Kuchangisha pesa kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kwa kutumia Uhisani wa YouTube

Mashirika yasiyo ya faida yanaweza kuchangisha pesa kwenye YouTube kupitia njia kadhaa tofauti. Mashirika yasiyo ya faida yanayostahiki nchini Marekani yanaweza kuchangiwa pesa kwa kutumia kitufe cha Kuchanga na vituo vinavyoweza kufikia Uhisani wa YouTube.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Ustahiki wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Mimi ni shirika lisilo la faida. Je, ninaweza kuchangisha pesa kwenye kituo changu cha YouTube?

Ili kuanzisha mchango wa Uhisani wa YouTube, kituo chako lazima kitimize masharti fulani ya kujiunga.

Ningependa kuhakikisha kuwa shirika langu lisilo la faida linastahiki kuchangiwa pesa na mtayarishi wa YouTube kwa kutumia Uhisani wa YouTube. Ninawezaje kufanya hivyo?

Watayarishi wanaostahiki wanaweza kuchanga pesa kwa shirika lako lisilo la faida kwa kutumia Uhisani wa YouTube. Ili kutimiza masharti ya kupokea pesa kutoka kwenye Michango ya Uhisani wa YouTube, shirika lisilo la faida linapaswa:
  • Kuwa limeombwa na mtayarishi.
  • Kuwa limesajiliwa kama shirika la Misaada ya Umma kwa mujibu wa sheria ya Marekani ya 501(c)(3).
  • Kuwa linashiriki kwenye mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.
  • Kuwa limejumuishwa kwenye michango ya mtandaoni kupitia GuideStar.
  • Kufuata sera za uchumaji wa mapato za YouTube, kwa wanaotumia na wasiotumia YouTube. Sera hizi zinajumuisha kufuata Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube.
Pata maelezo zaidi kuhusu Uhisani wa YouTube.

Shirika langu lisilo la faida linatimiza masharti ya Uhisani wa YouTube lakini haliwezi kupatikana wala kuombwa. Kwa nini?

Ili kutimiza masharti ya kupokea pesa kutoka kwenye mchango wa Uhisani wa YouTube, ni lazima shirika lisilo la faida litimize masharti ya kujiunga ya mashirika yasiyo ya faida.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazofanya shirika lisilo la faida unalotafuta lisionekane kwenye zana ya maombi:
  • Shirika lako lisilo la faida limejiondoa kwenye michango mtandaoni. Ni lazima mashirika yasiyo ya faida yakuruhusu uchangishe mtandaoni. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujijumuisha ili kupokea michango ya wengine.
  • Shirika lako lisilo la faida linafanya kazi chini ya jina tofauti. Uhisani wa YouTube hutumia data ya jina la shirika lisilo la faida kutoka GuideStar. Jaribu kutafuta kwa kutumia EIN kwenye zana ya maombi.
  • Shirika lako lisilo la faida halishiriki kwenye mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Shirika lisilo la faida linaweza kutuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.
  • Shirika lako lisilo la faida halijasajiliwa na Guidestar kwa mujibu wa sheria ya Marekani ya 501(c)(3). Angalia kwenye guidestar.org ili uthibitishe iwapo shirika lisilo la faida linapatikana hapo.

Shirika langu lisilo la faida halipatikani Marekani. Je, mtayarishi anaweza kuchangia shirika langu lisilo la faida?

Huduma ya michango ya Uhisani wa YouTube inapatikana kwa mashirika yasiyo ya faida ya Marekani pekee yanayotimiza masharti ya kujiunga. Ikiwa shirika lako lisilo la faida halitimizi masharti, zifuatazo ni baadhi ya njia nyingine za kuchangisha pesa kwenye YouTube.

Ni nini maana ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na ninawezaje kuomba akaunti yake?

Ili kutimiza masharti ya kupokea pesa kutoka kwenye michango ya Uhisani wa YouTube, shirika lisilo la faida lazima liwe na akaunti ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Pata maelezo zaidi kuhusu mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na jinsi ya kuomba akaunti yake.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanzisha michango ya Uhisani wa YouTube.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Usambazaji wa Michango

Je, shirika langu lisilo la faida hupataje michango iliyochangwa kupitia Uhisani wa YouTube?

Google hushirikiana na shirika la Network for Good ili kukusanya na kusambaza michango kupitia ombi la Google. Ili upate michango, unapaswa kujijumuisha ili upokee pesa kutoka kwenye shirika la Network for Good.

Kiasi chote cha michango hutumwa kwa shirika lisilo la faida na YouTube italipia ada za miamala. Kama inavyotakiwa na IRS ya Marekani, shirika la Network for Good lina udhibiti wa kipekee wa kisheria kwa michango baada ya kupokewa. Ikiwa shirika la Network for Good haliwezi kusambaza pesa kwa shirika lisilo la faida lililochaguliwa na mtayarishi wa YouTube, shirika la Network for Good litasambaza pesa hizo kwa shirika mbadala lisilo la faida la Marekani, ambalo linastahiki. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi mchakato wa kusambaza pesa wa Network for Good hufanya kazi.

Je, shirika langu lisilo la faida linawezaje kujijumuisha ili kupokea malipo ya michango?

Kabla ya kuanza: Hakikisha kama shirika lako linatimiza masharti ya kupata pesa kutoka Network for Good kwa kutafuta kwenye hifadhidata yake.
Fuata maagizo haya ya kujijumuisha ili kupokea michango ya wengine kupitia GuideStar.

Wakati wa malipo

Michango husambazwa na Network for Good, shirika la ufadhili lililosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Marekani ya 501(c)(3) linalokusanya na kusambaza michango kwa mashirika yasiyo ya faida. Inaweza kuchukua hadi miezi 2 kabla ya mchango kufikia shirika lako lisilo la faida. Iwapo mchango hauzidi $10, pesa hizo zitatumwa kila mwaka. Pata maelezo zaidi kuhusu usambazaji wa michango.

Kusasisha maelezo ya akaunti yako ya kutumiwa pesa

Mojawapo ya masharti ya michango ya Uhisani wa YouTube ni kufungua akaunti ya kuweka pesa moja kwa moja kwenye Network for Good. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufungua akaunti ya kuweka pesa moja kwa moja.
Kama inavyotakiwa na IRS, shirika la Network for Good lina udhibiti wa kipekee wa kisheria kwa michango baada ya kupokewa. Ikiwa shirika la Network for Good haliwezi kusambaza pesa kwa shirika lisilo la faida lililochaguliwa na mtayarishi wa YouTube, shirika la Network for Good litasambaza pesa hizo kwa shirika mbadala lisilo la faida la Marekani ambalo linastahiki, kwa hiari yake.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Maelezo ya Shirika Lisilo la Faida kwenye Uhisani wa YouTube

Wasifu wa GuideStar ni nini?

Baadhi ya maelezo ya shirika lisilo la faida (jina, nembo, nk.) yanayoonyeshwa na mchango wa Uhisani wa YouTube hutolewa kwenye wasifu wa GuideStar wa shirika lako lisilo la faida. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunda wasifu mpya wa GuideStar wa shirika lako au kusasisha wasifu uliopo.

Ninawezaje kusasisha nembo ya shirika langu lisilo la faida?

Kituo kinapoanzisha mchango wa Uhisani kwenye YouTube, kinaweza kuchagua kati ya nembo za kawaida na nembo ya shirika lisilo la faida iliyo kwenye GuideStar. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka, kuondoa au kubadilisha nembo inayohusishwa na wasifu wa GuideStar wa shirika lako lisilo la faida.

Ninawezaje kusasisha jina la shirika langu lisilo la faida?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha jina la shirika lako linaloonyeshwa kwenye wasifu wako wa GuideStar.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14815287167669538352
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false