Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Tazama ripoti zako zinazoweza kupakuliwa

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Ripoti za utendaji

Ripoti za video

Ripoti ya video huonyesha data kuhusu video katika Kidhibiti Maudhui cha mshirika.

  • Inapatikana mara 3 kwa wiki
  • Data ni pamoja na, lakini si tu: hali ya video, uwezeshaji wa matangazo, mara za kutazamwa, kitambulisho cha kipengee, sera n.k.
  • Haionyeshi data ya utendaji inayohusiana na mapato
  • Ikiwa video imedaiwa na vipengee vingi, kutakuwa na vitambulisho vingi vya vipengee katika safu wima ya Kitambulisho cha Kipengee lakini seti moja tu ya metadata ya kipengee.
Ripoti kamili ya vipengee

Ripoti kamili ya Vipengee huonyesha data kuhusu vipengee katika Kidhibiti Maudhui cha mshirika.

  • Inapatikana kila siku
  • Data ni pamoja na, ila si tu: maeneo ya umiliki, aina ya kipengee, kitambulisho cha kipengee cha awali, marejeleo yanayotumika/yasiyotumika, sera ya zinazolingana, nk.
  • Hati hii inawafaa washirika ambao wangependa:
    • Kukagua seti ya vipengee ili kuthibitisha iwapo maelezo ya umiliki ni sahihi
    • Kuambatisha vitambulisho vya vipengee vya awali kwenye vitambulisho vya vipengee vya kutunga
    • Kuangalia vipengee vyote vyenye sera mahususi ya zinazolingana
Ripoti ya mizozo ya kipengee

Ripoti ya mizozo ya kipengee inapatikana kwa washirika ambao wana vipengee vilivyo na mzozo.

  • Inapatikana kila siku
  • Ikilinganishwa na ripoti zingine za vipengee, ripoti ya mizozo ya vipengee huonyesha maeneo yoyote ya umiliki ambayo yana mizozo na maelezo ya mabadiliko ya mwisho ya umiliki.
Ripoti ya vipengee (vipengele)

Ripoti ya Vipengee (vipengele) huonyesha data kuhusu Vipengele katika Rekodi ya Sauti au Faili zenye Maelezo ya Umiliki wa Utungo na metadata inayohusiana ya mshirika.

  • Inapatikana kila siku kwa washirika wenye vipengele, kama vile washirika wa uchapishaji na lebo za muziki
  • Huonyesha data kuhusu vipengele mahususi, ikiwa ni pamoja na kipengele cha metadata na kipengee kikuu cha kipengele
Ripoti ya madai

Ripoti ya madai huonyesha data kuhusu madai yanayoendelea, yaliyokoma na yanayosubiri hatua ichukuliwe ya vipengee katika Kidhibiti Maudhui cha mshirika. Inajumuisha madai kuhusu video za faragha, zisizoorodheshwa na zilizozuiwa.

  • Inapatikana kila siku
  • Huonyesha data kuhusu madai yote ya kipengee na maelezo ya sera husika
  • Data ni pamoja na, lakini si tu: sera inayotumika, aina ya dai, chanzo, n.k.
Ripoti ya Video Fupi

Ripoti ya Video Fupi huonyesha ripoti 2: Ripoti ya Utayarishaji wa Vipengee vya Video Fupi na Ripoti ya Utazamaji wa Vipengee vya Video Fupi.

  • Ripoti ya Kipengee cha Video Fupi huonyesha idadi ya Video Fupi tofauti zilizotayarishwa kwa kutumia maudhui ya maktaba ya sauti za Video Fupi zilizopewa leseni zinazohusiana na kipengee, yaliyopangwa kulingana na nchi au eneo na mwezi, kwa mmiliki husika. Ripoti pia hujumuisha sehemu za metadata ya kipengee husika: ISRC, Kitambulisho cha kipengee, Jina la Kipengee, Lebo ya Kipengee, Kitambulisho Maalum, UPIC, GRID, Msanii na Albamu.

  • Ripoti ya Utazamaji wa Kipengee cha Video Fupi huonyesha idadi ya Video Fupi zilizotayarishwa kwa kutumia maudhui ya maktaba ya sauti za Video Fupi zilizopewa leseni zinazohusiana na kipengee zilizopangwa kulingana na nchi au eneo na mwezi, kwa mmiliki husika. Ripoti pia hujumuisha sehemu za metadata ya kipengee husika: ISRC, Kitambulisho cha kipengee, Jina la Kipengee, Lebo ya Kipengee, Kitambulisho Maalum, UPIC, GRID, Msanii na Albamu.

  • Inapatikana kwa mwezi ndani ya siku 25 baada ya kuisha kwa kila mwezi wa kalenda.

Ripoti ya marejeleo

Ripoti ya marejeleo huonyesha data kuhusu marejeleo yote yaliyoundwa na mshirika.

  • Inapatikana kila wiki
  • Huonyesha uambatishaji wa vitambulisho vya video ya marejeleo kwa vipengee vya kipengee na marejeleo
  • Hujumuisha pia maelezo kuhusu mtoa marejeleo, utengaji, aina, tarehe ya kuundwa, nambari ya madai yanayoendelea na kipengee kinachohusishwa.
  • Kumbuka: Si kila marejeleo yatakuwa na kitambulisho cha video ya marejeleo: Kitambulisho cha video ya marejeleo kinapatikana tu iwapo rejeleo linahusiana na video iliyopakiwa kwenye kituo.
Ripoti ya kampeni
Ripoti ya kampeni huonyesha data kuhusu kampeni maalum za kujifanyia mwenyewe ambazo zimeanzishwa na mshirika, ikiwa ni pamoja na vipengee na lebo za vipengee zinazotumika kwenye kila kampeni.
  • Inapatikana kila wiki.
  • Huonyesha data husika ya utendaji wa kampeni, kama vile idadi ya maudhui yaliyozalishwa na watumiaji (UGC) yalidaiwa pamoja na idadi ya mibofyo iliyokuwepo kwenye kadi za kampeni.
  • Hujumuisha tu data kuhusu kampeni maalum za kujifanyia. Haionyeshi data kuhusu kampeni chaguomsingi au kampeni za miamala.

Ripoti za fedha

Ripoti ya muhtasari wa malipo
Ripoti ya Muhtasari wa Malipo hujumuisha mapato yako ya jumla, yaliyochanganuliwa kulingana na aina ya mapato (kama vile matangazo, usajili, miamala). Hujumuisha pia marekebisho. Jumla ya mapato huripotiwa katika Dola za Marekani (USD) na sarafu ya malipo yako.
Ripoti ya mapato ya matangazo

Ripoti ya Mapato ya Utangazaji ina mapato na utazamaji unaohusiana na video zinazofadhiliwa na matangazo.

Kwa washirika wa TV na Filamu, maelezo kamili ya ripoti ya Mapato ya Utangazaji yanaweza kupatikana hapa.

Ripoti ya mapato ya usajili
Ripoti ya Mapato ya Usajili hujumuisha mapato kutoka YouTube Music, Muziki wa Google Play pamoja na YouTube Premium.
Ripoti ya mapato ya miamala

Ripoti ya Mapato ya Miamala ina mapato ya kukodi filamu (EST) na kukodi video (VOD).

Ripoti ya Mapato ya Miamala inapatikana kwa washirika wa Filamu na TV tu.

Ripoti ya mapato ya kitengo cha sauti
Ripoti ya Kitengo cha Sauti ina mapato ya YouTube Music kutoka kwa watumiaji ambao:
  • Wanatumia hali inayofanana na ya redio ambayo hawatumii wanapohitaji
  • Wanatumia vifaa visivyo na skrini kwa kutumia Mratibu wa Google (kwa mfano, Google Home)
Ripoti ya vipengele vinavyolipiwa
Ripoti ya Vipengele Vinavyolipiwa inajumuisha mapato kutoka:
  • Ununuzi wa Super Chat (SCT)
  • Uanachama (SPT)
  • Super Stickers (SST)
  • FameBit (FMT)
Ripoti ya mapato ya Video Fupi
Ripoti ya mapato ya Video Fupi ni muhtasari wa mapato kutoka Video Fupi za YouTube.
Ripoti ya matangazo kwenye Video Fupi
Ripoti za matangazo kwenye Video Fupi ina data ya mapato ya matangazo kwenye Video Fupi kwa ajili ya washirika wasio wa muziki.
Ripoti ya usajili kwenye Video Fupi
Ripoti ya usajili kwenye Video Fupi ina data ya mapato yaliyochumwa kupitia ugavi wa mapato kwenye usajili unaolipiwa kwa ajili ya washirika wasio wa muziki.
Ripoti ya mapato ya marekebisho ya matangazo

Ripoti ya mapato ya marekebisho ya matangazo hutoa muhtasari wa marekebisho ya mapato ya matangazo. Hii inaweza kujumuisha mapato yanayotokana na uchumaji wa mapato katika mzozo na mapato yanayotokana na kusuluhisha mzozo wa kipengee.

Ripoti hii huchapishwa tu baada ya marekebisho yanapofanyika kwa mwezi husika.

Ripoti ya mapato ya marekebisho ya vituo unavyofuatilia

Ripoti ya mapato ya marekebisho ya vituo unavyofuatilia hutoa muhtasari wa marekebisho ya mapato ya usajili.

Ripoti hii huchapishwa tu baada ya marekebisho yanapofanyika kwa mwezi husika.

Microsoft Excel katika kompyuta za Macintosh haitumii usimbaji wa UTF-8. Iwapo metadata yako inajumuisha herufi zozote zisizo za Kilatini, tumia programu tofauti ya lahajedwali kama vile Majedwali ya Google.

Ripoti nyingine

Ripoti ya Ukiukaji wa Video za Picha
Kumbuka Ripoti hii huonekana kwa washirika wa muziki pekee wanaotoa Video za Picha.

Ripoti ya Ukiukaji wa Video za Picha ni ripoti ya kila mwezi ambayo ina maelezo kuhusu video za picha zilizoondolewa kutokana na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya.

Ripoti inaonyesha video za picha zilizoathirika kutoka mwezi uliotangulia. Katika wiki ya kwanza ya kila mwezi, ripoti mpya zinaongezwa kwenye kichupo cha Zingine cha ukurasa wa Ripoti kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio. Ikiwa hakuna video za picha zilizoondolewa mwezi uliotangulia, ripoti itakuwa tupu. Ripoti zitaonekana kwa miezi 2, kisha zinafutwa ili kutii sera za kuhifadhi data.

Kidokezo: Pakua nakala ya ripoti yako ya kila mwezi ili urejelee baadaye.

Ikiwa video zako zozote za picha ziliondolewa kutokana na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya, wasiliana na Kituo cha Usaidizi kwa Watayarishi wa YouTube au ujaze Fomu ya Kuwasiliana Nasi katika Kituo cha Usaidizi. Ukiwasiliana nasi kupitia Fomu ya Kuwasiliana Nasi, hakikisha umeingia katika akaunti inayohusiana na akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui kabla ya kuwasilisha fomu.

Ripoti ya Hakimiliki ya Video za Picha
Kumbuka: Ripoti hii huonekana kwa washirika wa muziki pekee wanaotoa Video za Picha.

Ripoti ya Hakimiliki ya Video za Picha ni ripoti ya kila mwezi iliyo na maelezo kuhusu video za picha zilizoondolewa kutokana na ombi la kuondoa video.

Ripoti inaonyesha video za picha zilizoathirika kutoka mwezi uliotangulia. Katika wiki ya kwanza ya kila mwezi, ripoti mpya zinaongezwa kwenye kichupo cha Zingine cha ukurasa wa Ripoti kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio. Ikiwa hakuna video za picha zilizoondolewa mwezi uliotangulia, ripoti itakuwa tupu. Ripoti zitaonekana kwa miezi 2, kisha zinafutwa ili kutii sera za kuhifadhi data.

Kidokezo: Pakua nakala ya ripoti yako ya kila mwezi ili urejelee baadaye.

Ikiwa unaamini Video yako ya Picha iliondolewa kimakosa, unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha.

Ripoti ya Video za Picha zilizowekewa Masharti ya Umri
Kumbuka: Ripoti hii huonekana kwa washirika wa muziki pekee wanaotoa Video za Picha.

Ripoti ya Video za Picha zenye Masharti ya Umri ni ripoti ya kila mwezi yenye maelezo kuhusu video za picha zilizo na masharti ya umri, kumaanisha zinaweza tu kuchezwa na watumiaji waliongia katika akaunti wenye zaidi ya miaka 18.

Ripoti inaonyesha video za picha zilizoathirika kutoka mwezi uliotangulia. Katika wiki ya kwanza ya kila mwezi, ripoti mpya zinaongezwa kwenye kichupo cha Zingine cha ukurasa wa Ripoti kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio. Ikiwa hakuna video za picha zilizowekewa masharti ya umri mwezi uliotangulia, ripoti itakuwa tupu. Ripoti zitaonekana kwa miezi 2, kisha zinafutwa ili kutii sera za kuhifadhi data.

Kidokezo: Pakua nakala ya ripoti yako ya kila mwezi ili urejelee baadaye.

Ikiwa unaamini Video yako ya Picha iliwekewa masharti ya umri kimakosa, unaweza kukata rufaa ya kupinga uamuzi huo. Ili ukate rufaa, tafadhali wasiliana na timu yako ya usaidizi ya YouTube ukiwa na utambulisho wa video na sababu ya kuunga mkono rufaa yako.

Ripoti ya marekebisho katika kiwango cha chaneli

Ripoti ya Marekebisho katika Kiwango cha Chaneli hutoa muhtasari wa chaneli na mapato yote yaliyozuiwa au kurekebishwa kutokana na ukiukaji wa sera zetu za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube.

Ripoti hii inapatikana tu kwa washirika wa Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) wasio wa muziki na washirika wa MCN-A.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7495520778363652263
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false