Muhtasari wa zana za udhibiti wa hakimiliki

YouTube ina zana kadhaa ambazo wenye hakimiliki wanaweza kutumia kulinda na kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube. Zana za udhibiti wa hakimiliki zimebuniwa kwa ajili ya aina mbalimbali za watayarishi, kuanzia wapakiaji wa mara kwa mara hadi kampuni za maudhui.

Zana zetu za udhibiti wa hakimiliki ni pamoja na:

Kwa chaguomsingi, fomu ya wavuti  ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki inapatikana kwenye YouTube na kila mtu anaweza kuitumia. Upatikanaji wa zana zingine za kudhibiti hakimiliki unategemea:

  • Kuonyesha kuwepo kwa hitaji la udhibiti wa hakimiliki kila mara
  • Nyenzo zinazopatikana za kudhibiti haki na maudhui yako
  • Ufahamu wa mfumo wa hakimiliki wa YouTube

Huku tukijitahidi kupanua upatikanaji wa zana zetu, pia tumejitolea kutoa ulinzi dhidi ya usumbufu mkubwa unaoweza kusababishwa na matumizi mabaya ya zana hizo.

Kwa udhibiti wa hakimiliki usio wa mara kwa mara

Fomu ya wavuti ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Kila mtu aliye na Akaunti ya YouTube ana uwezo wa kufikia fomu yetu ya wavuti ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Ikiwa kazi yako ambayo imelindwa na hakimiliki imepakiwa bila ruhusa yako, unaweza kutumia fomu yetu ya wavuti ili utume ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ili maudhui hayo yaondolewe kwenye YouTube.

Kwa watu wengi wenye hakimiliki, fomu hiyo ya wavuti ni njia ya haraka na rahisi zaidi ya kuomba maudhui yanayokiuka hakimiliki yaondolewe. Fomu hii ya wavuti inapaswa kutumwa na mwenye hakimiliki au mwakilishi aliyeidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya mmiliki.

Pata maelezo zaidi kuhusu kutuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Kwa udhibiti wa hakimiliki kila mara

Ili upate zana inayokufaa kwa mahitaji yako ya mara kwa mara ya udhibiti wa hakimiliki, anza kwa kujaza fomu hii. Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti ile ile ya YouTube ambayo umetumia hapo awali kutuma maombi ya kuondoa video kupitia fomu yetu ya wavuti.

Majibu yako yatatupa maelezo zaidi kuhusu mahitaji yako ya udhibiti wa hakimiliki ili tuweze kutafuta zana zinazokufaa. Ukishatuma fomu hiyo, tutapitia majibu yako na kukutumia barua pepe yenye mapendekezo yetu kulingana na:

  • Mara ambazo wewe hupakia video
  • Mara ambazo video zako hupakiwa upya
  • Iwapo unadhibiti akaunti kwa niaba ya kampuni
  • Historia yako ya kutuma maombi kupitia fomu yetu ya wavuti. Haswa, jinsi maombi yako ya awali uliyoyatuma kupitia fomu ya wavuti yanaonyesha uelewa wa hakimiliki na hitaji la kuondolewa kwa maudhui mara kwa mara.

Maelezo zaidi kuhusu zana zetu za udhibiti wa kila mara wa hakimiliki yanaweza kupatikana hapo chini:

Copyright Match Tool

Copyright Match Tool inaweza kutambua kiotomatiki video ambazo ni nakala au ambazo huenda zimenakiliwa kutoka kwa video nyingine kwenye YouTube. Zana hii hutafuta video ambazo zinafanana na video zingine ambazo tayari zimepakiwa kwenye YouTube au zilizoondolewa kwa sababu ya ombi la kuondoa video. Video zinazolingana zikishapatikana, una uwezo wa kuchagua hatua utakayoichukua, kama vile:

  • Kumtumia aliyeipakia barua pepe kuhusu maudhui hayo yanayolingana
  • Kuomba maudhui yaondolewe
  • Kuweka maudhui yanayolingana kwenye kumbukumbu

Copyright Match Tool hutumia teknolojia ya kulinganisha maudhui sawa na inayotumika kwenye mfumo wa Content ID, lakini ni rahisi zaidi kudhibiti na inahitaji nyenzo chache.

Pata maelezo zaidi kuhusu Copyright Match Tool.

Mpango wa Kuthibitisha Maudhui

Ikiwa unahitaji kuondoa maudhui kila mara na awali ulituma maombi mengi halali ya kuondoa video, huenda ikawa umetimiza masharti ya kutumia Mpango wa Kuthibitisha Maudhui. Programu hii inawapa wenye hakimiliki zana ya kutafuta maudhui wanayoamini kuwa yanakiuka hakimiliki na kutuma maombi ya kuondoa video nyingi mara moja. 

Ikiwa huhitaji kutafuta na kuondoa video nyingi kila mara, fomu ya wavuti ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ndio chaguo bora.

Pata maelezo zaidi kuhusu Mpango wa Kuthibitisha Maudhui.

Content ID

Mfumo wa Content ID unapatikana kwa wenye hakimiliki walio na mahitaji makubwa zaidi ya udhibiti wa hakimiliki, kama vile studio za kurekodia au studio za filamu. Ili kutimiza masharti ya kutumia mfumo wa Content ID, ni sharti wenye hakimiliki wawe walituma maombi mengi halali ya kuondoa video na wawe na nyenzo za kudhibiti mfumo wa Content ID, miongoni mwa vigezo vingine.

Content ID ni mfumo wa kulinganisha maudhui unaotambua kiotomatiki maudhui yanayoweza kuwa ya ukiukaji. Video zinapopakiwa kwenye YouTube, zinachanganuliwa kwa kuzilinganisha na hifadhidata yenye faili zilizotumwa na wenye hakimiliki. Ikiwa mfumo wa Content ID utapata maudhui yanayolingana na mojawapo ya kazi zako, unaweza kuchagua hatua utayoichukua, kama vile:

  • Kuzuia video nzima isitazamwe
  • Kuchuma mapato kwenye video kwa kuonyesha matangazo, wakati mwingine kugawana mapato na aliyepakia video
  • Kufuatilia takwimu za watazamaji wa video

Hatua hizi huenda zikapatikana kwa kutegemea nchi au eneo ulipo. Kwa mfano, video inaweza kuchumiwa mapato katika nchi au eneo moja na kuzuiwa au kufuatiliwa katika nchi au eneo tofauti.

Pata maelezo zaidi kuhusu Content ID.

Madokezo

  • Hata matumizi mabaya ya mfumo wa Content ID bila kukusudia yanaweza kuwa na madhara mabaya kwa YouTube na watayarishi.
  • Mfumo wa Content ID una vidhibiti changamano vinavyohitaji udhibiti wa mara kwa mara na uelewa wa kina wa hakimiliki.
  • Wenye hakimiliki wanaotumia mfumo wa Content ID ni sharti wahakikishe kwamba maudhui yao yanatimiza masharti ya mfumo wa Content ID na ni salama kwa ajili ya teknolojia ya ulinganishaji otomatiki.
  • Wenye hakimiliki wengi wanapendelea kutumia watoa huduma wengine kudhibiti haki zao za kutumia mfumo wa Content ID. Watoa huduma hawa wa mfumo wa Content ID wanatenda kwa niaba ya wenye hakimiliki kwa ada fulani. Unaweza kupata mtoa huduma kwenye saraka hii.
Kumbuka:
  • Ukitumia zana zozote kati ya hizi za kudhibiti hakimiliki kutuma ombi la kuondoa video, utaanzisha mchakato wa kisheria.
  • Ukitumia vibaya zana hizi, kama vile kutuma taarifa ya uwongo, huenda akaunti yako ikasimamishwa au ukachukuliwa hatua nyingine za kisheria.
  • Ni muhimu kuzingatia iwapo matumizi ya haki, matumizi yasiyo ya biashara au mambo mengine yasiyofuata kanuni za hakimiliki yanatumika katika kila hali kabla ya kutuma maombi ya kuondoa video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15102771784126030726
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false