Sera kuhusu viungo vya nje

Viungo vinavyoelekeza watumiaji kwenye maudhui yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya haviruhusiwi kwenye YouTube. Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Kumbuka: Viungo fulani huenda visiweze kubofyeka. Pata maelezo zaidi hapa.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Unapochapisha maudhui

Usichapishe viungo katika maudhui yako kwenye YouTube ikiwa vinaelekeza watumiaji kwenye maudhui yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya. Sera hii inajumuisha viungo vinavyolingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini. Tafadhali kumbuka kuwa orodha hii haijakamilika.

  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti za ponografia
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au programu zinazoweka programu hasidi kwenye kifaa
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au programu za wizi wa data binafsi ya maelezo ya kuingia katika akaunti ya mtumiaji, maelezo ya kifedha n.k.
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti, programu au vyanzo vingine vinavyotoa ufikiaji usioidhinishwa wa maudhui ya sauti, maudhui ya video, michezo ya video, programu au huduma za kutiririsha maudhui ambazo kwa kawaida zinalipiwa.
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti za kuchangisha fedha au zinazotoa fursa ya kujiunga na mashirika ya kigaidi
  • Viungo vya tovuti zilizo na Maudhui Yanayoonyesha Unyanyasaji wa Watoto Kingono (CSAI)
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti zinazouza bidhaa zilizoainishwa katika mwongozo wetu wa bidhaa zilizodhibitiwa
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye maudhui yanayokiuka sera zetu dhidi ya chuki au unyanyasaji
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye maudhui yanayohimiza vitendo vya vurugu
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye maudhui ​​yanayoeneza maelezo ya kimatibabu yanayopotosha ambayo yanakinzana na maelezo ya matibabu kutoka kwa mamlaka ya afya katika eneo (LHA) au Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu COVID-19
  • Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au programu zinazoeneza maudhui ya kupotosha au danganyifu yanayoweza kusababisha madhara makubwa, kama vile kuathiri michakato ya kidemokrasia
  • Viungo vya tovuti za nje zilizo na matamko ya washambuliaji wenye vurugu

Sera hii inatumika kwa video, sauti, chaneli, maoni, maoni yaliyobandikwa, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Viungo vinaweza kuwa katika muundo wowote unaoweza kumwelekeza mtumiaji kwenye tovuti zilizo nje ya YouTube. Viungo hivi ni pamoja na: url zinazobofyeka, kuonyesha maandishi yenye url kwenye video au picha na url zilizofumbwa (kama vile kuandika "dot com" badala ya ".com"). Viungo hivi vinaweza pia kujumuisha kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine kwa kutamka, kuwahimiza watazamaji watembelee wasifu au kurasa za mtayarishi kwenye tovuti nyingine au kuahidi maudhui yanayokiuka sera kwenye tovuti nyingine. Orodha hii haijakamilika.

Kidokezo: Maudhui ya washirika hayakiuki Sheria na Masharti ya YouTube. Kuchapisha kupita kiasi maudhui ya washirika katika akaunti maalum kunaweza kukiuka sera zetu kuhusu maudhui taka. Ili upate maelezo zaidi kuhusu maudhui yanayoruhusiwa, angalia Sera zetu kuhusu taka, tabia za udanganyifu na ulaghai.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Video yenye maudhui ya ngono ambayo maelezo yake yanasema "bofya ili uone kilichopigwa marufuku kwenye YouTube!" na ina kiungo kinachoelekeza kwenye tovuti ya ponografia.
  • Maelezo ya video ya uchezaji yana kiungo kinachoahidi sarafu za ndani ya mchezo au salio la Google Store mtandaoni lakini viungo vinaelekeza kwenye tovuti inayoathiri kompyuta ya mtumiaji kwa kuiwekea programu hasidi.
  • Kuchapisha kiungo kinachoelekeza kwenye tovuti ya wizi wa data binafsi inayoiba maelezo na manenosiri ya akaunti ya benki.
  • Kuwaelekeza watazamaji kunakili na kubandika kiungo wasichoweza kubofya kwenye video ambacho kinawaelekeza kwenye tovuti ya ponografia au taka.
  • Kiungo chochote kinachoelekeza watumiaji kwenye tovuti, huduma ya upangishaji wa faili au chanzo kingine kinachowaruhusu kufikia au kupakua maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono.
  • Kuwaelekeza watazamaji wafungue tovuti ili wafikie wasifu au ukurasa fulani kwenye mfumo mwingine ili watazame maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
  • Kupachika URL katika video ya tovuti inayoweza kuwapotosha wapigakura kuhusu wakati, mahali, namna au masharti ya kustahiki kupiga kura.
  • Kiungo kinachoelekeza kwenye makala yanayodai kuwa chanjo za COVID-19 ni njama ya kupunguza idadi ya watu.

Kumbuka kwamba orodha haijakamilika. Iwapo unafikiri kuwa huenda maudhui yakakiuka sera hii, usiyachapishe.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9379671452391891694
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false