Chapa ya biashara

Chapa ya biashara ni neno, alama au mchanganyiko wa hayo ambao hutambulisha chanzo cha bidhaa na huitofautisha na bidhaa nyingine. Chapa ya biashara hupatikana kwa kampuni au huluki nyingine kupitia mchakato wa kisheria. Mmiliki wa chapa akishapata chapa ya biashara, ana haki za kipekee za kutumia kwa ajili ya bidhaa hizo.

Ukiukaji wa hakimiliki ya chapa ya biashara ni kutumia chapa ya biashara isivyofaa au bila idhini kwa namna inayoweza kusababisha utata kuhusu chanzo cha bidhaa hiyo. YouTube inapiga marufuku video na chaneli zinazokiuka chapa za biashara. Maudhui yako yakitumia chapa za biashara za mtu mwingine katika njia ambayo huenda ikaleta utata, video zako zinaweza kuzuiwa. Huenda chaneli yako pia ikasimamishwa.

Ikiwa unafikiria chapa yako ya biashara inakiukwa, kumbuka kuwa YouTube haishughulikii upatanisho wa mizozo ya chapa za biashara kati ya watayarishi na wamiliki wa chapa za biashara. Kwa hivyo, tunahimiza wamiliki wa chapa za biashara kuzungumza moja kwa moja na mtayarishi aliyechapisha maudhui husika. Kuwasiliana na aliyepakia kunaweza kurekebisha tatizo haraka zaidi kwa njia inayomfaa kila mtu. Baadhi ya watayarishi huorodhesha njia unazoweza kuwasiliana nao katika chaneli yao.

Iwapo wewe na mmiliki wa akaunti husika hampati suluhisho, tuma malalamiko kuhusu chapa ya biashara kupitia fomu yetu ya Malalamiko kuhusu chapa ya biashara. 

Tuma malalamiko kuhusu chapa ya biashara

YouTube iko tayari kufanya ukaguzi mdogo wa malalamiko adilifu na itaondoa maudhui katika hali ya ukiukaji wa wazi. Ili kusaidia kutatua mizozo, YouTube hutuma kila malalamiko kuhusu chapa ya biashara kwa aliyepakia kabla ya kuchukua hatua yoyote. Hatua hii humruhusu aliyepakia kushugulikia matatizo yoyote ya Chapa ya biashara. 

Tutakubali pia malalamiko kuhusu chapa ya biashara yasiyofuata mpangilio yaliyotumwa kupitia barua pepe, faksi na barua.

Ikiwa malalamiko yako yanahusu uuzaji au utangazaji wa bidhaa bandia, tafadhali fungua Malalamiko kuhusu bidhaa bandia.

Ikiwa malalamiko yako yanahusu kazi inayolindwa, kama vile wimbo, filamu au kitabu, tafadhali fungua Malalamiko kuhusu hakimiliki.

 

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9782684506274186594
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false