Pata maelezo kuhusu mipangilio ya maoni

Unaweza kuchagua kuzuia baadhi ya maoni ili yakaguliwe kabla hayajaonyeshwa kwenye video au kituo chako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya maoni.

Mipangilio ya maoni ya video

Unaweza kuchagua kuwasha, kusitisha au kuzima kipengele cha maoni kwenye video mahususi. Unapowasha kipengele cha maoni, unaweza kuamua ni yapi, ikiwa yapo, yatazuiwa ili yakaguliwe.

Kuwasha

Unapochagua Kuwasha kipengele cha maoni, pia utakuwa na chaguo la kuteua ikiwa yatazuiwa ili yakaguliwe. Unaweza kugusa menyu kunjuzi ya Udhibiti wa maoni ili uangalie chaguo zako: 

  • Kutozuia: Usizuie maoni yoyote. 
  • Uzuiaji wa kawaida: Zuia maoni ambayo huenda hayafai. 
  • Uzuiaji Madhubuti: Zuia aina nyingi za maoni ambayo huenda hayafai. 
  • Uzuiaji wa maoni yote: Zuia maoni yote.
Kidokezo: Ikiwa kuna maneno au sentensi ambazo unataka kuzuia ili zikaguliwe, ziweke kwenye orodha yako ya maneno yaliyozuiwa.

Maoni yaliyozuiwa ili yakaguliwe:

  • Huhifadhiwa kwenye Studio ya YouTube kwa hadi siku 60.
  • Hayaonekani kwa umma, isipokuwa ukiyaidhinisha.
  • Hupatikana ili yakaguliwe katika lugha zaidi ya 100.
Kusitisha

Unapoteua chaguo la Sitisha, utahifadhi maoni yako yaliyopo, lakini hutapokea tena mengine kwenye video hiyo hadi utakapowasha tena kipengele cha maoni. 

Unaweza kuchagua kusitisha kipengele cha maoni kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano, huenda ukahitaji muda zaidi wa kukagua ongezeko la ghafla la maoni kwenye video, bila kupokea maoni mapya. Ikiwa ungependa kuanza kupokea maoni mapya tena, unaweza Kuwasha kipengele cha maoni wakati wowote.

Kuzima 

Unapochagua Kuzima kipengele cha maoni, watazamaji hawawezi kutoa maoni kwenye video. Wataona ujumbe unaowafahamisha kwamba kipengele cha maoni kimezimwa.

Mipangilio ya maoni ya kiwango cha chaneli

Watumiaji waliofichwa

Unaweza kuchagua kuficha maoni ya watoa maoni mahususi kwenye video zote katika kituo chako.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuficha maoni kutoka kituo mahususi.
Kumbuka: Watumiaji waliofichwa pia hawataweza kutayarisha klipu za video zako na mtiririko mubashara. Pata maelezo zaidi.

Mtumiaji aliyeidhinishwa

Maoni ya watumiaji hawa huchapishwa kiotomatiki na hayatachujwa ili kubaini viungo vilivyozuiwa, maneno yaliyozuiwa au maudhui ambayo huenda hayafai. Watumiaji hawa pia wataweza kutuma ujumbe katika gumzo la moja kwa moja wakati hali ya washiriki kutuma maoni mubashara imewashwa.
Maneno yaliyozuiwa
Unaweza kuweka orodha ya maneno na sentensi ambazo hutaki zionyeshwe katika maoni kwenye orodha zako za maneno yaliyozuiwa.
Maoni yaliyo na maneno haya au yanayolingana kwa karibu nayo yanaweza kuzuiwa ili yakaguliwe kwa hadi siku 60, isipokuwa kama yametolewa na mtu aliye kwenye orodha ya watumiaji uliowaidhinisha. Ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ulio na maneno haya au unaolingana kwa karibu nayo pia utazuiwa.
Unaweza kukagua na kuidhinisha maoni yenye maneno yaliyozuiwa kwenye ukurasa wako wa Maoni, katika kichupo cha “Yaliyozuiwa ili yakaguliwe”.
Ili uweke maneno kwenye orodha zako za maneno yaliyozuiwa:
  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Katika upande wa kushoto, bofya Mipangilio and then Jumuiya.
  3. Kwenye kichupo cha "Vichujio vya Kiotomatiki", sogeza hadi "Maneno yaliyozuiwa."
  4. Weka maneno na sentensi zikiwa zimetenganishwa kwa koma.
  5. Chagua HIFADHI.
Kumbuka: Maneno yaliyozuiwa pia hayataweza kutumiwa wakati wa kutayarisha klipu za video zako na mtiririko mubashara. Pata maelezo zaidi.
Kuzuia maoni yaliyo na viungo
Unaweza kuzuia maoni yaliyo na URL ili yakaguliwe. Utaratibu wa kufanya hivyo:
  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Katika upande wa kushoto, bofya Mipangilio and then Jumuiya.
  3. Kwenye kichupo cha "Vichujio vya Kiotomatiki", chagua Zuia viungo.
Maoni yenye viungo hayazuiwi ikiwa yamechapishwa nawe, wadhibiti au watumiaji uliowaidhinisha.
Ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ulio na URL utazuiwa pia.
Unaweza kukagua na kuidhinisha maoni yenye alama za reli na viungo kwenye ukurasa wako wa Maoni, katika kichupo cha “Yaliyozuiwa ili yakaguliwe” kwa hadi siku 60.

Mipangilio chaguomsingi ya maoni

Unaweza kutumia mipangilio sawa ya maoni kwenye video zote mpya unazopakia. Hatua ya kubadilisha mipangilio yako chaguomsingi kwenye video mpya unazopakia haitaatiri video zilizopo.
Unaweza kuchagua mipangilio tofauti ya maoni kwenye video mahususi baada ya kuzipakia. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio yako chaguomsingi ya maoni kwenye video mpya.

Mipangilio ya maoni kwenye ukurasa wa kwanza wa kituo

Unaweza kubadilisha mipangilio yako kwa ajili ya maoni mapya kwenye kichupo cha Jumuiya cha kituo chako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya maoni.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu mipangilio ya maoni

Ninaweza kuzuia maneno, viungo au watumiaji fulani kwenye video moja mahususi?

Hapana. Mipangilio ya watumiaji waliofichwa, maneno yaliyozuiwa na kuzuia viungo hutumiwa kiotomatiki kwenye video zote na kwenye ukurasa wa kwanza wa kituo chako. Mabadiliko unayofanya kwenye mipangilio yako yanaweza pia kutumika kwenye video mpya na zilizopo.
Kumbuka: Mabadiliko unayofanya kwenye mipangilio yako ya maoni hutumika tu kwenye video mpya.

Ninaweza kukagua maoni kutoka kwa watumiaji waliofichwa?

Hapana, Maoni kutoka kwa watumiaji waliofichwa hayaonyeshwi kwenye Studio ya YouTube.

Ninaweza kukagua maoni yaliyozuiwa kutokana na viungo au maneno mahususi?

Ndiyo. Unaweza kukagua na kuidhinisha maoni yenye maneno yaliyozuiwa na viungo kwenye ukurasa wako wa Maoni, katika kichupo cha “Yaliyozuiwa ili yakaguliwe” kwa hadi siku 60.

Nikizima kipengele cha maoni kisha nikiwashe tena, maoni yangu ya zamani yatarejeshwa?

Ndiyo. Ukizima kipengele cha maoni kisha ukiwashe tena, maoni yaliyopo yataonekana tena.
Ukizima kipengele cha maoni, maoni yaliyopo hayawezi kuonekana kwenye ukurasa wa kutazama au kwenye Studio ya YouTube.

Je, nikibadilisha mipangilio yangu, maoni yaliyopo na yajayo yataathiriwa?

Mabadiliko kwenye mipangilio ya kiwango cha chaneli, mipangilio ya kiwango cha video na maneno yaliyozuiwa, watumiaji waliofichwa na viungo vilivyozuiwa, yote yatatumika katika maoni yajayo. 

Maoni yaliyopo yataathiriwa tu ikiwa:

  • Utazima kipengele cha maoni kwenye video. Kikizimwa, hutaweza kuona maoni yaliyopo hadi utakapokiwasha tena. 
  • Utamficha mtumiaji. Ukimficha mtumiaji, maoni aliyotoa hayataonekana kwenye video zako zozote.

Ni maoni ya aina gani yanayozuiwa ili yakaguliwe katika hali ya Uzuiaji wa Kawaida na Uzuiaji Madhubuti?

Hatua ya kuchagua udhibiti wa Kawaida wa maoni itazuia maoni kwenye Studio ya YouTube ambayo yanaweza kuwa taka, yanayojitangaza, yasiyoeleweka au huenda vinginevyo hayafai. Maoni haya yatachapishwa tu ikiwa utayaidhinisha. 

Ukihitaji kiwango cha juu cha ulinzi kwenye chaneli yako, hatua ya kuchagua udhibiti Madhubuti wa maoni itaongeza idadi ya maoni yaliyozuiwa ili yakaguliwe. 

Kwa kuwa mipangilio hii hutumia AI kutambua maoni yanayotakiwa kuzuiwa, huenda isiwe sahihi kila wakati. Wamiliki wa chaneli wanaweza kuchagua kupuuza, kuondoa au kuidhinisha maoni yanayoonekana kwenye video zao.

Unaweza kutoa maoni moja kwa moja kwenye bidhaa unapokagua maoni katika Studio ya YouTube kwa kuchagua Tuma maoni.

Huenda usahihi na idadi ya maoni yanayotambuliwa na mipangilio hii vikabadilika tunapojitahidi kuboresha mifumo yetu kadiri muda unavyosonga.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16054244222110802538
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false