Fahamu kushiriki kwa hadhira

Unaweza kutumia kichupo cha Kushiriki katika kiwango cha video kwenye Takwimu za YouTube ili kupata muhtasari wa kile kinachotazamwa na hadhira yako na jinsi inavyotumia maudhui yako. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha muda wa kutazama (saa) na wastani wa kipindi cha kutazama maudhui yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhesabu vipimo vya kushiriki.

Angalia ripoti yako ya kushiriki

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Kwenye menyu ya juu, chagua Kushiriki..

Video maarufu

Ripoti ya video maarufu huangazia video zako zilizo maarufu zaidi. Unaweza kutumia ripoti ya takwimu iliyopanuliwa ili kuona vipimo zaidi, kama vile mara za utazamaji na maonyesho.

Orodha maarufu za kucheza

Ripoti ya orodha Maarufu za kucheza hukuonyesha ni orodha gani kati ya orodha zako ambazo zimetazamwa zaidi. Haijalishi kama baadhi ya video katika orodha hiyo ya kucheza zinatoka kwenye vituo vingine. Unaweza kuona data ya orodha ya kucheza hata kama hujawahi kupakia video.

Machapisho maarufu

Ripoti ya machapisho Maarufu huonyesha machapisho yako maarufu zaidi kulingana na idadi ya mara za kupendwa au za kura kutoka kwenye vifaa vya mkononi. Unaweza kutumia ripoti iliyopanuliwa ya takwimu ili kuona maelezo zaidi, kama vile asilimia ya mibofyo.

Kadi maarufu

Ripoti ya kadi Maarufu hukuonyesha ni kadi zipi watazamaji wako walibofya zaidi, kwenye video zote katika kituo chako.

Video maarufu kulingana na shughuli kwenye skrini ya mwisho

Video maarufu kulingana na ripoti ya skrini ya mwisho hukuonyesha skrini ya mwisho ambayo watazamaji wako walibofya zaidi kwenye kituo chako chote.

Aina za vipengele vya skrini ya mwisho ambavyo watumiaji wamebofya zaidi

Aina za vipengele vya skrini ya mwisho ambavyo watumiaji wamebofya zaidi hukuonyesha aina ya kipengele ambacho watazamaji wako walibofya zaidi kwenye kituo chako chote.

Matukio makuu ya muda wa kutazama

Ripoti ya matukio makuu ya muda wa kutazama huonyesha jinsi matukio tofauti ya video yako yalivyowavutia watazamaji. Unaweza pia kutumia muda wa kawaida wa kutazama kulinganisha video zako 10 za hivi karibuni zenye urefu sawa.

Mara za kupendezwa zikilinganishwa na mara za kutopendezwa (kiwango cha video)

Ripoti ya mara za kupendezwa (ikilinganishwa na kutopendezwa) inatoa muhtasari wa idadi ya watazamaji waliopendezwa na ambao hawakupendezwa na video zako. Unaweza kuweka kipimo cha kupendezwa (dhidi ya kutopendezwa) ukitumia ripoti iliyopanuliwa ya takwimu katika kiwango cha kituo.

Asilimia ya mibofyo ya kipengele cha skrini ya mwisho (kiwango cha video)

Ripoti ya asilimia ya mibofyo ya kipengele cha skrini ya mwisho hukuonyesha mara ambazo watazamaji walibofya kila kipengele cha skrini ya mwisho kwenye video yako. Ripoti hii inapatikana tu baada ya kubofya video mahususi.

Miseto maarufu

Ripoti hii inaonyesha maudhui yako ambayo yalitumika kuandaa miseto ili kutayarisha Video Fupi. Ripoti hii pia huonyesha idadi ya mara ambazo maudhui yako yalitumika kuandaa miseto na idadi ya utazamaji wa miseto. Kupata maelezo zaidi kuhusu miseto, bofya au gusa ANGALIA ZAIDI.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kwa nini siwezi kuona data ya orodha mahususi ya kucheza?

Takwimu za YouTube huonyesha tu data ya orodha za kucheza ambazo zilitazamwa katika muda uliochaguliwa na zinapatikana hadharani.

Je, kuna athari zozote iwapo ninamiliki video zote kwenye orodha ya kucheza?

Hapana, ripoti hii inaonyesha data bila kujali umiliki wa video.

Je, iwapo sijawahi kupakia video, ninaweza kuona data ya orodha yangu maarufu ya video?

Iwapo hujapakia video zako mwenyewe, bado unaweza kuona data ya orodha zako za video.

Kwa nini idadi ya alama za nimeipenda ilibadilika?

Unaweza kuona idadi ya mara za kupendezwa na kutopendezwa zikibadilika kwa kuwa baadhi yazo zinaweza kubainishwa kuwa si sahihi na kuondolewa mara kwa mara kwenye hesabu. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera yetu kuhusu Mara za Kupendezwa.
Katika hali chache, unaweza kuona idadi kubwa ya mara za kupendezwa/kutopendezwa kuliko mara za utazamaji kwa sababu vipimo hivi hubadilishwa na mifumo tofauti ya uthibitishaji.

Kwa nini idadi ya mara za kupendezwa kwenye video yangu katika Takwimu ni tofauti na ukurasa wa kutazama?

Idadi ya alama za kupendezwa/kutopendezwa katika Takwimu za YouTube inaweza kuwa tofauti na unayoona kwenye ukurasa wa kutazama chini ya video. Hili ni suala linalojulikana na timu yetu inajitahidi kurekebisha suala hili. Kwa sasa, rejelea hesabu kwenye ukurasa wa kutazama wa video yako.

Vipimo unavyopaswa kujua

Wastani wa kipindi cha kutazama

Makadirio ya wastani wa dakika zilizotazamwa kwa kila tukio la kutazama katika kipindi na video uliyochagua.

Muda wa kutazama (saa)

Muda ambao watazamaji wametazama video yako.

Utazamaji

Idadi halali ya mara ambazo vituo na video zako zilitazamwa.

Mibofyo ya kadi

Idadi ya mibofyo iliyopatikana kwa kadi mahususi.

Idadi ya walioona maelezo ya kadi

Mara ambazo kadi imeonyeshwa. Kadi moja inaweza tu kuwa na onyesho moja kwa kila utazamaji.

Mibofyo ya kishawishi cha kadi

Idadi ya mibofyo iliyopatikana kutokana na kishawishi cha kadi. Mibofyo ya aikoni ya kadi inahusishwa na kishawishi cha mwisho kilichoonyeshwa.

Vishawishi vya kadi vilivyoonyeshwa

Jumla ya mara ambazo kishawishi kimeonyeshwa. Vishawishi vinaweza kuwa na maonyesho mengi kwa mwonekano mmoja.

Idadi ya waliobofya kila kadi

Ni mara ngapi watazamaji walibofya kadi ilipoonyeshwa.

Mibofyo kwa kila kipengele kilichoonyeshwa kwenye skrini ya mwisho

Mara ambazo watazamaji walibofya kipengele cha skrini ya mwisho kilipoonyeshwa.

Mibofyo kwenye vipengele vya skrini ya mwisho

Mara ambazo kipengele cha skrini ya mwisho kilibonyezwa.

Vipengele vya skrini ya mwisho vilivyoonyeshwa

Mara ambazo kipengele cha skrini ya mwisho kilionyeshwa.

Mibofyo ya vishawishi kwa kila kishawishi cha kadi kilichoonyeshwa

Wastani wa mibofyo ya kishawishi kwa kila onyesho.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1321407441670404612
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false