Pata video haraka zaidi

Unapoanza kutafuta kwenye YouTube, unaweza kupata unachotafuta kwa haraka zaidi ukitumia mapendekezo ya kiotomatiki. Mapendekezo haya yanajulikana kama utabiri wa utafutaji. Utabiri huu unatokana na hoja za utafutaji zinazohusiana na unachotafuta na yale ambayo watu wengine wametafuta tayari.

Jinsi utabiri wa utafutaji unavyotumika

YouTube hutabiri utafutaji kulingana na vigezo kama vile umaarufu au kufanana. Unapochagua utabiri, utapata matokeo yanayohusiana na hoja hiyo.

Chanzo cha utabiri wa utafutaji

  • Hoja za utafutaji unazoandika.
  • Ikiwa umeingia katika Akaunti yako ya Google na umewasha kipengele cha Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, utabiri hutokana na utafutaji uliofanya au video zinazohusiana ulizotazama awali.
  • Maudhui ambayo watu wengine wanatafuta, ikiwa ni pamoja na hoja za utafutaji zinazovuma. Hoja za utafutaji zinazovuma ni mada maarufu katika eneo lako zinazobadilika kila wakati na hazihusiani na historia ya mambo uliyotafuta.
Kumbuka kuwa, utabiri wa utafutaji huenda usionyeshwe wakati mwingine unapotafuta. Pia, si kauli za watu wengine au za YouTube kuhusu hoja zako za utafutaji.

Sababu za kutoona utabiri wa utafutaji

Usipoona utabiri wowote wa hoja ya utafutaji, huenda algoriti imegundua kuwa:

  • Hoja ya utafutaji si maarufu.
  • Hoja ya utafutaji ni mpya mno. Huenda ukahitaji kusubiri siku au wiki chache ili uone utabiri.
  • Hoja nyeti au ya matusi inahusishwa na neno fulani hivyo kizuizi kimewekwa.
  • Watumiaji wameripoti kuwa pendekezo halifai.
  • Hoja ya utafutaji inakiuka sera za YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera za kukamilisha hoja kiotomatiki.

Zima utabiri uliowekewa mapendeleo

Huenda ukaona utabiri uliowekewa mapendeleo iwe umeingia au umeondoka kwenye akaunti. Ili uzime utabiri wa utafutaji uliowekewa mapendeleo, futa historia ya mambo uliyotafuta na historia ya video ulizotazama au uzime kipengele cha Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu. Pata maelezo kuhusu kuzima Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu

Ripoti utabiri

Ingawa tunajitahidi kuzuia utabiri usiofaa, wakati mwingine huenda tukatatizika. Ikiwa unaamini kuwa utabiri unakiuka mojawapo ya Sera za kukamilisha hoja kiotomatiki, fuata hatua hizi ili uripoti kwenye Wavuti:

  1. Kwenye upau wa kutafutia, upande wa chini wa kisanduku cha utabiri, bofya Ripoti ya utabiri wa utafutaji.
  2. Toa maoni yako.
  3. Chagua Tuma.

Tutaangalia maoni yako lakini hatuondoi kiotomatiki utabiri unaoripotiwa.

Nina tatizo la kisheria kuhusu utabiri

Ili uwasilishe ombi la kuondolewa kwa maudhui ambayo unaamini yanakiuka sheria, jaza fomu hii.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11688122650698679648
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false