Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Suluhisha Matatizo ya Content ID

Vipengele vinavyofafanuliwa katika makala haya vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia mifumo ya ulinganishaji wa Content ID katika YouTube.

Ndani ya kichupo cha Matatizo katika Kidhibiti cha Maudhui utaona hatua ambazo unapaswa kuchukua na huenda zikaathiri madai, marejeleo au vipengee vyako. Huenda hali ya kutokagua vipengee ambapo unahitaji Kuchukua hatua ikasababisha upoteze umiliki na/au mapato. Matatizo ambapo unatakiwa Uchukue Hatua yanaweza kujumuisha:

Kulingana kwa marejeleo

Kagua vifungu vya marejeleo yako ambavyo vinalingana na marejeleo kutoka kwa wamiliki wengine wa maudhui na ubainishe mshirika ambaye anamiliki haki za kipekee za vifungu vinavyolingana. Hatua hii inaruhusu Content ID ihusishe madai na marejeleo yanayofaa.

Marejeleo yasiyo sahihi

Kagua marejeleo ambayo huenda si sahihi ili uthibitishe iwapo kifungu kimetimiza masharti ya Content ID. Madai yote ya baadaye yatakayofanywa dhidi ya sehemu ya marejeleo ambayo huenda si sahihi yatasubiri hadi tatizo la kifungu husika lisuluhishwe.

Ukinzani wa umiliki

Ukinzani wa Umiliki wa Vipengee hutokea wakati wamiliki wengi wa maudhui wanadai umiliki wa kipengee katika eneo mahususi kwa asilimia 100. Kagua maelezo ya kipengee ili uhakikishe kuwa umiliki wako umesasishwa, omba umiliki, au uwasiliane na wamiliki wengine ili usuluhishe mzozo.

Madai Yanayokatiwa Rufaa, Yaliyo na Mzozo au Yanayoweza Kutokea

Kagua na uchukue hatua dhidi ya madai ambayo Yanaweza Kutokea (madai yanayoweza kutokea yanayosubiri kukaguliwa, madai yanayotumwa kufanyiwa ukaguzi kutokana na sera ya mshirika) na Madai Yaliyokatiwa Rufaa na Yaliyo na Mzozo kutoka kwa watumiaji wanaodai umiliki kwenye video zao.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15866779127904597824
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false