Uchumaji wa Mapato wakati wa mizozo ya Content ID

Video zinaweza kuchuma mapato wakati zina mizozo ya Content ID kama mtayarishi wa video na mlalamishi wa Content ID wangependa video hiyo ichume mapato. Unaweza kupinga dai la Content ID wakati wowote. Ukipinga dai ndani ya siku 5, mapato yoyote kutoka kwenye video hiyo yatazuiwa, kuanzia siku ya kwanza ambapo dai liliwasilishwa. Iwapo utapinga dai la Content ID baada ya siku 5 kuanzia tarehe ambapo dai liliwasilishwa, tutaanza kuzuia mapato tarehe ambayo dai liliwasilishwa.

Katika mchakato huu wote wa kupinga dai, mapato yatazuiwa kivyake na baada ya mzozo kusuluhishwa, tutamtalipa mshirika atakayefaa.

Yafuatayo ni maelezo zaidi kuhusu kitakachofanyika kwenye video wakati wa mchakato wa kupinga dai la Content ID:

Kuwasilisha ombi la kupinga dai la Content ID

Baada ya dai la Content ID kuwasilishwa kuhusu video yako, una chaguo kadhaa za kujibu:

  • Kutochukua hatua yoyote na kuruhusu dai liendelee kwenye video yako: Baada ya siku 5 kuanzia tarehe ambapo dai liliwasilishwa, mapato yoyote yaliyozuiliwa yatatolewa kwa mlalamishi.
  • Kupinga dai ndani ya siku 5: Matangazo yataendelea kuonyeshwa. Mapato yote ambayo video inachuma yatazuiwa huku mlalamishi akiendelea kukagua mzozo wako.
  • Kupinga dai baada ya siku 5: Mapato kuanzia tarehe ambapo mzozo uliwasilishwa yatazuiwa huku mlalamishi akiendelea kukagua mzozo wako.

Pata maelezo zaidi kuhusu kitakachofanyika wakati unapinga dai la Content ID.

Kukata rufaa dhidi ya dai la Content ID

Ukichagua kukata rufaa dhidi ya dai la kurejesha maudhui au uelekeze kwenye rufaa, una chaguo kadhaa:

  • Kutofanya chochote na kuruhusu dai liendelee kuwepo kwenye video: Baada ya siku 5, mapato yoyote yaliyozuiliwa yatatolewa kwa mlalamishi.
  • Kukata rufaa ndani ya siku 5: Matangazo yataendelea kuonyeshwa. Mapato yote ambayo video inachuma yatazuiwa huku mlalamishi akiendelea kukagua rufaa yako.
  • Kukata rufaa baada ya siku 5: Mapato kuanzia tarehe ya kukata rufaa yatazuiwa huku mlalamishi akiendelea kukagua rufaa yako.

Pata maelezo zaidi kuhusu kitakachofanyika utakapo kata rufaa dhidi ya dai la Content ID.

Mapato kutokana na mizozo katika Takwimu za YouTube

Iwapo kuna dai la Content ID linaloendelea kwenye video yako na upinge au ukate rufaa dhidi ya dai hilo, data ya mapato ya video hiyo haitaonekana katika Takwimu za YouTube. Iwapo dai litaondolewa, data ya mapato ya kipindi cha mzozo itawekwa baadaye kwenye Takwimu za YouTube. Iwapo dai litatatuliwa mapema mwezi huu, data hii inapaswa kuonekana kati ya tarehe 10 na 20 ya mwezi ujao. Iwapo dai litatatuliwa karibu na mwisho wa mwezi, data inaweza kuonekana kati ya tarehe 10 na 20 miezi 2 baadaye.

Kwa mfano:
  • Ulipinga dai la Content ID tarehe 12 Julai na mzozo ukasuluhishwa kwa manufaa yako tarehe 6 Agosti. Data yako ya mapato ya tarehe 12 Julai hadi 6 Agosti itaonyeshwa kwenye Takwimu kati ya tarehe 10 Septemba na 20 Septemba.
  • Ulipinga dai la Content ID tarehe 4 Agosti na mzozo ukasuluhishwa kwa manufaa yako tarehe 29 Agosti. Data yako ya mapato ya tarehe 4 Agosti hadi 29 Agosti itaonyeshwa kwenye Takwimu kati ya tarehe 10 Oktoba na 20 Oktoba.
Iwapo una idhini ya kufikia Ripoti Zinazoweza Kupakuliwa katika Kidhibiti Maudhui, utapata maelezo haya katika Ripoti yako ya Marekebisho.
Unaweza kuchagua usichume mapato kwenye video wakati wa mzozo, kwa kuzima uchumaji wa mapato kwenye Ukurasa wa video katika Studio ya YouTube.

Pata usaidizi kuhusu Content ID

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9892582683560606738
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false