Kuanzisha Onyesho la kwanza la video mpya

Maonyesho ya kwanza ya YouTube hukuruhusu wewe na watazamaji wako kutazama na kufurahia video mpya pamoja katika muda halisi. Leta hamasa ya Onyesho lako la kwanza kwa kushiriki ukurasa wa kutazama ili watazamaji waweze kuweka vikumbusho, kupiga gumzo na kuacha maoni.

Maonyesho ya Kwanza kwenye YouTube

Kuanzisha Onyesho la Kwanza

Watazamaji wanaweza kutazama Onyesho la kwanza kwenye mfumo wowote kama vile kompyuta, iPhone, iPad, Android na wavuti wa vifaa vya mkononi.

  1. Katika kompyuta yako, nenda kwenye studio.YouTube.com.
  2. Katika sehemu ya juu, bofya Tayarisha kisha Pakia video.
    Kumbuka: Video Fupi hazitumiki kwa Maonyesho ya kwanza.
  3. Chagua video yako ili uipakie na uweke maelezo ya video.
    Kumbuka: 360/vr180 au mfumo unaozidi 1080p hautumiki kwa Maonyesho ya kwanza.
  4. Ili uanzishe onyesho la kwanza la video papo hapo, bofya Hifadhi au chapisha kisha Umma kisha Weka kuwa Onyesho la kwanza papo hapo. Onyesho la kwanza la video litaanza video ikimaliza kuchakata.
    Ili uratibu onyesho la kwanza kwa ajili ya baadaye, bofya Ratibu kisha Weka tarehe na saa kisha Teua Weka kama Onyesho la kwanza.
  5. Ili uchague mandhari ya muda uliosalia na urefu wa muda uliosalia, bofya Weka mipangilio ya Onyesho la kwanza.
  6. Bofya Nimemaliza au Ratibu.

Kidokezo: Unaweza pia kuanzisha Onyesho la kwanza kwa kupakia video kutoka kwenye programu ya YouTube. Kwenye ukurasa wa “Weka uonekanaji”, teua Weka kama Onyesho la kwanza.

Kinachofanyika unapotayarisha Onyesho la kwanza

Kabla Onyesho lako la kwanza lianze

Ukurasa wa kutazama hadharani huanzishwa kwa ajili ya video yako kuonyeshwa kama Onyesho la kwanza. Unaweza pia kushiriki URL ya ukurasa wa kutazama kwa kuwa ukurasa wa kutazama unaonekana hadharani kabla Onyesho la kwanza halijaanza. Maonyesho ya kwanza huonekana kwenye YouTube kama tu video za kawaida zilizopakiwa. Utayapata kwenye utafutaji, ukurasa wa kwanza na mapendekezo ya video.

Mtu yeyote anaweza kuja kwenye ukurasa wa kutazama na kuweka kikumbusho, kuacha maoni au kupiga gumzo (na pia kutoa Super Chat ikiwa zimewashwa). Ikiwa umepakia kionjo, kitacheza. 

Kumbuka: Ikiwa akaunti yako ina onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, Onyesho lako la kwanza halitachapishwa wakati wa kipindi cha adhabu. Onyesho lako la kwanza huwekwa kuwa “faragha” wakati wa kipindi cha adhabu, na inabidi kuiratibu upya kipindi hicho cha kuzuiwa kikiisha. Pata maelezo zaidi kuhusu maelezo ya msingi kuhusu maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Muhtasari wa ukurasa wa kutazama

Kipengele cha muda uliosalia hadi Onyesho la kwanza, na chaguo la 'Weka kikumbusho', kinaweza kupatikana kwa kubofya kishale kilicho upande wa kushoto wa gumzo.

Wakati wa Onyesho lako la kwanza

Mandhari ya muda uliosalia yataanza yanaporatibiwa kwa kipindi ulichochagua. Ikiwa Onyesho la kwanza liliwekwa lianze saa 6 mchana, muda uliosalia utaanza saa 6 mchana. Muda uliosalia unapoisha, watazamaji hutazama video pamoja katika muda halisi. Watazamaji wanaweza kurudisha nyuma video, lakini hawawezi kupeleka mbele zaidi ya pale walipoonyeshwa mubashara.

Wewe na watazamaji wako mnaweza kuendelea kuwasiliana katika maoni na gumzo la moja kwa moja.

Baada ya Onyesho la kwanza kuisha

Baada ya video yako kuonyeshwa kama Onyesho la kwanza, inabaki kwenye kituo chako kama video iliyopakiwa kawaida. Mandhari ya muda uliosalia hayatajumuishwa katika video. Kuonyesha gumzo tena kutapatikana kwa watazamaji wanaotaka kufurahia gumzo la Onyesho la kwanza baada ya onyesho hilo kuisha. 

Kwenye Studio ya YouTube, unaweza pia kutumia Takwimu za YouTube ili uone utendaji wa Onyesho lako la kwanza. Idadi ya waliotazama Onyesho la kwanza itahamishiwa kwenye video baadaye.

Pata Vidokezo kuhusu Onyesho la kwanza kwa ajili ya watayarishi.

Vidokezo

Wekea mapendeleo Onyesho lako la kwanza kwa kuchagua mandhari tofauti ya muda uliosalia, kuchuma mapato kwenye Onyesho lako la kwanza, au kuonyesha kionjo kwenye ukurasa wa kutazama kabla Onyesho lako la kwanza halijaanza.
Waelekeze watazamaji wako kwenye mtiririko wako mubashara. Waelekeze watazamaji wako kwenye mtiririko wako mubashara ukitumia kipengele cha Kuelekezwa Moja kwa Moja.
Leta hamasa kwa kuelekeza hadhira yako kutoka kwenye mtiririko mubashara kwenda kwenye Onyesho la kwanza.
Tuma URL ya ukurasa wa kutazama Onyesho lako la kwanza kwenye mitandao ya kijamii.
Weka Onyesho lako la kwanza liwe kionjo cha chaneli yako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya hivyo kwa kubadilisha muundo wa chaneli yako.
Wahimize watazamaji wako waweke kikumbusho kwa kuacha maoni au ujumbe wa gumzo kwenye ukurasa wako wa kutazama. Mtazamaji anakapoweka kikumbusho, atapata arifa dakika 30 kabla ya Onyesho la kwanza kuanza na arifa nyingine onyesho litakapoanza.

Ungependa kupata vidokezo zaidi vya kutayarisha Onyesho lako la kwanza linalofuata?
Download our Premieres Guide.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3885871686840533914
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false