Arifa

Our teams are currently experiencing high support volumes. Please expect longer than usual wait times for responses to questions from email, chat, and @TeamYouTube on Twitter

Maudhui yako ya YouTube na Hali yenye Mipaka

Hali yenye Mipaka ni mipangilio isiyo ya lazima ambayo imekuwepo tangu 2010. Sehemu ndogo ya watumiaji, kama vile maktaba, shule na taasisi za umma, ambazo zinataka hali mahususi ya utumiaji kwenye YouTube huwa zinatumia Hali yenye Mipaka.

Kumbuka: Hali yenye Mipaka imezimwa kwa watazamaji kwa chaguomsingi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasha au kuzima Hali yenye Mipaka.

Je, Hali yenye Mipaka hufanya nini?
Hali yenye Mipaka ilibuniwa ili kuwapa watazamaji udhibiti bora wa maudhui wanayoyaona. Hali hii inaweka mipaka kwa utumiaji wako wa YouTube kwa kukusudia.
Watazamaji wanaweza kuchagua kuwasha Hali yenye Mipaka katika akaunti zao binafsi. Inaweza pia kuwashwa kwenye kompyuta katika maktaba, shule na taasisi nyingine za umma na msimamizi wa mfumo wa taasisi hiyo. Watazamaji ambao wamewasha Hali yenye Mipaka hawawezi kuona maoni kwenye video. 
Hali yenye Mipaka hufanya kazi vipi?
Kuna sababu mbili zinazoweza kufanya video isipatikane wakati Hali yenye Mipaka imewashwa.
  • Kimsingi, mfumo wetu wa kiotomatiki huangalia ishara kama vile metadata ya video, kichwa na lugha ambayo imetumiwa kwenye video hiyo.
  • Baadhi ya video huenda zisiwepo katika Hali yenye Mipaka kwa sababu wakaguzi wetu ambao ni binadamu wameweka mipaka ya umri.
Tunaelewa kwamba mfumo wetu wa kiotomatiki wakati mwingine hufanya makosa unapotathmini video ambazo zinapatikana katika Hali yenye Mipaka. Tunalenga kila wakati kuboresha mifumo yetu ya kiotomatiki.
Je, maudhui yangu yataonyeshwa ikiwa watazamaji wangu wamewasha Hali yenye Mipaka?

Video zinazoonyesha maudhui ambayo huenda ni ya watu wazima hazitaonyeshwa kwa watazamaji ambao wamewasha Hali yenye Mipaka.

  • Dawa za kulevya na pombe: Kuzungumza kuhusu matumizi au matumizi mabaya ya dawa za kulevya au unywaji wa pombe kwenye video.
  • Hali zinazohusisha ngono: Mazungumzo ya kina sana kuhusu au yanayoonyesha ngono au vitendo vya ngono. Baadhi ya maudhui ya elimu na ya moja kwa moja kuhusu elimu ya ngono, mahaba, au utambulisho yanaweza kuonyeshwa katika Hali yenye Mipaka. Busu au mahaba ambayo si ya ngono kupita kiasi wala shabaha ya video pia yanaweza kuonyeshwa katika Hali yenye Mipaka.
  • Vurugu: Picha au video za kuogofya zinazoeleza kuhusu vurugu, vitendo vya vurugu, maafa na mikasa kutokana na hali asilia au vurugu kwenye habari.
  • Mada zilizokomaa: Video zinazoshughulikia maelezo mahususi kuhusu matukio yanayohusiana na ugaidi, vita, uhalifu na migogoro ya kisiasa iliyosababisha vifo au jeraha baya. Video hizi hazitaonyeshwa katika Hali yenye Mipaka, hata kama hakuna picha au video ya kuogofya inayoonyeshwa.
  • Lugha chafu na lugha ya watu wazima: Lugha isiyofaa, ikijumuisha lugha chafu.
  • Maudhui ya uchochezi na kushusha hadhi: Maudhui ya video ambayo ni ya uchochezi au ya kushusha hadhi ya watu au kundi la watu.
Tunafahamu kwamba kuna uwezekano wa kupoteza maudhui muhimu tunapotekeleza amri hizi bila kuzingatia muktadha. Tunathamini simulizi ambapo watu wanajadili hali wanazopitia na kushiriki hisia zao. Kushiriki simulizi kuhusu kukabiliwa na ubaguzi, kusema yaliyo moyoni kuhusu hali yako ya kingono na kukabili au kushinda ubaguzi ndiyo hufanya YouTube kuwa bora. Tutafanya juhudi ili kuhakikisha kwamba simulizi hizo zinajumuishwa kwenye Hali yenye Mipaka. Lakini, ni sharti maudhui yako yafuate mwongozo ulio hapo juu ili simulizi hizo zijumuishwe.
Je, Hali yenye Mipaka ni sawa na video zenye uthibitishaji wa umri au zilizowekewa mipaka ya umri?
Hapana, ikiwa video haipatikani katika Hali yenye Mipaka, hiyo haimaanishi kwamba imewekewa mipaka ya umri.
Maudhui yenye mipaka ya umri huenda yasifae kwa hadhira zote. Maudhui hayatapatikana kwa watumiaji ambao:
  • Wameondoka katika akaunti
  • Wana umri wa chini ya miaka 18
  • Wamewasha Hali yenye Mipaka
Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yaliyo na mipaka ya umri.
Je, ninawezaje kuangalia iwapo video zangu zimechujwa kupitia Hali yenye Mipaka ya YouTube? 
Ili uangalie, unaweza kuwasha Hali yenye Mipaka. Kisha, utafute YouTube ili uone ikiwa video hiyo itaonekana. Unaweza pia kuenda moja kwa moja kwenye URL ya video hiyo ili uone kama inaweza kutazamwa au la.
Kumbuka: Wakati mwingine, video hazipatikani katika Hali yenye Mipaka zinapopakiwa kwa mara ya kwanza kwa sababu ni sharti mfumo wetu uzikague. Ruhusu muda fulani kabla ya kuangalia ikiwa video yako inapatikana katika Hali yenye Mipaka.
Je, video yangu huchujwa katika Hali yenye Mipaka inaporipotiwa kama isiyofaa na jumuiya?
Video haichujwi kiotomatiki katika Hali yenye Mipaka jumuiya inapoiripoti.
Ukaguzi wa timu yetu uliripoti video kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu. Baadhi ya video hazikiuki sera zetu, lakini huenda zisifae watazamaji wote. Katika hali hizi, timu yetu ya ukaguzi inaweza kuweka mipaka ya umri kwenye video hiyo. Video zilizo na mipaka ya umri hazitaonekana kwa watumiaji ambao wamewasha Hali yenye mipaka.
Je, Hali yenye Mipaka huathiri uchumaji mapato wa video zangu?
Bado unaweza kuchuma mapato kutokana na video hata kama huenda zisipatikane unapowasha Hali yenye Mipaka.
Video zangu zinachujwa kupitia Hali yenye Mipaka. Ninaweza kufanya nini ili kuzuia uchujaji huu usifanyike?
Kama umehariri video hiyo, mfumo wetu unaweza kuikagua tena. Ikiwa baada ya kukagua mwongozo wetu, bado utahisi kuwa video yako inafaa kuonyeshwa katika Hali yenye Mipaka, tufahamishe kwa kutuma maoni yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8789720832590205987
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false