- Kukagua ili ubaini kuwepo kwa programu hasidi
- Kutumia ufunguo wa siri kwa Uthibitishaji wa Hatua Mbili
- Kuanzisha mpango wa mbinu za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti
Jinsi ya Kuzuia Utekaji na Kulinda Chaneli Yako ya YouTube
1. Kukagua ili ubaini kuwepo kwa programu hasidi
Programu hasidi ni programu inayoweza kufikia akaunti yako, kupeleleza shughuli, kufuta faili na kubadilisha ufikiaji wako wa mtandao. Kwa kawaida programu hasidi hupenya kwenye vifaa vyako kama faili zilizobanwa na zinazolindwa kwa nenosiri zinazoishia kwa .scr au .exe.
Chanzo cha programu hasidi kinaweza kuwa:
- Viungo vya kutiliwa shaka: Kubofya kiungo kwenye barua pepe taka au ya ufadhili wa kibiashara au udhamini bandia
- Upakuaji wa programu zilizoathiriwa: Kupakua programu kutoka kwenye chanzo kisichoaminika
- Masasisho bandia ya programu: Kuweka sasisho bandia la programu lenye programu hasidi
Tunapendekeza
- Utumie programu kingavirusi
- Uwashe Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa kwenye Google Chrome
| Washa Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa |
Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa kikikagua kiotomatiki faili iliyopakuliwa ili kubaini kuwepo kwa programu hasidi |
Maelezo zaidi kuhusu Kipengele cha Kuvinjari Salama KilichoboreshwaKwa sababu programu kingavirusi huenda isikague baadhi ya faili zilizosimbwa kwa njia fiche, tunapendekeza pia uwashe Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa ili faili zote zinazopakuliwa kwenye Google Chrome zikaguliwe ili kubaini kuwepo kwa programu hasidi. Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa hufanya ukaguzi wa usalama katika muda halisi ili kudumisha usalama wako kwenye bidhaa zote za Google unapotumia Google Chrome. |
2. Kutumia ufunguo wa siri kwa Uthibitishaji wa hatua mbili
Manenosiri yaliyoibwa ni mojawapo ya njia za kawaida ambazo akaunti huvamiwa. Ukishaunda nenosiri thabiti, unaweza kuwasha kipengele cha Uthibitishaji wa Hatua Mbili (pia unajulikana kama 2SV au uthibitishaji wa hatua mbili), ambao huongeza hatua ya pili ya uthibitishaji ili upate kiwango kingine cha ulinzi.
Unaweza kuchagua miongoni mwa aina tofauti za hatua za uthibitishaji, kila hatua ikiwa na kiwango tofauti cha ulinzi:
- Funguo za siri: Uthibitishaji wa kifaa kama vile alama ya kidole, uchanganuzi wa uso au mbinu ya kufunga skrini ya simu. Funguo za siri hukupa ulinzi thabiti dhidi ya wizi wa data binafsi.
- Funguo za usalama: Kifaa halisi cha uthibitishaji kinachokupa ulinzi thabiti dhidi ya wizi wa data binafsi.
- Vidokezo vya Google: Arifa ya simu ambayo ni salama zaidi kuliko namba za kuthibitisha za ujumbe wa maandishi.
- Kithibitishaji cha Google: Programu inayofanya kazi nje ya mtandao na hutayarisha namba za uthibitishaji wa mara moja.
- Uthibitishaji kwa namba za simu: Aina salama kidogo ya namba za kuthibitisha zinazotumwa kwa ujumbe wa maandishi au kupigiwa simu.
- Namba mbadala za uthibitishaji: Aina salama kidogo ya namba za kuthibitisha zinazopakuliwa na kuchapishwa.
Tunapendekeza
Ili upate ulinzi thabiti dhidi ya hatari kama vile wizi wa data binafsi, weka mipangilio ya Uthibitishaji wa Hatua Mbili kisha uchague ufunguo wa siri kama njia yako ya pili ya uthibitishaji.
Kuweka mipangilio ya Uthibitishaji wa Hatua Mbili kwa kutumia ufunguo wa siri
3. Kuanzisha mpango wa mbinu za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti
Ili uhakikishe kuwa unaweza kurejea katika Akaunti yako ya Google iwapo huwezi kuingia katika akaunti, unaweza kuweka chaguo za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti, kama vile namba ya simu na anwani yako ya barua pepe.
Chaguo za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti zinaweza kutumika:
- Kuzuia mtu asitumie akaunti yako bila ruhusa yako
- Kukuarifu ikiwa kuna shughuli ya kutiliwa shaka kwenye akaunti yako
- Kurejesha akaunti yako ikiwa umepoteza uwezo wa kuifikia au umesahau nenosiri lako
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi chaguo za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti zinavyoweza kutumiwa kudumisha usalama wa akaunti yako.
Tunapendekeza
Uweke chaguo za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti, kama vile namba ya simu na anwani yako ya barua pepe, kwenye akaunti yako ili uirejeshe kwa haraka iwapo itahitajika.
Je, umepoteza uwezo wa kufikia Akaunti yako ya Google? Kurejesha Akaunti yako ya Google.