Pata mpango wa familia wa YouTube ili uweze kutumia Uanachama wa YouTube unaolipiwa au Chaneli za Primetime (Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia na Uingereza pekee), pamoja na hadi wanafamilia wengine 5 wa nyumbani kwako.
Jinsi ya Kuanzisha Vikundi vya Familia kwenye YouTube na YouTube TV
Jinsi mpango wa familia unavyotumika
Mipango ya familia ya YouTube inakuwezesha kutumia manufaa ya uanachama na hadi wanafamilia 5 wanaoishi kwenye anwani sawa ya makazi.
- Msimamizi wa familia:
- Ni mmiliki wa akaunti ya msingi.
- Anaunda Kikundi cha familia kwenye Google na anaweza kualika wanafamilia kwenye kikundi.
- Wanafamilia:
- Hutumia akaunti zao wenyewe za Google ili kufikia uanachama unaotumiwa pamoja.
- Wanaweza kutazama maudhui ya Chaneli za Primetime yanayonunuliwa na msimamizi wa familia. Wanafamilia wanaweza pia kununua Chaneli ya Primetime yao wenyewe, ambayo haitashirikiwa na msimamizi wa familia.
- Watakuwa na maktaba yao binafsi, usajili na mapendekezo - hatutashiriki mapendeleo ya kuangalia au historia ya video walizotazama kwenye akaunti za wanafamilia.
- Mipaka ya umri inatumika kwa wanafamilia walio chini ya umri wa miaka 18.
- Vikundi vya familia hutumia kwa pamoja:
- YouTube Premium
- YouTube Music Premium
- Chaneli za Primetime za YouTube (Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia na Uingereza pekee)
- Na huduma nyingine za Google. Pata maelezo zaidi kuhusu vikundi vya familia kwenye Google.
Mipango ya familia kwenye YouTube Premium
Mipango ya familia kwenye YouTube Music Premium
Mipango ya familia kwenye YouTube TV
- Ingia katika akaunti kwenye YouTube TV.
- Chagua picha yako ya wasifu Mipangilio Kushiriki na familia .
- Chagua Weka mipangilio.
- Anzisha kikundi cha familia kwenye Google.
- Kubali Sheria na Masharti ya Huduma za YouTube Zinazolipiwa na Sera ya Faragha ya Google.
- Chagua Ghairi au Endelea.
- Wanafamilia wako watapokea barua pepe ya mwaliko wa kujiunga kwenye kikundi na wanaweza kuingia katika akaunti wakitumia akaunti zao za Google.
Mipango ya familia kwenye Chaneli za YouTube Primetime
Masharti ya kikundi cha familia
Masharti ya Msimamizi wa Familia
Ukiwa msimamizi wa familia, wewe ndiwe mtu pekee anayeweza kununua mpango wa familia wa YouTube au kufanya maamuzi ya uanachama kwa ajili ya kikundi cha familia. Utaweka maelezo ya mahali walipo wanafamilia na utaweza kualika au kuondoa wanafamilia.
Ili utumie mpango wako wa familia wa YouTube pamoja na kikundi chako cha familia, lazima:
- Uwe na umri wa miaka 18 au zaidi (au umri unaofaa eneo uliko).
- Uwe na Akaunti ya Google. Iwapo una akaunti ya Google Workspace, utahitaji kufungua au kuingia katika akaunti yako ya kawaida ya Google.
- Uwe unaishi katika nchi ambako YouTube Premium, YouTube Music Premium au Chaneli za Primetime zinapatikana.
- Kumbuka:
- Mipango ya familia haipatikani nchini Korea.
- Chaneli za Primetime zinapatikana tu nchini Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia na Uingereza.
- Kumbuka:
- Usiwe umejiunga na kikundi kingine cha familia.
- Uwe hujabadilisha vikundi vya familia katika miezi 12 iliyopita.
Masharti ya mwanafamilia
Msimamizi wa familia anaweza kualika hadi wanafamilia 5 wajiunge na kikundi cha familia. Ili ujiunge na kikundi cha familia kinachotumia kwa pamoja mpango wa familia wa YouTube, ni lazima:
- Uwe na akaunti ya Google. Iwapo una akaunti ya Google Workspace, utahitaji kufungua au kuingia katika akaunti yako ya kawaida ya Google.
- Uwe unaishi kwenye makazi sawa na msimamizi wa familia.
- Uwe unaishi katika nchi au eneo ambako YouTube Premium, YouTube Music Premium au Chaneli za Primetime zinapatikana.
- Usiwe umejiunga na kikundi kingine cha familia.
- Uwe hujabadilisha vikundi vya familia katika miezi 12 iliyopita.