Mbinu bora kuhusu maudhui yaliyo na watoto

Tungependa watayarishi waendelee kufurahia na kubuni, lakini tunaomba ufuate Mwongozo wetu wa Jumuiya. Unapaswa kuwa makini kuhusu maudhui unayochapisha mtandaoni na uombe ruhusa kabla ya kupakia video inayoangazia mtu mwingine kwenye YouTube.

Mtu yeyote anayechapisha maudhui yenye watoto ni sharti afanye yafuatayo:

  • Kuheshimu faragha. Kupata idhini kutoka kwa mzazi au mlezi anayetambulika kisheria wa mtoto kabla ya kumwangazia kwenye video yake. Hakikisha kuwa ushiriki wake katika video yako ni kwa hiari yake.
  • Kudhibiti maoni ya watumiaji kwenye video zako. Kuna zana unazoweza kutumia ili kuchuja na kukagua maoni, na unaweza kuripoti wakati wote maoni ya taka au matumizi mabaya.
  • Kudhibiti mipangilio ya video yako ya faragha na kupachika. Una chaguo kadhaa za kudhibiti nani anayeweza kutazama video yako na jinsi inavyoshirikiwa kwenye tovuti za nje.

Tafadhali hakikisha unaelewa na unafuata sheria. Ni sharti utii sheria, amri na kanuni zote zinazohusiana na kufanya kazi na watoto. Baadhi ya maeneo unayopaswa kufahamu kuhusu ni:

  • Vibali: Kagua sheria na kanuni za mahali ulipo kufahamu iwapo unahitaji kibali, usajili au leseni ili kuonyesha watoto katika video zako. Unapaswa kufahamu pia iwapo unahitaji kibali au idhini ya kuajiri watoto.
  • Mishahara/Ugavi wa Mapato: Ni sharti ufuate sheria zinazotumika katika masuala ya kulipa watoto kwa kazi yao. Katika hali fulani, huenda ukahitajika kulipa mshahara kwa watoto. Katika hali zingine, huenda ukahitajika kutoa mgawo wa mapato unayochuma kutokana na video kwa watoto moja kwa moja, au utenge kiasi ambacho kinalindwa kwa ajili ya mtoto.
  • Shule na Elimu: Ushiriki wa watoto katika maudhui yako ni sharti ufuate sheria zote zinazotumika ili kulinda dhidi ya ukatizaji wa shule na elimu inayofaa.
  • Mazingira ya Kazi, Saa na Mapumziko: Ni sharti mazingira ya kazi yawe salama kwa ajili ya mtoto. Ni sharti wawe na muda wa kupumzika, kusoma na kucheza kila siku. Watoto hawapaswi kufanya kazi mpaka usiku. Unapaswa pia kufuata sheria za mahali ulipo za saa za kazi na vikomo vya saa za kufanya kazi kila siku/wiki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15472923180196750057
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false