Chaneli yangu imeidhinishwa kuchuma mapato kutokana na Maswali Yanayoulizwa Sana

Vipengele vya uchumaji wa mapato

Je, ni njia gani tofauti za kuchuma mapato?

Uwezo wako wa kufikia vipengele unaweza kubadilika kulingana na idadi ya wafuatiliaji uliyo nayo na sehemu za mkataba ulizokubali. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vyetu tofauti na masharti ya kujiunga.

Ninatimiza masharti yote, kwa nini siwezi kuwasha kipengele maalum?

Wakaguzi wetu pia hukagua chaneli yako ili kuona kama inafaa kwako kuwasha kipengele fulani. Huenda usifikie baadhi ya vipengele kutokana na masharti ya kisheria ya eneo lako au uwezo wa usaidizi wa YouTube kwenye nchi au eneo au lugha yako. Kumbuka kukubali makubaliano yanayofaa ili ufungue vipengele fulani vya uchumaji wa mapato. 

Aikoni ya uchumaji wa mapato na rufaa za video

Aikoni zote zinamaanisha nini?

Kwa ujumla, aikoni hukufahamisha kuhusu hali ya uchumaji wa mapato ya video. Pata maelezo zaidi kuhusu aikoni ya uchumaji wa mapato na jinsi inavyoathiri mapato yako.

Je, ninaweza kukatia rufaa aikoni ya njano?

Unaweza kuangalia maudhui yako ukilinganisha na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji na mifano iliyotolewa. Ikiwa maudhui yako yanakidhi vigezo vyote vya "Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato ya matangazo," basi unaweza kukata rufaa.

Ufikiaji wa uchumaji wa mapato

Hatua gani itachukuliwa nikishuka chini ya upeo wa uchumaji wa mapato?

YouTube haitaondoa kiotomatiki idhini ya chaneli yako kufikia uchumaji wa mapato ikiwa itashuka chini ya upeo. Hata hivyo, YouTube inahifadhi haki, kwa hiari yake, kuondoa uchumaji wa mapato kutoka kwenye chaneli iwapo chaneli haitumiki na haipakii au kuchapisha Machapisho ya jumuiya kwa miezi 6 au zaidi.

Chaneli zitapoteza uwezo wa kuchuma mapato ikiwa zitakiuka sera zozote za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube, bila kujali idadi ya wanaovifuatilia, muda ambao video imetazamwa hadharani au utazamaji wa Video Fupi za umma.

Hatua gani itachukuliwa iwapo nitapoteza uwezo wa kufikia mpango wa uchumaji wa mapato?

Iwapo imebainishwa kuwa chaneli yako haitimizi tena masharti ya kuchuma mapato, chaneli yako itapoteza uwezo wa kufikia zana zote za uchumaji wa mapato na vipengele vinavyohusiana.

Iwapo tumeondoa chaneli yako kwenye mpango wa uchumaji wa mapato kwa sababu ya ukiukaji wa sera, unapaswa uanze kwa kwenda kwenye Sehemu ya kuchuma mapato ya Studio ya YouTube ili usome zaidi kuhusu sera iliyokiukwa na chaneli yako. Kisha, kagua video zako kulingana na sera zetu za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube na Mwongozo wetu wa Jumuiya. Hatua itakayofuata ni kubadilisha au kufuta video zozote zinazokiuka sera zetu.

Unaweza kuendelea kupakia maudhui halisi na kukuza hadhira yako kwenye YouTube. Iwapo chaneli yako imesimamishwa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ndani ya siku 21 au kutuma ombi tena kwenye mpango baada ya siku 90.

Mengineyo

Je, uchumaji wa mapato huathiri matokeo ya utafutaji?

Hali ya uchumaji wa mapato haitumiwi kufahamisha jinsi video zinavyoonyeshwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu uchumaji wa mapato na jinsi unavyofanya kazi na mifumo yetu ya Utafutaji na Ugunduzi. 

Sijapata jibu la swali langu. Usaidizi!

Iwapo unachuma mapato, unakuwa na uwezo wa kufikia Timu yetu ya Usaidizi kwa Watayarishi. Fahamu jinsi ya kupata usaidizi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13296234694802345375
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false