Kuchagua mipangilio sahihi ya mtiririko kunaweza kukusaidia kufikia hadhira sahihi na kupata mtiririko wenye ubora wa juu.
Kutumia tena mipangilio ya mtiririko
Unaweza kuanzisha mtiririko mpya kwa urahisi ukitumia mipangilio ya mtiririko uliotangulia. Mtiririko mpya utanakili metadata, mipangilio na ufunguo wa mtiririko uliotangulia. Utakuwa na nafasi ya kubadilisha mtiririko baada ya kuuanzisha. Ili uanze, chagua mtiririko wako na ubofye Tumia tena mipangilio.
Kubadilisha metadata
Chagua mipangilio hii unapotayarisha mtiririko au kwa kubofya Badilisha kwenye ukurasa wa mipangilio ya mtiririko au unaporatibu mtiririko.
Ukurasa wa maelezo
Faragha
Kwa watumiaji wa YouTube walio na umri wa miaka 13 hadi 17, mipangilio chaguomsingi ya faragha hubainishwa kuwa ya faragha. Iwapo una umri usiopungua miaka 18, mipangilio yako chaguomsingi ya faragha hubainishwa kuwa ya umma. Wote wanaotiririsha mubashara wanaweza kubadilisha mipangilio hii ili kufanya mtiririko wao mubashara uwe wa umma, wa faragha, au ambao haujaorodheshwa.
Vyanzo vya watazamaji wa Mtiririko Mubashara wa Kina
Aina
Lebo
Ratibu
Ukurasa wa uchumaji wa mapato
Ukurasa wa Usimamizi wa Haki
Ukurasa wa Kuelekezwa Moja kwa Moja
Baada ya mtiririko wako kuisha, unaweza kutuma hadhira yako kwenye Onyesho la kwanza au mtiririko mwingine mubashara. Vifuatavyo ni baadhi ya vidokezo:
- Weka mipangilio ya Onyesho lako la kwanza kabla hujaweka mipangilio ya mtiririko wako mubashara.
- Kumbuka kuambia hadhira yako kuwa mtiririko mubashara utakapoisha, wasubiri takribani sekunde 2 ili skrini zao zipakie Onyesho la kwanza.
Maoni na ukadiriaji
Mipangilio ya mtiririko
Kuongeza kionjo kwenye mtiririko wako mubashara
Changamsha hadhira yako kuhusu mtiririko wako mubashara ulioratibiwa kwa kuonyesha kionjo. Kionjo chako kitachezwa kwa watazamaji kwenye ukurasa wa kutazama kabla mtiririko mubashara haujaanza.
Vionjo vinaweza kuchezwa kwenye mitiririko iliyoratibiwa katika kichupo cha “Dhibiti” kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
- Kupakia kionjo chako kwenye kituo chako cha YouTube sawa na unavyopakia video ya kawaida.
- Nenda kwenye Studio ya YouTube Tiririsha Mubashara.
- Tayarisha mtiririko mubashara ulioratibiwa au uchague mtiririko ulioratibiwa kwenye kichupo cha “Dhibiti”.
- Kwenye upande wa juu kulia, bofya Badilisha.
- Bofya Weka mapendeleo.
- Chini ya “Kionjo,” bofya Weka.
- Chagua video yako ya kionjo.
- Bofya Hifadhi.
Masharti ya Kujiunga
Kipengele hiki kinapatikana kwa watayarishi walio na zaidi ya watu 1,000 wanaofuatilia, wasio na maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Masharti
- Aina ya video: Tumia aina yoyote ya video inayoruhusiwa kwenye YouTube.
- Urefu wa video: sekunde 15 – dakika 3.
- Uwiano na ubora: Tunapendekeza uwiano na ubora ule ule uliotumia kwenye video ya Onyesho la kwanza.
- Haki za sauti na video: Hakikisha kuwa kionjo hakikiuki haki za maudhui mengine.
Ufunguo wa mtiririko
Funguo za mtiririko ni sawa na nenosiri na anwani ya mtiririko wako wa YouTube. Huwa zinaelekeza programu ya kusimba mahali pa kutuma mipasho yako na kuruhusu YouTube iikubali. Utatunga ufunguo wa mtiririko kwenye YouTube, kisha uuweke kwenye programu yako ya kusimba.
Ili utumie tena ufunguo sawa wa mtiririko, tunga ufunguo maalum wa mtiririko. Chini ya “Chagua ufunguo wa mtiririko,” bofya Tunga ufunguo mpya wa mtiririko. Weka mipangilio unayopendelea na ubofye Tunga. Ufunguo wako wa mtiririko utaonekana katika orodha ya ufunguo wa mtiririko.
URL ya mtiririko
Muda wa kusubiri utiririshaji
Kuwasha Kirekodi Video cha Dijitali (DVR)
Video inayozunguka digrii 360
Unaweza kutiririsha katika mwonekano wa digrii 360 ukitumia Matukio ya Moja kwa Moja. Video za mwonekano wa digrii 360 hukusaidia kuweka hali ya mwonekano wa kina. Kwa wakati huu, YouTube inaruhusu mwonekano wa duaradufu pekee kwa video zinazozunguka digrii 360. Vifuatavyo ni baadhi ya vidokezo:
- Chagua kasi ya biti na ubora wa juu unaoruhusiwa unaoweza kutumia kutiririsha.
- Ubora wa 2160p au 1440p unapendelewa kwa video ya moja kwa moja inayozunguka digrii 360.
- Chagua uwiano wa 16:9 ili upate ubora wa video wa juu zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu uwiano.
YouTube huruhusu uingizaji wa mtiririko mubashara na uchezaji wa video za mwonekano wa digrii 360 kwenye kompyuta katika vivinjari vya Chrome, Firefox, MS Edge na Opera. Uchezaji wa digrii 360 pia unaruhusiwa katika programu za YouTube na YouTube Gaming.