Sera ya orodha za video

Orodha za video ni njia bora ya kujumuisha video ambazo jumuiya yako ingependa kutazama kama mfululizo. Tunajua kuwa mara nyingi si kimakusudi, lakini kuna mara ambapo orodha za video zina maudhui ambayo hayaruhusiwi kwenye mfumo na yanaweza kudhuru jumuiya yetu. Hii ina maana kuwa orodha za video ambazo zinakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu haziruhusiwi kwenye YouTube.

Huu ni mfano rahisi wa kufikiria hali hii: iwapo ungejumuisha video zote zilizo kwenye orodha za video kuwa video moja na video hiyo ikiuke Mwongozo wa Jumuiya yetu, basi orodha hiyo ya video inaweza kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu pia.

Ikiwa utapata maudhui yanayokiuka sera hii, tafadhali yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya yetu yanapatikana hapa. Ikiwa utapata video nyingi, maoni au chaneli yote ya mtayarishi ambayo ungependa kuripoti, tembelea zana yetu ya kupiga ripoti.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Iwapo unatayarisha orodha za video 

Usichapishe orodha za video kwenye YouTube iwapo zinalingana na maelezo yaliyo hapa chini.

  • Orodha za video zilizo na vijipicha, mada au maelezo ambayo yanakiuka mwongozo wetu wa jumuiya, kama vile zile ambazo ni za ponografia, au ambazo zina picha zinazolenga kugutusha au kuchukiza.
  • Orodha za video zilizo na mada au maelezo ambayo yanapotosha watazamaji ili wafirikie kuwa wanakaribia kutazama video tofauti na zilizo kwenye orodha hiyo ya video.
  • Orodha za video zenye video ambazo hazikiuki kimahususi sera zetu, lakini zimekusanywa katika njia ambayo inakiuka mwongozo wetu. Maudhui haya yanajumuisha haya na mengineyo: 
    • Maudhui ya kielimu ambayo yanaangazia mada za uchi au ngono kwa madhumuni ya kuchochea ngono 
    • Maudhui yasiyo ya ngono lakini yanaangazia sehemu mahususi za mwili au shughuli za kuchochea ngono 
    • Video za hali halisi zenye unyanyasaji uliokithiri kwa madhumuni ya kugutusha au kusifu
  • Orodha za kucheza zilizo na video nyingi ambazo zimeoondolewa kwa kukiuka mwongozo wetu. Iwapo utatambua kuwa video nyingi katika orodha za kucheza za umma zimeondolewa au kufutwa, tafadhali chukua muda uondoe video hizo kwenye orodha zako za video pia. Iwapo utatambua kuwa baadhi ya video katika orodha yako ya video ya umma zinakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, tafadhali ziripoti na uziondoe kwenye orodha yako ya video.
  • Orodha za video ambazo zinaonyesha unyanyasaji wa watoto kihisia, kingono au kimwili.

Tafadhali kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Orodha ya video yenye video ya habari kuhusu bomu za angani zikiambatana na mada kama vile “Bomu bora”. 
  • Orodha ya video yenye mada ambayo inahimiza ubaguzi wa watu wenye ulemavu wa kimawazo.
  • Orodha ya video ambayo inachapisha taarifa inayomtambulisha mtu isiyo ya umma kama vile namba ya simu, anwani ya nyumbani au anwani ya barua pepe kwa sababu dhahiri ya kuelekeza watumiaji au mtazamo mbaya upande wake.
  • Orodha ya kucheza ambayo inakusanya video za mizaha ya kutisha au hatari, kama vile orodha ya video ya ujambazi au uvamizi wa nyumbani ambao si wa kweli.
  • Orodha ya video yenye video zinazoangazia watoto zikiwa na mada kama vile "kuvutia kingono".

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3340570867637575108
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false