Wajibu wa mtayarishi

Watayarishi ni watu muhimu sana kwa YouTube. Kama sehemu ya kuwa mtayarishi humaanisha kuwa wewe ni mwanachama wa jumuiya kubwa na yenye ushawishi ulimwenguni. Unaweza kutusaidia kuhifadhi na kulinda kikundi hiki cha kipekee chenye hamasa.

Mpango wa YouTube wa Wajibu wa Watayarishi

Kama mtayarishi kwenye YouTube, unakubali kufuata:

Ni muhimu uelewe mwongozo huu na jukumu lake kwenye wajibu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa bora. Hatua ya kukiuka mwongozo huu inaweza kusababisha video zako kufutwa, chaneli yako kupewa maonyo au kwa ukiukaji mkubwa au unaojirudia, chaneli yako kuzuiwa au hata kusimamishwa.

Kupata pesa kupitia maudhui yako

Watayarishi wanaotaka kuchuma mapato kwenye maudhui lazima wafuate mwongozo zaidi:

Kwa kuheshimu mwongozo huu, utatusaidia kuzuia video ambazo huenda hazifai kuchuma mapato, jambo litakaloathiri mapato kwa kila mtu.

Ikiwa hutafuata mwongozo huu, huenda ikasababisha upewe adhabu, kama vile kuzima matangazo kwenye maudhui yako au kusimamisha chaneli yako kutoka kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera zetu za uchumaji wa mapato.

Kulinda jumuiya ya YouTube

Kama mtayarishi wa YouTube, unapaswa kuwajibika ndani na nje ya mfumo. Ikiwa tutaona kuwa tabia ya mtayarishi kwenye- na/au nje ya mfumo wa YouTube inawaathiri watumiaji, jumuiya, wafanyakazi au mfumo wetu, tunaweza kuchukua hatua ili kuilinda jumuiya.

Zaidi ya maudhui unayopakia kwenye YouTube, hii hapa ni baadhi ya mifano ya tabia kwenye- na/au nje ya mfumo tunayoweza kuchukulia kuwa haifai na inaweza kusababisha adhabu:

  • Kudhamiria kusababisha madhara ya kihasidi kwa wengine.
  • Kushiriki katika unyanyasaji au vurugu, kuonyesha ukatili au kushiriki katika tabia za kilaghai na danganyifu zinazopelekea madhara katika mazingira halisi.

Ingawa tabia hizi ni za nadra, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwenye jumuiya ya YouTube na kuharibu imani baina ya watayarishi, watumiaji na watangazaji.

Ukiukaji mkubwa unaosababisha madhara makubwa kwenye jumuiya unaweza kuwa na athari zaidi ya vitendo vya kawaida vya utekelezaji. Vizuizi hivi huenda vikajumuisha:

  • Hali ya utumiaji ya YouTube Originals na Studio ya YouTube: Huenda YouTube Originals ikasimamishwa, ikaghairishwa au kuondolewa na unaweza kupoteza idhini ya Studio ya Muda ya YouTube na mikusanyiko ya mtandaoni.
  • Uchumaji wa mapato, usimamizi wa washirika na fursa za matangazo: Chaneli yako inaweza kupoteza uwezo wa kuonyesha matangazo, kuchuma mapato na inaweza kuondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, ikiwemo kupoteza ufikiaji kwa msimamizi wa washirika na usaidizi kwa watayarishi. Ufikiaji wa Kidhibiti Maudhui cha Studio unaweza kupotea pia. Unaweza pia kuondolewa kwenye Chaneli maarufu kwenye YouTube Select.

Nyenzo za ziada

Tumia nyenzo hizi kupata maelezo zaidi kuhusu sera za YouTube:

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6089352619786278938
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false