Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Usijumuishe vituo kwenye madai ya Content ID

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.
Unapowasha kipengele cha ulinganishaji wa Content ID, YouTube hutengeneza kiotomatiki madai dhidi ya maudhui ya watumiaji wengine yaliyopakiwa yanayolingana na (sehemu za) faili zako za marejeleo.

Wakati mwingine, huenda ukapendelea kuzuia Content ID kudai video zinazopakiwa na vituo fulani vya YouTube. Kwa mfano, studio ya filamu huenda isidai video zinazopakiwa kupitia kituo kinachokadiria na kutangaza filamu zake. Unaweza kutojumuisha vituo dhidi ya madai ya Content ID kwa kuweka vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa.

Madokezo

Ongeza vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa

Unaweza kuongeza kituo kimoja au zaidi kwenye orodha yako ya walioruhusiwa ili visijumuishwe kwenye madai ya Content ID. Ili kuongeza vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Orodha ya walioruhusiwa.
  3. Kwenye kona ya juu kulia, bofya ONGEZA VITUO.
  4. Weka URL au kitambulisho cha chaneli Kitambulisho cha chaneli ni mfuatano wa herufi na nambari 24, unaoanza na 'UC' kwenye URL ya chaneli.
    • Ili uongeze zaidi ya kituo kimoja kwa wakati mmoja, bandika kwenye kisanduku cha maandishi orodha ya vitambulisho vya kituo vikiwa vimetenganishwa kwa koma.
  5. Bofya ONGEZA.

Baada ya kuongeza vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa, Content ID haitadai video zozote zinazopakiwa kwenye vituo hivyo kuanzia wakati huo. Lakini, madai yoyote yaliyowasilishwa kabla ya kuongeza vituo hivyo kwenye orodha ya walioruhusiwa hayataondolewa kiotomatiki. Pata maelezo kuhusu kuondoa madai.

Ikiwa maudhui yanamilikiwa na zaidi ya mshirika mmoja, kila mshirika sharti aongeze kituo kwenye orodha yake ya walioruhusiwa ili kuzuia madai dhidi ya maudhui hayo.

Ondoa vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa

Kuondoa vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa inamaanisha Content ID itaondolea vituo hivyo idhini dhidi ya madai. Vituo hivi vikipakia video zinazolingana na faili zako za marejeleo na vituo hivyo havipo tena kwenye orodha yako ya walioruhusiwa, Content ID itawasilisha madai. Ili kuondoa vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Orodha ya walioruhusiwa .
  3. Bofya upau wa kichujio kisha Kitambulisho cha kituo au Jina la kituo.
  4. Bandika vitambulisho au kituo au majina ya vituo yakiwa yametanganishwa kwa koma ya kisha TUMIA.
  5. Bofya visanduku vya kuteua vilivyo karibu na vituo unavyotaka kuondoa kwenye orodha ya walioruhusiwa.
    • Ili kuchagua vituo vyote, bofya kisanduku cha kuteua juu ya orodha ya matokeo ya utafutaji kisha Chagua vyote.
  6. Kwenye bango lililo sehemu ya juu, bofya ONDOA.
Kumbuka: Kuondoa kituo kwenye orodha ya walioruhusiwa hakufuti kituo kwenye YouTube.

Tuma maelezo kuhusu vituo kwenye orodha yako ya walioruhusiwa

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu chaneli kwenye orodha yako ya zilizoruhusiwa, kama vile kitambulisho cha chaneli, jina la chaneli na tarehe ya kuondolewa madai. Ili kutuma maelezo haya:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Orodha ya walioruhusiwa .
  3. Bofya visanduku vya kuteua karibu na vituo unavyotaka kutuma maelezo kuvihusu.
  4. Kwenye bango la sehemu ya juu, bofya Tuma  kisha uchague Data iliyotenganishwa na koma (.csv) au Majedwali ya Google (kichupo kipya). Faili itaanza kuchakatwa.
  5. Baada ya faili kumaliza kuchakatwa:
    • Kwa faili ya .csv: Bofya PAKUA kwenye bango la sehemu ya juu.
    • Kwa faili ya Majedwali ya Google: Bofya FUNGUA MAJEDWALI YA GOOGLE KATIKA DIRISHA JIPYA kwenye bango lililo sehemu ya juu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4791342526668558131
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false