Manufaa ya uanachama katika chaneli ya YouTube

Chaneli zilizowasha uanachama zinaweza kuanzisha manufaa ya wanachama pekee. Manufaa ya wanachama pekee yanapatikana kwa wanachama wako wanaolipia huduma. Manufaa yanajumuisha emoji maalum, beji na ufikiaji wa manufaa mengine unayotoa.

Kumbuka: Manufaa yote unayotoa ni lazima yafuate sera zetu za uanachama katika chaneli.

Uanachama Katika Vituo

Viwango vya uanachama katika chaneli

Unaweza kuweka viwango mbalimbali vya uanachama vyote vikiwa na bei tofauti. Kumbuka kwamba ikiwa una viwango vingi, manufaa yake hujumuisha ya viwango vingine. Hii inamaanisha kuwa viwango vya bei ya juu vinajumuisha manufaa yanayotolewa katika viwango vya bei ya chini.

Angalia maelezo kamili ya bei za viwango katika nchi zilizopo.

Weka kiwango

Unaweza kuweka hadi viwango 6 vya bei tofauti. Ni lazima kila kiwango kiwe na manufaa kati ya 1 hadi 5.

Kuweka viwango vya uanachama

  1. Nenda kwenye studio.youtube.com ukitumia chaneli yako yenye uanachama.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato.
  3. Katika dashibodi kuu, bofya Uanachama.
  4. Bofya Badilisha kwenye kisanduku kisemacho "Hatua ya 1: Weka viwango na manufaa".
  5. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini. Utakapokamilisha, bofya Chapisha.

Viwango na manufaa yako yatahitaji kukaguliwa kabla ya kuchapishwa. Mchakato huu utachukua takribani siku moja.

Jinsi viwango vinavyofanya kazi na beji na emoji

Beji za uaminifu na emoji maalum haziathiriwi na viwango. Wanachama wote hupokea beji sawa kulingana na uaminifu na wanachama wa viwango vyote wana ufikiaji sawa kwa emoji zote.

Kuondoa kiwango

Ukiondoa kiwango, utafuta wanachama wote walio katika kiwango hicho. Wanachama wote walio katika kiwango kilichoondolewa watapoteza uwezo wa kufikia manufaa papo hapo na watarejeshewa pesa yao ya mwezi uliopita.

Kuondoa kiwango

  1. Nenda kwenye studio.youtube.com ukitumia chaneli yako yenye uanachama.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato.
  3. Katika dashibodi kuu, bofya Uanachama.
  4. Bofya Badilisha kwenye kisanduku kisemacho "Hatua ya 1: Weka viwango na manufaa".
  5. Bofya kwenye kiwango unachotaka kukiondoa kisha bofya aikoni ya futa .
  6. Fuata maagizo mengine yaliyo kwenye skrini. Utakapokamilisha, bofya Chapisha.

Manufaa ya uanachama katika chaneli

Ni lazima uweke na uchapishe angalau manufaa moja (na hadi manufaa matano) ambayo utawapa wanachama wako. Ni lazima manufaa yako yafuate sera na sheria na masharti yetu, pia ni lazima uwasilishe marupurupu yanayotolewa na mtayarishi unayotoa. YouTube haiwajibikii marupurupu yako yanayotolewa na mtayarishi na ni lazima uzingatie kwa umakini ikiwa unaweza kuwasilisha manufaa unayotoa ili kuwaridhisha wanachama wako.

Machapisho ya Jumuiya ya Wanachama pekee
Unaweza kutumia kichupo cha jumuiya ili kushiriki maudhui na wanachama wako pekee. Ikiwa una viwango kwenye chaneli yako, unaweza pia kushiriki machapisho ya Jumuiya na wanachama katika viwango mahususi.
Fuata hatua hizi ili utayarishe Machapisho ya jumuiya ya wanachama pekee:
  1. Bofya picha yako ya wasifu  na uguse jina la chaneli yako.
  2. Bofya kichupo cha Jumuiya.
  3. Katika menyu kunjuzi, chagua kama utafanya chapisho kuwa la umma au la wanachama pekee. Kuwa la umma ndio mipangilio chaguomsingi.
  4. Weka chapisho lako kwenye sehemu ya maandishi.
  5. Bofya Chapisha.
Video ya wanachama pekee
Unaweza kuweka video ambayo itaonwa na wanachama wako wanaoendelea pekee. Mtu yeyote anaweza kupata video ya wanachama pekee, lakini wanachama walio katika viwango sahihi pekee ndio wanaweza kuitazama. Unaweza kuweka video iliyopo au mpya kuwa ya wanachama pekee kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi.
Video za wanachama pekee ni lazima ziwe za maudhui asili kabisa. Usiweke video zenye madai ya hakimiliki, zikiwemo video zenye madai kutoka kwa washirika wa muziki.

Kuweka video mpya kuwa ya kutazamwa na wanachama pekee

  1. Pakia video.
  2. Kwa ajili ya Uonekanaji, chagua Wanachama pekee.
    • Ikiwa una zaidi ya kiwango kimoja, chagua viwango vya uanachama ambavyo vinaweza kutazama video yako.
  3. Kamilisha mchakato wa upakiaji uliosalia.

Kuweka video iliyopo kuwa ya kutazamwa na wanachama pekee

  1. Tumia kompyuta kwenda kwenye Studio ya YouTube au fungua programu yako ya Studio ya YouTube kwenye kifaa chako cha mkononi.
  2. Chagua Maudhui
  3. Tafuta video ambayo ungependa kushiriki na wanachama wako pekee.
  4. Chagua Badilisha kisha Uonekanaji kisha Chagua Wanachama pekee kisha Chagua Hifadhi.
    • Ikiwa una zaidi ya kiwango kimoja, chagua viwango vya uanachama ambavyo vinaweza kutazama video yako.

Kutangaza video yako ya kutazamwa na wanachama pekee

Wanachama wako wanaweza kupata video za wanachama pekee kwenye vichupo vya Uanachama, Maudhui na Jumuiya kwenye chaneli. Video hizi pia zinaweza kujitokeza kwenye mipasho ya ukurasa wa Mwanzo na Usajili ya wanachama.

Watazamaji wanaopendekezewa maudhui yako, lakini si wanachama wanaweza pia kuona video za wanachama pekee kwenye Mipasho yao ya Ukurasa wa Kwanza. Kuonyesha video za wanachama pekee kwa wasio wanachama kunaweza kuwasaidia kugundua mipango ya uanachama katika chaneli ambayo wanaweza kutaka kujisajili. Watu wasio wanachama wanaweza kutazama kijipicha na jina la video, lakini hawawezi kutazama video ya wanachama pekee isipokuwa wakijisajili.

Ili uwafahamishe watazamaji wako kuwa video inapatikana, unaweza kushiriki URL hiyo hadharani kwenye:

  • Kadi
  • Jumuiya ya umma
  • Orodha za kucheza

Wanachama walio katika viwango sahihi wanaweza kutazama video za wanachama pekee papo hapo. Kidokezo kitaonekana kwa wasio wanachama kuwajulisha kuwa video inapatikana kwa wanachama tu, na namna wanavyoweza kuwa wanachama

Ufikiaji wa mapema kwa wanachama pekee

Unaweza kuweka maudhui unayopakia yafikiwe kwanza na wanachama pekee. Hali hii huwawezesha wanachama kuangalia na kushiriki kwenye maudhui yako kabla hujayachapisha hadharani. Wanachama wako wataarifiwa unapopakia maudhui kutoka kwa "Wanachama Pekee kuwa ya Umma". Video inapobadilika kuwa ya umma, watu wote wanaofuatilia kituo chako wataarifiwa. Tumegundua kuwa, kwa wastani, watayarishi walipowapa wanachama idhini ya kufikia video kwanza, utendaji wa video hizo haukubadilika na hazikuathiriwa vibaya baada ya kuchapishwa hadharani. (Kwenye chaneli zilizochapisha angalau video moja yenye idhini ya kufikiwa mapema na video moja ya umma pekee kati ya Januari na Februari 2023.)

Kuweka video mpya kuwa ya kutazamwa na wanachama pekee

  1. Pakia video.
  2. Kwa ajili ya Uonekanaji, chagua Kutoka ya wanachama pekee kuwa ya umma.
    • Ikiwa una zaidi ya kiwango kimoja, chagua viwango vya uanachama ambavyo ungependa vitazame video yako.

Chagua tarehe na saa ambazo ungependa video yako ibadilike kuwa ya umma.

Kutangaza video yako ya kutazamwa na wanachama pekee

Video za kutazamwa na wanachama pekee zinaweza kujitokeza kwenye mipasho ya wanachama ya ukurasa wa Mwanzo na usajili. Wanachama wanaweza pia kupata video kwenye vichupo vya maudhui na jumuiya vya ukurasa wa chaneli yako. Ili uwafahamishe watazamaji wako kuwa video inapatikana, unaweza kushiriki URL hiyo hadharani kwenye:

  • Kadi
  • Jumuiya ya umma
  • Orodha za kucheza

Wanachama wako wanaweza kutazama papo hapo video za kutazamwa na wanachama pekee katika viwango vyao sahihi. Wasio wanachama wataona dokezo linalosema kuwa inapatikana kwa wanachama pekee na wataonyeshwa njia za kuwa wanachama.

Mitiririko mubashara ya wanachama pekee

Unaweza kushiriki mitiririko mubashara na wanachama wako pekee.

Kwenye kompyuta:

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya ANZISHA .
  3. Bofya Tiririsha mubashara .
  4. Fuata hatua ili uanzishe mtiririko mubashara.
  5. Katika mipangilio ya uonekanaji, chagua ni wanachama gani wanaolipia wanaweza kutazama mtiririko wako mubashara:
    1. Mipangilio ya wanachama wote wanaolipia huruhusu mwanachama yeyote anayelipia kutazama mtiririko mubashara
    2. Kuchagua kiwango mahususi cha uanachama huruhusu wanachama wanaolipia katika kiwango kilichochaguliwa (na cha juu zaidi) kutazama mtiririko mubashara.
  6. Ili utayarishe chapisho la Jumuiya la wanachama pekee linalounganisha kwenye mtiririko mubashara, fuata vidokezo. Ikiwa wanachama wako wamewasha arifa, wataarifiwa unapoanzisha mtiririko mpya mubashara wa wanachama pekee.

Kwenye kifaa cha mkononi:

  1. Kwenye kifaa chako cha mkononi, fungua programu ya YouTube.
  2. Katika sehemu ya chini, gusa Anzisha kisha Tiririsha mubashara.
  3. Gusa Chaguo Zaidi kisha Onyesha zaidi.
  4. Katika mipangilio ya uonekanaji, chagua Wanachama tu kisha chagua ni wanachama gani wanaolipia wanaweza kutazama mtiririko wako mubashara:
    • Mipangilio ya wanachama wote wanaolipia huruhusu mwanachama yeyote anayelipia kutazama mtiririko mubashara
    • Kuchagua kiwango mahususi cha uanachama huruhusu wanachama wanaolipia katika kiwango kilichochaguliwa (na cha juu zaidi) kutazama mtiririko mubashara.
  5. Gusa Endelea kisha Tiririsha mubashara.
Gumzo la moja kwa moja la wanachama pekee
Unaweza kufanya gumzo liwe la wanachama pekee wakati wa mitiririko mubashara ya umma. Kila mtu bado anaweza kutazama mtiririko mubashara, lakini wanachama pekee ndio watakaoweza kuchapisha gumzo. Fuata hatua hizi kwenye kompyuta ya mezani ili uwashe gumzo la moja kwa moja la wanachama pekee:
  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika upande wa juu kulia, bofya ANZISHA  kisha Tiririsha moja kwa moja.
  3. Upande wa kushoto, bofya Tiririsha.
  4. Anzisha mtiririko:
    1. Ili unakili mtiririko wa awali: Chagua mtiririko wa awali kisha ubofye Tumia mipangilio tena.
    2. Ili uanzishe mtiririko mpya: Weka maelezo ya mtiririko wako kisha ubofye Anzisha mtiririko.
  5. Kwenye upande wa juu kulia, bofya Mipangilio .
  6. Kwenye sehemu ya "Gumzo la moja kwa moja," chagua Washa gumzo la wanachama pekee.
  7. Bofya Hifadhi.

Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama

Wanachama katika kituo wanaweza kutuma ujumbe mmoja maalum ulioangaziwa kila mwezi katika gumzo la moja kwa moja ili kutambua na kusherehekea muda ambao wamekuwa wanachama. Kipengele hiki kinapatikana kwa wanachama ambao wanatumia huduma, angalau, mwezi wao wa 2 mfululizo kama wanachama. Ujumbe unaweza kutumwa wakati wa mitiririko mubashara au Maonyesho ya kwanza na huonekana kwa watazamaji wote. 

(Ili uzime kipengele hiki, nenda kwenye Studio kisha Chuma mapato kisha Uanachama na uweke kipengele cha ‘Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama’ kuwa ‘Zima’.)

Kumbuka: Kwa kuwa wanachama wote wanaostahiki wanaweza kutumia Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama, unaweza kuona matumizi makubwa mara chache za kwanza unapotiririsha mubashara baada ya kipengele hiki kuwashwa. Kiwango kinapaswa kurekebishwa baada ya muda kwani kila mwanachama anaweza kutumia Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama mara moja kwa mwezi.

Rafu ya Kutambua Wanachama

Ili uwatambue hadharani wanachama katika chaneli yako, unaweza kuangazia avata zao kwenye rafu katika sehemu ya juu ya ukurasa wa chaneli yako. Rafu hii ni njia yako ya kuwashukuru wanachama katika kituo chako na kuwaonyesha wengine jinsi unavyothamini wanachama wako. Wanachama wanaoangaziwa huchaguliwa bila mpangilio na watabadilika mara kwa mara ili kuwapa wanachama zaidi nafasi ya kuonekana. Wanachama wanaotazama ukurasa wa chaneli yako watapata avata zao kwenye rafu kila wakati. Ikiwa mwanachama ataghairi uanachama wake, hataangaziwa tena kwenye rafu.  

Kumbuka: Kipengele hiki kitawashwa kiotomatiki, kituo chako kitakapokuwa na wanachama 8 au zaidi. 
Ni lazima wanachama wawe wanachangia na wanarejelea mara kwa mara ili waangaziwe kwenye rafu.

Ili uzime kipengele cha rafu ya kutambua wanachama:

  1. Tumia kompyuta ili uingie katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Nenda kwenye Chuma mapato kisha Uanachama.
  3. Zima "Rafu ya Kutambua Wanachama."

Beji za chaneli maaalum

Wanachama watatambulika kwenye gumzo la moja kwa moja, maoni na Kichupo cha jumuiya kupitia beji za wanachama pekee.

Muhtasari wa beji za Kituo maalum
Kuna beji nane tofauti na kila moja inaangazia muda ambao mtazamaji amekuwa mwanachama wa kituo chako mahususi. Muda wa beji huhesabu muda ambao kila mwanachama amelipia uanachama wake kwa jumla. Kwa mfano, ikiwa mwanachama mshiriki alijiunga na kituo chako mwaka mmoja uliopita, lakini akalipia jumla ya miezi 9 kati ya miezi 12 iliyopita, beji yake itaonyesha kwamba amekuwa mwanachama kwa miezi 9.
Hapa kuna muda unaohusishwa na kila beji kati ya beji 8:
  • Mpya
  • Mwezi 1
  • Miezi 2
  • Miezi 6
  • Mwaka 1
  • Miaka 2
  • Miaka 3
  • Miaka 4

Pakia beji za kituo maalum

Kuna beji chaguomsingi, lakini unapaswa kupakia na kuziwekea beji zako mapendeleo kwenye ukurasa wa Uanachama kisha Beji za Uaminifu.
Ikiwa hutapakia beji tofauti kwenye kila nafasi iliyopo, nafasi zozote zilizo tupu zitajazwa na beji maalum ya juu zaidi ambayo umeipakia au beji chaguo msingi ya YouTube kwa muda huo (iwapo umepakia tu beji maalum katika vipindi vya juu zaidi).

Vigezo vya beji za kituo maalum

Aina ya faili: faili za JPEG au PNG.
Ukubwa wa faili: Chini ya MB 1.
Ukubwa wa picha: Ukubwa wa chini wa pikseli 32 x 32.
Beji zitaonekana katika ukubwa wa pikseli 14 x 14 kwenye maoni na kichupo cha Jumuiya na pikseli 16 x 16 kwenye gumzo la moja kwa moja.

Emoji maalum

Kupakia emoji maalum
Wanachama watapata uwezo wa kufikia emoji moja au zaidi ya kipekee ambayo inaweza kutumwa kupitia YouTube katika maoni ya video. Inaweza pia kutumwa katika gumzo zako zozote za moja kwa moja. Kwa chaguomsingi, hakuna emoji maalum.
Ili upakie emoji maalum, nenda kwenye ukurasa wa Uanachamaa na uchague Badilisha kwenye kadi ya “Beji na emoji zako."

Jina la Familia

Custom emoji can be sent in video comments or any live chats.

Unapopakia emoji yako ya kwanza, utatengeneza jina la kiambishi awali la emoji zako zote, linaloitwa 'jina la familia. Wanachama watatumia jina hili kujaza emoji yako kiotomatiki. Unaweza pia kukamilisha kiotomatiki emoji za kituo chako na :_ .

Majina ya familia si ya kipekee kote kwenye YouTube na lazima yawe na herufi 3 hadi 10.

Kama mbinu bora, tunapendekeza uchague jina la familia ambalo linatambulika kwa urahisi kuwa chapa yako.

Jina la Emoji

Kila emoji itakuwa na jina ambalo wanachama wanaweza kutumia ili kujaza kiotomatiki katika gumzo la moja kwa moja. Ili ubadilishe jina la emoji, ni lazima ufute na upakie upya emoji. Majina ya emoji lazima yawe na herufi 3 hadi 10 zilichonganywa na nambari na yawe ya kipekee katika vikundi vyake vya emoji (lakini si kwenye YouTube).

Idadi ya emoji maalum unayoweza kupakia

Unapopata wanachama zaidi, utafungua nafasi za ziada kwa emoji maalum zaidi. Hutaarifiwa nafasi mpya zitakapofunguliwa.

# Wanachama # Emoji
0 4
2 5
5 6
10 7
15 8
20 9
30 10
40 11
50 12
75 13
100 14
125 15
150 16
175 17
200 18
225 19
250 20
300 21
350 22
400 23
450 24
500 25
600 26
700 27
800 28
900 29
1000 30
1200 31
1400 32
1600 33
1800 34
2000 35
2200 36
2400 37
2600 38
2800 39
3000 40
3200 41
3400 42
3600 43
3800 44
4000 45
4200 46
4400 47
4600 48
4800 49
5000 54
Vigezo vya emoji maalum
Muundo wa faili: Faili za GIF, JPEG na PNG ndizo zinazopendelewa. Kumbuka: GIF zitaonyeshwa kama picha tuli, si uhuishaji.
Ukubwa wa faili: Chini ya MB 1.
Ukubwa wa picha: pikseli 48 x 48 (ndio unaopendelewa) kuliko pikseli 480 x 480.

Tofauti za vifaa

Emoji itaonekana katika ukubwa tofauti kwenye vifaa vya mkononi na kwenye kompyuta. Hivi ndivyo jinsi ya kufanya emoji yako ionekane vizuri kwenye mifumo yote miwili:
Kwenye vifaa vya mikononi: Emoji huonekana kwa pointi 24x24. Picha hurekebishwa ili iendane na uzito wa pikseli wa kifaa.
Kwenye kompyuta nyingi: Emoji huonekana kwa pointi 24x24. Kwenye vifaa vya Retina and HiDPI, picha huonekana kwa pointi 48x48 au zaidi.

Ninaweza kubuni nini?

Emoji ni njia yako ya kueleza ubunifu wako. Pata maelezo zaidi kuhusu kubuni emoji.
Kumbuka kwamba manufaa yote ya wanachama pekee, ikiwa ni pamoja na beji, emoji, manufaa unayotoa, video, gumzo za moja kwa moja na maudhui mengine yanayotolewa kupitia uanachama wa YouTube yanategemea sera za uanachama.
Ikiwa una video za ziada, unaweza kuzitoa kama manufaa ya uanachama. Ni njia ya haraka ya kuwazawadia wanachama wako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12316433408822482938
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false