Kupata idhini ya kufikia vipengele vya wastani na vya kina

Ili kupata idhini ya kufikia vipengele vya wastani na vya kina, watayarishi wa YouTube wanapaswa kukamilisha hatua za uthibitishaji zilizofafanuliwa katika makala haya. Uthibitishaji huu huhakikisha jumuiya ya YouTube inaendelea kuwa salama kwa kufanya iwe vigumu kwa walaghai, watumaji wa taka na watendaji wengine wabaya kusababisha madhara.

Kumbuka: Wamiliki wakuu pekee wa chaneli ndio wanaweza kuthibitisha utambulisho wao ili waweze kufikia vipengele vya ziada. Pia, baadhi ya vipengele vinaweza kuwa na vigezo tofauti vya masharti ya kujiunga.

Kufikia vipengele vya wastani

Kukamilisha uthibitishaji kwa namba ya simu

Ukikamilisha uthibitishaji kwa namba ya simu, utapata idhini ya kufikia vipengele vya wastani. Hapa, unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kufikia vipengele vya kina.

  1. Katika kompyuta, ingia kwenye Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Chaneli.
  4. Bofya Masharti ya kipengele kisha Vipengele vya wastani kisha THIBITISHA NAMBA YA SIMU.

Utaombwa kuweka namba ya simu. Tutatuma namba ya kuthibitisha kupitia SMS au kupiga simu ya sauti kwenye namba hiyo ya simu.

Kufikia vipengele vya kina

Vipengele vya kina vinajumuisha, kwa mfano, maoni yaliyobandikwa pamoja na vikomo vya juu vya upakiaji wa kila siku. Watayarishi wanaweza kufikia vipengele vya kina kwa:

  1. Kukamilisha uthibitishaji kwa namba ya simu
  2. Kuunda historia ya kutosha ya chaneli au kuthibitisha utambulisho kwa kutumia kitambulisho halali au video
    • Kumbuka: Uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote. 
Kutotii Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube huchelewesha uwezo wa kupata vipengele. Kwa watayarishi ambao tayari wana idhini ya kufikia vipengele vya kina, mnaweza kupoteza uwezo huo wa kufikia kwa kutotii Mwongozo wa Jumuiya na kutodumisha historia bora ya chaneli.

Hatua ya 1. Kukamilisha uthibitishaji kwa namba ya simu

Ili kuthibitisha namba yako ya simu:

  1. Katika kompyuta, ingia kwenye Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Chaneli.
  4. Bofya Masharti ya kipengele kisha Vipengele vya wastani kisha THIBITISHA NAMBA YA SIMU.
  5. Weka namba ya simu. Tutatuma namba ya kuthibitisha kupitia SMS au kwa kupiga simu kwenye namba hiyo.

Hatua ya 2. Kuunda historia ya chaneli au kuthibitisha kwa kitambulisho au video

Baada ya kukamilisha hatua ya uthibitishaji kwa namba ya simu, unaweza kuchagua kuunda historia ya kutosha ya chaneli au kukamilisha uthibitishaji kwa kitambulisho au video. Kumbuka kuwa uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote.

Kuunda na kudumisha historia ya chaneli yako

Historia ya chaneli yako ni rekodi ya:

  • Shughuli zako kwenye chaneli (kama vile upakiaji wa video, mitiririko mubashara na ushirikishaji wa hadhira)
  • Data yako binafsi inayohusiana na Akaunti yako ya Google:
    • Wakati ambao akaunti yako iliundwa na jinsi ilivyoundwa
    • Mara ambazo akaunti yako hutumika
    • Njia yako ya kuunganisha na huduma za Google
Kumbuka: Chaneli nyingi zinazochapisha maudhui tayari zina historia ya kutosha ya chaneli ili kufikia vipengele vya kina. Lakini, tunaelewa kuwa wakati mwingine tunafanya makosa, kwa hivyo tunatoa chaguo za kuthibitisha kwa kitambulisho au video kwa ufikiaji wa haraka.

Kukamilisha Uthibitishaji kwa kitambulisho

Ili kuthibitisha utambulisho kwa kutumia kitambulisho halali:

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Bofya Chaneli.
  4. Bofya Masharti ya vipengele  kisha  Vipengele vya kina  kisha FIKIA VIPENGELE.
  5. Chagua Tumia kitambulisho chako, kisha ubofye Pata barua pepe . Google itakutumia barua pepe. Badala yake, unaweza pia kuchanganua msimbo wa QR.
  6. Kwenye simu yako, fungua barua pepe kisha uguse Anza uthibitishaji.
  7. Soma ufafanuzi wa jinsi Google itakavyotumia na kuhifadhi kitambulisho chako. Ili uendelee na uthibitishaji, bofya Ninakubali.
  8. Fuata vidokezo ili upige kitambulisho chako picha. Kumbuka: Hakikisha kuwa tarehe ya kuzaliwa iliyo kwenye kitambulisho chako inalingana na tarehe uliyoweka kwenye Akaunti yako ya Google.
  9. Bofya Tuma. Ukishawasilisha, tutakagua kitambulisho chako. Kwa kawaida mchakato huu huchukua saa 24.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi data ya uthibitishaji wa kitambulisho chako inavyotumika.

Kukamilisha uthibitishaji kwa video

Ili kuthibitisha utambulisho kwa kutumia video:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio .
  3. Bofya Chaneli.
  4. Bofya Masharti ya vipengele kisha Vipengele vya kina kisha FIKIA VIPENGELE.
  5. Chagua Tumia njia ya uthibitishaji kwa video, kisha ubofye Inayofuata kisha Pata barua pepe.
    • Google itakutumia barua pepe. Badala yake, unaweza pia kuchanganua msimbo wa QR.
  6. Kwenye simu yako, fungua barua pepe kisha uguse Anza uthibitishaji.
  7. Fuatilia vidokezo ili utekeleze kitendo, kama vile kufuatilia nukta au kugeuza kichwa chako.
  8. Ukishamaliza kupakia video yako ya uthibitishaji, tutaikagua.
    • Kwa kawaida ukaguzi huchukua saa 24. Utapokea barua pepe utakapoidhinishwa.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi data yako ya uthibitishaji kwa video inavyotumika.

Kumbuka: Kwa kawaida, uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho hufutwa ndani ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya mwaka 1 iwapo hujatumia vipengele vya kina.

Kutatua matatizo

Kuelewa ufikiaji wa vipengele uliochelewesha au kuzuiwa

Angalia mifano hapo chini ya vitendo vinavyoweza kusababisha ucheleweshaji au kiwango kilichodhibitiwa zaidi cha ufikiaji wa vipengele vya chaneli. Kumbuka kuwa hii si orodha kamili:

Kurejesha idhini ya kufikia vipengele

Ikiwa idhini yako ya kufikia vipengele vyovyote vya kina imezuiwa, utapokea barua pepe. Watayarishi wanaweza kurejesha idhini ya kufikia kwa kuboresha historia za chaneli au kwa kuthibitisha utambulisho wao wakitumia kitambulisho halali au video. Kumbuka kuwa uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote.

Chaneli zinazochapisha maudhui ambazo mara kwa mara zinafuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube zinaweza kuunda upya historia ya kutosha ya chaneli ndani ya miezi 2.

Ili uone hatua unazopaswa kuchukua ili ufikie vipengele vya kina, unaweza kuangalia hali yako ya sasa ya kutimiza masharti ya kupata vipengele katika Studio ya YouTube.

Ujumbe wa kawaida kuhusu hitilafu na maana yake

  • "Vipengele vya kina vya YouTube havipatikani katika akaunti hii": Hii inamaanisha kuwa umeingia katika akaunti ambayo wewe si mmiliki mkuu. Hii inaweza kutokea ikiwa umeingia katika akaunti inayosimamiwa na mzazi au umeingia katika Akaunti ya Biashara.
  • "Kagua kivinjari chako": Kivinjari chako hakioani. Hakikisha unasasisha kifaa chako ili kitumie toleo jipya zaidi la kivinjari na mfumo wa uendeshaji. 
  • "Uthibitishaji kwa kitambulisho haufanyi kazi kwenye kamera ya simu hii": Kamera yako haioani. Ingia katika akaunti ukitumia simu iliyo na kamera ya nyuma ya HD kamili ili utume kitambulisho chako.
  • "Huenda programu nyingine inatumia kamera yako. Funga programu zilizofunguliwa kisha ujaribu tena": Hii inamaanisha kuwa programu nyingine inatumia kamera yako. Funga programu zilizofunguliwa kisha ujaribu tena.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kwa nini YouTube inaomba namba yangu ya simu / uthibitishaji kwa video / kitambulisho halali?

YouTube hufunga mamilioni ya chaneli kila mwaka kutokana na maudhui na tabia zinazokiuka sera. Chaneli nyingi kati ya hizi huundwa na vikundi na watu binafsi wale wale wakitumia au kuvuka mipaka ya matumizi ya aina moja ya vipengele. Kusudi lao ni kuwadanganya, kuwalaghai au kuwatumia vibaya watazamaji, watayarishi na watangazaji. Kuthibitisha utambulisho wako ni njia mojawapo tunayotumia kukomesha matumizi mabaya na kubaini iwapo ulikiuka sera yetu hapo awali na kudhibiti maombi yanayojirudia.

Data yangu ya uthibitishaji kwa video na kitambulisho inatumikaje?

Namba ya simu

Ukichagua kuweka namba ya simu, tutaitumia ili:

  • Kukutumia namba ya kuthibitisha.

Uthibitishaji kwa kitambulisho

Ukishawasilisha kitambulisho halali (kama vile pasipoti au leseni ya udereva), tutaitumia ili kuthibitisha:

  • Tarehe yako ya kuzaliwa
  • Kuwa kitambulisho chako ni cha sasa na ni halali
  • Kuhakikisha kuwa hukusimamishwa awali kwa kukiuka sera za YouTube

Pia, itatusaidia kulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya na inaweza kuboresha mifumo yetu ya uthibitishaji.

Uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho utafutwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google ndani ya miaka 2. Kwa kawaida, hufutwa baada ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya mwaka 1 iwapo hujatumia vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta data yako ya uthibitishaji.

Uthibitishaji kwa video

Uthibitishaji kwa video ni video fupi inayoonyesha uso wa mtu. Tutatumia video hii ili itusaidie kuthibitisha:

  • Kuwa wewe ni mtu halisi
  • Kuwa umefikisha umri unaoruhusiwa kutumia huduma za Google
  • Kuwa hujasimamishwa kwa kukiuka sera za YouTube

Pia, itatusaidia kulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya na inaweza kuboresha mifumo yetu ya uthibitishaji.

Uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho utafutwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google ndani ya miaka 2. Kwa kawaida, hufutwa baada ya miezi michache ukishaunda historia ya kutosha ya chaneli au baada ya mwaka 1 iwapo hujatumia vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta data yako ya uthibitishaji.

Kufuta na kuhifadhi data

Unaweza kufuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho  wakati wowote katika Akaunti yako ya Google. Kumbuka kuwa, ukifuta uthibitishaji wowote kati ya chaguo hizi kabla ya kuimarisha historia ya chaneli yako ya YouTube, huwezi kutumia vipengele vya kina vya YouTube isipokuwa:

  •  Ukiimarisha historia ya chaneli yako ya YouTube

Au

  • Ukikamilisha tena kitambulisho na uthibitishaji kwa video

Ili kuhakikisha mtu binafsi au vikundi havikwepi vikwazo vyetu kwa kufungua akaunti mpya, tunatathmini ikiwa unaweza kuwa umekiuka sera za YouTube hapo awali na kudhibiti maombi yanayojirudia. Huenda Google ikahifadhi kitambulisho au video yako na data ya utambuzi wa sura kwa kipindi fulani ili kuidhibiti dhidi ya matumizi mabaya.

Data hii itahifadhiwa kwa muda usiozidi miaka 3 tangua mara ya mwisho ulipotumia YouTube.

Iwapo hungependa kutoa uthibitishaji kwa video au kitambulisho ili kufikia vipengele vya kina, huhitaji kufanya hivyo. Badala yake, unaweza kuunda historia ya kutosha ya chaneli. Hata hivyo, hadi wakati utakapokuwa tayari kufikia vipengele vya kina utakuwa umeunda historia ya kutosha.

Unapotumia huduma zetu, unaamini kuwa tutalinda taarifa zako. Tunafahamu kwamba huu ni wajibu mkubwa na tunajitahidi kulinda taarifa yako na kukupa udhibiti. Sera ya faragha ya Google inatumika katika kushughulikia taarifa zako kama inavyotumika katika bidhaa na vipengele vyetu vyote.

Kumbuka: Kamwe hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. 

Tayari nimetoa uthibitisho, ni kwa nini ninaombwa kuthibitisha tena?

Ili kuhakikisha kuwa tunafuata kanuni za data kwa kuwajibika, data ya uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho hufutwa kiotomatiki mara tu unapofikisha historia ya kutosha ya chaneli au huenda ikafutwa ikiwa hutatumia vipengele vya kina kwa mwaka 1. Unaweza pia kuchagua kufuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho wakati wowote katika Akaunti yako ya Google.

Ikiwa uthibitishaji wako umefutwa, utahitajika kuwa na historia ya kutosha ya chaneli au kutuma tena uthibitishaji kwa kitambulisho au video ili uendelee kutumia vipengele vya kina.

Kumbuka kuwa watayarishi wanaochagua kufikia vipengele vya kina kupitia uthibitishaji kwa kitambulisho au video bado wanapaswa kufuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube na kudumisha historia bora ya chaneli. Watayarishi wasiounda na kudumisha historia ya kutosha ya chaneli wanaweza kupoteza ufikiaji wao wa vipengele vya kina na wanaweza kurejesha idhini ya kufikia kwa kutuma tena uthibitishaji kwa kitambulisho au video.

Ninawezaje kufuta data yangu ya uthibitishaji?

Muhimu: Iwapo utafuta uthibitishaji wako kwa video au kitambulisho kabla hujaimarisha historia yako ya chaneli, utapoteza idhini ya kufikia vipengele vya kina.
  1. Ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Kwenye upande wa kushoto, bofya Taarifa binafsi.
  3. Bofya Hati ya utambulisho au Uthibitishaji kwa video.
  4. Bofya Futa Delete.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta data yako ya uthibitishaji.
Kwanini simu mahiri inahitajika? Je, siwezi tu kupakia video au picha ya kitambulisho changu?

Simu mahiri inahitajika kwa sababu inatoa ulinzi wa ziada na kufanya iwe vigumu kwa walaghai na watumaji taka kusababisha madhara.

Sijapokea namba ya kuthibitisha kwenye simu yangu. Je, kuna tatizo gani?

Unatakiwa kupokea msimbo papo hapo. Ikiwa hujapokea, unaweza kuomba utumiwe msimbo mpya. Hakikisha haukumbwi na moja ya matatizo haya ya kawaida:

  • Uwasilishaji wa SMS unaweza kuchelewa. Ucheleweshaji unaweza kutokea katika maeneo yaliyo na watu wengi au ikiwa huna mtandao thabiti. Ikiwa umesubiri kwa zaidi ya dakika kadhaa na bado hujapokea SMS yetu, jaribu njia ya kupiga simu ya sauti.
  • Iwapo tayari umethibitisha chaneli 2 ukitumia namba 1 ya simu, lazima uthibitishe namba tofauti ya simu. Ili kusaidia kuzuia matumizi mabaya, tunaweka kikomo cha idadi ya chaneli zinazoweza kuunganishwa na kila namba ya simu.
  • Baadhi ya nchi au maeneo na watoa huduma za simu hawaruhusu huduma ya kupokea SMS kutoka Google. Watoa huduma za simu wengi wanaruhusu huduma ya kupokea SMS kutoka Google. Ikiwa mtoa huduma wako haruhusu huduma ya kupokea ujumbe wa maandishi kutoka Google, unaweza kujaribu chaguo la kupigiwa simu ya sauti au utumie namba tofauti ya simu.
Uthibitishaji kwa kitambulisho changu halali umekataliwa. Ninaweza kufanya nini?

Iwapo jaribio lako la kwanza limekataliwa, utaarifiwa kwa barua pepe. Tunapendekeza ukague vidokezo kwenye barua pepe yako na uhakikishe kuwa kitambulisho chako:

Ikiwa jaribio lako la pili halikufanikiwa, unahitaji kusubiri siku 30 kabla ya kujaribu tena mojawapo ya mbinu za kuthibitisha. Unaweza pia kusubiri na kuunda historia ya chaneli badala yake.

Uthibitishaji wangu kwa video umekataliwa. Ninaweza kufanya nini?

Iwapo jaribio lako la kwanza limekataliwa, utaarifiwa kwa barua pepe. Tunapendekeza ukague vidokezo kwenye barua pepe yako na uhakikishe kuwa:.

  • Umeshikilia simu mbele ya uso wako na umeilinganisha na macho yako
  • Unarekodi katika eneo ambako kuna mwangaza wa kutosha; usiwe mwingi wala mchache zaidi
  • Unafuata vidokezo ili utekeleze kitendo, kama vile kufuata nukta au kugeuza kichwa chako
  • Ni wewe tu unayeonekana kwenye video
  • Umeunganisha kwenye mtandao wa Wi-Fi

Ikiwa jaribio lako la pili halikufanikiwa, unahitaji kusubiri siku 30 kabla ya kujaribu tena mojawapo ya mbinu za kuthibitisha. Ikiwa unafikiri uthibitishaji wako wa pili kwa video ulipaswa kuidhinishwa, unaweza kukata rufaa na kutueleza sababu. Unaweza pia kusubiri na kuunda historia ya chaneli badala yake.

Kwa nini sioni chaguo la kukamilisha uthibitishaji kwa kitambulisho au video?

Uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote. Badala yake, watayarishi wanaweza kuunda historia ya kutosha ya chaneli ili waweze kufikia vipengele vya kina. Kumbuka kuwa unaweza kuangalia hali yako ya sasa ya kutimiza masharti ya kupata vipengele katika Studio ya YouTube na pia kuona hatua unazopaswa kuchukua ili uweze kufikia vipengele vya kina.
Hali hii inafanyaje kazi kwenye chaneli zilizo na watumiaji wengi?

Iwapo una Akaunti ya Biashara:

Mmiliki mkuu pekee wa chaneli atatimiza masharti ya uthibitishaji wa utambulisho. Kulingana na hali yao ya uthibitishaji, watumiaji wote wa chaneli watakuwa na idhini ya kufikia vipengele sawa na mmiliki mkuu.

Iwapo huna Akaunti ya Biashara:

Ni mmiliki wa chaneli pekee atatimiza masharti ya kutekeleza uthibitishaji wa utambulisho. Kulingana na hali yao ya uthibitishaji, watumiaji wote wa chanlei watakuwa na idhini ya kufikia vipengele sawa na mmiliki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
18240084570250993271
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false