Maswali yanayoulizwa sana kuhusu matumizi ya haki

Matumizi ya haki ni kanuni ya kisheria inayosema kwamba unaweza kutumia tena nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki katika hali fulani bila ruhusa ya mwenye hakimiliki.

Hamna maneno yoyote maalum ya kuzingatia katika matumizi ya haki kiotomatiki. Unapotumia kazi ya mtu mwingine iliyo na hakimiliki, hamna hakikisho kuwa unalindwa chini ya matumizi ya haki.

Matumizi ya Haki - Hakimiliki kwenye YouTube

 

 

Maswali ya kawaida kuhusu matumizi ya haki

Matumizi ya haki hufanya kazi vipi?
Nchini Marekani, hakimu hukagua kesi mahususi kulingana na kundi la kanuni ili kuamua iwapo matumizi ya haki yatazingatiwa. Maeneo au nchi tofauti zina kanuni tofauti kuhusu wakati unaofaa kutumia nyenzo bila ruhusa ya mwenye hakimiliki. Kwa mfano, nchini Marekani, kazi za kutoa maoni, kukosoa, utafiti, mafunzo au kuripoti habari zinaweza kuchukuliwa kama matumizi ya haki. Baadhi ya nchi zingine zina dhana kama hii inayoitwa matumizi yasiyo ya biashara ambayo yanaweza kufanya kazi kwa njia tofauti.
Matumizi ya haki yanajumuisha nini?

1. Madhumuni na sifa ya matumizi, ikiwa ni pamoja na iwapo utumiaji huo ni wa asili ya kibiashara au ni kwa madhumuni ya elimu bila manufaa ya kifedha

Kwa kawaida mahakama hubaini iwapo matumizi “yanaleta mabadiliko.” Yaani, iwapo matumizi yanaongeza thamani au maana mpya kwenye nyenzo halisi, au iwapo yanarudia tu maana iliyo kwenye nyenzo halisi. Kuna uwezekano mdogo kuwa matumizi ya kibiashara yatachukuliwa kama matumizi ya haki, ingawa kuna uwezekano wa kuchuma mapato kupitia video na bado yawe matumizi ya haki.

2. Hali ya kazi iliyo na hakimiliki

Kutumia nyenzo kutoka kwenye kazi za ukweli kimsingi kunaweza kuzingatiwa kama matumizi ya haki kuliko kutumia kazi za kubuni.

3. Kiasi na umuhimu wa sehemu iliyotumiwa ikilinganishwa na kazi iliyo na hakimiliki kwa jumla

Kuazima sehemu ndogo za nyenzo kutoka kwenye kazi halisi kuna uwezekano mkubwa wa kuchukuliwa kuwa matumizi ya haki kuliko kuazima sehemu kubwa. Hata hivyo, kama ni “sehemu kuu” ya kazi, hata kiasi kidogo kinaweza kuathiri matumizi ya haki katika hali fulani.

4. Athari ya matumizi kwenye soko tarajiwa, au thamani ya, kazi iliyo na hakimiliki

Matumizi yanayodhuru uwezo wa mwenye hakimiliki wa kupata faida kutokana na kazi yake halisi yana uwezekano mdogo wa kuwa matumizi ya haki. Wakati mwingine mahakama hazifuati kanuni chini ya kigezo hiki katika kesi zinazojumuisha miigo ya kubeza.

Matumizi ya haki hurejelewa wakati gani?
Kumtaja mwenye hakimiliki, kuchapisha kanusho kama vile "hamna ukiukaji unaonuiwa," au kuongeza maudhui halisi kwenye maudhui ya mtu mwingine hakufanyi maudhui yawe matumizi ya haki kiotomatiki. Utumiaji unaojaribu kubadilisha kazi halisi badala ya kutoa maoni kuhusu au kukosoa yana uwezekano mdogo wa kuchukuliwa kuwa matumizi ya haki.
Content ID hufanya kazi vipi pamoja na matumizi ya haki?

Ukipakia video iliyo na maudhui yaliyo na hakimiliki bila ruhusa ya mwenye hakimiliki, huenda ukapokea dai la Content ID. Dai hilo litakuzuia usichume mapato kwenye video, hata kama utatumia tu sekunde chache, kama vile matumizi mafupi ya nyimbo maarufu.

Mifumo ya kiotomatiki kama vile Content ID haiwezi kuamua matumizi ya haki kwa sababu uamuzi huo ni wa kipekee na hulingana na kila kesi. Ni mahakama pekee zinazoweza kuamua. Ingawa hatuwezi kuamua matumizi ya haki au kuleta upatanisho katika mizozo ya hakimiliki, bado matumizi ya haki yanaweza kuwepo kwenye YouTube. Iwapo unaamini kuwa video yako iko chini ya matumizi ya haki, unaweza kujitetea kupitia mchakato wa kupinga dai la Content ID. Uamuzi huu haupaswi kuchukuliwa kwa urahisi. Wakati mwingine, utahitaji kuendeleza mchakato huo wa kupinga dai kwenye hatua ya kukata rufaa na mchakato wa arifa ya kukanusha wa DMCA.

Iwapo wewe na mlalamishi mtajaribu kuchuma mapato kwenye video mnayozozania, bado video hiyo itachuma mapato hadi mzozo utatuliwe. Kisha, tutatuma mapato yatakayokusanywa kwa mhusika atakayefaa.  

Chaguo unazoweza kutumia kusuluhisha madai nje ya mchakato wa kupinga dai

Njia rahisi zaidi ya kushughulikia madai ya Content ID ni kuyaepuka kwanza. Usitumie nyenzo zilizo na hakimiliki isipokuwa ni muhimu kwenye video yako. Angalia Maktaba ya Sauti kwenye YouTube ili uone muziki unaoweza kutumia bila malipo katika video zako. Ukichagua kupata muziki kutoka kwenye tovuti nyingine za kutoa leseni au ambazo hamna mirabaha, hakikisha umesoma sheria na masharti kwa umakini. Huenda baadhi ya huduma hizi zisitoe haki za kutumia au kuchuma mapato kupitia muziki kwenye YouTube, kwa hivyo huenda bado ukapata dai la Content ID.

Ukipata dai la Content ID kwa muziki ambao si muhimu kwenye video yako, jaribu kuuondoa au kuubadilisha na utumie nyimbo zinazoweza kutumiwa bila ruhusa ya mwenye hakimiliki kutoka kwenye Maktaba ya Sauti. Unaweza pia kupakia mabadiliko yote mapya ya video bila maudhui yanayodaiwa katika URL mpya.

Je, ninalindwa na matumizi ya haki iwapo...

Nilimtaja mwenye hakimiliki?

Kwa kawaida, mabadiliko ni muhimu katika uchanganuzi wa matumizi ya haki. Kumtambulisha mmiliki wa kazi iliyo na hakimiliki hakutafanya nakala ya kazi isiyoweza kuleta mabadiliko ya nyenzo yake kuwa matumizi ya haki. Kauli kama vile “haki zote ni za mtunzi” na “Similiki” hazimaanishi kiotomatiki kuwa unafanya matumizi ya haki ya nyenzo hiyo. Pia, hazimaanishi kuwa una ruhusa ya mwenye hakimiliki.

Nilichapisha kanusho kwenye video yangu?
Hamna maneno yoyote maalum ya kuzingatia katika matumizi ya haki kiotomatiki unapotumia kazi ya mtu mwingine iliyo na hakimiliki. Kujumuisha kauli hii “hamna ukiukaji unaonuiwa” hakutakulinda kiotomatiki usipokee dai la ukiukaji wa hakimiliki.
Ninatumia maudhui kwa maudhumuni ya "burudani" au "yasiyo ya faida"?

Korti itakagua kwa umakini madhumuni ya utumiaji wako ili kutathmini iwapo ni matumizi ya haki. Kubainisha kuwa maudhui uliyopakia ni “ya madhumuni ya burudani pekee,” kwa mfano, huenda kusibadilishe kipimo cha kubaini matumizi ya haki. Vilevile, matumizi “yasiyo ya faida” hupendelewa katika uchanganuzi wa matumizi ya haki, lakini hayatoshi kutumiwa kujitetea kivyake.

Niliongeza nyenzo halisi niliyobuni kwenye kazi ya mtu mwingine iliyo na hakimiliki?
Hata kama umeongeza kitu kwenye maudhui ya mtu mwingine, huenda matumizi yako yasichukuliwe kuwa ya haki. Iwapo kazi yako haiongezi maana, ujumbe au thamani mpya kwenye kazi halisi, kuna uwezekano kuwa si matumizi ya haki. Kama ilivyo katika hali nyingine zote zilizojadiliwa hapa, mahakama zitazingatia vigezo vyote vinne vya jaribio la matumizi ya haki, ikiwa ni pamoja na kiasi cha maudhui halisi yaliyotumiwa.
Je, nikiwa nje ya Marekani?
Ingawa mara kwa mara sheria kuhusu hali zisizofuata kanuni za hakimiliki hufanana kote duniani, zinaweza kutofautiana. Nchi na maeneo mbalimbali yanaweza kuwa na sheria tofauti kuhusu ni wakati upi ni sawa kutumia maudhui yanayolindwa na hakimiliki bila ruhusa ya mwenye hakimiliki.
Mahakama huamua kesi za matumizi ya haki kulingana na ukweli wa kila kesi. Huenda ungependa kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa mtaalamu kabla ya kupakia video zinazotumia maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki.

Maelezo zaidi

Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya haki, kuna nyenzo nyingi zinazopatikana mtandaoni. Tovuti zifuatazo ni za madhumuni ya kielimu pekee na hazijaidhinishwa na YouTube:

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17968191179996820700
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false