Sera ya vijipicha

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu vijipicha na picha nyinginezo zinazokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya. Picha zinajumuisha mabango, ishara, Machapisho ya jumuiya na vipengele vingine vya YouTube vilivyo na picha.

Iwapo utapata vijipicha au picha nyinginezo zinazokiuka sera hii, ziripoti. Ikiwa utapata video au maoni machache ambayo ungependa kuripoti, unaweza kuripoti kituo.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Usichapishe kijipicha au picha nyingine kwenye YouTube ikiwa inaonyesha:

  • Picha za ponografia
  • Vitendo vya ngono, matumizi ya vifaa vya ngono, picha za matamanio au zinazochochea ngono
  • Uchi, ikijumuisha sehemu ya siri
  • Picha zinazoonyesha onyesho la ngono lisilotakikana
  • Picha ya vurugu inayonuiwa kuogofya au kukera
  • Picha za kuogofya au za kutatiza zilizo na umwagaji damu au za kutisha
  • Lugha chafu
  • Kijipicha kinachopotosha watazamaji kudhani kuwa wanakaribia kuona kitu ambacho hakipo kwenye video

Kumbuka: Orodha iliyo hapa juu si kamili.

Vijipicha vilivyowekewa mipaka ya umri na kuondolewa kwa vijipicha

Wakati mwingine, huenda kijipicha hakifai kwa hadhira zote, lakini hakikiuki Mwongozo wetu wa Jumuiya. Hali hii ikitokea, huenda tukawekea video hiyo mipaka ya umri au huenda tukaondoa kijipicha, lakini hatutoi onyo kwa kituo chako. Tutakufahamisha iwapo tutaondoa kijipicha na unaweza kupakia kijipicha kingine.

Huwa tunaangazia yafuatayo tunapoondoa au kuwekea mipaka ya umri aina hizi za vijipicha:

  • Iwapo kijipicha hicho kinalenga matiti, makalio au sehemu nyeti
  • Iwapo mhusika anaonyeshwa katika hali au mavazi yanayonuiwa kuamsha hisia za kingono kwa watazamaji
  • Iwapo kijipicha kinalenga kuonyesha picha za vurugu au za kutisha
  • Iwapo maandishi yaliyoandikwa yananuiwa kuwa ya lugha chafu au kuogofya au kukera watazamaji
  • Iwapo nia ya jina, maelezo, lebo au data nyingine ni ya kuwaogofya au kuudhi watazamaji

Ni nini kinachotokea ikiwa vijipicha vinakiuka sera zetu

Ikiwa kijipicha kina ponografia, tunaweza kusimamisha kituo chako. Ikiwa kijipicha chako kinakiuka sera zetu, tunaondoa kijipicha na tunaweza kutoa onyo dhidi ya akaunti yako. Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuchapisha maudhui yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, utapata tahadhari bila adhabu kwenye akaunti yako. Unaweza kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa mojawapo ya vijipicha vyako kitakiuka sera sawa ndani ya kipindi cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na kituo chako kitapewa onyo. Ikiwa utakiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ukipata maonyo matatu ndani ya siku 90 au kituo chako kinachapisha maudhui ya ukiukaji kila mara, kituo chako kitasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10278944638372157168
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false