Kuunganisha akaunti yako ili upate zawadi za nje ya mfumo

Unaweza kupata zawadi za nje ya mfumo unapotazama mitiririko mubashara inayotimiza masharti kwenye YouTube kwa kuunganisha Akaunti yako ya Google na akaunti ya mshirika.

Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.

Kuunganisha au kutenganisha akaunti zako

Kwenye mipangilio ya YouTube

Kuunganisha akaunti

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu  kisha uchague Mipangilio  .
  3. Nenda kwenye sehemu ya Programu zilizounganishwa.
  4. Bofya UNGANISHA karibu na mshirika ambaye ungependa kuunganisha.
    1. Ikiwa huna akaunti, fuata maagizo yaliyo kwenye tovuti ya mshirika ili ufungue akaunti. Kisha uanzie hatua ya 2.
  5. Fuata hatua za kuingia katika akaunti yako ya mshirika.

Kutenganisha akaunti

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Bofya picha yako ya wasifu  kisha uchague Mipangilio  .
  3. Nenda kwenye sehemu ya Programu zilizounganishwa.
  4. Bofya TENGANISHA karibu na akaunti ya mshirika ambayo ungependa kuitenganisha.

Kwenye Ukurasa wa Kutazama wa YouTube

Kuunganisha akaunti

  1.  Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video au mtiririko mubashara wowote unaotimiza masharti ya zawadi.
  3. Kwenye Ukurasa wa kutazama, bofya UNGANISHA  chini ya kichezaji.
  4. Fuata hatua za kuingia katika akaunti yako ya mshirika.

the sign-in will appear as a pop-up in the center of the page.

Kutenganisha akaunti

  1.  Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video au mtiririko wowote mubashara unaotimiza masharti.
  3. Kwenye Ukurasa wa kutazama, bofya IMEUNGANISHWA  chini ya kichezaji.
  4. Bofya TENGANISHA.

Kwenye Akaunti yako ya Google

Unaweza kutenganisha akaunti ya mshirika na Akaunti yako ya Google.

  1. Ingia katika akaunti yako ya Google.
  2. Nenda kwenye myaccount.google.com/accountlinking.
  3. Karibu na akaunti unayotaka kutenganisha, bofya Tenganisha.
Kumbuka: ​Baada ya kutenganisha akaunti zako, hutastahiki tena kupata zawadi kwenye programu hiyo kwa kutazama video au mitiririko mubashara inayotimiza masharti. Huenda washirika wetu wakahifadhi kumbukumbu ya maudhui uliyotazama hata ikiwa umetenganisha akaunti. Rejelea akaunti yako ya mshirika ili udhibiti data yako.

Akaunti za washirika

Activision
Activision ndiyo kampuni iliyounda Call of Duty. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Activision, tazama mitiririko mubashara mahususi ya Call of Duty ili ustahiki kupata zawadi.
Battle.net (Blizzard)
Blizzard ndiyo kampuni iliyounda Battle.net, Overwatch na Hearthstone. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Battle.net, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya Blizzard ili ustahiki kupata zawadi.
Electronic Arts 
Electronic Arts (EA) ndiyo kampuni iliyounda FIFA na Madden. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya EA, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya EA ili ustahiki kupata zawadi.
Epic Games
Epic Games ndiyo kampuni iliyounda Fortnite. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Fortnite, tazama maudhui mahususi ya Kombe la Dunia la Fortnite ili ustahiki kupata zawadi.
Garena
Garena ndiyo kampuni iliyounda Free Fire.  Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Garena Free Fire, tazama maudhui mahususi ya Garena Free Fire ili ustahiki kupata zawadi.
MLBB
Moonton ndiyo kampuni iliyounda Mobile Legends: Bang Bang (MLBB). Baada ya kuunganisha akaunti yako ya MLBB, tazama mitiririko mubashara mahususi ya MLBB ili ustahiki kupata zawadi.
NFL
Ili upate zawadi za nje ya mfumo kutoka NFL, unganisha akaunti yako ya NFL ID.
PlayerUnknown's Battlegrounds ya Vifaa vya Mkononi (PUBG ya Vifaa vya Mkononi)
Tencent Games ndiyo kampuni iliyounda mchezo wa PlayerUnknown’s Battlegrounds (PUBG) wa Vifaa vya Mkononi. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara mahususi ya mchezo wa PUBG wa Vifaa vya mkononi ili ustahiki kupata zawadi.
Riot Games
Riot Games ndiyo kampuni iliyounda League of Legends, Legends of Runeterra na Teamfight Tactics. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara inayotimiza masharti ili upate zawadi.
Supercell

Supercell ndiyo kampuni iliyounda Clash Royale. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Supercell, tazama mitiririko mubashara mahususi ya Clash Royale au Ligi ya Clash Royale ili ustahiki kupata zawadi.

Ubisoft
Ubisoft ndiyo kampuni iliyounda Assassin's Creed na Tom Clancy's Rainbow Six. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya Ubisoft ili ustahiki kupata zawadi.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Nimeunganisha akaunti zangu na ninatazama mtiririko mubashara unaotimiza masharti. Kwa nini sijajishindia zawadi yoyote?

Washirika wetu hubainisha ni watazamaji wagani wanaostahiki ambao watashinda kulingana na sheria za kila mtiririko. Sheria zinaweza kutofautiana kulingana na mshirika.  
Ili kuhakikisha kuwa unastahiki, hakikisha kuwa umeunganisha akaunti na unatazama kwenye kompyuta yako, programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi au tovuti yetu ya vifaa vya mkononi. Iwapo unatazama kwenye vichezaji vilivyopachikwa, programu ya YouTube ya televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti au kwa kutuma maudhui, hutastahiki kupata zawadi.
To check if the video is eligible, you can look at the videos’ Player Settings, where eligible videos will include an option for you to review your linked account state.
Iwapo unatazama kwenye Android au iOS, hakikisha kuwa unatumia toleo jipya zaidi la YouTube

Nitajuaje kuwa nimepata zawadi?

Baada ya kujishindia, zawadi zitasambazwa kwenye akaunti yako ya mshirika. Zawadi hizi zinaweza kuchukua hadi siku moja kabla hazijaonekana. Pata maelezo zaidi moja kwa moja kwenye tovuti ya mshirika.

Je, kipengele hiki kinapatikana kwenye vifaa vya mkononi?

Zawadi zinapatikana unapotazama kwenye kompyuta, programu ya vifaa vya mkononi, kwenye tovuti yetu ya vifaa vya mkononi m.youtube.com na kupitia hali ya kupachika picha ndani ya picha nyingine. Iwapo unatazama kwenye vichezaji vilivyopachikwa, hutastahiki kupata zawadi.
Nimeshindwa kuunganisha akaunti yangu. Ninapaswa kufanya nini?
Kwanza, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti. Huenda ukahitaji kuwasha madirisha ibukizi kwenye kivinjari chako ili uweze kuunganisha akaunti zako. Iwapo umeshindwa kuunganisha kwenye Safari, jaribu kivinjari kingine. 
Kumbuka: Unaweza tu kuunganisha akaunti binafsi, si Akaunti za Biashara. Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti binafsi unapojaribu kuunganisha.
Iwapo video imebainishwa kuwa Inalenga watoto, kipengele cha kuunganisha akaunti hakitapatikana.

Nilipokea ujumbe kwamba akaunti zangu zimeunganishwa, lakini hazionyeshi kuwa zimeunganishwa. Je, bado ninastahiki kupata zawadi?

Wakati mwingine kuna ucheleweshaji baina ya wakati akaunti zako zinaunganishwa na wakati zinaonyesha kuwa zimeunganishwa.
Tembelea ukurasa huu ili uthibitishe kuwa akaunti zako zimeunganishwa. Kwenye ukurasa huu, unaweza kuangalia huduma zote zilizounganishwa kwenye akaunti yako. Unaweza pia kutenganisha huduma yoyote.
Ilimradi ukurusa huu unaonyesha kuwa akaunti zako zimeunganishwa, unastahiki kupata zawadi.
Iwapo akaunti zako hazionyeshi kuwa zimeunganishwa, unaweza pia kujaribu kuzitenganisha, kisha uziunganishe tena.

Ninajaribu kutenganisha akaunti zangu lakini bado zinaonyesha kuwa zimeunganishwa. Kwa nini?

Wakati mwingine kuna ucheleweshaji baina ya wakati akaunti zako zinatenganishwa na wakati zinaonyesha kuwa zimetenganishwa.
Tembelea ukurasa huu ili uthibitishe kuwa akaunti zako zimetenganishwa. Ikiwa huduma haijaorodheshwa kwenye ukurasa huu, inamaanisha kuwa akaunti zako hazijaunganishwa.

Ninapounganisha akaunti yangu, maelezo ya aina gani huruhusiwa yafikiwe baina ya Google na akaunti yangu ya mshirika?

Baada ya kuunganisha akaunti yako kwenye YouTube, YouTube inaweza kushiriki maelezo ya utazamaji na hali yako ya usajili na mshirika anaweza kushiriki maelezo ya msingi ya akaunti na Google au YouTube. Maelezo haya yatatusaidia kujua akaunti zinazostahiki kupata zawadi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11183929118029989564
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false