Chagua mkakati wa kufikia hadhira za kimataifa

Kadri kituo chako kinavyokuwa na kufikia watazamaji ulimwenguni kote, tunashauri ufungue akaunti tofauti kwa lugha tofauti au nchi/maeneo. Hapa chini kuna mikakati mitatu ya kufikia hadhira za kimataifa. Ili kusaidia kufikia hadhira zaidi ya kimataifa, unaweza kutumia manukuu ya kiotomatiki, kuweka tafsiri mwenyewe, au kutumia zana na huduma za wahusika wengine.

Tumia akaunti moja yenye maudhui katika lugha nyingi

Weka maudhui yako yote katika kituo kimoja. Pakia video katika lugha nyingi kwa jiografia tofauti.

Kuweka chapa

Chapa yako itafanana katika nchi/maeneo tofauti. Ikiwa hadhira yako inatumia hoja zile zile za utafutaji za chapa yako bila kujali lugha, kituo chako kitakuwa rahisi zaidi kugunduliwa.

Kushirikishwa

Kutumia kituo kimoja huleta pamoja watazamaji na wanaofuatilia. Inawarahisishia pia watazamaji hatua ya kupata kituo chako katika Utafutaji kwenye YouTube.

Kituo chako kitapata machapisho, maoni na taarifa za mipasho katika lugha nyingi tofauti. Hali hii inaweza kutatiza hadhira yako.

Ili kusaidia hadhira yako:

Usimamizi

Ukiwa na maudhui yako katika sehemu moja, timu yako inaweza kujikita katika kudhibiti kituo kimoja, hatua inayorahisisha mchakato wa kudumisha chapa na mwonekano kimataifa.

Fungua vituo tofauti kwa ajii ya lugha tofauti

Kufungua vituo tofauti kwa ajili ya lugha na jiografia tofauti. Mkakati huu hufaa lugha zenye alfabeti au hoja za utafutaji zinazotofautiana.

Kuweka chapa

Unaweza kuwekea kila kituo mapendeleo ya hadhira ya mahali na kujumuisha kwa urahisi matukio na matangazo ya mahali. Ikiwa chapa yako inatofautiana kidogo katika nchi/maeneo tofauti, mkakati huu hukuruhusu kujumuisha tofauti hizo katika mkakati wa kituo chako.

Kushirikishwa

Vituo tofauti hukupa mawasiliano yanayofaa hadhira zako tofauti. Vipengee vyote katika kila kituo vitafaa hadhira mahususi, hatua itakayopelekea hali bora zaidi ya utazamaji. Watazamaji watakuwa na uwezekano mdogo wa kutatizika au kuacha kutazama kwa sababu ya maudhui ya lugha tofauti.

Ili kuboresha uwezo wa kutambulika:

  • Bainisha lugha au jiografia ya kila kituo ili watazamaji waweze kupata kituo chao katika utafutaji kwenye YouTube.
  • Tangaza chaneli zako za lugha tofauti katika vyombo mbali mbali vya habari kati ya vituo vyako vingine ili uboreshe uwezo wa kutambulika.
  • Weka chaneli zinazovutia kwenye sehemu ya “chaneli zinazoangaziwa” ya ukurasa wa chaneli yako.

Usimamizi

Kila kituo binafsi kitahitaji kushughulikiwa na matunzo endelevu. Hakikisha kuwa chapa yako inaweza kutenga rasilimali za kutosha kudumisha kila kituo ili kuwa na ratiba ya kawaida ya kupakia na kushiriki.

Kufungua kituo kimoja cha kimataifa na vituo vingine vya mahali

Tumia kituo kimoja kama kituo kikuu cha chapa yako ili kuonyesha kampeni za kimataifa. Fungua vituo tofauti vya mahali vya lugha na nchi/maeneo tofauti.

Kuweka chapa

Tumia kituo chako kikuu kwa maudhui ya kimataifa na vituo vya mahali kwa matukio na ofa. Tayarisha violezo vinavyofanana kwa ajili ya metadata na vijipicha ili kudumisha mwonekano katika vituo vyako vyote.

Kushirikishwa

Ingawa watazamaji na wanaofuatilia watakuwa wamegawanywa kati ya vituo vingi, watazamaji watapata hali bora ya utazamaji iliyojanibishwa. Tumia kituo kikuu kuelekeza watumiaji kwenye vituo vyako vya mahali ukitumia metadata ya video, maelezo ya kituo na ratiba inayoangaziwa ya kituo.

Kupakia video mara kwa mara kwenye vituo vya mahali kunaweza kusaidia upatikanaji wake katika utafutaji kwenye YouTube.

Usimamizi

Muundo huu wa kupanga kituo unahitaji ushirikiano kati ya timu za kimataifa na zilizo mahali ulipo lakini hukuruhusu kuweka ujumbe wa biashara unaofaa masoko ya mahali ulipo. Mkakati huu unahitaji muda na jitihada nyingi ili kuudumisha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11874915546229571795
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false