Ikiwa mmiliki wa video amewasha kipengele cha maoni, unaweza kuchapisha maoni na kuweka alama ya nimeipenda, sijaipenda au kujibu maoni ya watu wengine kuhusu video, wimbo au podikasti katika programu ya YouTube na YouTube Music. Unaweza pia kubadilisha au kufuta maoni yako yoyote. Majibu ya maoni huwekwa chini ya maoni halisi ili uweze kufuatilia mazungumzo.
Chapisha maoni kwenye video
Maswali Yanayoulizwa Sana kwenye sehemu ya kukagua maoni
Kuwasiliana kupitia maoni kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti
Sasa unaweza kuangalia na kuwasiliana kupitia maoni unapotazama maudhui katika televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video. Ili uangalie maoni ya video, nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa video na uchague mada ya video. Sehemu ya Kuhusu itaonekana, ikiangazia kidirisha cha maoni ya video. Chagua kigae cha maoni ili uone orodha kamili ya maoni ya video, ikiwa ni pamoja na:
- Maoni ambayo mtayarishi amebandika
- Mara za kupendwa
- Idadi ya majibu
Chagua maoni mahususi ili uyasome yote, uangalie majibu, uweke alama ya imenipendeza au haijanipendeza katika maoni hayo.
Ili ujibu au uchapishe maoni, sawazisha televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video na simu yako na utoe maoni kwa kutumia simu yako.
Ili uweke maoni au jibu:
- Fungua programu ya YouTube kwenye simu yako.
- Hakikisha kuwa umeingia katika Akaunti sawa ya Google kwenye vifaa vyote viwili.
- Dirisha ibukizi litafunguka kwenye programu yako ya YouTube, litakalokuomba uunganishe YouTube kwenye televisheni yako.
- Gusa kipengele cha Unganisha.
- Maoni ya video unayotazama kwenye televisheni yako yatapakiwa kwenye programu ya YouTube, hali itakayokuruhusu kuyachapisha na kuyashughulikia kwa urahisi.