Ondoa uwezo wa kufikia Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako

Iwapo wewe ni mtayarishi mshirika na unaamini kuwa mkataba wako na Mtandao wa Vituo Mbalimbali unakuruhusu kufanya hivyo, unaweza kuanza mchakato wa kuondoa uwezo wa kufikia Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika dashibodi ya Kituo, utaona kadi ya Uhusiano wa mtandao.
  3. Bofya Ondoa uwezo wa kufikia katika kadi hiyo ili uondoe uwezo wa kufikia wa Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako. Utaona skrini ya dirisha ibukizi​ ikionyesha Mtandao wa Vituo Mbalimbali una siku 30 kujibu ombi lako, la sivyo ufikiaji utaondolewa kiotomatiki ndani ya siku 30 au chini ya hapo.
  4. Bofya ONDOKA KWENYE MTANDAO ili uthibitishe.
Muhimu: Iwapo utaondoka kwenye Mtandao wa Chaneli Mbalimbali, utahitaji kuweka mipangilio ya uchumaji wa mapato kisha uunganishe akaunti yako na AdSense katika YouTube ili uendelee kuchuma mapato na kulipwa.

Nini kitatokea nikibofya ili kuondoa uwezo wangu wa kufikia Mtandao wa Chaneli Mbalimbali ilhali muda wa mkataba haujaisha?

Kabla ya kubofya ili kuondoa uwezo wa kufikia, unapaswa kukagua masharti ya mkataba wako na Mtandao wa Vituo Mbalimbali. Iwapo bado uko chini ya mkataba na Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali, hatua ya kuondoa uwezo wa kuufikia inaweza isikutoe katika wajibu wowote wa kisheria na kufanya hivyo kunaweza kukuweka katika hatia ya ukiukaji wa mkataba. Vituo vya washirika ambavyo havina uhakika na maana ya wajibu huo huenda vikahitaji kujadili na Mtandao wa Vituo Mbalimbali au mshauri wao kisheria.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7505846910385661503
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false