Kuangalia arifa za wanaofuatilia chaneli

Watayarishi mara nyingi hujiuliza ni vipi arifa huathiri mara ambazo video zao hutazamwa. Unaweza kutumia kadi ya "Arifa za kengele za wanaofuatilia" na "Arifa za Kengele zilizotumwa" kwenye Studio ya YouTube ili upate maelezo kuhusu athari za arifa. Kadi hizi zitaonekana kiotomatiki ukiwa na wafuatiliaji wa kutosha wanaoweza kufikiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu chaguo za arifa kwenye YouTube.

Were Notifications Sent to My Subscribers?

Kuangalia vipimo vya arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Chagua Hadhira.
  4. Tafuta kadi ya “Arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli”.

Kupata maelezo kuhusu vipimo vya arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli

Kadi ya "Arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli" hukupa wazo la asilimia ya wafuatiliaji wa chaneli yako ambao wanapokea arifa kutoka kwenye chaneli yako ikiwa ni pamoja na: arifa za video mpya unazopakia, maonyesho ya kwanza na mitiririko mubashara.

Wafuatiliaji waliowasha kipengele cha “Arifa zote” za chaneli yako: Kipimo cha “Wafuatiliaji waliowasha “Arifa zote” za chaneli yako” kinawakilisha asilimia ya wafuatiliaji wa chaneli yako ambao wamechagua kupokea arifa zote.

Wafuatiliaji waliowasha kipengele cha “Arifa zote” za chaneli yako na kuruhusu arifa kutoka YouTube: Kipimo cha Wafuatiliaji waliowasha “Arifa zote” za chaneli yako na kuruhusu arifa kutoka YouTube hukueleza ni asilimia ngapi ya wafuatiliaji wa chaneli waliowasha arifa zote za chaneli yako. Wafuatiliaji hawa pia wameruhusu arifa kwenye vifaa na Akaunti zao za Google.

Wafuatiliaji wakibofya aikoni ya kengele, lakini wazime arifa za YouTube kwenye akaunti au programu yao ya kifaa cha mkononi, hawatahesabiwa katika kipimo hiki. Wafuatiliaji ambao "wameruhusu arifa za YouTube" wameingia katika akaunti na wanaweza kupokea arifa kwenye angalau kifaa kimoja. Wafuatiliaji hawa wamewasha arifa za akaunti:

  • Kwenye kompyuta katika Mipangilio kisha Arifa kisha Chaneli unazofuatiliia AU
  • Kwenye kifaa cha mkononi katika Mipangilio kisha Arifa kisha Chaneli unazofuatilia

na pia wameruhusu arifa za YouTube kwenye angalau kifaa kimoja:

  • Kwenye kompyuta, washa Mipangilio kisha Arifa kisha Arifa za kompyuta
  • Kwenye vifaa vya mkononi, hakikisha kuwa arifa za programu ya YouTube zimeruhusiwa katika mipangilio ya kifaa chako

Kuangalia vipimo vya arifa za kengele zilizotumwa

Kadi ya "Arifa za Kengele zilizotumwa" huonekana kiotomatiki kwenye kichupo cha Ufikiaji cha Takwimu za YouTube unapokuwa na wafuatiliaji wa kutosha. Kadi inapatikana kwenye video mahususi.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya jina au kijipicha cha video.
  4. Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu kisha Ufikiaji.
  5. Tafuta kadi ya "Arifa za kengele zilizotumwa".

Kupata maelezo kuhusu vipimo vya arifa za kengele zilizotumwa

  • Arifa za kengele zilizotumwa: Idadi ya arifa za kengele zilizotumwa kwa wanaofuatilia chaneli ambao wanapokea arifa zote kutoka kwenye chaneli yako na wamewasha arifa za YouTube kwenye akaunti na kifaa chao.
  • Asilimia ya mibofyo (CTR) ya Arifa: Asilimia ya watazamaji waliobofya arifa ya kengele waliopata kuhusu video yako.
  • Utazamaji uliotokana na arifa za kengele: Utazamaji uliopata kutoka kwa watazamaji ambao walibofya arifa ya kengele na kutazama video yako papo hapo. Namba hii haijumuishi watazamaji walioona arifa yako ya kengele na kutazama video yako baadaye. Unaweza kupata uainishaji wa utazamaji uliotokana na arifa za programu ikilinganishwa na utazamaji uliotokana na arifa kwa barua pepe katika Ripoti yako ya ufikiaji.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli

Ni nini maana ya "amewasha "Arifa zote" za chaneli yako"?

Kuna aina kadhaa tofauti za kengele ili kuwasaidia watazamaji waelewe aina tofauti za arifa za YouTube:

  •  Zote: Wanaofuatilia chaneli watapata arifa zote kutoka kwenye chaneli yako, isipokuwa arifa zinazozidi vikomo vya kila siku.
  • Zilizowekewa mapendeleo: Wanaofuatilia chaneli watapata tu arifa zilizowekewa mapendeleo kutoka kwenye chaneli yako.
  • Hakuna: Wanaofuatilia chaneli wataona aina hii ya kengele iwapo hawawezi kupokea arifa kutoka kwa chaneli yako kutokana na mipangilio ya kifaa chao.

Kipimo cha Wafuatiliaji waliowasha "Arifa zote za chaneli yako" hakijumuishi wafuatiliaji waliochagua kupokea arifa zilizowekewa mapendeleo au wale waliozima arifa kutoka kwenye chaneli yako katika kidhibiti cha Chaneli wanazofuatilia au mipangilio ya Chaneli. Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio inayoathiri arifa.

Je, nitafanyaje ili watazamaji wangu wafuatilie arifa zote kutoka kwenye chaneli yangu?

Baadhi ya watazamaji hawatataka kupata arifa zote kutoka kwa kila chaneli wanayofuatilia. Kwa wengine, arifa zote zinaweza kuwa nyingi kupita kiasi na zinaweza kusababisha mtazamaji azime arifa kabisa.

Wahimize wanaofuatilia chaneli yako wachague kiwango cha arifa kinachowafaa. Iwapo una watazamaji wanaotaka kupata arifa zote, lakini wanatatizika kuzipata, watumie kitatuzi cha arifa.

Niko chini ya kiwango cha "Kawaida kwenye YouTube". Je, kuna tatizo lolote?

Wafuatiliaji waliowasha "Arifa zote" za chaneli yako

Chaneli nyingi haziko katika kiwango hiki lakini bado zinafanya vizuri. Arifa ni mojawapo ya vyanzo vingi vya watazamaji (kwa mfano: sehemu ya Inayofuata, Mwanzo au utafutaji). Chaneli mbalimbali zitapata asilimia tofauti ya watazamaji kutoka vyanzo tofauti vya watazamaji.

Kuna vigezo kadhaa vinavyoathiri iwapo mtu anayefuatilia chaneli anataka kupokea arifa zote za chaneli kila wakati. Chaguo la arifa la mtu anayefuatilia chaneli linaweza kuathiriwa na mambo kama vile mara ambazo unapakia video, mada za video au chaneli zingine anazofuatilia.

Wafuatiliaji waliowasha "Arifa zote" za chaneli yako na kuruhusu arifa za YouTube

Iwapo uko katika kiwango cha kawaida cha wafuatiliaji waliowasha arifa zote za chaneli yako, lakini chini ya kiwango cha arifa zilizowashwa, zingatia kuwaomba watazamaji watumie kitatuzi cha arifa. Watazamaji hawa walionyesha nia ya kupata arifa zote kwa kubofya aikoni ya kengele. Huenda wasijue kuwa hawawezi kupata arifa.

Je, ninaweza kuona vipimo vyangu vya arifa za wanaofuatilia chaneli kwa vipindi vya muda uliopita?

Kadi ya Arifa za kengele za wanaofuatilia chaneli huonyesha vipimo vya sasa pekee. Thamani za kihistoria hazipatikani.

Nikipata wafuatiliaji wapya wa chaneli, je, vipimo vya watu wanaofuatilia chaneli yangu vitaongezeka mara moja?

Vipimo vya watu wanaofuatilia chaneli husasishwa kila siku, lakini vinaweza kucheleweshwa kwa siku 2. Ukichapisha video Jumatatu na upate wafuatiliaji wapya, wataonekana katika vipimo vyako Jumatano.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu arifa za kengele zilizotumwa

Je, ninapaswa kutumia vipi kadi ya "Arifa za kengele zilizotumwa"?

"Arifa za kengele zilizotumwa" hufanya kazi pamoja na kadi ya "Arifa za kengele kwa wanaofuatilia chaneli":
  • Kadi ya "Arifa za kengele kwa wanaofuatilia chaneli" huonyesha ni sehemu gani ya watu wanaofuatilia chaneli yako walibofya kengele  ili wapate arifa zote kutoka kwa chaneli yako yote. Inaonyesha pia ni wangapi kati ya watu wanaofuatilia chaneli wanatimiza masharti ya kupokea arifa, kulingana na mipangilio ya kifaa na akaunti zao.
  • Kadi ya "Arifa za kengele zilizotumwa" huonyesha ni watazamaji wangapi walipata arifa yako ya kengele, wakaibofya na kutazama video yako. Kadi hii pia inaonyesha idadi ya wafuatiliaji uliokuwa nao wakati wa kuchapisha video yako ambao wanatimiza masharti ya kupokea arifa ya kengele.

Je, asilimia ya mibofyo (CTR) ya arifa zangu inatofautiana vipi na asilimia ya mibofyo (CTR) ya kijipicha changu?

Asilimia ya mibofyo (CTR) ya arifa zako huwakilisha idadi ya watazamaji walioona arifa ya kengele ya video yako na wakaibofya. Asilimia ya mibofyo (CTR) ya kijipicha chako inawakilisha idadi ya watazamaji walioona kijipicha cha video yako kwenye YouTube na wakakibofya. Pata maelezo zaidi kuhusu maonyesho na asilimia yako ya mibofyo (CTR).

Ni kwa nini asilimia ya mibofyo (CTR) ya arifa zangu iko chini kuliko asilimia ya mibofyo (CTR) ya maonyesho yangu?

Ni kawaida kwa asilimia ya mibofyo (CTR) ya arifa zako kuwa chini kuliko asilimia ya mibofyo (CTR) ya maonyesho yako.
Watu hupata arifa siku nzima, lakini hawawezi kutazama video. Huenda wako kazini au wanapika chakula cha jioni. Asilimia ya mibofyo (CTR) ya maonyesho yako hupimwa kulingana na shughuli kwenye YouTube. Inawakilisha tabia kutoka kwa watazamaji wanaotafuta kitu cha kutazama kwenye YouTube, si watazamaji wanaoendelea na shughuli zao za kila siku.
Je, ni kwa nini arifa zangu zote hazikutumwa?
Zifuatazo ni sababu za kawaida za kipimo chako cha "Arifa za kengele zilizotumwa" kuwa chini ya asilimia 100:
  • Chaneli yako tayari imetuma idadi ya juu ya arifa 3 za video inayoruhusiwa katika kipindi cha saa 24.
  • Umechapisha zaidi ya video 3 katika kipindi cha muda mfupi.
  • Idadi ya wanaofuatilia chaneli yako ilibadilika kwa kiwango kikubwa katika saa 24 zilizopita. Pata maelezo zaidi.
  • Ulibadilisha mipangilio ya faragha ya video yako kabla ya arifa zote kutumwa.
  • Umeruka arifa za video hii.
Je, mabadiliko katika idadi ya wanaofuatilia chaneli yangu yanaathiri vipi asilimia yangu ya arifa za kengele zinazotumwa?
Ni kawaida kwa idadi ya wanaofuatilia chaneli yako kubadilika mara kwa mara. Iwapo kwa sababu fulani idadi ya wanaofuatilia chaneli yako itabadilika kwa kiasi kikubwa punde tu kabla ya kuchapisha video, huenda ukaona kipimo cha chini ya asilimia 100 cha arifa za kengele zilizotumwa.
Katika hali hizi, bado tutawaarifu watu wote wanaofuatilia chaneli ambao wanatimiza masharti, lakini kadi inaweza kuonyesha chini ya asilimia 100 kutokana na kucheleweshwa kwa ripoti.

Niko chini ya kiwango cha "Kawaida kwenye YouTube" cha asilimia ya mibofyo (CTR) ya arifa. Je, kuna tatizo lolote?

Kuna mambo mengi yanayoathiri iwapo mtu anayefuatilia chaneli atabofya ili afungue arifa. Huenda watazamaji wasibofye arifa kulingana na wakati wa siku, wanachofanya na kadhalika.
Chaneli nyingi haziko katika kiwango hiki lakini bado zinafanya vizuri. Arifa ni mojawapo tu ya vyanzo vingi vya watazamaji. Vyanzo vingine ni pamoja na sehemu ya Inayofuata, Mwanzo, utafutaji, vyanzo vya nje na Mipasho ya chaneli unazofuatilia. Chaneli mbalimbali hupata asilimia tofauti za watazamaji kutoka kwenye vyanzo tofauti vya watazamaji.

Je, ninaweza kuangalia kadi ya "Arifa za kengele zilizotumwa" kwa vipindi vya muda uliopita?

Thamani za kihistoria hazipatikani kwenye kadi ya "Arifa za kengele zilizotumwa". Ukibadilisha kipindi katika Takwimu za YouTube, data iliyo kwenye kadi haitabadilika.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1495837128619539595
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false