengele vyovyote vya kina imezuiwa, utapokea barua pepe. Chaneli zinaweza kupata tena idhini ya kufikia kwa kuboresha historia za chaneli au kwa kutoa uthibitishaji. Chaneli zinazotumika mara kwa mara ambazo zinafuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube kwa kawaida zinaweza kuunda upya historia ya chaneli ndani ya miezi 2.

Kumbuka kuwa uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote. Wakati wowote, hali yako ya sasa ya ustahiki wa vipengele kwenye Studio ya YouTube itakuonyesha hatua unazopaswa kuchukua ili ufikie vipengele vya kina.

Kutatua matatizo

  • Ukipata ujumbe unaoeleza "Vipengele vya kina vya YouTube havipatikani katika akaunti hii":
    Inamaanisha umeingia katika akaunti ambayo wewe si mmiliki mkuu. Hali hiyo inaweza kutokea ikiwa umeingia katika akaunti inayosimamiwa na mzazi au umeingia katika Akaunti ya Biashara.
  • Iwapo utapokea ujumbe unaosema "Kagua kivinjari chako":
    Kivinjari chako hakioani. Hakikisha unasasisha kifaa chako ili kitumie mfumo wa uendeshaji na kivinjari cha toleo jipya zaidi. 
  • Iwapo utapokea ujumbe unaosema "Uthibitishaji kwa kitambulisho haufanyi kazi kwenye kamera ya simu hii":
    Kamera yako haioani. Ingia katika akaunti ukitumia simu iliyo na kamera ya nyuma ya HD kamili ili kuwasilisha kitambulisho chako.
  • Ukipokea ujumbe unaosema "Huenda programu nyingine inatumia kamera yako. Funga programu zilizofunguliwa na ujaribu tena":
    Hii inamaanisha kuwa programu nyingine inatumia kamera yako. Funga programu zilizofunguliwa kisha ujaribu tena.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kwa nini YouTube inaomba nambari yangu ya simu / uthibitishaji kwa video / kitambulisho halali?

YouTube inafunga mamilioni ya vituo kila mwaka kutokana na maudhui na tabia zinazokiuka sera. Vituo vingi kati ya hivi vinaundwa na vikundi na watu binafsi walewale wakitumia au kuvuka mipaka ya matumizi ya aina moja ya vipengele wakikusudia kuwadanganya, kuwalaghai au kufanya matumizi mabaya dhidi ya watazamaji, watayarishi na watangazaji. Kuthibitisha utambulisho wako ni njia mojawapo tunayotumia kukomesha matumizi mabaya na kubaini ikiwa ulikiuka sera yetu hapo awali na kudhibiti maombi yanayojirudia. 

Data yangu ya uthibitishaji kwa video na kitambulisho inatumikaje?

Nambari ya simu

Ukichagua kuwasilisha nambari ya simu, tutaitumia ili:

  • Kukutumia nambari ya kuthibitisha.

Uthibitishaji kwa kitambulisho

Ukishawasilisha kitambulisho halali (kama vile pasipoti au leseni ya udereva), tutaitumia ili kuthibitisha:

  • Tarehe yako ya kuzaliwa
  • Kuwa kitambulisho chako ni cha sasa na ni halali
  • Kuhakikisha kuwa hukusimamishwa awali kwa kukiuka sera za YouTube

Pia, itatusaidia kulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya na inaweza kuboresha mifumo yetu ya uthibitishaji.

Uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho utafutwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google ndani ya miaka 2. Kwa kawaida, hufutwa baada ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya mwaka 1 iwapo hujatumia vipengele vya kina.Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta data yako ya uthibitishaji.

Uthibitishaji kwa video

Uthibitishaji kwa video ni video fupi ya uso wa mtu. Tutatumia video hii ili itusaidie kuthibitisha:

  • Kuwa wewe ni mtu halisi
  • Kuwa umefikisha umri unaoruhusiwa kutumia huduma za Google
  • Kuwa hujasimamishwa kwa kukiuka sera za YouTube

Pia, itatusaidia kulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya na inaweza kuboresha mifumo yetu ya uthibitishaji.

Uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho utafutwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google ndani ya miaka 2. Kwa kawaida, hufutwa baada ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya mwaka 1 iwapo hujatumia vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta data yako ya uthibitishaji.

Kufuta na kuhifadhi data

Unaweza kufuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho wakati wowote katika Akaunti yako ya Google. Kumbuka kuwa, ukifuta njia yoyote kati ya hizi kabla ya kuimarisha historia ya chaneli yako ya YouTube, huwezi kutumia vipengele vya kina vya YouTube isipokuwa:

  •  Ukiimarisha historia ya chaneli yako ya YouTube

Au

  • Ukikamilisha tena kitambulisho na uthibitishaji kwa video

Ili kuhakikisha mtu binafsi au vikundi havikwepi vikwazo vyetu kwa kufungua akaunti mpya, tunatathmini ikiwa unaweza kuwa umekiuka sera za YouTube hapo awali na kudhibiti maombi yanayojirudia. Huenda Google ikahifadhi kitambulisho au video yako na data ya utambuzi wa sura kwa kipindi fulani ili kuidhibiti dhidi ya matumizi mabaya.

Data hii itahifadhiwa kwa muda usiozidi miaka 3 tangua mara ya mwisho ulipotumia YouTube.

Iwapo hupendi kutoa uthibitishaji kwa video au kitambulisho ili kufikia vipengele vya kina, huhitaji kufanya hivyo. Badala yake, unaweza kuunda historia ya kutosha ya chaneli. Hata hivyo, hadi wakati utakapokuwa tayari kufikia vipengele vya kina utakuwa umeunda historia ya kutosha.

Unapotumia huduma zetu, unaamini kuwa tutalinda taarifa zako. Tunafahamu kwamba huu ni wajibu mkubwa na tunajitahidi kulinda taarifa yako na kukupa udhibiti. Sera ya faragha ya Google inatumika katika kushughulikia taarifa zako kama inavyotumika katika bidhaa na vipengele vyetu vyote. 

Kumbuka: Kamwe hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. 

Tayari nimetoa uthibitisho, ni kwa nini ninaombwa kuthibitisha tena?

Ili kuhakikisha kuwa tunafuata kanuni za data kwa kuwajibika, uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho hufutwa kiotomatiki pindi tu unapofikisha historia ya kutosha katika chaneli au huenda ukafutwa ikiwa hutatumia vipengele vya kina kwa mwaka 1. Unaweza pia kuchagua kufuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho wakati wowote katika Akaunti yako ya Google

Iwapo uthibitishaji wako umefutwa, utahitajika kuwa na historia ya kutosha kwenye kituo au uwasilishe upya uthibitishaji kwa video au kitambulisho ili uendelee kutumia vipengele vya kina. 

Je, ninawezaje kufuta data yangu ya uthibitishaji?

Muhimu: Iwapo utafuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho kabla hujaunda historia yako ya chaneli, utapoteza idhini ya kufikia vipengele vya kina.
  1. Ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Kwenye upande wa kushoto, bofya Taarifa binafsi.
  3. Bofya Hati ya utambulisho au Uthibitishaji kwa video.
  4. Bofya Futa Delete.
Kwanini simu mahiri inahitajika? Je, siwezi tu kupakia video au picha ya kitambulisho changu?

Simu mahiri inahitajika kwa sababu inatoa ulinzi wa ziada na kufanya iwe vigumu kwa walaghai na watumaji taka kukuhatarisha.

Sijapokea nambari ya kuthibitisha kwenye simu yangu. Je, kuna tatizo gani?

Unatakiwa kupokea msimbo haraka. Ikiwa hujapokea, unaweza kuomba utumiwe msimbo mpya. Hakikisha haukumbwi na moja ya matatizo haya ya kawaida:

  • Uwasilishaji wa SMS unaweza kuchelewa. Uchelewashaji unaweza kutokea katika maeneo yaliyo na watu wengi au ikiwa huna mtandao thabiti. Ikiwa umesubiri kwa zaidi ya dakika kadhaa na bado hujapokea SMS yetu, jaribu njia ya kupiga simu ya sauti.
  • Iwapo tayari umethibitisha vituo 2 ukitumia nambari 1 ya simu, lazima uthibitishe nambari tofauti ya simu. Ili kusaidia kuzuia matumizi mabaya, tunaweka kikomo cha idadi ya vituo vinavyoweza kuunganishwa na kila nambari ya simu.
  • Baadhi ya nchi au maeneo na watoa huduma za simu hawaruhusu huduma ya kupokea SMS kutoka Google. Watoa huduma za simu wengi wanaruhusu huduma ya kupokea SMS kutoka Google. Ikiwa mtoa huduma wako haruhusu huduma ya kupokea SMS kutoka Google, unaweza kujaribu njia ya kupiga simu au utumie nambari tofauti ya simu.
Uthibitishaji wangu kwa video au kitambulisho changu halali umekataliwa. Nifanye nini?

Ikiwa jaribio lako la kwanza limekataliwa, utaarifiwa kwa barua pepe. Tunapendekeza ukague vidokezo kwenye barua pepe yako.

Ikiwa jaribio lako la pili halikufanikiwa, unapaswa kusubiri siku 30 kabla ya kujaribu tena mojawapo ya mbinu za kuthibitisha. Ikiwa unafikiri uthibitishaji wa pili kwa video ulipaswa kuidhinishwa, unaweza kukata rufaa na kutueleza sababu.

Unaweza pia kusubiri na kuunda historia ya kituo badala yake.

Kwa nini sioni chaguo la kukamilisha uthibitishaji kwa kitambulisho au video?

Uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote, kwa hivyo ni lazima ukuze historia ya kutosha ya kituo chako ili uweze kufikia vipengele vya kina. Wakati wowote, hali yako ya sasa ya kustahiki kufikia vipengele katika Studio ya YouTube itakuonyesha hatua unazopaswa kuchukua ili ufikie vipengele vya kina.
Je, hali hii inafanyaje kazi kwenye vituo vilivyo na watumiaji wengi?

Iwapo una Akaunti ya Biashara:

Mmiliki mkuu pekee wa kituo atastahiki kutekeleza uthibitishaji wa utambulisho. Kulingana na hali yao ya uthibitishaji, watumiaji wote wa kituo watakuwa na idhini ya kufikia vipengele sawa kama mmiliki mkuu.

Iwapo huna Akaunti ya Biashara:

Mmiliki wa kituo pekee atastahiki kutekeleza uthibitishaji wa utambulisho. Kulingana na hali yao ya uthibitishaji, watumiaji wote wa kituo watakuwa na idhini ya kufikia vipengele sawa kama mmiliki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1801665504671406703
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false