Kupata muhtasari kuhusu utendaji wa chaneli

Kichupo cha Muhtasari katika Takwimu za YouTube kinakupa muhtasari wa kiwango cha juu kuhusu utendaji wa chaneli na video zako kwenye YouTube. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha mara ambazo maudhui yako yametazamwa, muda wa kutazama, wanaofuatilia na mapato yanayokadiriwa (iwapo umejiunga katika Mpango wa Washirika wa YouTube). 
 
Kumbuka: Huenda baadhi ya ripoti zisipatikane kwenye vifaa vya mikononi.

Angalia ripoti zako za muhtasari

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Kichupo cha Muhtasari kitafunguka kwa chaguomsingi. Utaona aikoni kwenye kadi ya vipimo muhimu ya kuashiria wakati ulichapisha video, kama vile mtiririko mubashara .

Kumbuka: Huenda ukaona ripoti za muhtasari zilizowekewa mapendeleo zinazoonyesha ulinganishaji wa utendaji wako wa kawaida. Maarifa haya yatafafanua kwa nini huenda mara ambazo chaneli yako imetazamwa zimeongezeka au kupungua kuliko kawaida.

Maudhui mapya zaidi

Ripoti hii inakupa muhtasari ya mara ambazo video yako imetazamwa hivi karibuni. Ripoti hii pia inakupa maelezo kuhusu asilimia ya mibofyo kwenye maonyesho na wastani wa kipindi cha kutazama.

Mseto maarufu

Ripoti hii inaonyesha maudhui yako ambayo yametumika kutayarisha Video Fupi. Ripoti hii pia huonyesha idadi ya mara ambazo maudhui yako yalitumika kuandaa miseto na idadi ya utazamaji wa miseto.

Maudhui maarufu

Ripoti ya video maarufu huangazia video zako zilizo maarufu zaidi. Kwa chaguomsingi, ripoti hii huonyesha video maarufu kwa kutazamwa.

Muda Halisi

Ripoti ya Muda Halisi inakupa maarifa ya mapema kuhusu utendaji wa video ulizochapisha hivi majuzi. Ripoti hii pia inakupa maelezo kuhusu video zako maarufu na idadi ya wanaofuatilia. Unaweza pia kuangalia ripoti ya takwimu iliyopanuliwa ili ulinganishe utendaji wa dakika 60 na wa saa 48.

Vipimo unavyopaswa kujua

Mara za kutazamwa

Idadi halali ya mara ambazo vituo na video zako zilitazamwa.

Muda wa kutazama (saa)

Muda ambao watazamaji wametazama video yako.

Wanaofuatilia

Idadi ya watazamaji ambao wanafuatilia kituo chako.

Mapato yanayokadiriwa

Jumla ya mapato yanayokadiriwa (mapato halisi) kutoka kwa miamala na matangazo yanayouzwa na Google katika kipindi na eneo lililochaguliwa.

Wastani wa kipindi cha kutazama

Makadirio ya wastani wa dakika zilizotazamwa kwa kila tukio la kutazama katika kipindi na video uliyochagua.

Maonyesho

Mara ambazo vijipicha vyako vilionyeshwa kwa watazamaji kwenye YouTube kupitia maonyesho yaliyohesabiwa.

Asilimia ya mibofyo kwenye maonyesho

Mara ambazo watazamaji walitazama video baada ya kuona kijipicha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3554805083602921117
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false